joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,111
- 46,621
Ndio sababu nikasema mkuu mbona sikuekewi?Mkuu ninachokiweka sawa hapa ni hizo Nguvu za kijeshi unazojinasibu nazo kuhusu Misri...najaribu kukuambia tuu hiz Nguvu sio chochote ktk Ushindi wa kivita mkuu...Misri ina waasi wa Kijihadi huko Penusila ya Sinai wanamletea changamoto kubwa sana....sasa ukizungumzia vita kamili mie nashangaa, tena budjet yake ya kijeshi inakuwa supported na US.
Swala la vita Kuhusu Nchi na Nchi ni Ngumu sana kuamuliwa kwa namna ya Nani mwenye Nguvu zaidi kijeshi na ndo maana ya mifano yangu Hapo juu....Iran wakati anapigana na Iraq,Iraq ilikuwa ni Nchi yenye Nguvu za Kijeshi kuliko Nchi yoyote Mashaiki ya kati na ilikuwa inasurpotiwa na major Powers US na Europe mpaka Usovieti lkn Iran Ilishinda....Uganda Wakati ametuvamia sisi alikuwa na Nguvu nyingi sana Kijeshi na pia support Nyingi,Vietnam Na US hiyo Nguvu ya US ilishindikana kabisa kufua Dafu...sasa mkuu ukizungumzia mambo ya Manowari na Ndege Vita,huo sio Lushindi wa kumtisha mtu Nyau....Bwawa lonaendelea kujaaa Maji mkuu.
1)Kwanza sijasema kwamba kuna Vita au kutatokea Vita, ila nimesema Egypt ana nguvu za kijeshi za kuweza kulivunjilia mbali hilo bwawa bila Vita kutokea.
Sasa mkuu unasema maneno mengi bila kuangalia Geography ya hizi nchi mbili, hizi nchi hazijapakana kama hizo Iran na Iraq, sasa hiyo vita itatokeaje wakati nchi moja inao uwezo wa kutuma silaha toka mbali na kulivunja wakati Ethiopia haina jinsi ya kufika Egypt kulipiza kisasi?.
Kuhusu uwezo wa majeshi kuwa ni kigezo cha kushinda Vita, ninashangaa sana kwa kupinga hilo, sasa kigezo cha kushinda Vita ni kipi kama sio uwezo wa jeshi?, unategemea Tanzania tushinde vita dhidi ya Urusi, China, USA, UK au India.
