Jeshi la Polisi laonya wanaojichukulia Sheria mkononi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Jeshi la Polisi Nchini limesema hivi karibuni kumejitokeza tabia ya baadhi ya watu kujichukulia sheria mkononi kwa kufanya vitendo vya kihalifu ambavyo havikubaliki,


Misime11.jpg
Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari leo Februari 28, 2024 Msemaji wa Jeshi la Polisi Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime amesema Februari 21, 2024 huko mkoani Manyara, wilaya ya Babati, katika eneo la Magugu, wananchi wakifanya vurugu na kufunga barabara wakishinikiza Jeshi la Polisi liwakabidhi mtuhumiwa aliyekuwa akituhumiwa kumbaka kisha kumuua mtoto wa miaka saba.

Pia, DCP Misime amesema Febuari 27, 2024, mkoani Tanga katika wilaya ya Korogwe, eneo la Msambiazi, waendesha bodaboda waliteketeza kwa moto basi la Kampuni ya Sai Baba linalofanya safari zake Dar es Salaam Arusha baada ya basi hilo kumgonga dereva wa bodaboda ambaye alifariki Dunia.

Amesema Jeshi la Polisi nchini linatoa onyo kwa baadhi ya watu wanaojichukulia sheria mkononi kuacha tabia hiyo ambayo ni kinyume cha sheria na ukiukwaji wa misingi ya haki za binadamu.

Ameongeza kuwa Kitendo cha kuchoma basi kimedhulumu haki za watu wengine ambao hawakuhusika na tukio hilo la ajali.

Msemaji wa Jeshi hilo amesema Jeshi la Polisi linatoa wito kwa baadhi ya waendesha pikipiki za miguu miwili maarufu bodaboda kuacha tabia ya kujichukulia sheria Mkononi

Vilevile amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka wale wote waliohusika na uhalifu huo wa kuchoma basi Wilayani Korogwe ili wafikishwe katika vyombo vya sheria.

PIA SOMA
- Korogwe: Bodaboda wadaiwa kuchoma basi la Saibaba baada ya mwenzao kugongwa
 
Hapa boda boda ndipo walipoonyesha kuwa wao ni Mbu Mbu mbu according to rage

Unachoma basi unamkomoa nani Sasa

Hilo basi Lina bima ambayo itamfanya mmiliki kupata lingine

Nukuu Toka Kwa lowasa ( rip)
Elimu .......elimu ....elimu
 
Nje ya maada 😁wale wanaojichukulia Sheria mkononi kwa kukwea mnazi kwa mkono mmoja wanahusika hapa?
 
Jeshi la Polisi nchini limewaonya baadhi ya watu wenye tabia ya kujichukulia sheria mkononi kuacha tabia hiyo kwakuwa ni kinyumbe na sheria na inakiuka haki za msingi za binadamu.

Onyo hilo ni kufuatia baadhi ya bodaboda ambao hivi karibuni walichukua uamuzi wa kuchoma moto na kuliteketeza basi la abiria mali ya kampuni ya Saibaba tukio ambalo lilitokea Februari 27, 2024 mkoani Tanga katika wilaya ya Korogwe eneo la Msambiazi.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini amesema tukio la kuchoma moto basi hilo ni kudhulumu haki za watu wengine na jeshi la polisi litatumia nguvu zote kuwasaka watuhumiwa ili wafikishwe mahakamani.

Mjanja M1 ✍️
 
Unfortunately there are a few good bodaboda riders but many are holding a 'wild west theory' towards their beliefs or presence.
Many bikes don't even have registration number plates and equally don't have valid insurance (image the revenues if all had a policy)
The traffic sadly are somehow very unethical towards approaching these type of riders fearing of being knocked down etc.
Each day hundreds of bikes are being brought onto the roads. I wonder when and how will the riders be disciplined...
 
Naona watu mmekalia "bodaboda" tu, kwani wao pekee ndio hujichukulia Sheria mikononi? halafu hivyo vitendo vya kujichukulia Sheria mikononi vimeanza Leo? mbona ni miaka mingi tu yaani mtaani watu wakisikia "mwizi "

basi ni kutafuta mawe,sime,mapanga na kila aina ya silaha kwenda kumponda na kutafuta mafuta ya petroli na kiberiti !

na hayo maonyo yasiyokoma ya jeshi la Polisi tumeyachoka!

huyo kamanda aache "siasa" kwenye mambo ya kisheria,afanye kazi zake kwa mujibi wa kanuni,Sheria na taratibu
 
Back
Top Bottom