Askari Polisi wa Mpwapwa, Rashid Mohamed Juma ambaye afariki akiangalia Mchezo wa Simba na Yanga

FORTALEZA

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
9,978
2,000
Afande Rashid wa kituo cha polisi Mpwapwa, amepoteza maisha baada ya timu yake ya Yanga kuifunga Simba jana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

Afande alishikwa na furaha iliyopitiliza hali iliyosababisha kukutwa na mauti huko Mpwapwa, Dodoma!

Poleni sana wafiwa, kwa kupoteza mpendwa wenu, hizi timu inabidi tuzipende kwa kiasi!

====

Askari Polisi wa Kituo cha Polisi Mpwapwa, Rashid Mohamed Juma ambaye ni Shabiki wa Yanga amefariki Dunia jana wakati akitazama mchezo wa Simba na Yanga kwenye TV, Shuhuda aliyekuwa akitazama nae mpira amesema alifika pale dakika ya pili ya mchezo na hakuchukua zaidi ya dakika tano alianza kuishiwa nguvu

"Alianza kuguna akiwa amesimama na nikamdaka baada ya kumlaza chini ndio akaendelea kuguna kama ng'ombe na kurusha mikono baadaye akaguna mara ya mwisho na kunyoosha miguu na mikono baadaye walikuja Askari kumchukua baadaye wakasema ameshafariki sio kwamba amefariki baada ya goli hapana, wakati anaendelea kurusha mikono goli ndio lilikuwa linaingia" ——— Joseph Ndani Mutalima, Mkazi wa Mpwapwa

Mwili wa Rashid umesafirishwa kuelekea Rukwa kwa ajili ya mazishi, Marehemu ameacha mjane na Watoto wawili na mazishi yanatarajiwa kufanyika keshokutwa.
 
kikiboxer

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
1,554
2,000
Mbona taarifa kama inaficha baadhi ya mambo.
Yani mtu afurahi kisha ndio amefariki? Alikuwa mgonjwa au baada ya kufurahia akapiga tungi na mambo mengine?
Naona kama sijaelewa hii taarifa.
 
Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
17,981
2,000
Afande Rashid wa kituo cha polisi Mpwapwa, amepoteza maisha baada ya timu yake ya Yanga kuifunga Simba jana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

Afande alishikwa na furaha iliyopitiliza hali iliyosababisha kukutwa na mauti huko Mpwapwa, Dodoma!

Poleni sana wafiwa, kwa kupoteza mpendwa wenu, hizi timu inabidi tuzipende kwa kiasi!

View attachment 1953513
Alikua anaijua PGO?
 
Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
14,597
2,000
Afande Rashid wa kituo cha polisi Mpwapwa, amepoteza maisha baada ya timu yake ya Yanga kuifunga Simba jana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

Afande alishikwa na furaha iliyopitiliza hali iliyosababisha kukutwa na mauti huko Mpwapwa, Dodoma!

Poleni sana wafiwa, kwa kupoteza mpendwa wenu, hizi timu inabidi tuzipende kwa kiasi!

View attachment 1953513
Askari wa Simon siro alipatwa na kitu ambacho kitaalamu tunakiita Takotsubo syndrome.

Wataalamu wenzangu watakuwa wamenielewa.
 
1954

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
9,721
2,000
Hawajui
Mbona taarifa kama inaficha baadhi ya mambo.
Yani mtu afurahi kisha ndio amefariki? Alikuwa mgonjwa au baada ya kufurahia akapiga tungi na mambo mengine?
Naona kama sijaelewa hii taarifa.
Kuandika...wasamehe..au inawezekana ni umbeya tu..
 
Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
15,324
2,000
IMG-20210926-WA0025.jpg

Inaonyesha Yanga walibshatisha Sana kale kagoli kamoja ndio maana wanashangilia hadi kufa.Poleni sana watani.RIP Askari.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom