Nakuliza wewe uliwahi kumuona babu yako au baba wa babu yako sio wewe au hakuna hata mmoja wetu ambaye amewahi kuona, au kusikia, au kuhisi, au kunusa, au kuona mababu zetu lakini tunaamini kwamba walikuwepo.
Mababu zetu walikuwepo na hili linafahamika wazi kabisa.
Kutokana na point yako hakuna hata mmoja wetu anayepaswa kuamini kwamba mababu zetu walikuwepo, kwa kuwa hakuna ushahidi wa kuthibitisha hili.
Ushahidi wa kuthibitisha upo, kuna picha za mababu zetu.
Kumbukumbu za mababu zetu, ikiwemo picha zao, makazi yao, nguo zao na hata vitu vyao walivyotumia wakati wa uhai wao vipo na vimehifadhiwa kama kumbukumbu.
Na hapo tunapata uthibitisho tosha kwamba mababu zetu walikuwepo.
Akili yako una sema Mungu hayupo sababu hakuna aliye muona ukweli akili yako haiko sawa, unataka kusema sisi tusio waona babu tuseme hatuna mababu.
Mungu
hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika zaidi ya hadithi uchwara za vitabuni zisizo na uthibitisho wowote ule.
Hakuna mwenye ushahidi wala kitu chochote kile kinachothibitisha uwepo wa Mungu.
Hii point inatuweka kwenye hatua ya unafiki, unawezaje kuwa na imani kama hiyo, lakini unaamini kwamba mababu zako walikuwepo, nina hakika wengi, ikiwa sio wanao amini Mungu wote wanaamini uwepo wa mababu zao.
Mababu zetu
hawa aminiki walikuwepo.
Mababu zetu
wanajulikana kabisa kwamba walikuwepo.
Kumbukumbu zao zipo na zimehifadhiwa. Picha zao, makazi yao waliyo ishi, vitu vyao walivyotumia vipo na vimehifadhiwa.
Pia makaburi yao yapo na yanathibitisha wazi kabisa kwamba mababu zetu walikuwepo na waliishi.
Sasa huyo Mungu wako wa
kufikirika hayupo kwa namna yoyote ile na
hakuna ushahidi wala uthibitisho wowote ule wa uwepo wake.
Mnapiga porojo tu na hadithi uchwara za kusadikika za hekaya za Biblia.
Wewe unasema Mungu hayupo kwa sababu tu fikra zako ziko ki Atheist zina dosari, sayansi imehitimisha kuwa hakuna kitu kama bahati nasibu. Huo ni ushahidi muhimu unaoonyesha kuwepo kwa Mungu.
Huyo Mungu kama yupo ajitetee mwenyewe sio wewe unahangaika kumuelezea na kumtetea.
Unahangaika sana kumuelezea Mungu ambaye hayupo kujieleza mwenyewe.
Unahangaika kufosi uwepo wa Mungu na wala huna uthibitisho wowote ule wa kuthibitisha uwepo wake.
Hakuna Mungu.