Mama’ke Mama - Simulizi ya kusisimua kutoka katika ulimwengu wa giza

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,358
153,996

MAMA’KE MAMA - 1​

IMEANDIKWA NA : GEORGE IRON MOSENYA
********************************************************************************
Simulizi : Mama’ke Mama
Sehemu Ya Kwanza (1)

Laiti kama leo ingekuwa ni miaka ishirini iliyopita basi ningewekewa dau la dola milioni moja na kuambiwa nikifanikiwa kuandika simulizi yoyote ile basi zile dolali ni halali yangu basi kila mmoja angeweza kunicheka kwa sababu hakuna ambacho ningeweza kushinda. Bali ningekuwa upande wa kushindwa!!! Sikudhani kama ipo siku nitakuwa na simulizi ya kuandika hasahasa miaka ishirini iliyopita.....

Ama laiti kama asingekuwa mama yake mama, nd’o kabisaa nisingekuwa na simulizi ya kusisimua na yenye kuelimisha na kuonya kizazi mpaka kizazi.....

******
Angali nikiwa na miaka tisa, siku moja mama alikuwa mwenye furaha sana na alikuwa akitusimulia mambo kadha wa kadha kuhusu enzi zao, mengi yalikuwa ya kuchekesha sana kwa sababu laiti kama yangefanyika enzi hizi za utandawazi kingekuwa ni kituko. Alielezea ubaguzi wa vyakula jinsi wasichana walivyozuiwa kula mayai na mapaja ya kuku pamoja firigisi. Akaelezea pia juu ya utamaduni wa wanaume kuchaguliwa wanawake wa kuwaoa.
Hapa tulicheka sana, alitueleza kuwa zama zile hapakuwa na mambo ya kujichagulia mume..... kasha akanong’ona kuwa hata yeye alikutana na baba siku ya ndoa yao ya kimila tu....
Hakika ilifurahisha!!
Hatimaye akafikia suala la majina, alieleza kuwa kizazi cha sasa mzazi anajisikia tu jina lolote anamuita mtoto wake, lakini zamani mtoto angeweza kukaa mwezi mzima pasipo kuwa na jina rasmi hadi pale linapopatikana jina lililobeba maana kubwa ndani yake. Sio jina ilimradi jina unalojisikia kuita.
Mama akataja baadhi ya majina, yalikuwa magumu sana kutamka kila alivyotamka sisi tulikuwa tunacheka tu.
Baadaye mdogo wangu akamuuliza mama kuhusu sisi majina yetu, mama akamjibu kuwa kwa sababu tulizaliwa kijijini na sisi tulipewa majina yenye maana.
“Tena kama wewe Fred ulibadilishwa majina mara tatu.” akanigeukia mimi, hapo sasa mada ikageuka mdogo wangu, mpwa pamoja na dada yangu mkubwa wote wakataka kujua kuhusu mimi. Huu ulikuwa utaratibu wa utotoni ilimradi wapate tu cha kunitania kutokana na hiyo simulizi atakayotoa mama. Nilitamani mama asisimulie lakini nisingeweza kumzuia.
Mama akawatuliza kisha akasimulia kuwa jina langu la kwanza kabisa ambalo yeye na marehemu baba walinipa lilikuwa TABULO lakini baada ya kupewa jina lile nilianza kulia sana bila kukoma, wakadai kuwa huenda lile jina lina urithi mbaya, akaja babu kizaa baba na yeye akanibatiza jina jingine akaniita KIRENGE..... kuanzia siku nilipopewa jina lile kila usiku nilikuwa nashtuka na nikishashtuka silali tena, wakalazimika kunipeleka kwa mganga wa kienyeji baada ya siku sita za jina lile, mganga akashauri kuwa nibadilishwe jina lile jina halinifai hata kidogo na ni hatari sana kwa afya yangu, basi ikawa zamu ya mama kunichagulia jina akaniita Ngomeni, idhini hii alipewa na baba yangu!!
Jina lile likawa kama baraka likanituliza nikawa na amani tele na mwenye furaha.
Kilichobaki haikuwa simulizi kutoka kwa mama tena bali ni mimi nakusimulieni kilichojiri katika maisha yangu. Sina miaka tisa tena ni mtu mzima sasa....
Tafadhali makinika ili ujifunze.

Nilidumu na jina lile kwa mwaka mmoja kabla ya kupata ubatizo kanisani ambapo baba alinipa jina la ubatizo FREDI.
Naam! kwa sababu ubatizo ule niliupata wakati huo tukiwa tumehamia mjini tayari basi nikazoeleka kama FREDI na hatimaye lile jina NGOMENI ama kwa kifupi NGOME likapotea.
Nikaanza shule ya awali kwa majina FREDI Boniphace.
Mara moja moja sana mama yangu alikuwa akiniita jina NGOMENI na hapa ni pale anapokuwa anazungumza kikabila ama akiwa amekumbuka enzi hizo.
Basi ataniita na kunisemesha kikabila angali nilikuwa naambulia maneno machache tu.

Nikamaliza shule ya awali na hatimaye shule ya msingi nikijulikana kama Fred Boniphace.
Mdogo wangu pamoja na dada yangu wote wakalisahau lile jina Ngomeni, na walipokuwa wakiniita jina lile nilikuiwa napatwa na hasira sana kwa sababu niliona kama halifai jina lile hasahasa pale mjini.
Nilisoma hadi darasa la tano, upeo wangu darasani ulikuwa mkubwa kiasi kwamba mkuu wa shule akamshauri mama kama inawezekana anitafutie nafasi kidato cha kwanza nivushwe darasa.
Mama akafanyia kazi lile wazo na hatimaye siku moja akaja nyumbani na taarifa ya kufurahisha akanieleza kuwa amepata nafasi shule moja ya serikali kuna kijana aliyechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza lakini hajaweza kuripoti shuleni hivyo nafasi ile ipo wazi, hiyo pekee haikuwa habari ya kufurahisha lakini habari kubwa ni kwamba jina la kijana yule lilikuwa sawa na jina langu la ukoo. Yaani Ngomeni!!
Ni kweli jina lile lilikuwa linanichukiza lakini kwa sababu ilikuwa nafasi ya kwenda kidato cha kwanza bila kumaliza darasa la saba ilikuwa habari njema sana kwangu.
Ikawa habari na kisha ikahamia kwenye matendo, nikaingia kidato cha kwanza huku nikiitwa Ngomeni Paulo, jina lisilokuwa langu.
Nilikuwa na mwili mdogo sana kiasi kwamba kwa pale darasani nilionekana kwa kila aliyeingia kwa urahisi sana.
Mdogo na ninakaa nafasi za mbele.
Lakini ule udogo haukuwa upande wa akili, nilikuwa naelewa upesi na nilifanikiwa kuwashawishi waalimu upesi kunitazama kwa jicho la tatu.
Wanafunzi waliokuwa wakubwa kwa miili na umri. Kila nilipowazidi darasani, wqaalimu walkinitumia kama mfano ili kuwadhalilisha.
Mimi sikuwa najali sana kuhusu hayo... niliitazama elimu na kuipa kipaumbele.
Huku jina Ngomeni likiwa sio tatizo tena kwangu.

Amakweli wakati mwingine nyakati mbaya huanza kwa dalili kuwa nzuri sana.
Ulikuwa ni mwezi wa tano wakati tukiwa katika maandalizi ya mtihani wa kufunga shule kwa ajili ya likizo ndefu ya mwezi mmoja. Nilikuwa nimeupania sana mtihani na nilijiona kuwa nipo tayari hata kama wataleta mtihani mgumu kiasi gani.

Siku tatu kabla ya mtihani kuanza, niliamka asubuhi kama ilivyokuwa kawaida yangu kwa ajili ya kusoma na kujiandaa na shule, lakini siku hii niliamka shingo ikiwa inauma sana. Nikapuuzia na kuona ni hali ya kawaida kuwa huenda nimeilalia vibaya, nikajaribu kujinyoosha wakati ninanawa uso lakini hapakuwa na nafuu.
Shingo ikazidi kukakamaa huku maumivu yakizidi na ikinilazimu kuigeuzia upande wangu wa kulia ili kupunguza yale maumivu.
Hilo likawa kosa la jinai, nilipogeuzia upande ule ikawa shughuli pevu kuirudisha upande wa kushoto ili niweze kutazama mbele.

Wanafunzi wakubwa kiumbo na umri walikuwa wakinipenda sana kutokana na ule udogo wangu akili darasani na pia nilikuwa mpole hivyo nashukuru kuwa hawakuwahi kunionea.
Hata nilipokumbwa na hali ile na kuanza kuangua kilio walinijali haraka sana. Wakajaribu kunichua lakini hali ilikuwa tasa isiyozaa matunda. Hapo wakaamua kunipeleka kwa kiongozi wa bweni ambaye alichukua dhamana ya kunipeleka kwa mwalimu wa zamu.
Mwalimu akaniingiza katika orodha ya wanafunzi wagonjwa, nikapakiwa garini na kupelekwa nje ya shule ambapo palikuwa na zahanati iliyokuwa inatuhudumia.

Nilipewa kipaumbele cha kwanza kabisa, nilipokewa na wauguzi wakinibeba mgongoni kama mtoto wao wakanipeleka kwa daktari.
Daktari alinitazama na kunigonga gonga kisha akanichoma sindano na kunisihi nitulie kwa muda na nisiiilazimishe shingo yangu kugeuka.
Kweli baada ya takribani nusu saa shingo yangu ilirejea katika hali ya kawaida nikawa ninao uwezo wa kupeleka kushoto na kulia.
Baada ya wenzangu kuhudumiwa tukarejea shuleni.
Mwalimu wa zamu alinisihi nijipumzishe kwa siku hiyo kwa sababu ulikuwa utaratibu waliopewa na daktari.
Kweli nikapumzika huku mara kwa mara wanafunzi wenzangu wakifika kunitania na kunipa pole.
Siku ile ikapita na siku za kuufikia mtihani zikazidi kujongea, bado nilijihisi kuwa nipo tayari kuliko mwanafunzi yeyote yule katika kuukabili mtihani wangu huo mkubwa wa kwanza kwa shule ya sekondari.

Nakumbuka ulikuwa usiku wa jumapili, siku hiyo kabla haijawa usiku mvua ilinyesha kwa wastani wake na kuleta kiubaridi. Ilikuwa ni kama mvua ya kuukaribisha mtihani uliotakiwa kufanyika siku ya jumatatu.
Wanafunzi katika vitanda vyao walikesha wakikariri tayari kwa kujibu mtihani. Mimi nililala mapema sana, hadi pale nilipokuja kushtuka giza likiwa nene sana.
Lakini sikuwa katika hali ya kawaida.

Mwili wa mwanadamu ni wa ajabu sana jamani, usiombe ukajeruhiwa inaweza kuwa kitu kidogo tu lakini madhara yake mwili mzima ukauma.
Hii ilikuwa upande wangu, awali nilidhani ni muwasho wa kawaida tu nikaingiza kidole sikioni na kujikuna. Hilo likawa kosa, nilipofanya vile sasa kwa akili zangu kabisa nikasikia kitu ambacho kipo hai kikiwa ndani kabisa ya sikio langu kikitembea.
Nikajaribu kwa uoga kujikuna tena. Sasa kile kiumbe hai ndani ya sikio langu nacho kikawa kama kinapambana aidha kwenda ndani zaidi ama kutoka nje..........
Balaa likaanzia hapo, nikapiga mayowe nikiita jina la mama huku nikiwa nimelishika sikio langu.
Yule kiumbe hai naye akazidi kutapatapa, kila alipokuwa anatapatapa na mimi nazidi kupata maumivu!!

Awali nilidhani ni muwasho wa kawaida tu nikaingiza kidole sikioni na kujikuna. Hilo likawa kosa, nilipofanya vile sasa kwa akili zangu kabisa nikasikia kitu ambacho kipo hai kikiwa ndani kabisa ya sikio langu kikitembea.
Nikajaribu kwa uoga kujikuna tena. Sasa kile kiumbe hai ndani ya sikio langu nacho kikawa kama kinapambana aidha kwenda ndani zaidi ama kutoka nje. Ikawa kama tunapambana

Yule kiumbe hai naye akazidi kutapatapa, kila alipokuwa anatapatapa na mimi nazidi kupata maumivu makali sana ndani ya sikio!!!!

ENDELEA

Nilipiga mayowe makubwa sana kiasi kwamba bweni zima hakuna ambaye hakuamka na hapo upesi taarifa zikatolewa jenereta likawashwa mwanga ukapatikana, zikaanza harakati za kunituliza.
Haikuwa rahisi hata kidogo!!
Haikuwa rahisi kwa sababu ile karaha na maumivu nilikuwa napata mimi na si wao. Hivyo niliwazuia wasiutoe mkono wangu katika sikio langu kwani ile nd’o njia pekee niliyoona ni sahihi kabisa ya kupunguza maumivu yale.
Mwalimu wa zamu tayari alikuwa amefika eneo lile akiwa na waalimu wengine kadhaa waliokuwa wakiishi katika nyumba za waalimu pale shuleni, upesi waliwasiliana na dereva aliyekuwa na jukumu la kuendesha gari la shule. Lakini dereva hakupokea simu bila shaka alikuwa amelala hoi usiku ule ama la alikuwa yu mbali na simu yake.
Mwalimu wa zamu alivyoona hali inazidi kuwa mbaya alilazimika kuendesha gari yeye mwenyewe akaamuru wanafunzi kadhaa wenye ubavu zaidi yangu wanikamate kwa nguvu kabisa. Maana nilikuwa sina utulivu hata kidogo na kila jambo lililokuwa linafanywa kwa ajili yangu nililitazama katika namna ya kwamba sio jambo sahihi. Ajabu sikujua lipi linaweza kuwa sahihi kwa muda ule.
Walifanikiwa kunidhibiti japokuwa nakumbuka nilijaribu kutapatapa huku nikifanikiwa kumng’ata mmoja wapo mkononi.
Ndugu yangu unayesikiliza ama kuusoma mkasa huu, hali ile niliweza na ninaweza mimi tu kuisimulia na usiombe ikakukuta wewe. Nilihisi nanyanyaswa, nanyimwa haki zangu za msingi.
Nilifikishwa hospitalini kama mgonjwa wa akili anavyokuwa, nilifungwa kamba kikamilifu wakati napelekwa chumba cha daktari ambaye kama bahati tulimkuta usiku ule.... alishangazwa na hali ile nilimshuhudia alivyokuwa na hofu, sijui ni kutokana na muonekano wangu ama ni vile nilivyokuwa nimefungwa kamba.
Upesi wakamuelezea kama kilio changu kilivyokuwa kikijieleza.
Daktari akanifikia kisha akawaita vijana wawili wanafunzi wale waliofanikisha zoezi la mimi kufungwa kamba.. akawaambia wanigandamize kichwa ili aweze kunimulika sikioni atazame kunani.
Walinigandamiza kwa nguvu sana kiasi kwamba hata ningefanya nini nisingeweza kuwaponyoka. Ni mdomo tu uliobaki kupiga mayowe kuwa naumiaaa naumiaaaa! Lakini sikuweza kujitikisa sehemu nyingine tena.
Ndugu zanguni, nilijua wazi kuwa ile ingeweza kuwa siku yangu ya mwisho kuishi ulimwenguni kwa hali ile nilivyokuwa najisikia. Nilihisi kama kichwa kitapasuka muda wowote, niliamini hapatakuwa na lolote la kuiweka tena sawa hali yangu ile.
Nilimsikia daktari akiwaeleza kuwa haoni kitu chochote sikioni mwangu.
Alipoyasema hayo nilistaajabu kwa sababu nilikuwa nikisikia kabisa mdudu ananitembea ndani kabisa ya sikio.
“Daktari yumo mdudu yumo ananitembelea.. ananiumiza daktari naumiaaaa naumiaa” nilimweleza huku nikimkazia macho kumaanisha nilichokuwa nasema.
Daktari aliwaambia kuwa amenitazama kwa makini na hakuna kitu chochote kile.
Majibu yale ya daktari yalifanya niingiwe na hofu mpya!
Nilimsihi sana daktari kuwa mdudu yule anazidi kuniumiza.
Daktari akasema aniwekee dawa kama mdudu yumo basi atakufa lakini yeye hajaona kitu chochote kile. Na akasisitiza kuwa kifaa alichokitumia kimemuweza kuona ndani kabisa ya sikio.

