Atheists wanaweza kuwa wagonjwa wa akili?

Mkuu, tena umeonyesha akili zao zinavopingana zenyewe kuhusiana na INTELLIGENT DESIGN.
'wanaamini kitanda kimetengenezwa na mtu mwenye akili' ila hawaamini binadamu hata dunia imeumbwa kiakili. Mifano ni mingi, mimi hupenda kuutumia huu ufuatao - mzunguko wa hewa tunayopumua ... ili tuishi tunavuta ndani oxijeni inayopumuliwa nje na mimea, nayo mimea ili kuishi inavuta ndani CO2 ambayo sisi tunayopumua nje... huu ni muundo ama uumbaji wa kiakili, sio umetokea tu
Haifafanui chochote.
Tuseme kilichopo ni matokeo ya intelligent design,sasa bas taja kile unacholinganisha nacho ambacho kwenye mantiki Yako sio intelligent design!
Hautaweza, maana ntakwambia hata ambacho hakipo ni intelligently restricted!
 
Atheists ni washirikina ambao wamemkanusha Allah kwa jeuri, kiburi na matamanio ila wakachukua Sifa zake wakazipeleka kwa "nature", "sayansi", "ulimwengu" kisha wanaziabudu kinyume na Allah.

Hawa ni waabudu nature kama waabudu nature wa zamani na wa sasa wanaoendelea kuabudu nature. Tofauti yao ni wale waabudu nature wa zamani (kama waabudu Jua, Mwezi, Nyota, milima) wale walikuwa wazi na direct. Hawa "atheists" wa leo wanajificha nyuma ya Sayansi, Usomi, Mantiki, na Falsafa falsafa na ujanja ujanja wa kucheza na lugha.

Kila mtu ameumbwa na maumbile ya kutambua kuwepo kwa Muumba ambaye Analea na kuruzuku na kutambua kuwa Muumba huyo Ana uwezo juu ya kila kitu hivyo anapaswa kumnyenyekea na kumtii na kumuabudu. Ila yale maumbile yakiwa misguided ataabudu watu, wanyama, mazingira, na kadhalika. Kila mtu ameumbwa na hiyo fitra ya kuhitaji kumuabudu Muumba wake, lile hitaji la kuabudu lipo ndani ya MwanaAdamu, sasa wengine kwa sababu mbali mbali wanai misplace wanaabudu viumbe badala ya Muumba, ila ile hali ya kuhitaji kuabudu ipo ndani yao.

Asipomuabudu Muumba wake ataabudu viumbe wenzake tu.

Asipokubali kuwa mtumwa wa Muumba wake na kumnyenyekea na kumdhalilikia, atakuwa mtumwa wa viumbe tu. Kwa sababu hitaji la kuabudu lipo ndani ya maumbile yake.

Atheists ni watu tu kwa kiburi na matamanio wanaamua kujidanganya ila ndani ya nafsi zao wanajua kuwa yupo Muumba, ila wameamua kuabudu nature, ulimwengu or whatever kinyume na Muumba wao ila kwa kiburi wanajificha nyuma ya maneno maneno meeengi.

Kazakh destroyer
Waabudu nature ni theists sample ya mwenye Uzi LIKUD
Zaidi ya hapo neno kuabudu ,unalitumia vibaya
 
You said it all shekhe wetu, kwa ufupi mkubwa mwanadamu lazima awe na muabudiwa, lazima aabudu na hakuna budi isipokuwa hivyo.

Sasa itakapokuwa wamemkataa yule muabudiwa wa kweli aliyewaumba na anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini basi wataabudu vingine tu katika viumbe wenzao.

Huenda wakaabudu matamanio ya nafsi zao, elimu zao, mapenzi ya kupenda vitu vya kidunia au kuabudu kisichojulikana kama kusema huyu muabudiwa wa waislamu na wakristo sisi hatumkubali ila tunaamini yupo wa kweli, al muhimm wanahangaika na watahangaika mpaka siku ya kufa kwao na mwisho watakutana na Allah mbele yao, naye atawapa hesabu ya matendo yao na Allah ni mpesi wa kuhesabu.

Nashukuru kwa kuniita ustadh Baljurashi
Tuonyeshe ushahidi unao onyesha lazima binadamu aabudu au kiumbe chochote kile?

