Mungu ametuleta hapa duniani kuja kufanya mtihani na moja wapo ni kumuamini bila kumuona usipo muamini wewe utakuwa umepotea.
Huyo Mungu akiaminiwa anafaidika nini?
Huyo Mungu asipoaminiwa anapungukiwa nini?
Huyo Mungu kama alitaka kuaminiwa na binadamu wote, Alishindwaje kuumba binadamu wema watakao mtii na kumwamini siku zote na wakati wote?
Huwezi kumuona Mungu ukaishi ndio sababu, angetaka umuone ukaishi angeweza lakini hakutaka hilo na hio ni amri yake yeye.
Kama Mungu haonekani, Ni nani aliwahi kumuona huyo Mungu akajua kweli yupo?
Au unajaribu tu, kufosi imani yako uliyoaminishwa?
Bila uthibitisho wowote ule.
Leo akikufungulia tu umuone malaika mtoa roho basi ujue unakwenda ni bye bye hubaki.
Huyo Mungu kama haonekani na hataki aonekane, Ni nani alimuona akajua yupo?
Thibitisha Mungu yupo na si imani zako za vitabuni ulizo aminishwa.
Sa we kama unamini hakuna Mungu ulizaliwa tu kutokana na shahawa za baba yako kwanini wengine wakizaliwa tu wanakufa wengine wanaishi?
Kuzaliwa na kufa ni hatua za kila binadamu na kila mmoja lazima atazipitia hatua hizi. Hazikwepeki.
Wewe kuzaliwa na kuishi, Haimaanishi kwamba hutakufa. Kila mtu atakufa.
Tunatofautiana tu muda na wakati wa kufa. Wapo wanaozaliwa na kufa hapohapo.
Wapo wanaozaliwa na kuishi na wapo wanaoishi lakini mwishowe hufa.
Kwanini hizo shahawa zifanye hivyo hivi huoni hapo ni Mungu ndio anapanga vile shahawa zitapanga vipi.
Kuhusisha Mungu na Shahawa ni kufanya logical fallacy ya non-sequitur.
Unaunganisha vitu viwili tofauti visivyo na uhusiano wowote ule kuunda hitimisho potofu.
Mungu na Shahawa hazina uhusiano wowote ule.
Mungu hapangi chochote.
We unauhakika gani mpaa kesho utaishi. Au bada ya saa au nusu saa.
Either uwe una mwamini Mungu au haumwamini, Hakuna mwenye uhakika kwamba kesho ataendelea kuishi.
Binadamu hawaumbwi.
Binadamu tunazaliana wenyewe kwa wenyewe.
Hakuna Mungu aliyeumba binadamu. Binadamu ndio wamemuumba Mungu kupitia imaginations tu.
Hakuna Mungu aliyeumba kitu chochote kile.
Mungu hayupo.
si kwa ajili ya haja ya kuabudiwa tu, ni kwa ajili ya kuwajaribu na kuwaruhusu kuchagua kumwabudu kwa uhuru.
Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Anatujaribu ili agundue nini?
Kuna kipi asichokijua hadi atujaribu?
Hivi huyo Mungu ana jielewa kweli?
Kumwona Mungu moja kwa moja kungepuuza jaribu hili, kwani kungelazimisha ibada kwa woga au badala ya imani ya kweli. Ulimwengu huu ni mtihani, katika huo mitihani vitu visivyo onekana na moja ya hivyo ni uwepo wa Mwenyezi Mungu humuoni, na ni sehemu ya mtihani huo.
Kama Mungu haonekani, Ni nani alimuona akajua yupo?
Kama Mungu haonekani, ulijuaje na unathibitishaje yupo?