Mkuu mbona sikuelewi?, inaonekana hujafuatilia huu mjadala kwa urefu.
1)Kila mtu ana maslahi yake katika huu mto, Ethiopia anataka umeme, Egypt anataka chakula na kazi kwa watu wake, nani mwenye maslahi muhimu zaidi?
2)Ethiopia alipaswa kabla ya kujenga ashauriane na wenzake kukubaliana jinsi ya kuzuia athari kwa majirani, hakufanya hivyo yeye alijali maslahi yake tu, haijalishi hata kama angejenga la $20B, hiyo sio sababu ya kuathiri uchumi na maisha ya wengine kwa sababu ya $7B.
3)Hapa hakuna vita vitakavyotokea, kitakachofanyika ni kulivunja hili bwawa kutokea mbali ili lisifanye kazi kwa kurusha ndege na cruse missiles kutokea mbali.