Na kwa nini iwe binadamu tu, na sio Simba, Nyangumi au Tembo?
 
chimbuko la binadamu ni lipi ilikuweje mpaka kikapatikana kiumbe ambacho ni binadamu maana tunajua ukichaganya siment, mchanga, na kokoto unapata zenge
Ukichanganya mbegu ya baba na yai la mama, Mimba inatungwa na mtoto anazaliwa.

Hilo ndilo chimbuko.

Huelewi nini?
je binadamu alitokea tu?
Binadamu anazaliwa kutoka kwenye tumbo la Mama yake.
Na mawe miti n.k vililetwa na nan dunian?
Havikuletwa.

Vimekuwepo milele.
 
Mkuu, tena umeonyesha akili zao zinavopingana zenyewe kuhusiana na INTELLIGENT DESIGN.
'wanaamini kitanda kimetengenezwa na mtu mwenye akili' ila hawaamini binadamu hata dunia imeumbwa kiakili. Mifano ni mingi, mimi hupenda kuutumia huu ufuatao - mzunguko wa hewa tunayopumua ... ili tuishi tunavuta ndani oxijeni inayopumuliwa nje na mimea, nayo mimea ili kuishi inavuta ndani CO2 ambayo sisi tunayopumua nje... huu ni muundo ama uumbaji wa kiakili, sio umetokea tu
Mkuu, oxygen na CO2 zinaonyesha kwamba viumbe vinategemeana; hujathibitisha kwamba huo uhusiano uliundwa kwa akili, kwa sababu mfumo wa asili unaweza kuwa na mpangilio kutokana na sheria zake bila kuwa na mpangaji, na ukweli kwamba sisi tunafaidika na oxygen ya mimea hauonyeshi kwamba mimea iliundwa kwa ajili yetu , kama unadai vinginevyo, onyesha kwa nini huo mfumo usingeweza kutokea bila Intelligent Designer; maana “imepangwa” si ushahidi wa “najua nani aliyeipanga.”

Na hapa ndipo mfano wa kitanda unaposhindwa: kitanda tunajua kina mtengenezaji kwa sababu tuna ushahidi wa mtengenezaji. Nature kuwa na mpangilio hakutupi moja kwa moja mtengenezaji.
 
Haifafanui chochote.
Tuseme kilichopo ni matokeo ya intelligent design,sasa bas taja kile unacholinganisha nacho ambacho kwenye mantiki Yako sio intelligent design!
Hautaweza, maana ntakwambia hata ambacho hakipo ni intelligently restricted!
kwa hiyo - kwako wewe - recycling ya hewa tunazopumua sisi na mimea na matokeo ya bahati mbaya na sio intelligent design???
 
You said it all shekhe wetu, kwa ufupi mkubwa mwanadamu lazima awe na muabudiwa, lazima aabudu na hakuna budi isipokuwa hivyo.

Sasa itakapokuwa wamemkataa yule muabudiwa wa kweli aliyewaumba na anayewaruzuku kutoka mbinguni na ardhini basi wataabudu vingine tu katika viumbe wenzao.

Huenda wakaabudu matamanio ya nafsi zao, elimu zao, mapenzi ya kupenda vitu vya kidunia au kuabudu kisichojulikana kama kusema huyu muabudiwa wa waislamu na wakristo sisi hatumkubali ila tunaamini yupo wa kweli, al muhimm wanahangaika na watahangaika mpaka siku ya kufa kwao na mwisho watakutana na Allah mbele yao, naye atawapa hesabu ya matendo yao na Allah ni mpesi wa kuhesabu.

Nashukuru kwa kuniita ustadh Baljurashi
Unasema mwanadamu lazima aabudu, lakini hujathibitisha hilo. Kuna tofauti kati ya kuwa na kitu unachokithamini sana na kukiabudu. Mtu anaweza kupenda familia yake, elimu, kazi au maisha yake bila kuviabudu.

Na mtu akisema ‘sina sababu ya kuamini Mungu yupo,’ hiyo haimaanishi ameanza kuabudu elimu yake, matamanio yake au dunia. Kukataa kuwepo kwa Mungu si sawa na kuchagua kitu kingine kiwe Mungu.
 
kwa hiyo - kwako wewe - recycling ya hewa tunazopumua sisi na mimea na matokeo ya bahati mbaya na sio intelligent design???
Tatizo kwenye swali lako ni kwamba umeweka ‘bahati mbaya’ kama alternative ya Intelligent Design, wakati si lazima iwe hivyo. Kuna option ya tatu: NATURAL PROCESSES zinazofuata sheria za nature.

