Sawa, tukubali kwamba tetemeko lenyewe si UOVU kwa sababu ni natural event. Lakini tatizo si kuLitaja tetemeko kuwa mwovu. Tatizo ni matokeo yake kwa viumbe wenye uwezo wa kuhisi maumivu na mateso.
Mtoto anayekufa kwenye tetemeko hajafanya uamuzi wowote, hajachagua dhambi, wala hajamsingizia Shetani. Ameangukiwa na jengo na kufa. Sasa kama Mungu aliumba hiyo nature, anaijua kila itakachotokea, na ana uwezo wa yote, kwa nini ameruhusu mfumo wa asili ambao unazalisha mateso kama hayo?
Huko mwingine ngoja aje kukujibu mwenyewe.