Mimi ni miongoni mwa watu ambao hawana hofu ya kifo sababu jehanam sijui motoni au peponi.
Hakuna adhabu yeyote baada ya kufa.
Hakuna kufufuka.
Ukifa nishati (uhai) iliyopo kwako inabafilika aina (form) wala haipotei.
Inakuwa chakula ya viumbe wengine katika food chain kisha unarudi duniani kupitia vizazi vya viumbe waliozaliwa kwa nishati yako toka kwa wazazi wao.
Hivyo Mimi ni samaki, ndege, mimemea waliyo kula mababu zangu na ambavyo vilikufa ili nizaliwe.
Ufufuo na adhabu au tunu baada ya kufa Ni ubatili, uongo na vitisho tu ili niishi kwa maadili yanayo saidia kusitokee kuangamiza kizazi cha binadamu.
Mungu ametuumba akatuacha tuwe huru na chochote tupendacho duniani.
Unaweza kuwa sahihi au usiwe sahihi.
Kwa nini?
Kwa sababu Imani na Sayansi ni maarifa mawili yanayoshughulikia "Ukweli" mmoja kwa njia mbili tofauti.
Sayansi inatumia "vipimo". Inaeleza kwa jinsi gani. Imani inatumia "ufunuo wa Mungu". Inaeleza kwa nini.
Jambo lililo wazi kuhusu sayansi ni kwamba inatusaidia kuelewa kwa undani jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na ulivyotokea.
Pia sayansi ni maarifa yanayoweza kusahihishwa. Kwa nini? Kwa sababu ni maarifa yanayokua na kuendelea. Jambo lililojulikana kuwa liko hivi linaweza kubatilishwa kuwa halikuwa kweli ukipatikana uthibitisho mwingine bora zaidi.
Kitu muhimu ambacho hatupaswi kuchanganya kati ya Imani na Sayansi ni kuwa:-
Sayansi inamesema "Kama hatuwezi kupima kitu au jambo basi kitu au jambo hilo halipo."
Hapa kuna vitu viwili.
1. Ukweli. Ukweli hautegemei kipimo au kuwepo kwa kipimo ili uwepo. Ukweli upo daima. Ni jinsi mambo yalivyo.
2. Kipimo. Hapa tunazungumzia maarifa. Leo sayansi haiwezi kipima vitu vingine kwa sababu maarifa ya hivyo vipimo hayajapatikana. Mfano hatuwezi kusafiri kwenda kwenye galaxy nyingine nje ya galaxy yetu kwasababu hatuma kifaa cha kutufikisha huko kwa sasa.
Kadiri ya sayansi mwili ukisha kufa maisha ya mtu yameisha. Kwa sayansi ni sahihi kwa sababu sayansi hadi sasa ina vifaa vya kupima mwili tu haina vifaa vya kupima roho.
Kwa hiyo kwa sayansi maisha ni mwili tu sio roho. Sio roho kwa sababu hakuna kifaa au kipimo cha kupima roho.
Swali hapa si kifaa au hatuna kipimo cha kupima roho. Swali ni Ukweli? Roho ipo au roho haipo?