Onyo: Ikiwa si mzalendo hii post haikuhusu, kaa pembeni. Niepushe na dhambi tafadhali.
Hello wazalendo wenzangu. Hapa natype mikono inatetemeka but I have to. Mara tu baada ya tangazo nilifuta social networks zote. Honestly nilijua here comes the hard time. Kwa kweli sikuweza ku-stand kejeli against the man.
Neno moja nawaambia watu wangu wazalendo. Kama alivyosema bro Magu: Watanzania tumtangulize Mungu. Huyu Mungu huyu aliyetuaacha tudhalilike sasa hivi anao mpango wake.
Mungu si kama sisi wanadamu. Yeye anaona mbali. Hajatuacha wala hajatutelekeza. Angeweza kutuacha tuendelee na safari huku tukiambatana mbwa mwitu na manyang'au miongoni mwetu.
Ila nani anajua Musa wetu angeweza kupambana nayo? Nani alijua kuwa kuna mbwa mwitu bado wana ndoto na Bagamoyo Port? Mbwa mwitu anayedai JNHPP ni bogus project tungemtambua kwa macho? Ndiyo, huyuhuyu ambae Magu alimtengua TRA akampeleka mkoani ajifunze. Alipoona kajifunza kampeleka kwenye ukaguzi. Leo ndiyo anatumika ku-liuza taifa!
Hakika nawaambia, macho yetu yasingewaona.
Pia angalie Mungu alivyo wa ajabu. Amewapa upofu ili watuondolee watu wasafi wakakae huko stoo ili waje kuwa hazina mara tu kazi itakapoanza upya. Amewapa upofu sasa wanajaribu kumchafua Musa wetu bila kujua kuwa wao pia wanajichafua.
Mtinange utakapoisha wao watakuwa wachafu kuliko kaburi la Magu.
Tusilie wanapomchafua Magu bali tufurahie maana wanajichafua wenyewe ili wakati utakapofika wasiwe na uhalali wa kuyasogelea malango yetu ya utawala.
Amini nawaambia: Sisi ndilo taifa pekee duniani tuliamua kusimama na Mungu hadharani. Nyakati ambapo kusimama na Mungu ni ushamba. Musa wetu alipomtangaza Mungu kuwa kiongozi wetu aliitwa Kinjekitile, mshamba, na mshirikina.
Hakuna nchi nyingine, hata hizo ambazo huitwa teule zilizoamua kuonesha kuwa Mungu ndiye muweza. Mungu alisema tumtumainie katika kila kitu. Wala hakusema tumtumainie katika yote isipokuwa "hizo sayansi".
Daima Taifa hili litasimama imara. Kwa sasa tupo tu kwenye mapumziko mafupi ili wanafiki wote akina Yuda wajionyeshe hadharani. Kisha Mungu atamuinua Joshua kwa wakati atakaoona sahihi na safari itaandelea.
Narudia: Ikiwa bango hili halikuhusu, tafadhali potezea uniepushie ban.