Oxygen na CO2 kubadilishana hakuthibitishi design kwa sababu tunaweza kueleza how hiyo process inavyofanya kazi bila kudhani kwamba kulikuwa na akili iliyokaa na kupanga huo mfumo. Sasa wewe unapaswa kuonyesha kwa nini hiyo explanation haitoshi na kwa nini lazima tuongeze Intelligent Designer.

Kwa sababu kusema "ANGALIA JINSI ZILIVYOPATANA" hakutoshi. Kitu tunachokiona ni INTERDEPENDENCE.

Kwa hiyo ntelligence iliyounda hiyo interdependence” ni conclusion yako.
 
Mkuu, oxygen na CO2 zinaonyesha kwamba viumbe vinategemeana; hujathibitisha kwamba huo uhusiano uliundwa kwa akili, kwa sababu mfumo wa asili unaweza kuwa na mpangilio kutokana na sheria zake bila kuwa na mpangaji, na ukweli kwamba sisi tunafaidika na oxygen ya mimea hauonyeshi kwamba mimea iliundwa kwa ajili yetu , kama unadai vinginevyo, onyesha kwa nini huo mfumo usingeweza kutokea bila Intelligent Designer; maana “imepangwa” si ushahidi wa “najua nani aliyeipanga.”

Na hapa ndipo mfano wa kitanda unaposhindwa: kitanda tunajua kina mtengenezaji kwa sababu tuna ushahidi wa mtengenezaji. Nature kuwa na mpangilio hakutupi moja kwa moja mtengenezaji.
Mkuu, binafsi, huku 'kutegemeana' ka ulivotamka, ni muundo wa kiakili flani - na ndo ushahidi, kwa sababu sayansi imeweza kutuambia mfumo lakini haijaweza na haitaweza kutuambia kwa nini mfumo uko ivo. Sidhani utaweza pia.
Sasa unaposema ni kwa sheria... sheria za nani?

Pia mkuu, tafakari dini inatuambia muumbaji alituumba kwa udongo tutarudi kuwa udongo... sayansi inatufafanulia decomposition lakini haiwezi kutuambia kwa nini ... ama kwa nini maggots na vultures na mafisi wametokea ama kuumbwa kuwa na kazi maalumu ya kusafisha mizoga hata ile isiyozikwa, mfano wanyama.
Intelligent design hio... yaani isingekuwa ivo, dunia leo ingekuwa inanuka kinoma, kuna akili ilitumika kuepusha hilo
 
Udongo/mchanga ni kitu kisicho na uhai
Mchanga umeumbwa na silicon oxides.

Maisha asilimia 99.99 ni carbon based, iwe mimea au wanyama kwa hapa duniani.

Sasa ikiwa mliumbwa kwa udongo ambayo ni silicon oxide, ikawaje mkawa na maisha ambayo ni carbon based?

Na ikiwa ni binadamu tu aliyeumbwa kwa Imani zenu, kwa nini maisha yake, bado ni carbon based sawasawa na mimea iliyoambiwa itokee tu.

Hapa unagundua hii stori nzima ina walakini ndani yake
 
Kama uwezekano wa binadamu kuumbwa na Mungu ni 99%,

Na kama kila chenye chanzo lazima kiwe na chanzo,

Je, uwezekano wa Mungu kuumbwa na Mungu mkubwa kupita yeye ni asilimia ngapi?

Na kama Mungu alitokea tu bila kuhitaji chanzo chochote, kwanini binadamu ashindwe kutokea tu, bila kuhitaji chanzo chochote?
 
Umejibu ontology ya uovu, lakini hujajibu problem of evil. Swali si uovu ni kitu gani? , swali ni kwa nini Mungu mwenye uwezo wote anaruhusu suffering ambazo angeweza kuzizuia?’
Kama mateso yapo ni kwa sababu Mungu anaweza kuyazuia.

Tatizo si kuzuia mateso. Tatizo mateso ni nini?

Uvumbuzi wote wa binadamu, maarifa ya binadamu hayawezi kufafanuliwa bila kuhusishwa kwa mateso.

Aidha, tungeweza vipi kupima upendo bila mateso? Ni kwa namna gani tunaweza kuongea upendo bila mateso?

Kama mateso yasingekuwepo ulimwengu usingekuwepo. Ulimwengu unaendelea kwa sababu ya mateso.

Kwa hiyo kujibu swali lako Mungu akizuia mateso ulimwengu hautakuwepo.