Daktari alimwita nesi na kumuagiza dawa iliyokuwa katika mfumo wa kimiminika akawaita wale wanafunzi walioniinamisha na kunigandamiza tena, daktari akanimiminia matone kadhaa sikioni.
Mungu wangu weee! Bora asingeniwekea dawa ile maana nilikuwa kama niliyechokoza vita, sasa haikuwa mitambao ya kawaida bali muungurumo mkubwa iliyoambatana na mitikikisiko, nilipiga kelele sana hadi nikawa najisikia mimi mwenyewe tu. Sikusikia yeyote katika eneo lile.
Kama ile haitoshi mara nikasikia sauti nyingi sana zikiniita jina langu la shuleni ‘Ngomeni’ zilikuwa sauti za kike nikajiuliza wale manesi wamejuaje jina langu na mbona wananiita kwa sauti ya juu vile.
Nilizidi kupagawa nikigeuka huku na kule sasa hakuna aliyekuwa anajihangaisha na mimi katika kunishika pale kitandani ni kamba zilikuwa zinanidhibiti.
“Tunatoka tukitaka tunatoka na tutarudi tena tukitaka kurudi!!!” nilizisikia sauti zile zile za kike zikiniambia vile. Nikajiuliza hawa manesi wananiambia kitu gani hiki nisichokielewa asilani, na palepale nikajikuta nikiwa nakumbwa na nguvu za ajabu sana. Nikajikakamua na kisha nilivyofyatuka nikakatakata zile kamba nikatoka mbio sana nisijue mbele yupo nani. Nikajikuta namkumba mwalimu wangu wa zamu. Ilikuwa bahati mbaya sana kwake kwani alikumbana na kichwa changu katika mdomo wake. Nilianguka chini na yeye akaanguka chini lakini hakuishia kuanguka tu, aliacha meno mawili palepale.
Nilitulia kwa muda huku nikihema juu juu... sikupata kuisikia tena ile mitapotapo ya yule mdudu katikia sikio langu.
Sikio lilikuwa linauma tu lakini hapakuwa na mdudu.
Wanafunzi wenzangu walikuwa wananishangaa na ni kama walikuwa na hofu ya waziwazi juu ya kile kilichokuwa kimetokea.
Kitendo cha kijana mdogo kama mimi kukata kamba ngumu kama zile kiliwaacha midomo wazi.
Hata mimi nilipoziona kamba zile nilishangazwa mno, niliwezaje kuzikata kamba zile. Lakini lile halikuwa na nafasi ya kujadiliwa badala yake mwalimu alikuwa anapata tiba ya kwanza baada ya dhahama ile.
Tukio lile ukawa mwanzo wa kila kitu kisichopendeza katika maisha yangu.

Tulirejea shuleni majira ya mchana.
Nikapitwa na mitihani mitatu ya siku hiyo.
Mtihani wa hisabati, Kiswahili na historia.... mojawapo kati ya masomo niliyokuwa nayapenda sana. Sikuumizwa sana na kuikosa mitihani hii, nilibaki kushangazwa na kile kilichonisibu.
Lile tukio liligoma kufutika kichwani kwangu upesi, na kikuu kilichonisumbua ni sauti za wale manesi wengi walioniambia maneno yale kuwa watatoka wakitaka, na baada ya hapo kitendo cha kuzikata zile kamba pale kitandani, kamba ngumu kabisa ambazo hata uwe na nguvu kiasi gani inakuwa shughuli pevu kuzikata.
Eti mimi na kimwili changu hiki nikaweza kuzikata.
Wakati huo nilikuwa ninayo miaka kumi na mbili tu!!

Siku iliyofuata niliamka nikiwa mzima wa afya kabisa nikafanya mitihani yangu vyema hadi siku ya kumaliza. Lakini kutokana na kukosa kufanya mitihani ya awali nikajikuta nakuwa mwanafunzi wa sitini kati ya wanafunzi mia moja.
Niliumia sana kutokana na matokeo yale mpenzi msikilizaji na wewe unayeusoma mkasa huu.
Waalimu walinifariji sana na kuniambia kuwa laiti kama ningefanya masomo yale ningekuwa wa kwanza lakini haikuniingia akilini kabisa. Utoto ulikuwa bado pamoja nami...
Naam! Shule ikafungwa, sasa sikuwaza tena juu ya mdudu sikioni mwangu badala yake nilifikiria juu ya kuangukia nafasi mbaya kabisa darasani.

_____________________

Kitendo cha kukuta sijajaziwa masomo matatu kikamfanya mama anihoji ni kwanini sikufanya mitihani yangu, nilimweleza kuwa sikufanya mitihani ya masomo matatu, mama alistaajabu sana na hakulilazia jambo lile damu. Kumbe kimya kimya bila kunieleza alienda shuleni kuulizia kuwa ilikuwaje nikakosa kufanya masomo yale. Uzuri wakati anauliza alikuwepo yule mwalimu wa zamu, akamuelezea kila kilichojiri.
Mama aliporejea nyumbani aliniuliza ni nini kilitokea nikamueleza kuanzia habari ya shingo kugoma kugeuka na kisha mdudu katika sikio langu!!!
Mama alishangaa sana ni kama kuna kitu alitaka kusema lakini akashindwa kusema kwa sababu alizokuwa akizijua yeye mwenyewe.
“Mama yule mdudu sikioni alikuwa anaongea!!” nilimwambia mama baada ya kimya cha muda. Mama alitabasamu kisha akanichukua na kunikumbatia.
Nikiwa nayasimulia haya na utu uzima huu hata mimi mtoto wa miaka kumi na mbili akinieleza jambo la kustaajabisha kama lile ni vigumu sana kumuamini zaidi nitahisi ni akili za kitoto.
Bila shaka hata mama yangu alihisi kuwa zile ni akili za kitoto tu!! Mdudu anaanzaje kuongea katika sikio langu!

Mzaha mzaha jipu hutunga usaha!

Mama naye hakutilia maanani hata kidogo. Hili yawezekana lilikuwa mojawapo ya kosa lililokomaza tatizo.

Nilipokuwa nyumbani kipindi cha ile likizo nikiwa nasoma masomo ya ziada hakuna kilichokuwa kinaenda vibaya kila kitu kilienda sawa sawia.
Hatimaye nikasahau yale yote kuhusiana na mdudu aliyeongea katika sikio langu. Nikajiwekea dhana yawezekana nilikuwa naota angali nimefumbua macho.
Siku zikahesabika na hatimaye tukafungua tena shule.
Niliendelea kufanya vizuri hatimaye hata wanafunzi na waalimu wakasahau juu ya yule mdudu na kama kunikumbushia walifanya kama utani tu. Nikacheka na wao wakacheka, maisha ya shule yakaendelea.
Kama kawaida ya shule kipimo cha mwanafunzi ni mitihani.
Ikafikia tena wakati wa mitihani, hapo ikiwa imebaki kama siku siku nane kabla ya kufanya mtihani. Hii ya sasa ilikuwa ile ya kumaliza mwaka wa masomo.
Nilikuwa si mtu wa michezo sana kwa sababu nilikuwa naogopa sana kuteguka, hivyo kwenye michezo mimi nilikuwa mtu wa kushuhudia tu wenzangu. Hofu yangu kuu ilikuwa kuumia mkono na kisha kushindwa kuandika vyema.
Safari hii sikuwa tayari litokee jambo lolote lile la kunizuia kufanya mitihani yangu vizuri.
Lakini waneni wanasema kuna mambo hayakwepeki na hata ukijaribu kuyakwepa kumbe wajipeleka kwenye njia yao mbadala.

Siku moja nilichelewa kuamka, haikuwa kawaida yangu na hata hii niliihesabu kama ajali tu.
Kuchelewa huku kuamka nikachelewa kuhesabu namba, wachache walioenda shuleni hata wewe hapo msikilizaji najua wajua kero za kuhesabu namba!
Basi siku hiyo sikuhesabu namba, na sikuwaza sana kwa sababu nilijua kuwa kwa sababu ni kawaida yangu kuhesabu namba kila siku basi siku hiyo hata nikiomba msamaha mwepesi tunaweza kusamehewa.
Kumbe siku hiyo watu wengi sana walipuuzia hawakuhesabu namba!
Jambo hili likawa kero kubwa sana kwa mwalimu wa zamu, ule muda wa kuwa mstarini akaagiza wote waliohesabu namba wapite mbele.
Hapo sasa mapigo ya moyo yakaongeza kasi yake nikiamini kuwa na kile kiubaridi cha asubuhi nikichapwa bakora nitaumia sana. Nikafikiria cha kujitetea.
Kweli wakatoka mbele wakahakiki namba zao na kisha wakaruhusiwa kwenda darasani.
Wengi tuliosalia tukaambiwa tupige magoti chini, mwalimu akawaomba waalimu wenzake wamsaidie kutuchapa bakora tatu tatu kila mmoja. Wanawaume tuchapwe makalio na wasichana wachapwe mikono.
Kweli waalimu wakaanza kutushambulia, nilikuwa naogopa kila mwalimu naona anachapa kwa nguvu sana.
“Ngomeniii!” hatimaye nilisikia sauti ya mwalimu ikiniita, alikuwa mwanamke na ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona bila shaka alikuwa mgeni.
Sikujiuliza sana amelijua vipi jina langu kwa sababu ule umri wangu mdogo ulikuwa umaarufu tosha achana na uchapakazi wangu lilipokuja suala la masomo.
Nilinyanyuka kinyonge kwenda kwa yule mwalimu.
“Kwanini haujahesabu namba leo” aliniuliza kiupole sana huku akinishika shika mashavu yangu.
Katika umri ule sikujiuliza juu ya kauli yake lakini katika umri huu najiuliza aliposema sikuhesabu namba leo anamaanisha siku zilizopita alijuaje kama nilikuwa nahesabu namba wakati mimi namuona ni mgeni kabisa kwangu?

“Madam... leo nimepitiwa tu nisamehe!!” nikamjibu kinyonge katika hali ya kumshawishi asinichape.
“Kukusamehe kwangu nakuchapa kamoja tu sikuchapi tatu.. ili kesho ukumbuke kuamka mapema na ninakuchapa mkononi....haya tega mkono.” akaniambia huku akiiandaa fimbo yake ndogo.
Niliiona ahueni kuadhibiwa na mwalimu huyu, tena kiboko kimoja.. nikautega mkono wangu wa kulia ili anichape.
Ndugu zanguni mnaofuatilia mkasa huu, Yule mwanamke hata hakuunyanyua mkono wake juu sana, hilo likanipa ujasiri sana. Nikaamini hakuwa na nia ya kuniadhibu bali alifanya geresha kasha aniache.
Akaishusha fimbo yake, ni kama nilivyodhania awali kuwa sitapata maumivu sana.
Ilikuwa hivyo sikuumia sana, akaniruhusu niende darasani.
Nikakimbia upesi kuelekea darasani.
Nilipofika darasani nikachukua siti yangu na kufungua madaftari kwa ajili ya kuanza siku hiyo.... punde akaingia mwanafunzi mwingine ambaye naye hakuhesabu namba moja kwa moja akanifuata huku akicheka.
“Dogo mjanja wewe umetimua mbio haujachapawa daah! halafu kidogo ticha Haule akuone ungekoma leo.....” alinieleza yule mwanafunzi huku akionyesha uhakika kabisa machoni pake.
Nilimweleza kuwa nimechapwa akakataa katakata nikanyoosha mkono wangu ili aone kuwa ni kweli nimechapwa.
Mama yangu!! Mkono wangu ulikuwa umevimba na kuna mchirizi wa damu iliyovilia ilionekana ndani kwa ndani.
Sio mimi tu niliyeshtuka hata yule mwanafunzi alishtuka, kushtuka kwake kukawashtua na watu wengine, watu waliponizunguka kwa akili ya utoto nikaona lililonikuta ni balaa nikaanza kulia. Wakanipooza.
Sasa yakaanza maumivu kunitambaa.
Nikajaribu kuyazoea lakini haikuwezekana, nilipojaribu kushika kalamu sikuweza kabisa, mkono ulikuwa unauma sana.
Mwalimu wa hisabati alipoingia darasani na kuanza kuandika ubaoni mimi sikuweza kabisa kuandika, alipogeuka nilinyoosha mkono akanifuata, nikamweleza mkono unaniuma sana siwezi kuandika.
“Wewe Ngomeni wewe mbona unakuwa kahuni wakati bado kadogo, si ulitoroka wewe hata haujachapwa nikakuona nikajikausha tu.. sasa nini kinakuuma tena.....” mwalimu alisema huku akicheka na kusababisha darasa liangue kicheko.
Kasoro mimi tu ambaye kwa macho yangu nilishuhudia nikichapwa. Nilichapwa na mwalimu mgeni tena ni mwanamke na alinichapa mkononi.
Nikamkatalia mwalimu na kumweleza kuwa kuna mwalimu mgeni alinichapa ila alinichapa bakora moja tu mkononi.
“Ona sasa huyu naye, waalimu wote hakuna hata mmoja aliyemchapa mtoto wa kiume mkononi we Ngomeni wewe uongo sio mzuri sawa mwanangu!! Kwanza hakuna mwalimu mgeni hapa shulenikwetu” alinieleza kiupole. Akionekana kabisa kuwa katika kunisihi.
“Mwalimu nimechapwa na madam mgeni, mimi sio muongo hata kidogo...naapa mwalimu” nilimkatalia.
“Haya baada ya kipindi utanifuata ofisini!!” alinieleza kisha akaendelea kufundisha.

ITAENDELEA

Simulizi : Mama’ke Mama

Sehemu Ya Pili (2)

Baada ya kipindi nikaondoka naye nikimbebea boksi la chaki.

Tulifika hadi ofisi ya waalimu akanisimamisha katikati.

“Huyu mtoto ameshindwa kuandika leo darasani anadai kuna mwalimu wa kike amemchapa kiboko kimoja sasa mkono umevilia damu na unamuuma sana... haya Ngomeni ni mwalimu gani kati yetu hapa....nikigundua unanidanganya nitakupa adhabu kali sana. Sitaki kabisa watotyo kuwa waongo” Mwalimu wa hisabati alizungumza na kunitupia mpira.

Niliangaza huku na kule kama nitamuona yule mwalimu lakini ajabu sikumuona wala kumfananisha kati ya wale waliokuwa pale.

“Ni mwalimu mgeni kabisa, aliniita akanichapa kiboko kimoja!!” nilizungumza huku nikishangaa.

“Ngomeni mwanangu, hapa hatunaye mwalimu mgeni hata mmoja mbona. Hebu sema ukweli huo mkono umeufanya nini... sema kama uliruka sarakasi ukastuka au umejichoma na mwiba....” alizidi kunisihi.

Nikajikuta nalia nikishindwa kuongea kabisa, mwalimu mmoja wa kike akafika na kunikumbatia begani... akauchukua mkono wangu na kuutazama.

“Jamani waalimu hii ni fimbo aliyochapwa huyu mtoto wala sio mwimba au mkono kuteguka hebu njooni muone... aliwaita ambao walikuwa hawajaniona akawaonyesha na wao wakakiri kweli ni fimbo.

“Sasa kama hayupo aliyemchapa hii bakora ina maana amechapwa na shetani au?” Mwalimu mmoja wa kiume alihoji huku akiwa katika mshangao.

Maumivu ya mkono nayo yalizidi kunisumbua. Mwalimu mmoja akaingia katika ofisi nyingine na kuchukua dawa ya kuchukua akanichua, lakini sikuipata nafuu yoyote.

Mkono ulikuwa unauma, maumivu ya mkono yakaanza kusambaa hadi kichwani, kichwa kikaanza kuuma sana, na hatimaye yakawa maumivu ya mwili mzima.....

Ikawa ni homa!!!

Siku zikazidi kwenda mbele, siwezi kuandika na mwili unauma, hadi ikafikia siku ya kufanya mtihani nikaishia kuuona hivihivi mtihani. Mkono haushiki kalamu kabisa kama ni hospitali walikuwa wamenipeleka lakini hakuna kilichosaidia kabisa.

Mitihani mitatu ya kwanza ikapita.... mitihani ya siku ya pili ikapita nikiwa mtu wa kulala tu na kulia.

Siku ya tatu na ya mwisho ya kufanya mitihani nikaamka nikiwa ninayo alama ya damu kuvilia lakini mkono wangu ukiwa na nguvu sana na imara!

Niliweza kushika kalamu na kufanya lolote lile ambalo nilikuwa siwezi kufanya siku za nyuma.

Nikafanya mitihani ya siku hiyo!!

Mwalimu mkuu msaidizi ambaye alikuwa mwanamke baada ya hali yangu kuwa njema aliniita na kuniambia kuwa napewa ruhusa ya kurejea nyumbani na huko niende nikamueleze mama yangu kila kitu juu ya kila kilichonitokea shuleni.

Hakuongeza neno katika kauli zake badala yake alinisihi sana nisimfiche kitu chochote kile!!

Sikuelewa kwanini alinisisitiza sana juu ya kumweleza mama kila kitu.

Huu ukawa mwanzo wa kumchanganya mama yangu mzazi!!

