Arusha: Jeshi la Polisi lamtia mbaroni mtuhumiwa anayedaiwa kumuua Beatrice Minja

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Beatrice James Minja ambayo aliyafanya huko Tarekea Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjro Tarehe 12.11.2023 na mtuhumiwa aliyefanya aliyefanya tukio hilo kukimbia.

Akitoa taarifa hiyo leo kwa vyombo vya Habari Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema kuwa baada ya taarifa hizo kufika Jeshi la Polisi lilianza mara moja uchunguzi kumtafuta aliyefanya tukio hilo ambapo mapema leo Disemba 31.12.2023 Jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata Mtuhumiwa Lukas Paul Tarimo.

SACP Misime amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa mafichoni huko Kijiji cha Jema kata ya Olondonyosambu Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha.

Aidha amebainisha kuwa baada ya Mtuhumiwa kuhisi atafikiwa na Mkono wa sheria alijaribu kunywa sumu ya kuuwa wadudu lakini Jeshi hilo lilifanikiwa kuwahi sehemu alipo mtuhumiwa huyo na jitihada za kumkimbiza katika kituo cha afya zilifanyika ambapo alipata matibabu na anaendelea vizuri huku akisubili taratibu za kisheria.

Pia Msemaj wa Jeshi hilo amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wao na Jeshi la Polisi kitendo kilichopelekea mtuhumiwa wa mauaji kukamatwa huku akiwaomba wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.
 
Huyu ndio msaidizi wa nyumbani wa Waziri ? Mbona kama mlisita sita weer....hadi semaji kuu limeingilia kati hakuna RPC wala RC Mkoa husika ? Kuna deal.hapo kati. RPC amekuwa vompromised na nguvu za Waziri ? Sasa vipi Waziri mwenyewe akitekeleza kitu kama hicho atakamatwa kweli ? Kuna shida mahali, hakuna mtu alue juu ya sheria. Prof Mkenda alichokifanya sio haki kumlinda muuaji kusa madaraka yake ... Waziri
 
Huyu ndio msaidizi wa nyumbani wa Waziri ? Mbona kama mlisita sita weer....hadi semaji kuu limeingilia kati hakuna RPC wala RC Mkoa husika ? Kuna deal.hapo kati .....RPC amekuwa vompromised na nguvu za Waziri ? Sasa vipi Waziri mwenyewe akitekeleza kitu kama hicho atakamatwa kweli ? Kuna shida mahali.....hakuna mtu alue juu ya sheria....Prof Mkenda alichokifanya sio haki....kumlinda muuaji kusa madaraka yake....Waziri
"hadi semaji kuu limeingilia Kati"
 
hao mawaziri ni watu wadogo sana sana, nafasi za uteuzi hata sio za kupandisha mabega, ona PAULINE GEKUL alivyofyatuliwa amesumbuliwa hadi na vinyangarika kama kina madeleka tu na maelezo polisia amechukuliwa na bila shaka yupo nje kwa dhamana akitakiwa kuhudhuria polisi kwa muda fulani. naashauri polisi ukiona hao viongozi wana tuhuma, nenda tu kakamate waandikwe maelezo na upelelezi uendelee.
 
Jeshi la Polisi nchini, limesema limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa aliyemuua Beatrice James Minja, kwa kumchoma kisu, mnamo Novemba 12, 2023, huko Tarakea wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro.
.
Akitoa Taarifa hiyo, leo Disemba 31, 2023, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, SACP David Misime, amesema Mtuhumiwa huyo ambaye jina lake ni Lukas Paul Tarimo, alikamatwa akiwa amejificha katika Kijiji cha Jema, kilichopo Kata ya Olondonyosambu, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha, na kwamba alijaribu kujiua kwa kunywa sumu ya kuua wadudu lakini Jeshi hilo lilifanikiwa kuwahi sehemu alipo na kumkimbiza katika kituo cha afya, ambapo alipata matibabu na anaendelea vizuri.
#ITVUpdates
 
hao mawaziri ni watu wadogo sana sana, nafasi za uteuzi hata sio za kupandisha mabega, ona PAULINE GEKUL alivyofyatuliwa amesumbuliwa hadi na vinyangarika kama kina madeleka tu na maelezo polisia amechukuliwa na bila shaka yupo nje kwa dhamana akitakiwa kuhudhuria polisi kwa muda fulani. naashauri polisi ukiona hao viongozi wana tuhuma, nenda tu kakamate waandikwe maelezo na upelelezi uendelee.
Mkuu wanasiasa wana nguvu kama hujielewi watakusumbua akili yako
 
Kwanza I would like to ask an academic question. Yule mwanamke alichomwa kisu mara 27, ilikuwaje aliendelea kuishi siku 45?
Kwa nini polisi walikuwa wanavuta miguu kwenda kumsaka mtuhumiwa?(Lakini, hapa labda kuna simple explanation)
Huyu Lucas Paul Tarimo ni dini gani? Amewezaje kumchoma mtu kisu mara 27?
 
Aidha amebainisha kuwa baada ya Mtuhumiwa kuhisi atafikiwa na Mkono wa sheria alijaribu kunywa sumu ya kuuwa wadudu lakini Jeshi hilo lilifanikiwa kuwahi sehemu alipo mtuhumiwa huyo na jitihada za kumkimbiza katika kituo cha afya zilifanyika ambapo alipata matibabu na anaendelea vizuri huku akisubili taratibu za kisheria.
Swali kwa jeshi hilohilo
  1. Mbona hamjajitokeza kuzungumzia wale vijana wawili waliopigwa risasi Vingunguti?
  2. Mbona huyu aliyetaka kujiua kwa sumu mmemhangaikia kuokoa maisha yake wakati wale vijana wadogo nao mlikuwa na uwezo wa kunusuru uhai wao wakafikishwa kwenye vyombo vya sheria sawi na Tarimo?
 
1000006565.jpg
 
Eti mtu unaua unakimbilia oldonyosambu ukidhani serikali inamkono mfupi kiasi hicho,hapo angetakiwa akimbilie Kongo ndani ndani huko ajiunge na waasi.
 
Back
Top Bottom