Kila kitu cha asili kinapitia mateso kwa sababu ndio njia ya kukua na kuendelea. Wavumbuzi wanapitia mateso. Kupona ugonjwa kunaambatana na maumivu.

Anayekataa mateso anakataa kukua na kuendelea. Anachagua kufa.

Mateso kwa yenyewe si adui ni mwalimu mkali.
 
kwa hiyo - kwako wewe - recycling ya hewa tunazopumua sisi na mimea na matokeo ya bahati mbaya na sio intelligent design???
Kwamba mifumo na kuathiriana ndo inaonesha intelligent design. Kummanisha Kila kitu kingekuwa kimejitenga bila kuhusiana na vingine ndo kitakuwa sio intelligent designed?
 
Japo hujaniuliza swali Mimi

Nikiangalia mimea, wanyama, binadamu, sayari na galaxies, naona nature ikifanya kazi kwa sheria na michakato yake.
Sahihi.
Vitu hivyo asili ukivilinganisha au ukivifananisha vina muundo thabiti au havina?
 
Kama mateso yapo ni kwa sababu Mungu anaweza kuyazuia.

Tatizo si kuzuia mateso. Tatizo mateso ni nini?

Uvumbuzi wote wa binadamu, maarifa ya binadamu hayawezi kufafanuliwa bila kuhusishwa kwa mateso.

Aidha, tungeweza vipi kupima upendo bila mateso? Ni kwa namna gani tunaweza kuongea upendo bila mateso?

Kama mateso yasingekuwepo ulimwengu usingekuwepo. Ulimwengu unaendelea kwa sababu ya mateso.

Kwa hiyo kujibu swali lako Mungu akizuia mateso ulimwengu hautakuwepo.

Kila kitu cha asili kinapitia mateso kwa sababu ndio njia ya kukua na kuendelea. Wavumbuzi wanapitia mateso. Kupona ugonjwa kunaambatana na maumivu.

Anayekataa mateso anakataa kukua na kuendelea. Anachagua kufa.

Mateso kwa yenyewe si adui ni mwalimu mkali.
Unamaanisha bila njaa , maisha yasingepo! au kusingekuwepo maangaiko ya kutafuta chakula?.
Yani unamaanisha kansa IPO ili tutafute dawa ya kuitibia?😅😅😅
 
Mungu anaweza kuzuia uovu, ajali, magonjwa, majanga, mateso na kifo ?
Mungu anaweza kuzuia uundaji wa magari? Mungu anaweza kuzuia uvumbuzi, ugunduzi au utengenezaji wa dawa?
Mungu anaweza kuzuia watu wanaotaka kupata mtoto? Mungu anaweza kuzuia watu wasiendeshe magari, ndege, meli, pikipiki, au baisekeli?

Kama hazuii uvumbuzi, ugunduzi, utengenezaji wa mitambo, dawa, kuzaa kwa nini azuie uovu, ajali, magonjwa, majanga, mateso na kifo?

Kwa nini unataka Mungu azuie kifo lakini husemi azuie kuzaa?
 
Wewe ni kichaa au mwendawazimu?
 
Naona ukiepuka swali langu.

Unaposema ulimwengu una muundo thabiti, unakuwa umeufananisha na upi?
Muundo thabiti ni jinsi kitu kilivyo kwa nje na kwa ndani na jinsi kinavyofanya kazi.

Si suala la kulinganisha au kufananisha ulimwengu huu na mwingine. Ni jinsi vitu vya asili vilivyo na vinavyofanya kazi.
 
D
Mungu anaweza kuzuia uundaji wa magari? Mungu anaweza kuzuia uvumbuzi, ugunduzi au utengenezaji wa dawa?
Mungu anaweza kuzuia watu wanaotaka kupata mtoto? Mungu anaweza kuzuia watu wasiendeshe magari, ndege, meli, pikipiki, au baisekeli?

Kama hazuii uvumbuzi, ugunduzi, utengenezaji wa mitambo, dawa, kuzaa kwa nini azuie uovu, ajali, magonjwa, majanga, mateso na kifo?

Kwa nini unataka Mungu azuie kifo lakini husemi azuie kuzaa?
Dini ndo inasema Mungu hapendi uovu
Inasema anatenda ndani ya wakati(immanent)
dai ni kwamba kama mlinzi yupo, tunauliza mbona basi panaibiwa?
 
Back
Top Bottom