Lakini ningefanya nini kwa sababu ilibidi tu nifanye hivyo!!

Hakuongeza neno katika kauli zake badala yake alinisihi sabna nisimfiche kitu chochote kile!!

Mwalimu alinipatia wanafunzi wawili waliokuwa kidato kimoja juu yangu na hata kiumri walikuwa wakinizidi mbali. Hawa walipewa jukumu la kunifikisha nyumbani salama. Utaratibu huu wa mwanafunzi kusindikizwa nyumbani ulikuwa ni utaratibu maalumu kabisa pale shuleni pindi mwanafunzi mmoja anapokuwa katika matatizo.

Kweli walinifikisha nyumbani na kunikabidhi kwa mama yangu mzazi niliyemkuta akiwa anafua nguo!

Mama alistaajabu kuniona nyumbani wakati ule lakini wale vijana walizungumza naye na kumtoa hofu, kisha wakaaga na kuondoka.

Kitu cha kwanza mama aliniuliza nini kimetokea na mimi kama nilivyoelezwa na yule mwalimu mkuu msaidizi. Nikalazimika kuelezea kwa tuo.

Ujue akili ya utoto safi sana ulichoagizwa unakieleza kama kilivyo, nikamueleza mama kuanzia kuchelewa namba. Kuchapwa na mwalimu hadi mauzauza yote ya mkononi yaliyojitokeza.

Tofauti na awali nilipomueleza mama juu ya kuingiwa na mdudu sikioni, siku hii mama alitilia maanani zaidi.

Na kile kitendo cha kuagizwa kumueleza kila kilichonitokea kilileta uzito zaidi.

Mama akaniambia nipumzike kwanza ndani tutazungumza baadaye, lakini nikiwa na akili zangu nilipatwa hofu kwa mambo yaliyoendelea, mama aliacha kufua ghafla. Na hakuwa na utulivu kabisa. Namjua vyema mama yangu, akiwa sawa najua akivurugwa najua vyema.

Nikiwa naingia ndani akaniita tena.

“Umesema huyo mwalimu aliyekuchapa alikuwa amevaaje?” aliniuliza huku akionekana kutetemeka waziwazi.

“Alikuwa amevaa sketi nyekundu na blauzi kama nyeupe hivi na kichwani ana nywele fupi tu......” nilimjibu.

“Je viatu unaweza kuvikumbuka......” mama akaniuliza.

Hapo sasa mapigo yangu ya moyo yakapiga maradufu, kuna kitu nilikiona na kukipuuzia na kisha akili yangu ikasahau. Hata nilipokuwa nawasimulia waalimu juu ya kilichojiri sikukumbuka kipande kile.

Mwalimu yule alikuwa peku!

“Ngomeni... we Ngomeni,... niambie alikuwa amevaaje miguuni!!” mama alikazia baada ya kuona nimeshtushwa na hata nisiseme lolote.

Nilimjibu kuwa yule mwalimu hakuwa na viatu miguuni.

Hapo sasa mama akaifungua kanga yake na kujifunga upya kiunoni. Nilimsikia akilalamika kikabila sikuambulia maana ya maneno aliyokuwa anasema lakini nilijua analalamika. Hapo awali nilikueleza kuwa nilizaliwa mjini hivyo sikuwa naelewa sana kabila langu.

Nakusihi nawe unayenisikiliza jitahidi kujua walau kwa asilimia hamsini tu juu ya kabila lako. Ipo siku utaujua umuhimu wa kulijua kabila lako.

Aliondoka bila kuniaga sikujua alipoenda, na hakurejea siku hiyo hadi aliporudi siku iliyofuata na taarifa kuwa baba yetu mzazi alikufa akiwa safarini huko Dodoma amekutwa ametupwa mtaroni. Hana jeraha lolote lile.

Ilikuwa taarifa nzito sana hakika, ikabidi msiba ukae pale nyumbani.

Kuna baadhi ya ndugu walikuwa wanaishi Dodoma wakashauri baba azikwe huko. Hali ya uchumi haikuwa nzuri sana nyumbani ikalazimika mama na kaka yangu waende msibani mimi na mdogo wangu tukabaki pamoja na mama yetu mdogo.

Japokuwa nilikuwa mdogo nilikuwa naielewa vyema maana ya msiba.

Niliumia sana.

Ni kweli baba yetu hakuwa mtu anayeijali sana familia yake. Lakini hii haibadili hata nukta ya yeye kuwa baba pekee wa familia ile kwa uhalali.

Baada ya siku takribani kumi mama alirejea nyumbani akiwa amenyoa nywele zake ishara ya ujane. Alikuwa yu mpole sana na hapo mi nikiwa najiuliza mama alikuwa ana maana gani kuniulizia juu ya yule mwalimu, ina maana alikuwa amewahi kumuona ama?

Mama alituita familia nzima kwa ujumla na kutuelezea kuwa kifo cha baba yetu ni mipango ya Mungu tu na tusimsikilize na kumuamini mtu atakayetwambia vinginevyo. Alijaribu kurejea vifungu kadhaa vya maandiko matakatifu kwa ajili ya kutuimarisha katika imani.

Neno la mama likawa neno lililoaminika zaidi.

Mama amesema!!

Na baada ya hapo akatupatia picha kadhaa walizopigwa huko Dodoma msibani ikiwa ni pamoja na santuli (CD) ya siku ya maziko.

Tulizitazama zile picha zote kwa utulivu, picha zilizoleta msiba upya pale nyumbani. Kuwaona akina mama wadogo, shangazi na wengineo wakiweka shada za maua juu ya kaburi alilozikwa baba. Ilitonesha sana.

Hapakuwa na namna ya kubadilisha maana ya kile kilichotokea!

Mama naye alituruhusu tulie kwa uchungu ili kuzipa ahueni nafsi zetu.

Nakumbuka siku kama nne baada ya mama kurejea nikiwa na mdogo wangu sebuleni niliikumbuka CD aliyokuja nayo mama, nikaiweka katika deki tukaanza kuitazama mimi na mdogo wangu, haikutuumiza sana kuona jeneza lililombeba baba ujue utoto nawe ushawahi kuwa mtoto nadhani unaelewa!! Tulishalia mara moja siku ya kuziona picha. Sasa hatukulia tena.

Wakati tukiendelea kutazama ile CD mara ukafika wakati wa kuaga mwili wa marehemu.

Ni hapo ambapo nilikutana na kisanga cha kutisha.

Alianza mdogo wangu tukawa tunashindana kumtafuta mama atakayekuwa wa kwanza kumuona anamfinya mwenzake, hivyo kila mmoja alikuwa makini kutazama katika luninga. Naukumbuka utoto kuna muda nautamani tena. Lakini kamwe hautarudi!

Nikiwa makini kabisa kuwatazama watu wanaoaga mara ghafla macho yangu yakakutana na mtu niliyewahi kumuona hapo awali, alikuwa amevaa nguo zilezile juu hadi chini.

Alikuwa katika msafara wa watu wanaoenda kuaga mwili wa marehemu baba yangu.

Alikuwa ni nani yule? Nilijiuliza hata nisipate jibu upesi.

Shangazi? Hapana

Ma’mdogo Samira? Hapana.

Ma’mkubwa Suzy? Siye?

Paaah! Moyo ukapiga kwa nguvu sana. Nilikuwa nimemkumbuka.

Alikuwa ni mwalimu aliyenichapa siku ile na kunizulia balaa katika mkono wangu.

Balaa lililosababisha nikashindwa kufanya mitiahani yangu. Sasa nipo nyumbani.

Nilijikuta napiga kelele kubwa sana za hofu, kelele zilizomfikia mama chumbani nikamsikia akituonya kuwa tukacheze nje lakini mimi niliendelea kupiga mayowe.

Hatimaye mama alikuja akiwa mwenye hasira, alipokuja nilimkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu, hapo sasa ghadhabu zikamwisha akaingia katika uoga akiniuliza nimekumbwa na nini.

Nikamweleza mama kuwa nimemuona yule mwalimu akiwa anaenda kuaga mwili wa baba....

Mama alikataa katakata, nikamsisitiza kuwa nimemuona katika ile CD aliyoileta.

Mama akaketi pamoja na mimi kuitazama ile CD kwa umakini ili na yeye awe shuhuda wa kile nilichokuwa nakisema.

Ndugu msikilizaji kama hujawahi kukutana na maluweluwe basi omba sana yasije yakakosea njia yakakutana na wewe.

Ninachokusimulia ndicho kilichojiri.

CD ilionyesha vizuri kabisa kuanzia mwanzo, ajabu sasa ilipofikia sehemu ya kuaga ilisikika sauti tu hakuna picha iliyoonekana hadi watu wanamaliza kuaga.

Mama akaanza kutokwa jasho!!

“Mwanangu huyo mwalimu ndiye aliyemuua baba yenu. Ni huyooo” mama aliniambia huku akiwa anatetemeka sana. Kauli ya mama iliniacha hoi lakini mama akatulia na kunisimulia,

Alinieleza kuwa baba akiwa Dodoma alimpigia simu na kumueleza kuwa amekaa siti moja na dada mmoja ananukia marashi makali ambayo yamemsababisha kichwa kimuume sana. Akaelezea muonekano wa huyo dada na muonekano huo ni sawa kabisa na muonekano wa mwalimu wa maajabu aliyenichapa na kuniletea hitilafu kubwa katika mwili wangu.

Mama akakamilisha simulizi yake kwa kunieleza kuwa mwanadada huyo hakuwa na viatu miguuni, sasa inakuwaje wafanane kila kitu?

Bila shaka huyu ni mtu mmoja......

Anataka nini sasa katika familia yetu??

Hili lilikuwa swali la muhimu sana mbalo jibu lake halikuwa hadharani!!!

Mama akaniambia kuwa yatupasa tusafiri hadi kijijini tukamueleze babu yangu ambaye ni baba yake marehemu baba juu ya huu utata. Kwa sababu yeye ni mtu mzima basi anaweza kujua ni kitu gani cha kutushauri ama kutusaidia!!!

Ndugu msikilizaji ile ikawa mwanzo wa safari yangu ya misukosuko isiyokuwa na ahueni hata kidogo!!!

Siku iliyofuata alfajiri kabisa mama aliniamsha akaniandalia nguo za kuvaa na kisha safari ikafuatia.

Tulianza kutembea kwa miguu kwa mwendo kama wa dakika tano tukaifikia barabara. Tukasubiri gari kwa takribani nusu saa. Gari lilifika likiwa limejaa, mama akashauri tupande hivyohivyo, tukapanda na kujiunga na abiria wengine waliokuwa katika mbanano ule.

Njia ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba nilikuwa namuonea huruma mama kila gari lilipokuwa linayumba alienda huku na kule hadi jasho likawa linamtoka.

Ndugu zanguni, sitaki kusema kuwa baba zetu hawana upendo kwetu lakini acha akinamama wapewe heshima yao kwa upana wa hali ya juu. Wanafanya mambo mengi sana kwa ajili yetu sisi watoto wao. Wanafanya hata ambayo hayajawahi kuwa katika ndoto zao.

Mama alikuwa anafanya yote haya kwa ajili yangu!

Ilikuwa safari ya masaa matano hadi kufikia kijijini, mama alikuwa yu hoi sana.

Tuliposhuka ilikuwa yapata saa sita za mchana, jua lilikuwa kali sana mama akaniuliza iwapo nilikuwa na njaa. Kweli nilikuwa nina njaa kali lakini nilisema kuwa sina njaa.

“We Ngomeni kuna kamwendo kwenda kwa babu yako, kama una njaa ni heri useme ule kabisa....” alinisihi mama yangu.

Nikakataa kwa mara nyingine. Safari ikaanza tena, mama alikuwa amechoka sana lakini hakutaka nijue, jasho lilikuwa linamtoka kwa wingi na nilimsikia akihema juu juu. Lakini hakunyanyua kinywa chake kulalamika kuwa amechoka.

Mungu wabariki akinamama hawa!

Wakati ule sikuwa na chuki kali juu ya wanadamu lakini ninapoyasimulia haya nikimkumbuka na mama yangu nawachukia sana wanadamu wa dunia ya giza, dunia ya kujifanya wao ni miungu watu!!

Tuliendelea kutembea hadi tulipouona mji wa babu, mama akanieleza kuwa hatimaye tumekaribia kufika.

Tulipiga hatua kama kumi hivi mama akalalamika kuwa kuna kimwiba kimemchoma, nakumbuka alisema kimwiba akimaanisha kidogo tu!

Akainama aweze kukitoa, alijaribu akiwa ameinama ikawa ngumu. Akasema ngoja atembee mbele zaidi akifika kwa babu atakitoa hicho kimwiba. Mimi nikawa mtazamaji tu na zaidi nikimpa pole.

Lakini hakuweza kupiga hata hatua tano, akadai anajisikia uchungu sana ngoja tu akae aweze kukitoa kile kimwiba ili aweze kuwa sawa. Mama akaketi, akatoa pini katika pindo la nguo yake, akaanza kujichokonoa ili aweze kujitoa hicho kimwiba.

“Ngomeni ujue nilisikia ni kimwiba kidogo ila naumia kweli, halafu naona weusi tu nakitoa hakitoki!!” mama alilalamika huku akitabasamu kumaanisha kuwa hata yeye anaona tukio lile kama ni mzaha tu.

Ikawa dakika mbili lakini hadi zinafika kumi mama hakuwa amefanikiwa kukitoa kimwiba kile.

“Ngomeni, kabla sijalalalmika huu mwiba hamna kitu chochote umesikia?” aliniuliza, sasa alikuwa ameacha kujishughulisha tena kuutoa ule mwiba. Na uso wake haukuwa na tabasamu tena.

Jasho lilikuwa likimtiririka mama yangu.

Nilifikiria kwa muda kidogo sikupata muafaka kabisa wa kitu gani cha tofauti nilikuwa nimekisikia.

“Hebu fikiria, fikiria kitu gani umekisikia mwanangu, huu sio mwiba hata sio mwiba huu... nakataa hakuna mwiba hapa mwanangu.” alisema mama, sasa hofu ilikuwa wazi katika macho yake.

Mama aliponisihi kuwa mtulivu nikatulia kweli na hapo nikakiri kweli kuna kitu cha tofauti nilikuwa nimekihisi.

“Mama nilisikia jotooo!!” nilimwambia.

Mama akapiga mayowe makubwa sana kabla hajanieleza kuwa kuna mtu anawaroga na anataka kuiangamiza familia yetu wote. Na lile joto nililohisi sio bahati mbaya, bali nilikuwa nimepishana na mchawi.

Nilikuwa mdogo lakini kuhusu wachawi nilikuwa nafahamu fika, haya mambo ya kishirikina hata shuleni tulikuwa tukihadithiana na kuna nyakati yalikuwa yakiwatokea baadhi ya wanafunzi.

Sasa nilikuwa nashuhudia kwangu.

“Ngomeni kimbia nenda kwa babu yako, nyumba ilee yenye bati ulizia mzee Uwele, mwambie upesi aje hapa siwezi kusimama Ngomeni mguu unawaka moto. Kimbia mwanangu kimbia na njia nzima mwambie Mungu awe na sisi mwambie Mungu hatutaki kufa kwa dhamira ya mwanadamu...mkatalie kabisa Mungu mwambie hatutakufa kwa hila zao.” mama alinisihi. Nikakimbia sana huku nikikumbuka kusema kama alivyonisihi. Nilimwambia Mungu awe na sisi.

Nilifika katika ile nyumba na kuulizia kwa mzee Uwele, aliyenipokea akanieleza ni kijiji cha mbele nikimbie kuelekea mbele zaidi nitakutana na nyumba nyingine ya bati.

Kwa sababu ya kupagawa niligeuka na kutaka kukimbia kama alivyioniagiza, lakini mara nikajisikia mwili wangu wote ukisisimka vibaya mno. Kuna kitu akili yangu ilikuwa imekitambua, nikajaribu kukimbia mwili ukawa mzito na hapo nikaamua kugeuka kama mwili ulivyotaka.

Naam! Ilikuwa kama akili yangu ilivyohisi, yule aliyenielekeza hakuwepo tena eneo lile, na nina uhakika kwa sababu nilimuona hapo awali na kumsikia.

Nikamkumbuka!

Aliyenipokea na kunielekeza ni yule mwalimu aliyenichapa kiboko mkono ukalemaa kwa juma zima, ni yule mwanamke ambaye baba alisema kuwa walikaa naye garini na hatimaye akapoteza maisha na ni yuleyule niliyemuona akiwa katika msafara wa kuaga mwili wa baba.

Hatimaye nakutana naye tena huku kijijini!!

