Atheists ni washirikina ambao wamemkanusha Allah kwa jeuri, kiburi na matamanio ila wakachukua Sifa zake wakazipeleka kwa "nature", "sayansi", "ulimwengu" kisha wanaziabudu kinyume na Allah.
Hawa ni waabudu nature kama waabudu nature wa zamani na wa sasa wanaoendelea kuabudu nature. Tofauti yao ni wale waabudu nature wa zamani (kama waabudu Jua, Mwezi, Nyota, milima) wale walikuwa wazi na direct. Hawa "atheists" wa leo wanajificha nyuma ya Sayansi, Usomi, Mantiki, na Falsafa falsafa na ujanja ujanja wa kucheza na lugha.
Kila mtu ameumbwa na maumbile ya kutambua kuwepo kwa Muumba ambaye Analea na kuruzuku na kutambua kuwa Muumba huyo Ana uwezo juu ya kila kitu hivyo anapaswa kumnyenyekea na kumtii na kumuabudu. Ila yale maumbile yakiwa misguided ataabudu watu, wanyama, mazingira, na kadhalika. Kila mtu ameumbwa na hiyo fitra ya kuhitaji kumuabudu Muumba wake, lile hitaji la kuabudu lipo ndani ya MwanaAdamu, sasa wengine kwa sababu mbali mbali wanai misplace wanaabudu viumbe badala ya Muumba, ila ile hali ya kuhitaji kuabudu ipo ndani yao.
Asipomuabudu Muumba wake ataabudu viumbe wenzake tu.
Asipokubali kuwa mtumwa wa Muumba wake na kumnyenyekea na kumdhalilikia, atakuwa mtumwa wa viumbe tu. Kwa sababu hitaji la kuabudu lipo ndani ya maumbile yake.
Atheists ni watu tu kwa kiburi na matamanio wanaamua kujidanganya ila ndani ya nafsi zao wanajua kuwa yupo Muumba, ila wameamua kuabudu nature, ulimwengu or whatever kinyume na Muumba wao ila kwa kiburi wanajificha nyuma ya maneno maneno meeengi.
Kazakh destroyer