Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
Tulieleza kutokana na mazingira yaliyokuwa yamezunguka tukio hilo ilitubidi kushirikisha wataalam mbalimbali wakiwepo wachunguzi wa matukio ya vifo. Timu hiyo katika uchunguzi wake ilibaini kifo chake hakikuwa cha kawaida bali ni Mauaji. Baada ya kubaini hivyo ilichunguza nani aliyefanya mauaji hayo na kwa malengo au madhumuni gani. Hivyo kwa kutumia uchunguzi wa kisayansi waliweza kubaini waliohusika na mauaji hayo na malengo yao yalikuwa ni kumpora Omary Saimon Masamo chochote kile watakacho mkuta akiwa nacho.
Waliohusika na mauaji hayo tayari wamekamatwa na wamekutwa wakiwa na simu ya marehemu ila fedha walizompora kiasi cha Shilingi 200,000/= walikuwa wameshagawana na kuzitumia. Waliweza kumpora baada ya kumpiga kisogoni na kudondoka chini.
Waliokamatwa ni Anthony Paskali ambaye anajulikana kwa jina maarufu Lulu na Emmanuel Godwin Jeseph anayejulikana kwa jina maarufu la Emma wote wakiwa ni wakazi wa Karatu. Taratibu zilizobaki za kiuchunguzi zinakamilishwa ili hatua nyingine za kisheria ziweze kufuata.
Jeshi la Polisi linaendelea kutoa tahadhari kwa baadhi ya watu kuacha kueneza taarifa za uwongo, chuki na uzushi dhidi ya mtu mwingine au taasisi kwa ajili ya malengo yao binafsi kwani kwakufanya hivyo watakuwa wanaukaribisha mkono wa sheria uweze kuwafikia na kuchukuliwa hatua.
Imetolewa na:
David A. Misime - DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania
Picha: Omary Saimon Msamo enzi za uhai wake