Nilibaki nikiwa nimesimama wima nisijue ni kitu gani cha kufanya. Nikiwa nimesimama vilevile damu ikinichemka sana, akatoka ndani mtoto wa kike, akaniuliza ninatafuta nini pale. Huyu ndiye aliyenirejesha katika ulimwengu wa kawaida tena, nikamuulizia mzee Uwele akaniambia yupo ndani amelala.

Nikamueleza kuwa mimi naitwa Ngomeni na nimetumwa na mama upesi sana, yule mtoto akaendelea kuniuliza maswali mengimengi nikaona ananipotezea muda nikaita kwa sauti ya juu. Babuuuuuu!

Babu akatoka nje, kumbe hata hakuwa amelala. Aliponiona tu akanitambua japokuwa sio kwa jina lakini alijua tayari damu iliyopo pale inamuhusu.

Akaniuliza mimi ni nani nikajieleza.

Na sikusubiri aulize nini kilichonipeleka hapo ama nimefika na nani.

Nikajieleza kila kitu kuhusu mama upesiupesi.

Mimi nilikuwa bado kijana na ningeweza kukimbia zaidi ya babu lakini ajabu babu alitoka mbio kali, akielekea huko nilipomuelekeza mama.

Alifika na mimi nikafika.

Mama yangu alikuwa sio mweupe sana lakini ungeweza kumuita mweupe katika kundi la weusi, basi ilikuwa ni kazi rahisi sana kuuona mguu wake jinsi ulivyokuwa mwekundu!!

Mama alikuwa anatokwa jasho na alikuwa ameuma meno yake sana kumaanisha kuwa alikuwa anaumia. Babu alipiga mayowe kwa nguvu sana, alikuwa amepagawa pia, kelele zake ziliwavuta wanakijiji.

Acha bwana! Kijijini kuna ushirikiano mjini unafiki ndo umetanda. Watu hawakulazimishwa walifika eneo lile kumshuhudia mama, wakambeba mama yangu huku akilia kilio na machozi na kamasi vyote vikimtoka kama mtoto mdogo.

Ukimuona mtu mzima katika hali hii tambua kuwa anaumia sana.

Kilio cha mama kikanifanya na mimi niungane naye katika kulia, nililia sana kwa sababu licha ya utoto nilitambua kuwa kuna jambo lisilokuwa la kawaida lilikuwa linatokea kwa mama yangu.

Mama alipelekwa kwa bibi mmoja ambaye alikuwa hajiwezi hata kusimama bila kutumia mkongojo wake, bibi yule alimminyaminya mama mguu wake kisha akautazama na kuanza kuongea kikabila.

Sijui hata alichokuwa anasema ila ni babu alikuja kunieleza katika siku za usoni kuwamama alikuwa amewekewa tego la kuua!

Na kama isingekuwa kuwahishwa kwa yule bibi ilitakiwa afie palepale akiwa ameketi chini.

Tiba iliendelea kwa masaa mengine manne zaidi hali ya mama ilikuwa mbaya, hatimaye yule bibi naye akasalimu amri akasema alipofanya ndio mwisho wa utaalamu wake.

Mama akabebwa na kupelekwa kwa mtaalamu mwingine, kila muda mama alikuwa akiniita na kuninong’oneza kuwa nimuombe sana Mungu amwokoe kwani anajiona hana namna yoyote ile ya kuiona kesho.

Mara nyingine aliniita na kunieleza kuwa nisome sana kwa bidii pia niikusanye familia yangu iendelee kuwa moja siku zote.

Maneno haya ya mama niliyafananisha maneno ya kwenye filamu pindi muhusika anayeigiza kuumwa anapokaribia kukata roho.

Nililia sana hakika kwa sababu niliiona waziwazi hali ya hatari.

Tulipofika kwa mtaalamu wa pili, huyu alimchanja mama ili amuwekee dawa.

Ajabu damu ya kijani ikamtoka mama, mtaalamu yule akaruka kando na kuongea lugha zisizoeleweka na hapo akataja kitu kama skadi ama vinginevyo, ila nakumbuka alisema skadi!!

Hakuendelea tena kumwekea mama dawa.

Badala yake aliuliza ikiwa katika umati ule yupo mtoto wa mgonjwa, babu akanishika mkono na kumwonyesha yule bwana tabibu wa kijijini katika sekta ya tiba asilia.

Yule tabibu akaniita na kwenda kusimama nami kando, akaniuliza swali moja huku akitetemeka.

“Unamuamini Mungu! nikakiri kuwa ninamuamini.

“Wewe ni mtoto mdogo, wewe ni sawa na malaika tu japokuwa sio katika kiwango cha mtoto mchanga..... sogea pembeni pale kaa kimya mwambie Mungu hautaki mama yako afe katika namna hii ya mkono wa mtu... mwambie Mungu hautaki kuwa yatima. Nenda sasa!!” akanisogeza kando.

Ndugu zanguni, hii sio simulizi ya dhahania. Yalinitokea haya......

Nikafanya kama alivyoniagiza nikafumba macho, nikasema maneno yale kama mara nne hivi...... wakati nasema maneno yale nikasikia zile sauti zilizosema katika sikio langu siku ile shuleni. Sauti hizi zilifoka sana na kusema kuwa zinatoka kwa muda tu lakini zitarejea.

Nikapatwa na fahamu zangu sauti zile zikiwa zimepotea... nikageuka na kuukuta ule umati ukiwa umemzunguka mama.

Sijui kuna jambo gani lilikuwa linatokea lakini nilipatwa hofu kwa jinsi walivyokuwa wakihangaika huku na kule huku wamemzunguka mama.

Nilihisi jambo baya ambalo sikutaka litokee lilikuwa limetokea.

Nilihisi mama yangu alikuwa ameaga dunia!!!

JIFUNZE!!

Nakusihi tena, wapo wanaoishi wakisema hawana dini wala imani yoyote na hawa wanajiita wapagani.

Naam! Si tatizo hata kidogo kuinama chini huku ukijitazama miguu yako na kisha kufungua kinywa chako na kusema HAUNA DINI.

Lakini tafadhali usije ukajipa ujasiri wa kukinyanyua kichwa chako juu na kisha kusema HAKUNA MUNGU!!

Nakusihi!!!

ITAENDELEA

MAMA’KE MAMA - 3​

Simulizi : Mama’ke Mama
Sehemu Ya Tatu (3)

Nilipiga hatua fupifupi hadi nikafika eneo lile ambalo mama alikuwa amezungukwa na wanakijiji.
“Ngomeni...” niliisikia sauti ya mama ikiniita na hapo babu akanishika mkono na kunipitisha nikafika mbele za mama... sasa alikuwa ameketi kitako na alikuwa anatabasamu tu!! Japo lilikuwa tabasamu la kujilazimisha.
Haikujalisha kitu kwangu, mama yangu alikuwa yu hai. Ilitosha.
“Ngomeni, sasa najisikia vizuri usiwe na mashaka sawa eeh!” alizungumza huku akimpatia babu mkono, babu akamnyanyua.
Mama aliweza kusimama peke yake, akawashukuru wote waliomuhangaikia hadi hapo alipokuwa alisema anaweza kutembea vizuri kabisa.
Mimi nilikuwa mdogo na hali hiyo ilinifanya niogope kusema kitu ambacho nilikisikia wakati ule nilipokuwa katika kusali kama yule mtaalamu alivyokuwa amenielekeza nilijua hata nikisema nilichokisikia hakuna atakayeniamini.
Nikalazimika kuwa kimya huku nikitegea muda nitakaobaki na mama pekee ndipo nitamueleza kuhusu zile sauti za wanawake na pia juu ya kupokelewa pale nyumbani kwa babu na yule mwanamke ambaye alikuwa shuleni kama mwalimu akanichapa kiboko kilichoniletea kizaazaa.
Mwanamke yuleyule ambaye mama yangu alimshutumu kuwa alimuua baba yangu.
Tulitembea hadi nyumbani kwa babu tukisindikizwa na baadhi ya wanakijiji huku wakiizungumzia hali iliyomkuta mama kuwa si yeye wa kwanza kutokewa na hali ile jambo la msingi wakamsihi sana kuwa ajitahidi ajilinde, sikuelewa ni kitu gani wanamaanisha hadi ukubwa huu ndo naelewa nini maana yake.

Mama alizungumza na babu kwa kirefu baada ya kufika kisha akaniita na mimi na kuniomba nimuelezee babu kila kitu kama nilivyomueleza yeye hapo awali. Nikajieleza kwa babu kila nilichokuwa nakumbuka. Safari hii sasa hata zile sauti zilizonijia masikioni wakati mama anapigania uhai wake nilisimulia.
Babu alikuwa mtulivu sana katika kutusikiliza, na ni kama aliyeonekana kujua mambo mengi sana ama la! Basi lile halikuwa jambo geni sana kwake.
Babu alitusihi sana tusilale hapo kijijini bali tumwachie yeye kazi ya kutazama hilo tatizo linasababishwa na nini. Alimwambia mama kuwa tatizo lililopo lazima litakuwa kubwa na anayelileta tatizo hilo amejipanga vyema katika mashambulizi.
Mama alitii alichoshauri babu, tukaondoka kurejea nyumbani.
Tulifika tukiwa tumeanza kuyasahau mambo kadha wa kadha yaliyotutokea tukiwa kule kijijini.
Tukala chakula na kisha kila mmoja akiwa amechoka kwa kiwngo chake, akaingia kupumzika.
Ni mimi ndiye niliamka kama nilivyokuwa siku iliyopita lakini mama aliamka ule mguu wake sasa ukiwa umevimba maradufu, ulikuwa umekuwa wa kijani huku misuli ikiwa inaonekana kusisimka sana yaani alitisha kumtazama.
Hiki nini? Tulijiuliza mimi na ndugu zangu. Mama aliyelala akiwa salama kabisa, anaamka akiwa katika namna hii ya kutisha.
Mama alikuwa hawezi kuongea bali alikuwa akitokwa na povu tu mdomoni, tulilia sana familia nzima hadi majirani wakajaa pale na kufanikiwa kumpeleka mama hospitali.
Hospitali walijaribu kupambana mguu ule uweze kutulia lakini ule uvimbe na ukijani ukazidi kutambaa kuelekea juu ya goti.
Ushauri wa haraka ukatolewa, ili kunusuru maisha ya mama basi mguu ule unatakiwa ukatwe.
Akaagizwa mtoto mmoja aweze kuzungumza na mama juu ya jambo hili. Weakati wengine wakijiuliza ni nani aende.
Nikajichagua mimi na kwenda moja kwa moja katika chumba alichokuwa amelazwa mama. Sindano ya kupunguza maumivu aliyokuwa amedungwa ilikuwa imesaidia sana. Aliweza kuongea japokuwa kwa tabu.
Nilimweleza mama juu ya shauri la daktari. Akanishika mkono wangu huku akiwa ananitazama.
“Ngomeni!” aliniita na kisha kuzungumza kwqa kabila letu, kabla hajaanza kuzungumza kiswahili.
Uso wake ukiwa na kitu kinachofanania na tabasamu.
“Jana uliona nilivyokuwa natembea?”
“Nilikuona mama.” Nilimjibu nisijue anataka kusema nini zaidi.
“Utanisaidia kuwasimulia wajukuu zangu kuwa mama aliwahi kuwa na miguu yake yote miwili. Alikubeba wewe mgongoni pamoja na wadogo zako, aliwatafutia chakula na aliwapenda sana.” Mama alizungumza huku ule mfano wa tabasamu bado ukiwa usoni pake.
“Nguvu za giza kamwe hazijawahi kupata ushindi wa kudumu katika vita yoyote ile. Ushindi wao siku zote ni batili. Nikikatwa huu mguu na nisiamke tena, tambua kuwa mimi ni mshindi. Nawe uwe mshindi siku zote, najua hawataishia kwangu tu. Watakuja tena kwako... hakikisha unawashinda kwa ajili yangu. Usiwaache wakushinde kwa sababu hawajawahi kuwa washindi. Kamwambie kaka yako atie saini wanikate tu huu mguu, napatwa na maumivu makali sana!” mama alimaliza kuzungumza, akauachia mkono wangu.
Niliondoka pale nikiwa tayari na picha ya kuwa baada ya masaa kadhaa mama yangu atakuwa hana mguu mmoja.
Niliumia sana lakini sikuwa na lolote ambalo ningeweza kufanya juu ya lililojiri.
Naam! Mama akahamishiwa chumba cha upasuaji.
Ilichukua masaa mawili kabla kaka yangu ambaye awali aliweka sahihi yake juu ya upasuaji huo kuitwa katika chumba cha daktari.
Yeye hakuchukua muda mrefu sana kabla hajarejea na taarifa ya msiba!
Mama alipoteza maisha katika chumba cha upasuaji. Ni maajabu tupu yaliyojiri huko lakini yote yaligota katika hitimisho la mama kupoteza maisha.
Mimi niliyeyashuhudia mengi nilibaki na chuki kubwa sana juu ya wanadamu.
Ndani ya kipindi kifupi sana tukageuka kuwa yatima.
Lakini hiyo bado ilikuwa haitoshi.
Ni kama mambo yale yaliisha, tukabaki kutangatanga na dunia, leo kwa mjomba kesho kwa ma’mkubwa.
Mwaka mmoja ukazaa mwingine, msoto ukazoeleka.
Ikawa miaka, na mabalaa yakamaliza likizo yao na kurejea tena kuweka kambi.
Sasa ikawa ni vita yangu!

Tafadhali nakusihi unisikilize kwa umakini neno kwa neno huenda haya yaliyonikuta mimi na wewe yanakutokea bila kujua.
_________________
Nilipofikisha umri wa miaka kumi na tisa nikiwa kijana ambaye sikupata elimu kubwa zaidi ya kuishia kidato cha nne na kuanza kujishughulisha mwenyewe nilikutana na msichana ambaye nilisoma naye shule moja hadi kidato cha nne. Wakati tupo shuleni dada huyu aliyeitwa Jasmin alikuwa kama dada yangu kwani alinizidi umri na umbo vilevile, lakini baada ya miaka kuwa imepita nikiwa nimekutana na suluba mtaani katika utafutaji wa maisha nikiwa kiokote nilikutana naye. Sasa mwili wangu haukuwa mdogo tena bali kipande cha mtu.
Siku ya kwanza tulikumbushiana mambo mengi sana ya kishuleshule..... ikawa hivyo mara kadhaa za kukutana.
Lakini ukaribu ule ulivyozidi kama ilivyo ada! Tukajikuta tukiangukia penzini.
Jasmine alikuwa akifanya kazi kwa muda katika ofisi moja ya kupokea na kusafirisha mizigo, huku mimi nikiwa ni mtu wa kushika lolote linalokuja mbele yangu likiwa halali. Ilimradi kuingiza chochote mfukoni.
Nilikuwa si maskini wa kutupwa na hii ni kutokana na utafutaji wangu katika juhudi kubwa.
Nilikuwa nimepanga chumba kimoja huku nikiwa namsomesha mdogo wangu!!
Alikuwa yu kidato cha sita wakati huo!!
Mapenzi yetu yalianza kama utani, mara anitanie kuwa mimi ni mdogo wake, mara siku nyingine ananilazimisha nimsalimie.
Ilianza hivyo, hadi siku tuliyojikuta tukishindwa kuzizuia nafsi zetu kuutangaza ukweli uliokuwa ukijifichaficha!!
Haya yalikuwa mahusiano yangu ya kwanza kabisa katika maisha yangu ambayo nilijikuta nikiyapa uzito mkubwa kabisa.
Kabla ya kukutana faragha yoyote na Jasmin tuliendelea kuonana sehemu za wazi nikamweleza Jasmini juu ya maisha kiujumla na ugumu wake, nikamsihi afanye kazi kwa bidii sana ili hatimaye aje kuwa na maisha bora hata kama hatakuwa katika mahusianio na mimi.
Zaidi ya mwezi mzima ulipita pasi kukutana na Jasmini faragha. Sikuwahi kujali juu ya hilo.
Hadi ilipofika siku aliyoomba sana aje nyumbani kwangu kunisaidia kufua nguo, hapo nilikuwa nimelalamika kuwa nina nguo nyingi sana za kufua na sijisikii vizuri kiafya.
Ile siku ya kwanza kumkaribisha Jasmin nyumbani kwangu ndipo nilikuwa nimelikaribisha balaa kubwa kupita lile balaa ambalo nilikuwa nimelisahau miaka kadhaa nyuma wakati nikiwa mdogo.
Ni hapa nilipokiri kuwa hakika wanadamu tunafanana nyuso lakini mioyo yetu imebeba fumbo zito kubwa sana.

ILE SIKU ilianza vizuri kabisa, asubuhi majira ya saa tano hivi tayari Jasmin alikuwa nyumbani kwangu, ilikuwa ni chumba kimoja nilichoishi lakini kwa sababu kilikuwa kikubwa kwa kiasi cha kutosha nilikigawanya kwa kutumia pazia hivyo kuwa kama chumba na sebule.
Kujituma kwangu kulizaa matunda yaliyokuwa yakionekana wazi.... nilikuwa nina samani za kukidhi haja za kile chumba.
Jasmine alipoingia alinisifia sana, kisha moja kwa moja akaingia kufanya kile kilichokuwa kimemleta pale nyumbani, akatoa kanga katika mkoba wake akavua nguo alizokuja amevaa akajivika kanga na kuingia katika zoezi la kufua.
Alianza na nguo nyeupe akazifua wakati huo akinisihi mimi niende sokoni kuhemea mahitaji ili aweze kunipikia pindi atakapomaliza kufua.
Nilisuasua sana kuondoka nikawa naingiza mada nyingine lakini baada ya mada niliyoizalisha kumalizika alinisihi tena kuwa niende sokoni kwanza.
Hatimaye nikaondoka, nilianzia buchani kisha nikaingia sokoni nikahemea mahitaji yote ya msingi.
Uzuri ni kwamba japokuwa sikuwa na utaratibu wa kupika pale nyumbani lakini nilikuwa nina vyombo vyote vya ndani.
Wakati narejea mapigo yangu ya moyo yalikuwa yanaenda kasi sana kana kwamba kuna kitu kimenitokea. Nilijishangaa kwa muda kisha nikatabasamu. Nikapuuzia mabadiliko yale katika mwili wangu.
Nilitembea hadi katika kona moja hivi ambayo baada ya hapo unakuwa umefika katika kibanda changu ninachoishi. Nikasikia kama sauti ikiita jina langu, ilikuwa sauti ya kike.
Unaweza ukaniuliza ni kwa nini nilihisi ni mimi ninayeitwa wakati kuna uwezekano wa kufanana majina.
Kilichoniweka katika hali ile ni kwamba jina Ngomeni lilikuwa jina langu peke yangu pale mtaani. Lilikuwa ni jina la ukoo, na yeyote ambaye angeitwa jina lile basi alikuwa na nasaba na mimi.
Niligeuka na kutazama nyuma lakini sikuona mtu yeyote akijishughulisha na mimi. Nikaamini kuwa niliwaza tu, haukuwa uhalisia.
Nikaendelea mbele kidogo, mara ikanikumba hali fulani hivi ambayo iliwahi kunikumba enzi za utoto wangu. Mwili wangu ulikumbwa na joto kali. Joto lililodumu kwa sekunde chache tu.
Yaani ni kama niliyepishana na jiko linalowaka moto.
Nakumbuka enzi hizo nilipokumbwa na hali hii mama yangu aliniuliza kisha likatokea jambo ba yasana mama akachomwa na mwiba uliosababisha purukushani ya aina yake na hadi anakata roho alidai kuwa alikufa ile siku alipochomwa na ule mwiba wa ajabu.
Na hapo hapo nikakikumbuka kitabu cha simulizi kiitwacho mama yangu anakula nyama za watu kilichoandikwa na mtunzi Irene Ndauka. katika kitabu hiki kuna ukurasa mmoja unazungumzia juu ya hii hali ya kukumbwa na joto ghafla. Sasa nilikuwa mimi katika kuhakiki.
Ndugu msikilizaji ukijikuta katika hali hii basi yumkini kuna mchawi ambaye ametanua miguu yake na kupita juu yako hii ikiwa ni dalili mbaya kabisa ya kukuzulia tatizo. Hivyo kama imewahi kukutokea hali hii basi ulikuwa unapita chini ya miguu ya mchawi.
Hii hutokea pia kitandani, ukihisi joto la ghafla basi haujalala peke yako!
Kama una imani thabiti, inuka fanya dua.
Mungu wetu kamwe huwa halali.
Nilipounganisha matukio hayo nikapatwa na hofu na hapa sasa nikatambua kuwa moyo wangu ulikuwa unapiga kwa kasi sana kwa sababu ya hali ile.
Niliongeza mwendo hadi nikaikaribia nyumba niliyokuwa naishi, kwa mbali kabisa nilitazama pale alipokuwa Jasmini akifua nguo, hakuwepo lakini vyombo vya kufulia vyote vilikuwepo.
“Au ameenda kuanika nguo huyu?” nilijiuliza huku miguu yangu ikiwa mizito sana kutembea. Hofu ya kukutana na mchawi ilikuwa imetanda.
Nilipiga hatua mbili zaidi kisha nikaliita jina la binti yule mara mbili, kimyaa!!
Hakuna alichojibu.
Nikakitua kile kikapu chini, nikajivuta hatua nyingine sasa nikaufikia mlango nikawa kama ninayechungulia ndani, nikamuita tena Jasmini.
Safari hii aliitika kutokea ule upande wa pili wa chumba changu niliotenganisha kwa pazia.
Uuuh! Moyo ukapata nafuu, Jasmin alikuwepo.
“Una nini mbona upo ndani?” nilimuuliza hapo nikiwa nimepiga hatua nyingine mbele. Nikijilazimisha kuwa katika hali ya kawaida.
“Tumboooo... Tumbo linaniuma” niliisikia sauti yake ikijibu kwa tabu sana.
Alipolalamika vile nilisahau kuhusu ule uoga nikaingia ndani. Nikafunua upande wa pili na kuingia, alikuwa Jasmin amelalia tumbo.
Nikafika na kumgusa taratibu huku nikimsihi kuwa niende kumnunulia dawa!
Hakunijibu badala yake alikuwa anakema tu!!
“We Jasmin.. nikakununulie dawa ipi.. au sio tumbo la kawaida?” nilizidi kumuhoji huku nikimtikisa kwa utaratibu.
Mara ghafla Jasmin aligeuka kwa nguvu sana, ile naushangaa ule mgeuko wake mara ghafla nikashtukia nikiwa nimenaswa kibao kikali sana.
Lahaula! Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilikuwa nakutana na mauzauza ya waziwazi huku macho yangu yakishuhudia mchana kweupe.
Hakuwa Jasmini bali ni kibibi kizee katika mavazi ya Jasmini.
Sura yake ilikuwa imefanya makunyanzi yaliyokuwa yanadhihirisha kuwa alikuwa amekula chumvi nyingi.
Alipozungumza neno la kwanza nikakiona kinywa kisichokuwa na jino hata moja ndani yake.
“Unataka nife mara ngapi ndio uje?” aliniuliza kwa sauti imara kabisa tofauti na sura yake.
Swali lake sikulielewa kabisa..... akabaki kunitazama huku akihema juu juu.
“Nakuuliza wewe kiumbe!!” alikoroma sasa allipiga hatua kunisogelea.
Nilitetemeka sana huku nikilia kama mtoto na kamwe sauti isitoke.
“Nisamehe...nisamehe” nilijikuta naomba msamaha usiokuwepo. Yaani niliomba msamaha bila kujua hata ni kosa gani nilikuwa nimefanya lililostahili mimi kuomba huo msamaha.
Kiumbe yule wa ajabu hakunijibu lolote alinifikia na kisha akainama akanipa mkono wake, nilisita kuushika.
Kwa kufanya vile akanizaba kofi kali sana usoni!! Na wakati naugulia maumivu akanisimamisha wima.
Alikuwa na nguvu jama!
“Naondoka nikirejea tena ni aidha tunaenda kwa lazima... ama la nitakufanya kitu kibaya ambacho hujawahi kufanyiwa maishani.
Alipomaliza kusema vile akanipuliza, nikausikia mwili wangu ukiwa unaishiwa nguvu nilijaribu kujizuia lakini haikuwezekana nikajikuta natua chini kama mzigo, ile naugua pale chini nikasikia kama upepo mdogo ukivuma na kisha kutoweka.
Nilibaki kujivutavuta pale chini, sikuwa na cha kufanya nilikuwa natokwa jasho.
Nikiwa vilevile nilisikia sauti ya Jasmini ikiiniita nje. Iliita kama mara tatu mimi nikiwa kimya tu, hakuna kitu kingine nilichokuwa nawaza zaidi ya yale maluweluwe yaliyonitokea.
Baada ya kama sekunde kumi hivi, mara mlango ukafunguliwa. Mawazo yangu yakiwa bado hayajafikiria kitu kinachoitwa maamuzi, yuel aliyeufungua akapiga hatua moja mbele, nikaiona ile nguo ya Jasmine ambayo baadaye niliiona ikiwa imevaliwa na kiumbe yule wa ajabu kabisa.
Aliyeufungua akapiga hatua ya pili, mimi bado nilikuwa pale pale chini. Mkojo ukiwa umejiamria wenyewe kutoka na kulowanisha nguo yangu.
Nilikuwa naogopa mno! Haya mambo hadithiwa tu kama hivi. Ni mazito
“Ngomeni wewe... umerudi saa ngapi.... hee! Mbona umelala hapo chini sasa? We ngomeni mbona jasho linakutoka hivyo!!” ilikuwa ni sauti ya Jasmini na sura ya Jasmini ikinihoji vile.
Alipojaribu kunisogelea mimi nilirudi nyuma kwa kutambaa huku nikimsihi anisamehe, yaani sikuamini kabisa kuwa yule ni Jasmini.
Nilimuogopa kupita kawaida.
“We Ngome wewe una nini lakini? Alizidi kushangaa..
“Ulienda wapi?” nilimuuliza.
“Nilienda kuanika nguo kule uliponielekeza vipi kwani?”
“Aliyeingia humu ndani unamjua??” nilimuuliza huku nikiwa pale chini hofu ikiwa imetawala.
“Ngomeni yaani hizo dakika mbili za kuanika nguo usitake kunambia eti tumevamiwa?” alinijibu kwa mshangao mkubwa sana.
“Jasmini... we Jasmini unanipenda kweli!” nilimuuliza, kwa kuropoka. Sikujua hata mantiki ya swali langu.
Hapo sasa akanisogelea huku akipiga goti, nikajisogeza nyuma zaidi hadi nikafikia kitanda, hapo sasa sikuweza kurudi nyuma zaidi.
“Nimekukosea nini Jasmini eeh! Nimekukosea nini nisamehe kama kuna baya nimekufanyia, Jasmini mimi sina baba wala mama, nina mdogo wangu namsomesha naomba uniache kama kuna lolote nimekukosea nisamehe... baba yangu na mama yangu si wametosha au?” nilimuuliza huku natetemeka.

Wakati nazungumza haya nikakumbuka kuwa chini ya uvungu wangu kuna panga huwa nalihifadhi hapo kwa sababu za kiusalama.
Nilichowaza kwa kipindi kile ni kupambana na kiumbe huyu aliyepo mbele yangu, kama mama alivyonieleza kabla hajafariki kuwa jisaidie na Mungu atakusaidia.
Nikapapasa na hatimaywe nikalishika vyema lile panga.
Wakati nimelishika vizuri Jasmini naye akazidi kunisogelea huku akitembea kwa kutumia magoti yake.
Kitendo cha kutembea kwa kutumia magoti kikanifanya nizidi kumuogopa na hapo nikakusudia kumfyeka.
Liwalo na liwe!!!

BONASI: Kama kawaida kwa wasomaji wenye ari shirikishi... LIKE, COMMENT bila kusahau muhimu kabisa SHARE simulizi hii. Nami nitakutembelea inbox na sehemu inayofuata ya simulizi hii.

Fisi yule akaondoka kwa utulivu kabisa akamfukuza fisi aliyekuwa amemdhibiti yule kijana, na mara akamrukia na ndani ya nukta moja yule kijana alikuwa anatokwa na kilio kikubwa sana huku fisi akitafuna sikio lake la mkono wa kuume.
Ilitisha sana kutazama!!
Niliusikia mkojo ulipokuwa unanitoka lakini sikuweza kuuzuia hata kidogo.
Nilijua kuwa baada ya kijana yule kupewa onyo kwa kukatwa sikio na kisha sikio kutafunwa na fisi ilikuwa inafuata zamu yangu!
Mkojo ulimwagika hadi ukamalizika lakini haukusaidia kuipunguza hofu iliyokuwa inanikabili.
“Ngomeni tunaenda ama nikuache na huyu fisi?” aliniuliza kikongwe yule huku akiyaacha mapengo yake yaonekane waziwazi. Na hakurudia swali lake bali alinikazia macho yake makali, ni kama macho yap aka mwenye hasira.
Nilijiuliza kidogo tu kuwa yule mwenzangu amekwanguliwa sikio lake na nimeshuhudia kwa macho yangu fisi akilitafuna na kulimeza, kile kilio chake cha uchungu hata nisingekisia bado ningeweza kuukadiria uchungu mkubwa aliopitia.
Mimi je?
Nikakubali upesiupesi kuwa nipo tayari kwenda bila kujua ni wapi ambapo ninapelekwa.
Yule bibi alicheka sana kwa sauti ya juu, kinywa chake kisichokuwa na meno kikiendelea kufanya dhihaka. Na mara nikazisikia ngurumo mithiri ya dalili ya mvua.
Kisha zikatoweka na yeye akaacha kucheka halafu akaniuliza.
“Unataka uende kwa usafiri gani, huu hapa ama unahitaji usafiri mwingine. Nikuagizie” aliniuliza akimaanisha kupanda katika mojawapo ya fisi kama yeye alivyokuwa amepanda.
Nilikataa kata kata kuwa siwezi kupanda juu ya fisi, akasikitika kisha akaniambia kuwa nisijali jambo lolote nitaenda kwa usafiri mwingine.
Ndugu msikilizaji tega sikio lako kwa makini zaidi katika kulisikiliza hili kisha umshike Mungu wako kwa nguvu zote.
Tambua kuwa hakuna mchawi mwenye nguvu kuzipita zile nguvu za mwenyezi Mungu lakini hii huja panapo imani, ukiwa na imani dhaifu kama niliyokuwanayo mimi basi bila shaka lolote lile huwezi kuwazuia wala kuwatetemesha viumbe hawa. Wachawi hawa wana uwezo wa kutikisa nyumba za viongozi wa kiroho na kuwatoa jasho.
Siwezi kusema wao wana imani kali sana. Lakini abadani! Imani za wengi ni dhaifu zaidi.

Baada ya kuwa ameniambia kuwa nitaenda kwa usafiri wowote ninaouhitaji zile ngurumo zikarejea tena, sasa anga ilibadilika na kuwa kiza kinene, fisi walitoweka kwa kasi wakatuacha tukiwa peke yetu yaani mimi pamoja na kile kikongwe, kikongwe kisichokuwa na meno kinywani.
Mara ikawa mvua, kadri mvua ilivyokuwa inanyesha ndipo nikagundua kuwa maji yaliyokuwa yanamwagika, kwanza hayakuwa maji ya kawaida na pili yalikuwa maji yaliyokuwa na rangi mithiri ya damu na yalipomwagika hayakuzama ardhini bali yalijaa kuja juu. Ni kama kwa muda ule ardhi ilikuwa imetiwa saruji. Wakati haya yote yanatokea kikongwe yule alikuwa anacheka tu na kunifanya nione kero kubwa sana. Sauti yake ilikuwa inakwaruza kama mtu ambaye baada ya dakika kadhaa hataweza kusema tena.
Lakini huyu aliendelea kucheka.

ITAENDELEA

Simulizi : Mama’ke Mama

Sehemu Ya Nne (4)

Sasa maji yale mithiri ya damu yalikuwa yamenifikia magotini ndipo yule kikongwe akazungumza.

“Jitahidi sana uogelee kwa bidii zako, ukithubutu kuyameza haya maji utakuwa ni mwisho wako, utakufa kwa uchungu sana kwa sababu umeitwa kwa hiari yako unaleta ujanja ujanja....” alizungumza vile na kama kawaida yake aliendelea kunicheka.

Mvua ilizidi kuongezeka, nilikuwa nimeuziba mdomo wangu ili nisije kumeza yale maji kama alivyonionya yule kikongwe.

Hayawi hayawi hatimaye maji yalikuwa shingoni, sasa nikalazimika kuogelea katika lile dimbwi la maji, nilikata maji kwa kutapatapa lakini yule kikongwe yeye alikuwa amesimama tu.. yaani ni kama alikuwa anazidi kurefuka kadri maji yale yalivyokuwa yanaongezeka.

Nilipiga mbizi mpaka nikaisikia mikono ikiwa imeshika ganzi na hapo nikasalimu amri nikijisemea na liwalo na liwe.

Nikaacha kupiga mbizi nikasubiri kifo kama alivyokuwa ameniahidi. Kifo cha uchungu mkali.

Nilipoacha kupiga mbizi maji yale yakakauka na nikajikuta katika ardhi kavu kabisa isiyokuwa na hata dalili ya kulowana. Nikajiuliza ile mvua ilikuwa imetokea kweli ama nilikuwa naota, lakini nilipojigusa nguo zangu zilikuwa zimelowana sana.

Na nilihisi muwasho na harufu ya damu.

“Mkuu nimeufikisha ujumbe uliokuwa unauhitaji...” mara nikaisikia sauti nyuma yangu, ilikuwa sauti ya mwanamke.

Sikuwa na haja ya kugeuka kwa sababu nilishatambua kuwa alikuwa ni yule kikongwe, nikatazama ni nani anayeambiwa vile. Sikuona mtu yeyote yule zaidi ya kuisikia sauti ikinikaribisha katika ufalme aliouita ufalme wa pepo.

Wakati sauti ile ikinisifia na kunikarimu yule kikongwe aliinama na kuninong’oneza kuwa kila nitakaloulizwa nikubali, la si hivyo nitauwawa kifo kibaya sana.

Nilitishika sana lakini nililazimika kutii, kweli kila nilichoulizwa nilikubaliana nacho kwa kutikisa kichwa.

Sikujua nilikuwa najiingiza katika jambo zito nisilolijua.

Baada ya kukubali kila kitu nilishtuka kutoka katika usingizi, nilikuwa kitandani kwangu. Jasho likinitoka huku nikiwa natetemeka sana. Niliketi kitako na kujiuliza ile ilikuwa ndoto ya aina gani. Ndoto ya kutisha vibaya mno, nilijaribu kujipapasa huku na kule, kwa mbali niliihisi ile harufu ya majimaji yanayofanana na damu niliyoota nikiwa naogelea.

Nilikurupuka na kuwasha taa, nikatazama saa ilikuwa ni saa nane na nusu usiku, niliitafakari siku yangu nzima ilivyokuwa kuanzia asubuhi hadi inakwisha, kuna baadhi ya matukio ambayo sikuweza kuyakumbuka kwa ufasaha kabisa, ni kama kuna mambo yalitokea katika siku yangu na kisha yakafutika katika ubongo wangu.

Nilishindwa kulala kabisa usiku huo!! Nilijiuliza sana juu ya lolote lile lililotokea, nilijiaminisha kuwa nimeota ndoto ndefu sana inayohusisha ujio wa Jasmini nyumbani kwangu kisha ikawa maluweluwe ya kutokea mtu mwingine ambaye aliiharibu kabisa siku yangu.

Nikajaribu kulala, nikakumbuka tukio la mimi kwenda sokoni, nikajiuliza kama ile nayo ni ndoto basi sitakuta kitu chochote kinachohusisha manunuzi yale ya sokoni. Nikajitia ujasiri nikasimama tena nikaenda upande wa pili wa pazia yangu, nikajikuta nashusha pumzi zangu kwa nguvu sana. Hapakuwa na kitu chochote kilichonunuliwa kutoka sokoni hivyo basi hii ilimaanisha kuwa yote yaliyotokea ilikuwa ni ndoto tupu hapakuwa na uhalisia wowote.

Ghafla! Harufu ikakutana na pua zangu.

Harufu ya uozo.

Nikazinusa nguo zangu, harufu pekee ilikuwa harufu ya damu kwa mbali ambayo sasa nilianza kuipuuzia.

Uozo unatoka wapi?

Nikajaribu kupekua huku na kule. Huenda ni panya amefia sehemu fulani ndani ya nyumba yangu.

Harufu gani ya ghafla kiasi kile sikuweza kuibaini mchana kutwa? Nilijiulizaq huku nikiendelea na msako.

Nikauona mfuko wa plastiki. Nikaufunua...

Uozo!!

Nyanya, vitunguu, karoti, nyanya chungu pamoja na hoho. Vyote vimeoza.

“Jamani, hivi si nilinunua...” nikasita. Hapo sasa nikakumbuka kuwa safari ya sokoni haikuwa ndoto. Nilienda sokoni.

Nilinunua mahitaji kwa ajili ya kupikiwa na mchumba wangu Jasmin.

Nikiwa najiona dhahiri nikiupoteza ujasiri ndani ya chumba changu, nikalisogelea sufuria ambalo lilikuwa mkabala na kile kifuko kilichobeba uozo.

Nililifunua huku hofu ikizidisha makazi ya kudumu katika moyo wangu.

Ngomeni mimi nilikuwa nimepatikana.

Waaa! Likafunuka.

Harufu kali ikatapakaa na kuzifikia pua zangu.

Nyama ile ilikuwa imeoza kiasi kwamba ilikuwa inatoa wadudu aina ya funza.

Nilipagawa!

Nilie? Namlilia nani?

Nikimbie? Nakimbilia wapi?

Nilijaribu kujiweka sawa lakini wapi? Nilibaki kujiongopea tu. Nilikuwa natetemeka sana.

Nyama na viungo vyote vimeoza angali nilivinunua ndani ya masaa kadhaa yaliyopita.

Usingizi uligoma, kila kilichonigusa nilikuwa nashtuka. Sikuzima taa wala sikuweza kujifunika shuka.

Niliamini kuwa sitaweza kupata usingizi, na haikuwa nia yangu kusinzia.

Kwa raha na amani ipi katika moyo wangu?

Tofauti na matazamio. Nilisombwa na usingizi, sasa na dakika nisiyoikumbuka.

__

Siku iliyofuata asubuhi majira ya saa nne ndipo nilishtuka kutoka usingizini, nilihisi viungo vyangu vikiwa vinauma sana. Na nikatambua kuwa nilikuwa nimelala kwa muda mrefu kupita kawaida yangu ya kudamka mapema sana kufanya mazoezi ya viungo kisha kuingia katika harakati zangu za siku zote.

Ilikuwa imetimu saa nne asubuhi.

Upesi nikakurupuka na kufunua pazia linalotenganisha kitanda changu na pahali pa kuitwa jiko na sebule.

Labda nilikuwa naota?

Hiki ndicho nilichojiuliza huku nikilazimisha jibu liwe ndiyo.

Haikuwa!

Vile viungo na mboga yenyewe, hakika vilikuwa vimeoza na kunuka.

Funza wakifanya riaria ya hapa na pale ndani ya chumba changu.

Hofu ikaanza upya.

Nikiwa katika kutojiamini, nikaufungua mlango na kutoka nje. Nilikuwa nakiogopa chumba ambacho kilikuwa paradise yangu siku za nyuma.

Nini hiki?

Nikiwa bado katika tafakari ile, mara akapita jirani yangu mmoja tusiyekuwa na ukaribu sana zaidi ya ujirani, akanisalimia huku akiniuliza habari za kupotea.

Nilishangaa lakini nikahisi ni ulimi tu uliokosa mfupa ulikuwa umepitiwa nikamjibu kuwa ni njema ni tu.

“Anauliza habari za kupotea wakati nilikuwa nimeonana naye siku iliyopita tu. Au nd’o yale ya habari za jioni kuulizwa asubuhi kimakosa?”

Nikapuuzia salamu ile!!

Mwili wangu uliotota katika uchovu ulihitaji walau maji niweze kuupata uchangamfu.

Nilipata faraja kuwa bafu la chumba nilichopanga lilikuwa nje. Nikaingia upesi na kuchukua ndoo moja. Nikajikokota kuelekea kuchota maji. Mitaa miwili kutoka nilipokuwa nimepanga.

Huko napo, nikakutana na mwanadada mmoja ambaye alikuwa ni muuza vitumbua na mara kwa mara nilikuwa nikienda kununua vitumbua kwake ama la!, hunipitishia nyumbani kwangu. Na yeye akanisalimia huku akiniuliza habari za kuhadimika.

“Tuwe tunaangana kaka, si unajua tena haya maisha tunaweza kuwa tunalindiana hata nyumba.” Alizungumza kwa uchangamfu.

Huyu sasa nikapatwa na kigugumizi katika kumjibu. Isingewezekana watu wawili watumbukie katika kosa lilelile.

Tena huyu! Hata siku mbili hazikuwa zimekatika tangu ninunue vitumbua kwake.

Nimehadimikaje sasa! Nilijiuliza.

Nilijilazimisha kutabasamu huku nikiamini kuwa na huyu naye amepitiwa.

Nikachota maji na kuondoka zangu, nikamfikiria huyu dada na yule jirani yangu! Lakini katu sikusahau kufikiria juu ya kizaazaa cha uozo kilichokuwa ndani ya nyumba.

Hawa watu vipi? Nilijiuliza.

Nilipofika nyumbani nilikuta kuna ugeni, wageni wale walikuwa wageni kabisa machoni kwangu, alikuwa ni mwanamke mmoja na wanaume wawili.

Waliponiona kwa mbali niliona yule mwanamke akinyoosha kidole kunielekea mimi.

Nilijitoa hofu kuwa sikuwa na tatizo lolote na mtu...... hivyo nilijongea na ndoo yangu mkononi hadi nikawafikia.

“Karibuni jamani.. shkamooni!!” niliwakaribisha na kuwasalimia.

Mwanamke pekee ndiye aliyenijibu lakini wale wanaume wawili watu wazima hawakujibu. Ni kama watu waliokuwa wanaisubiri shari ilipuke washangilie.

“Samahani wewe ndiye Ngomeni?” aliniuliza mwanamke yule, nikakubali kuwa ni mimi hawajakosea. Sura ya muulizaji haikuwa ngeni sana, lakini sikukumbuka pahala tulipokutana.

Nilipokubali kuwa ujio wao haujapotea njia, wale wanaume wakaonyesha jazba yao waziwazi.

“Kaka eeh! Sikia, hii ni wiki ya tatu tunakuja hapa kukutafuta bila mafanikio...sasa leo tumekupata yaani..” alizungumza kisha akasita nikagundua kuwa anajaribu kukabiliana na hasira iliyokuwa inamtawala.

“Wiki? Mbona... mhh! Ujue sielewi.. mimi nipo hapa kila siku jamani..” niliwajibu huku nikikumbwa na mshangao. Na hapo kichwani kwangu zikarejea kumbukumbu za kuulizwa habari za siku nyingi na za kuhadimika.

Kikazuka kizaazaa!

Baadaye sana nilimuuliza Mariam hiyo inawezekana vipi, fisi kukimbia kwa kasi vile bila kusababisha ajali wakati kuna watu barabarani?

Mariam akanieleza wale wote ninaowaona ni aidha watu ambao wameshikwa kimadawa na wanatembezwa bila wao kujua ama ni wachawi wengine kazini. Nikakumbuka niliwahi kuzisikia simulizi za wale watu ambao huota ndoto usiku na kujikuta wanafungua mlango na kutoka nje wakiwa wamefumba macho.

Kumbe sio ndoto za kawaida, bali wanakuwa wameitwa kichawi.

“Ngomeni, sio kila mchawi anaweza kumuona mchawi… inategemea una nguvu kiasi gani…. Mfano bibi yako ni hatari sana…. Anaona mno! Ni ngumu kumlaghai yule, hata sisi tumeamua tu kujilipua.”

KILE Kitendo cha mimi kukimbia ni kama kilihalalisha viumbe wale kutambua kuwa mimi nina ugeni katika ile sayari yao hivyo wakaanza kunifuata kwa kasi nikiwa sijui ni lipi lengo lao. Sijui hata ni nani aliwaamuru!

Kwa jinsi walivyonifuata kwa wingi nilijikuta hata Mariam simuoni tena, nikayakumbuka maneno yake alisema kwamba nikifanya kosa mimi na yeye tutakufa, sasa sikujua kama tayari alikuwa ameuwawa ama vipi.

Nikabaki kujipigania mimi kama mimi katika ulimwengu wa kiza.

Nilizidi kukimbia nikivuka makaburi yenye misalaba na yasiyokuwa na misalaba mbele yangu, nilikuwa sijui ni wapi ninaelekea na wakati huo wale viumbe wakizidi kunikimbiza, huku wanaunguruma.

Walikuwa wanatisha sana kuwatazama, walikuwa ni wanadamu lakini ni kama akili zao zilikuwa zimewaruka tayari, walikuwa na nywele ndefu na miili yao ilikuwa michafu. Wachache wakiwa na viungo kamili, wengi wakikosa baadhi ya viungo hususani mikono na miguu.

Kadri nilivyozidi kukimbia nilizidi kwenda porini na mara ardhi ilianza kuwa na unyevu unyevu, sikuwa na uwezo wa kusimama ili kujiuliza niliendelea kukimbia, kiumbe mmoja aliyekuwa anakimbia kwa kasi kubwa sana hatimaye alinifikia akanirukia, ilikuwa bahati yangu nikawa nimemzidi hatua moja mbele.. akaishia kunidaka shati langu huku akianguka chini, shati likachanika nikabaki kifua wazi nikaendelea kukimbia kuelekea katika uelekeo nisioujua.

Nilikuwa nalia kama mtoto, nilikuwa naomba msamaha lakini hakuna nilichojibiwa.

Ardhi nayo, ikazidi kuwa matope, sasa uwezo wa kukimbia kwa kasi ukapungua nikawa nazama katika matope na kuibuka.

Hii sasa haikuwa ndoto!

Nikakiona kifo kikinimendea, kadri nilivyozidi kwenda mbele matope nayo yalizidi kuongezeka kina chake kuelekea chini.

Nilipogeuka nyuma wale viumbe walikuwa wametoweka… hakuwepo kiumbe hata mmoja… nilikuwa peke yangu katika eneo hili linalotisha sana.

Eneo likiwa na ukimya, zikisikika sauti za ndege na mivumo ya miti.

Hapo sasa nikaanza kurudi kinyume nyume ili nisiendelee kuzama katika tope, nilifanikiwa kunyayua mguu wangu wa kulia lakini nilipojaribu kunyanyua mguu wa kushoto haikuwezekana.

Mguu ulikuwa mzito.

Nilivuta kwa nguvu nikagundua kuwa nilikuwa nimenasa katika kitu yawezekana ni mzizi ama chochote kile, nikavuta kwa nguvu sana lakini mguu ulikuwa unanyanyuka kidogo kisha unarudishwa kwa kasi.

Wakati nafikiria kuhusu ule mguu mmoja ulionasa, nikahisi kitu. Nikalazimika kutulia ili nipate uhakika.

Kweli! Kulikuwa na kiumbe hai katika lile tope kikiupapasa mguu wangu mwingine.

Nikajaribu kutapatapa huku napiga kelele. Kile kiumbe hai ndani ya tope kikanishika vyema.

Safari hii miguu yote miwili ilikuwa imekamatwa, huku ikivutwa kwenda chini zaidi katika lile tope.

Najirusha huku na kule, kiumbe hakiniachii. Tope linanuka sana name nazidi kudidimizwa.

Tope likafika kiunoni, kelele hazitoki koo limekauka.

“Niachiee, Niachie.” Ni kama nilikuwa najisemesha.

Mikono miwili yenye nguvu inazidi kunizamisha chini.

Tope kifuani. Kile kiumbe kikajiimarisha, kikahamisha mikono kutoka katika miguu na kuipandisha katika mapaja.

Kama huwa kuna hisia za kufakufa, huenda hizo ndo nilizokuwa nazo kwa wakati ule.

Sikuweza kutulia zaidi, nikaingiza nami mikono yangu katika lile tope, liwalo na liwe.

Nikaanza kuitoa ile mikono iliyonishika mapaja, nikawa naifinya, naipigapiga.

Mmoja ukaachia, nikawa narusha miguu, natukana matusi, natoa vitisho, mara namuita Mungu!

Yote ni katika kuutimiza ule usemi wa mfa maji…

Kikaachia mkono wa pili, nikaanza kutapatapa nijitoe katika yale matope. Naanguka uso ukiyasalimia yale matope, napiga kelele naendelea kutapatapa.

Nikatoka katika lile tope.

Nikabai pembeni nikihema juu juu, nikaisikia michakato katika lile tope. Nguvu zikanijia tena, nikaanza kukimbia.

Hofu ilikuwa imenitanda!!!

Nililiona kwa mbali kundi la watu, ulikuwa ni kama mji. Nikaufuata kwa tahadhari kubwa.

Kadri nilivyozidi kuusogelea nikaanza kuutambua. Ulilikuwa ni eneo nililokuwa nalifahamu.

Eneo ambalo huwa inafanyika gulio la kijiji chetu.

Na palikuwa na gulio.

Nikajitazama, tope limeniganda.

Nikajaribu kujifuta ilimradi tu, nisingeweza kutakata.

Nikaanza kukutana na watu. Nikiwa nimejiandaa kutomjibu mtu yeyote ambaye ataniuliza juu ya masaibu yaliyonikuta.

Hapa sasa nikakiri kuwa kuna wanadamu wana uwezo wa ajabu sana… wapo kinyume na matakwa na Mungu lakini mambo wanayoyafanya ukihadithiwa unaweza kukataa. Mpaka siku yanakutokea, hautapata nafasi ya kuwaomba radhi wale uliowaletea ubishi walipokusimulia.

Mimi nakusimulia! Ni uamuzi wako, kuniamini leo, ama kusubiri yakutembelee uamini kivyako.

Nilikuwa nawafahamu watu wengi niliokuwa nakutana nao, lakini ajabu sasa kila nilipotaka kuwaita majina nilikuta nayasahau majina yao… waliendelea na shughuli zao kuingia na kutoka mimi nikiwatazama tu.

Wengine walinipita kwa karibu kabisa, najiandaa kuwasalimia. Hawajali wananiacha hapo.

Kuna mmoja niliamua kumzibia njia kabisa, aliponifikia akanigonga kama hanioni. Kisha akayumbayumba akaanguka chini.

Akageuka nyuma na kutazama chini, ni kama mtu aliyejikwaa bahati mbaya katika ubovu wa ardhi.

Ina maana hawanioni!!

Nilistaajabu.

Nilijiuliza kwenda nyumbani kwangu lakini mwili ukawa mzito. Akili inaniambia nenda,mwili umefungwa kamba, hakuna kwenda.

Hadi gulio linamalizika mimi nilikuwa nazurura na sikuwa na maamuzi.

Nikabaki tena peke yangu.

Taratibu eneo lile la gulio likaanza kuingiliwa na wakazi wapya. Wakitanguliwa na wanama mbalimbali, paka na fisi wakiongoza katika orodha.

Nikarejea tena katika maisha yamashaka.

Nimejificha nyuma ya mti natazama yanayoendelea. Nikaliona tukio lililonikumbusha enzi ninasoma shule ya msingi.

Mwalimu akituagiza kukusanya vifuniko vya soda kwa ajili ya kujifunza somo la hesabu. Wanafunzi tulikutana katika kumbi za starehe, kila mmoja akiwania kuokota vifuniko vya soda kwa wingi.

Hawa walikuwa ni watu wazima, wakiwania kuokota alama za unyayo katika ile ardhi.

Sijui hata waikuwa wanazibagua vipi, sikuelewa walihitaji nyayo za nani na zipi hawakuhitaji.

Kuna sehemu walifikia hatua ya kukwidana, kisa fulani aliwahi alama ya unyayo ambayo mwenzake aliiwahi pia.

Hatimaye na hawa wakaondoka, nikabaki peke yangu. Kiu na njaa vikanikumbuka……

Ningepata wapi chakula na maji hili lilikuwa swali gumu sana.

Ndugu msikilizaji usiombe akili yako ikashikwa na watu hawa wabaya wanakufanya watakavyo, wakati wewe unajiona ni mjanja sana wao wanakuona mpumbavu na unakuwa unawafurahisha…..

Nilianza kuzurura kutafuta maji, kiu na njaa vilikuwa vinanisumbua…..

Sikufanikiwa hadi mwanga uliporejea, nikatembea hadi katika ule mji tena niliokuwa naufahamu, lengo langu likiwa moja tu… kuhakikisha nakutana na mtu ambaye namfahamu na kumueleza kile kilichokuwa kinanikabili. Safari hii nilijiahidi nikimuona mtu ninayemfahamu hata kama sio kwa jina, namkaba kwa nguvu mpaka anisikilize.

Mwili wangu ulikuwa unawasha sana na kunuka…. Nilikuwa ninazo siku kadhaa bila kuoga. Lile tope bado likiendelea kuning’ang’ania.

Nilipoufikia mji ule hakuna aliyejishughulisha na mimi, kwa saa zima nilikuwa nashangaa tu, kila ninayemsemesha ananitazama bila kunijibu anaondoka zake.

Sijui walikuwa wanaonana nini?

Nilimfikia mtu mmoja, alikuwa makamo yangu huyu nilipomsemesha alinijibu.

Sikuamini, nikashukuru sana kuwa hatimaye shida zangu zitatatuliwa.

Nikamueleza kuwa nina kiu na njaa kali.

Akanitazama, kisha akainama na kufungua deli lililokuwa mbele yake.

ITAENDELEA

Simulizi : Mama’ke Mama

Sehemu Ya Tano (5)

Yeye alikuwa anauza maji ya mifuko ambayo kwa jijini Dar yamezoeleka kama maji ya Kandoro. Maji ambayo hutumiwa zaidi na watu wa daraja la chini sana kimaisha, kutokana na unafuu wake katika bei.

Akaniuliza kama nina hela nikamwambia sina kitu.

Akafungua deli lake akatoa pakiti moja.

Lahaula! Maji yale yalifanana na damu, lakini yeye hata hakushtuka. Aliponipa niligoma kuyapokea nikimuuliza kulikoni maji yapo vile.

Akanitazama !

“Ngomeni ndugu yangu… usipokuwa makini njaa itakuua…” aliniambia na mara akaja mteja…. Alikuwa anahitaji maji. Huyu mtu amenijuaje? Nilijiuliza.

Nikasubiri amuhudumie yule mteja kwanza.

Yule kijana akafunua na kumpatia pakiti moja, akanywa kwa fujo akaongeza pakiti nyingine.

Nilikuwa nimeikunja sura yangu nikistaajabu yule mtu anayekunywa damu.

Na hajui kama ni damu!

Hapo sasa nikakumbuka kuwa kuna dawa Mariam alinipaka ya kuweza kuona mambo ambayo wengine wa macho ya kawaida hawawezi kuona.

Nikasikitika kuona wanadamu wanavyolishwa vitu vibaya bila wao kujua.

Yawezekana hata mimi nilikula sana vitu hivyo nikiwa na macho yangu ya kawaida.

“Ngomeni.. wewe ni mwenzetu lakini unavyojikimbiza utadhani utafanikiwa kutoroka mdogo wangu…. We bora utulie tu maana isingelikuwa kuandaliwa kumrithi bibi yako we ungeshakatwa ulimi zamani sana kwa tabia ulizoonyesha…. Wenzako wote waliojifanya wajuaji kama wewe waliishia kukatwa ndimi zao….” Aliniambia huku akiwa anatazama mbele.

Nilibaki kushangaa tu…. Akaendelea kuzungumza.

“Hapa utazunguka sana lakini kurudi nyumbani kirahisi, hiyo sahau kabisa…. Sikia kuwa mjinga nenda ukatulie upewe cheo chako uanze kula raha tu…..” alinieleza kana kwamba yale ni mambo ya kawaida kabisa aliyokuwa akisema.

Nilitaka kujibu kitu lakini maneno hayakuwa yamepangana sawa kichwani.

“Ngomeni… bibi yako anakupenda sana….. usije ukamkasilisha kwa kujifanya mjuaji… mi nakusihi sana kwa sababu nipo katika falme hizi mwaka wa sita sasa… ukiwa mpole wala hawana habari na wewe……” alimaliza… akawa ameitwa na mtu aliyekuwa anahitaji maji. Akaondoka na kuniacha pale nikiwa nimegwaya tu bila kujua ni kipi natakiwa kufanya kwa usahihi zaidi kulingana na hali ile.

Kuhusu kuwa mtawala wa falme za kichwawi sikuwa tayari hata kidogo.

Lakini kuhusu nini naweza kufanya kujitoa katika hali ile sikuwa najua pia.

Niliendelea kuwa eneo lile, hadi aliporejea yule kijana nikamsihi anisaidie niweze kupata chakula.

Alinitazama kwa masikitiko kisha, akaniambia nimsogelee. Akanishika macho yangu na kunipaka vitu nisivyovijua.

Alipoitoa mikono akanipa pesa niende kuata chakula. Sasa nilikuwa naonekana, watu akanisalimia na kuniuliza nini kimenisibu.

Nikijitazama, matope yalikuwa yamenitawala.

Niliwaongopea kuwa kuna mahali tunafanya ujenzi wa nyumba ya matope.

Baada ya kumaliza kula niligundua kuwa wateja wote wanaokula pale maji wanayokunywa ni kutoka kwa yule kijana ambaye nimegoma kunya maji yake ambayo ni damu na sio maji kama wanavyodhani.

Bado sikuweza kuyanywa yale maji japokuwa yalionekana kuwa safi kabisa tofauti na awali nilipoyaona kama damu.

Nilipomaliza kula nilirejea tena kwake akaniuliza ikiwa nataka kuendelea kubaki na hali ileile ama anirudishie macho yangu.

Nikawa najiulizauliza, hakunisubiri nimjibu akanigusa tena nikarejea katika ile hali.

Nilipogeuka kule kwenye chakula nilishuhudia mambo ya ajabu sana nikajaribu kujitapisha lakini haikuwezekana tayari nilikuwa nimemeza.

Hakika dunia hadaa, walimwengu shujaa!

Ndugu msomaji na msikilizaji wa simulizi hii, nilijifunza jambo kutokana na maswali yangu mengi.

Huyu kijana alinieleza kuwa nyama ya wanadamu ina tabia ya kuwa kama ulevi wa kudumu. Ukilishwa nyama ya mwanadamu utatamani tena na tena kuipata.

Wanapokuisha hautafahamu kama hii nd’o nyama ya mwanadamu.

Utaiona kwa jicho lako la kawaida, utaishika kwa mkono wako dhaifu, kisha bila shurti utaitia kinywani.

Utaitafuna, utaimeza! Kisha utabeua….

Yawezekana unapenda sana mishkaki, ama unapenda nyama ya mbuzi kupindukia, yawezekana u mlevi wa nyama ya ng’ombe. Wachawi hupitia humuhumu, anakulisha nyama ya mwanadamu katika mgahawa mmoja, unaondoka pale ukiisifia sana pasi na kujua kama ni nyama ya mwanadamu.

Utasema, mishkaki ya bwana yule mitamu sana.

Kesho utarejea tena, kisha utawaleta na rafiki zako. Wote wataisifia mishkaki.

Hata wasijue kuwa wapo katika kuila nyama ya mwanadamu!

Migawaha ya namna hii, muhusika akipoteza maisha. Hata ajitokeze mtu wa kupaendeleza kwa biashara ileile ya kuuza nyama hawezi kufanikiwa. Biashara itakufa!

Kwa sababu aliyeondoka alikuwa anauza nyama za wanadamu, anayemrithi anauza nyama za kawaida. Anauza mishkaki ya kawaida kabisa.

Wateja wataondoka huku wakilalamika kuwa marehemu kaondoka na utamu wake.

Jitafakari sana ndugu yangu!

Wewe ni mlevi wa nyama gani?

Nikiwa nimefumba macho vilevile mara nilishtuka nikimwagikiwa na majimaji ya moto, kisha nikasikia yowe kubwa likimtoka bibi.

Nikafumbua macho yangu na kujikuta damu ikiwa imenitapakaa sana, nilipagawa na kupiga mayowe.

Nilipomtazama bibi nilimuona akiwa anavuja damu katika bega lake, upanga ulikuwa umeanguka chini na alikuwa akipambana kukabiliana na damu ile.

“Washenzi nyie nitawachinja kama kuku…” alinikoromea huku akinitazama kwa jicho kali sana.

Nikiwa bado katika mshangao niliisikia sauti ikinisihi nikimbie, niliangaza huku na kule ni nani anaye nitazama lakini sikuona mtu yeyote Yule, sauti iliendelea kunisihi… nikajitoa katika yale matope. Sasa niliweza kutoka, nikawa narudi kinyumenyume bibi akinitisha kuwa nikiondoka ananiua.

Sikukubali kirahisi kumsogelea, nikarudi hadi nilipostuliwa na mlio mkubwa wa paka.

Nilipogeuka nikakutana na paka mweusi mwenye macho yenye rangi ya dhahabu, paka Yule alikuwa ananitazama akiwa ananikazia macho… niliogopa sana nikajaribu kumfukuza lakini badala aondoke akanyoosha mguu wake mmoja juu akawa ananifanyia ishara ambazo sikuwa nazielewa.

Ni kama naye alielewa wazi kuwa sizielewi zile ishara… akaanza kutoa miungurumo… sasa nikawa namuogopa.

Nilipomtazama vyema nikaona akitoa makucha yake, yalikuwa makucha marefu sana na kama angefikia hatua ya kunirarua lazima angenijeruhi vibaya mno.

Nikaanza kujiuliza, sasa nirudi makaburini kule kwa bibi ama nikabiliane na huyu paka.

Wanasema zimwi likujualo halikuli likakwisha… nami nikaona ni heri bibi anaweza kuwa na huruma na mjukuu wake japokuwa alionyesha waziwazi kutaka kuniua.. na sikuwa najua ni kitu gani kilitokea hadi akashindwa kutimiza azma yake.

Nilipoanza kurudi kinyume nyume mara ghafla yule paka aliunguruma kwa nguvu na hapohapo akanirukia kwa kasi ya ajabu kifuani makucha yake yakiwa yamechomoka vilevile.

Kumbuka sikuwa nimevaa shati hivyo yalijikita moja kwamoja katika kifua changu na kunisukuma kwa nguvu sana nikaanguka chini, ule muda nilipoanguka chini hapohapo nikaona kitu kama mkuki kikipita kwa kasi sana eneo lilelile nililokuwa nimesimama.

Yule paka alibaki akiwa juu yangu amenigandamiza, mimi nilikuwa natweta tu… kama ni kujikojolea nilikuwa nimejikojolea mpaka mkojo ukaisha.

Sasa nilikuwa mtu wa kupiga mayowe, na sauti nayo ilikuwa imekauka sikuweza kupiga mayowe kwa muda mrefu.

Nikiwa bado pale chini, paka yule akafanya mlio mkubwa sana ulionipagawisha, alifanya vile kama mara mbili. Na punde wakatokea fisi wawili, wale fisi walipofika walimnusanusa kisha akaondoka ikawa zamu ya wale fisi kunigandamiza pale chini.

Ilikuwa ni kama ndoto ya kutisha, ndoto inayongoja jua lichomoze, jogoo wawike nami niwaweke watu kitako kuwasimulia ndoto hii.

Lakini hii haikuwa!

Paka akaondoka kwa kasi sana, na baada ya sekunde kadhaa kutoka katika kile kichaka alitokea mtu na si paka tena, alikuwa hana nguo ya juu…. Na alikuwa msichana.

Alikuwa ni Bi. Mariam, alikuwa amejeruhiwa hapa na pale lakini alikuwa anatabasamu.

Nilishangaa sana kumuona kwa sababu hapo awali nilielezwa kuwa alikuwa amekatwa viungo vyake na kugeuzwa kuwa chakula.

“Bibi yako ni mtu mmoja hatari sana… lakini pambano ndo kwanza limeanza nitamnyoosha ama ataniua…” alizungumza bi Mariam. Mimi nikiwa nimepigwa butwaa tu.

“Ilikuwa akuue ule mkuki alioutuma ulikuwa umeelekezwa kwenye moyo… wewe nakwambia uiname unanitazama tu… sasa hivi ungekuwa umegongwa gari huko uraiani na ungezikwa…. Huko duniani sasa wanashangaa jinsi ulivyokoswakoswa na gari……” aliendelea kuzungumza.

Maelezo haya ya Mariam yalinikumbusha mambo kadhaa niliyowahi kuyasikia na mengine kuyashuhudia. Mtu anagongwa na gari, wanaenda kuzika kisha baadaye wanaingiwa mashaka wakifukua wanakutana na kinu ama chungu cha kupikia.

Ninakiri kuwa kama ni uhuru basi viumbe hawa walipewa uhuru mkubwa sana. Uhuru wa kufanya lolote dhidi ya imani dhaifu kabisa ya wanadamu.

Pasi na kuhitaji kuridhika, Mariam akasema sehemu ile si salama tuondoke, safari hii sikusubiri kufundishwa kumpanda fisi nilipanda mwenyewe, tukaondoka huku Mariam akinisimulia kilichojiri baada ya mimi kufanya makosa ya kukimbia na kisha kugundulika na wafuasi wa falme ile na kisha taarifa kumfikia bibi yangu kuwa kuna ujanja najaribu kuufanya ili kupingana na matakwa yake.

Akanieleza kuwa alikamatwa na kupewa adhabu kubwa kubwa lakini ikawa bahati yake pale ambapo mtu aliyepewa kumlinda alipomtamani kimapenzi na kujikuta akilegeza kamba alizomfunga.

“Ujue nisingeonyesha kumkubali basi wangenikata mikono na miguu.. na hadi sasa wanajua kuwa sina mikono wala miguu.. ndo maana bibi yako amepagawa nilipompiga skadi kwenye bega wakati anakaribia kuikata shingo yako… lakini ukweli ni kwamba sikukatwa kiungo chochote nilimkubalia yule bwana kuwa naye katika mapenzi akamkata mtu mwingine na kudanganya kuwa amenikata mimi… kosa alilofanya ni kuniamini na kunivujishia siri nyingi sana… alipolegeza kamba tu, nikamsubiri anisogelee nikaivunja shingo yake kwa mikono yangu mwenyewe kisha nikakizika kabisa kivuli chake asije akatoa ushahidi wowote na hapo nikatoroka na baadhi ya silaha.

Bila hivyo nisingeweza kukukomboa….” Alimaliza kunisimulia huku akiniacha na viulizo kibao….. hasahasa kile kitendo cha kubadilikana kuwa paka kiliniacha katika giza.

Tulifika eneo jingine ambalo alinieleza kuwa kidunia ni kama boda, kutoka mji huu wa kwanza kuelekea mji wa pili akanieleza kuwa baada ya boda hiyo kuna boda nyingine ambayo ndipo wanaofanikiwa kuivuka huweza kurejea duniani kama misukule iliyotoroka ama kutajwa kama watu waliofufuka.

Si kweli kuwa wanafufuka bali wanafanikiwa kuvuka boda kuu!!

Boda ya hatari kupita zote…..

Mariam hakusita kunieleza bayana kuwa si jambo jepesi kabisa kuivuka boda ile. Akanisihi sana nijitahidi kukubaliana na ukweli kuwa pale hatupo duniani bali tupo malimwengu ya giza.

Hivyo natakiwa kuishi kama itakiwavyo kule, nikijaribu kuyapeleka mambo kidunia basi yatanikuta mabaya sana.

Tulifika mahali tukashuka katika zile fisi akaziruhusu ziondoke, wakati zinaondoka akageuka kuzitazama na kisha akanyoosha mikono yake juu na alipoishusha niliona wale fisi wakiruka huku na kule kabla ya kutulia chini na kuwa wakimya.

Kabla hata sijamuuliza ni kitu gani kimetokea akanieleza kuwa amewanyamazisha fisi wale kwa sababu wakirudi kambini wanaweza kutoboa siri kwani kila tunachozungumza wanakisikia.

Baada ya hapo akawaendea wale fisi sijui alichofanya lakini alirejea akiwa amevaa shati la kiume.

“Ngomeni….” Akaniita. Nikaitika akanitazama na kunieleza jambo.

“Tunataka kuondoka katika ngome hii ya wachawi…. Sikufichi kuwa mimi ni mchawi ambaye nahitaji kutubu na kumrejea muumba wangu… amini usiamini huku wanamuogopa sana Mungu lakini ni ubishi tu… na hili la hawa watu kumuogopa Mungu ndo linanifanya na mimi nione haina haja ya kuendelea kuishi huku.

Lakini Ngomeni kabla hatujaondoka nahitaji nikueleze jambo ambalo ni wewe utafanya maamuzi juu yake. Unamjua Chausiku!!”

Nilimuuliza Chausiku yupi akanijibu.

“Yule aliyemchukua mama yako na baba yako….” Alinijibu kwa utulivu.

“Mama na baba yangu walikufa mbona muda mrefu sana umepita…..” nilimjibu huku nikiwakumbuka wazazi wangu na namna ya vifo vyao ilivyokuwa.

“Mh! Huko kwenu wamekufa lakini huku wanaishi…. Nasikitika kuwa watakufa ikiwa utafanikiwa kuivuka ngome hii…. Je upo tayari wafe sisi tuondoke zetu ama nini tunafanya…..” alinihoji kwa utulivu.

“Mariam ni nini unamaanisha?? Yaani wazazi wangu wapo hai?? Kivipi…”

“Huyo Chausiku ndiye alipewa jukumu la kuwaleta huku ili kujenga mazingira mazuri ya kumchukua mama na baba yako…… aah!! Kwani unakumbuka tarehe aliyokufa baba yako huko duniani…. Na mama yako je?” aliniuliza huku akitabasamu.

Nikafikiria kidogo nikakumbuka kuwa mama alikufa tarehe moja na baba lakini miezi tofauti.

Nikamuuliza hiyo ina maana gani.

“Tarehe sita.. hiyo ni siku yetu ya damu na kafara…. Wazazi wako wangekuwa wametolewa kafara zamani sana tatizo ulikuwa wewe… walitaka urithishwe kwanza ufalme ndipo wawaondoe,, lakini wameteseka sana….. ukiwaona hautawakumbuka kabisa…..” alizidi kunieleza.

Tukiwa bado tumesimama pale pale mara kwa mbali tuliwaona wanawake wawili wakitufuata, walikuwa wasichana warembo sana.

“Wakikusemesha usijibu hovyo bila kufikiria… ukiona huwezi kujibu nitawajibu mimi…. Sawa!!” Mariam alininong’oneza.

Wasichana wale wakatufikia…….

Mmoja akasimama pembeni yangu na mwingine pembeni ya Mariam.

Niliiona hofu machoni mwa Mariam.

Jambo hilo liliniogopesha sana. Kama Mariam ambaye ni mzoefu anaogopa, mimi nina kipi hadi niridhike?

Tulisubiri wazungumze hawakuzungumza walikuwa wanatutazama tu. Mariam naye hakuzungumza alibaki kuwatazama tu.

Mara ghafla….. ilikuwa ghafla sana si mimi wala Mariam aliyetegemea, wasichana wale ambao walikuwa wanazungumza kwa ishara zao wenyewe walifanya jambo la kustukiza mno.

Ghafla akina dada wale ambao walikuwa hawajasema neno lolote lile, walishikana mikono kisha wakapiga kelele sana. Wakati wanapiga kelele hizi kimbunga kikali kilivuma....

Kelele zao zilipokoma na kimbunga nacho kikawa kimeishia pale.

Lakini kulikuwa na maajabu mengine mapya, akina dada wale walitoweka na akatokea bibi yangu.

Mariam akanivuta na kuninong’oneza.

“Nenda kule makaburini, tafuta kaburi uulilozikwa hakikisha unalifukua mpaka ukipate kivuli chako. Mimi niache napambana na huyu kiumbe... najua ni hatari lakini usiogope lolote lile hakikisha unapambana.... ukifanikiwa kuingia kaburini jichane ili damu yako ikiite kivuli chako” alinisihi kisha mara moja akanisukuma.

Nikalazimika kukimbia huku nyuma nikiacha kivumbi kikali sana.

“Ngomeee.....” niliisikia sauti ya Mariam ikiniita, nilipogeuka nilimuona fisi mkubwa akinijia kwa kasi nikataka kukimbia lakini Mariam akanielekeza kuwa nipande katika mgongo wa yule fisi. Nikafanya vile upesi sana, sasa nilikuwa na ujasiri na nilikuwa nimeyasahau kwa muda mambo ya kidunia.

Fisi aliondoka kwa kasi sana na mimi nikiwa nimeshikilia.

Tulitumia muda kama dakika nne tu.. tayari tulikuwa makaburini, nikaongozana na yule fisi hadi nikayafikia makaburi, nikaanza kusoma majina katika makaburi, tulitafuta sana hatimaye tukalifikia kaburi lililokuwa na jina langu lile la Ngomeni.

Nikaanza kujaribu kuchimba lilikuwa gumu sana. Nikaanza kukata tamaa.

Ndugu msikilizaji umewahi kusikia kitu kinachoitwa fisi mtu. Kama unadhani ni hadithi tu basi fisi mtu wapo...

Huyu alikuwa fisi mtu, alipoona ninasota peke yangu akasogea hadi pale kaburini, akatanguliza miguu yake ya nyuma, kilichofuata ulikuwa ni mtafutano kati yangu na vumbi, fisi yule alifukua kwa kasi kubwa sana.

Baadaye vumbi lilitulia, nilimtazama yule fisi na kwa mara ya kwanza nikamuonea huruma kiumbe huyu wa ajabu, ulimi ulikuwa umemtoka nje na alikuwa akihema juu juu.

Nikawa najiuliza nini cha kufanya, yule fisi alikuwa amertulia akaniachia mimi ukumbi.

Nikalazimika kuingia pale kaburini huku nikiwa natetemeka. Bado nilikuwa siamini kuwa nilikuwa nimezikwa.

Nilianza kufukua zaidi, nikaanza kukutana na nguonguo zilizooza...

Hatimaye nikaanza kukutana na mbaombao.....

Nilivyofukua zaidi nikaliona jeneza.... jeneza lile halikufanania na la mtu aliyezikwa siku za karibuni bali aliyezikwa miaka mingi iliyopita.

Ile naendelea kufukua zaidi nikamsikia fisi yule akilia kwa sauti kuu.

Alilia sana huku akichungulia pale shimoni..... sikujua ni kitu gani kinaendelea nilikuwa nimebabaika tu.

Nikiwa sina hili wala lile mara ukasikika mshindo mkubwa sana, mchanga uliofukuliwa ukaanza kurudi ndani ya kaburi...

Kumbuka wakati huo sijatoka na tauyari shimo lilikuwa refu, nikawa natapatapa kupanda ili nitoke mchanga ukaniingilia machoni hapo sasa sikuiwa naona tena mbele. Nikawa natapatapa huku mchanga ukizidi kuingia mle shimoni.

Nikajiona nikizikwa angali nipo hai kabisa.... nilipatwa hofu ya kifo.

Mchanga ukazidi kuingia shimoni kwa kasi sana.

“Ngomeni...... rudishaaaaaa rudishaaaa jina kwake..... likatae jina...” niliisikia sauti ikinisihi ilikuwa sauti ya Mariam, baada ya sauti ile kusihi mchanga nao ukakoma kurudi shimoni bila shaka aliyekuwa anaurudisha alikuwa amesita... nikajaribu kupekecha macho yako, jicho moja likaweza kuona mbele.

Nilichokiona kilikuwa hakifai hata kukisimulia, alikuwa ni Mariam lakini sio Mariam yule... huyu alikuwa amelowa damu vibaya mno,. Japokuwa sikuwa naona vizuri lakini niliweza kutambua kuwa hakuwa na jicho lake moja.

Mkono mmoja pia haukuwepo...na alikuwa amefungwa kamba katika mti.

Mara nikamuona bibi yangu akijivuta kuelekea alipokuwa mariam, nikatapatapa niweze kujitoa katika ule mchanga lakini haikuwezekana tayari miguu yangu ilikuwa imenasa.

Sikuwa naelewa nalikataaje jina langu, je ni kwa kusema silitaki jina langu ama ni kwa kufanya nini.

Nikajaribu kusema kuwa silitaki jibna lile lakini sikuona mabadiliko......

Mariam akapaza sauti tena, akanisihi nijichane nitokwe damu iingie kaburini. Na hapo nikakumbuka jinsi alivyonieleza mwanzo

Aliposema vile nikaona bibi anaweweseka ni kama aliyekuwa anajiuliza aende kwa mariam ama aje kwangu.

Kuona vile na mimi nikaona niitumie nafasi ile ya mwisho kupambana na watu hawa wabaya.

Hamna kitu kigumu kama kujijeruhi wewe mwenyewe, ona tu katika filamu mtu anajichana na kisu.... lakini katika maisha ya kawaida kujijeruhi ni kazi ngumu.

Nikajaribu kujing’ata lakini sikutokwa damu zaidi ya kuumia na kuacha kufanya vile.

Bibi alinitazama kisha akacheka kwa sauti ya juu, bila shaka aligundua kuwa siwezi kufanya kile nilichokuwa najaribu kukifanya.

Nikiwa bado palepale, mara nilisikia kishindo, na mara nilikuwa nimebanana mle kaburini na yule fisi mtu.

Fisi hakupoteza muda licha ya mimi kupiga mayowe alinirukia na kunirarua mkono wangu kwa kutumia makucha yake.....

Hapohapo damu ikaanza kunitoka na kaburi nalo likaanza kutetemeka, fisi akaruka na kutoka nje.

Ilikuwa kweli kilichotokea, nikashangazwa kujisikia nikiwa imara sana, bibi aliporejea pale sikuwa namuogopa tena nilijiona mtu mpya kabisa nisiyekuwa na hofu dhidhi ya watu hawa wabaya.

Alifika na kutoa amri zake lakini sikudhurika.......

Nikawa natembea huku nikiwa nashangaa.

Mara akapiga miluzi mikali na baada ya muda kidogo kiza kikatanda.

Na kimya kikachukua nafasi yake hadi alivyopiga miluzi tena mwanga ukarejea.

Nikamuona bibi akiwa na upanga mkali sana. Na mbele yake kulikuwa kuna watu wawili wachafu sana.

“Ukijifanya mjuaji nawachinja watu hawa mbele yako....” alinisemesha huku akicheka.

Nikakumbuka maneno ya Mariam aliniambia kuwa baba na mama yangu wapo hai lakini wamezeeka na wameteseka sana.

Mungu!

Inakuwaje tangu awali sikukumbuka kuwa kuna Mungu?? nilistaajabu

Nikafumba macho yangu palepale ili nisiweze kushuhudia lile ambalo lilitakiwa kutokea. Wazazi wangu kuchinjwa...

Nilipofumba macho mara nikakumbuka nilipokuwa mdogo, siku ambayo mama yangu alikuwa amekumbwa na pigo la ajabu kijijini kwa babu kuna mganga aliniuliza kama ninamuamini Mungu. Nilipokubali akaniambia niwe mkimya niseme na Mungu nimwambie kuwa sitaki mama yangu afe katika mazingira yale.

Kweli baada ya kusema na Mungu kuna muujiza ulitokea lakini kutokana na ule utoto sikukumbuka kusema asante kwa Mungu kwa sababu nilikuwa siujui vyema utukufu wake.

Nikazungumza katika nafsi yangu, kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu nikasema na Mungu wangu, nikamwambia kuwa atende muujiza kwa sababu sisitahili kufa kwa amri ya watu wale wabaya.

Ajabu iliyoje hii.....

Alinisikia na leo hii naweza kusema hadharani kuwa hakuna chenye uwezo popote pale zaidi yake Mungu.

Niliposema naye tu mara bibi na wenzake wakaanza kutetemeka, mara wakimbie huku mara kule...

Nami nikajikuita natetemeka sana na kisha nikaanguka chini.

Sikujua kilichoendelea zaidi hadi pale niliporejewa na fahamu zangu, nikajikuta nipo maeneo ya makaburini.

Nilikuja kupatwa na fahamu zangu tena nikiwa nimelala chini nikiwa nimezingirwa na watu.

Kamera zikiwa zinanimurika na nilikuwa nipo eneo la makaburini, kitu cha kwanza kusikia nilisikia watu wakisema kuwa nimefufuka.

Wengine walisema nimetoroka kutoka katika misukule.

Nilisimama nikiwa dhaifu sana, nikajitazama jinsi nilivyo. Nilikuwa nimechafuka sana.

Nikanyanyua macho yangu, waandishi wa habari wakawa wananipiga picha.

Mwandishi mmoja akanisogelea na kuniuliza jina langu, aliponiuliza hivyo nikakumbuka juu ya jina la NGOMENI…. Sikujitambulisha vile.

“Naitwa Fredric naombeni maji ya kunywa nina kiu sana…..” nilimjibu, upesi wakanipatia maji nikanywa.

Wasamaria wema wakanichukua kwa ajili ya kunipatia maji ya kuoga.

Baada ya kuoga nikapewa chakula… hapo nikapata nguvu upya.

Na punde baada ya hayo yote nikakutana na mwandishi wa mkasa huu, akaanza kuniuliza swali moja baada ya jingine.

Naam! Chanzo cha hayo yote alikuwa ni mama yake mama…..

Lakini aliyenitoa katika suluba ile hakuwa mwingine bali mwenyezi Mungu muweza wa yote.

Nashukuru kuwa baada ya mkasa huu… wasamaria wema walijitolea michango yao…. Viongozi wa dini mbalimbali walichangisha michango ikanifikia.

Nikayaanza maisha yangu mapya nikiwa nimelikataa jina la Ngomeni nikaendelea kuishi kama Fredrick nikiwa sina tatizo na mtu. Sikuwqahi kujua hatma ya wazazi wangu kwa sababu miili yao haikuonekana tena, sikujua kuhusu Mariam lakini Jasmin nilionana naye akiwa yu salama bin salmini alinieleza kuwa ile mimba niliyompa ilitoka yenyewe akiwa amelala usiku

Nimesimulia mengi ila napenda kukusihi mzazi na mzazi mtarajiwa, usimpe mwanao jina kwa sababu tu unapenda jina hilo… kuna baadhi ya majina yanazunguka na balaa yanamsubiri atakayepewa jina hilo ili balaa litue juu yake.

ZE HENDI HIZI HIYA!!
 
Yaan nasoma huku naogopa lkn Kuna mahali vpande vnaruka kwel mfano pale Jasmin alvyoenda kwake mara inakuja amekutana na bb haionyesh ilikuwaj mpk wakakutana na bb na Jasmin alienda wap..pia n vp alkutana na Mamu n sehem nyng sana ... Mwisho wa yte Hadith n tamu sanaa
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom