The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 3,622
- 9,301
View: https://youtu.be/a3x3e1QFasQ?si=WxGatqMY68D7RZ8v
Hili ni swali la Ansbert Gurumo kupitia Youtube Channel yake (SK Media Online TV)
Na huyu hapa 👇🏻👇🏻ni mmoja wa watazamaji wake waliotoa maoni yake akijitambulusha kuwa yeye alikuwa msimamizi wa kituo cha kupigia kura huko Shintanga, Manispaa ya Shinyanga, Kata ya Ndala, kituo cha kupigia kura ✖ akieleza kilichofanyika kwenye vituo vya kupigia kura ili kumshindisha Samia
===============================================
"....Ansbert Ngurumo mimi nilikuwa msimamizi wa kituo cha kupigia kura katika uchaguzi huu mkoa wa Shinyanga, manispaa ya Shinyanga kata ya Ndala.
Si unajiuliza Tume ya Uchaguzi wamewatoa wapi wapiga kura 32,000,000 nchi nzima waliompa ushindi wa 98% Samia? Soma kwa makini utapata jibu
Sikiliza bwana. Mpango mzima ulikuwa hivi ndugu Ansbert Ngurumo:
Matokeo tokana na wapiga kura hewa ya kura za Rais yalishaandaliwa na kupelekwa majimboni hata kabla ya siku ya uchaguzi kwa kuwatumia wasimamizi wa majimbo ya uchaguzi na wa kata kwa idadi ya kata na vituo vya kupigia kura vilivyomo kwenye maeneo yao.
Wenyewe walikuwa wanasema kila mtu alipewa target "special votes target" kwa kila jimbo, kila kata na kila kituo chakupigia kura" bila kujali wapiga kura wangekuja kupiga kura ama la. Wakati wa kujumuisha matokeo ya kura kuanzia ngazi ya kata na jimboni, sisi wasimamizi wa vituo vya kupigia kura hutukutakiwa kabisa kwenda ktk kituo cha kujumuisha matokeo ya kura na matokeo halisi ya waliopiga kura isipokuwa yale ya target ya NEC kwa kila ngazi; kata (diwani), jimbo (mbunge) na Rais..!!!.
Jimbo lilishusha matokeo hayo kwa kila kata na wasimamizi wa kata wakayapeleka kwenye kila kituo cha kupigia kura na kutulazimisha wasimamizi kutangaza hayo.
Kwa mfano, mimi kwenye kituo changu ✖ (kwa usalama wangu sitakitaja kwa sasa) nilikuwa na wapiga kura 439.
Siku hiyo ya uchaguzi tarehe 29/10 mpaka kufikia saa 10:00 jioni muda wa kufunga vituo vya kupigia kura, ni wapiga kura 32 tu kati ya 439 waliokuwa wamekuja kupiga kura.
Kabla hata ya kuanza kuhesabu hizo 32 kisha tutangaze matokeo, ikaletwa fomu za matokeo yaliyokwisha kujazwa tayari kwa diwani, mbunge na Rais na kutulazimisha wasimamizi wa kituo kugonga muhuri na kusaini na kisha kuyabandika kana kwamba ndiyo matokeo halisi ya kituo. Ilifanyika hivyo kwenye vituo vyote. Matokeo hayo ya kubumba kwa Urais, yalionesha kuwa kura zilizopigwa ni 411 na Samia ana kura 367 kwenye kituo chetu🤔🤔 na 44 waligawiwa wagombea wengine, mwenye kupata 2, 1, 3 na 0 walipewa. Hatujui hizo kura zilipigiwa wapi maana sisi ndio tuliokuwa wasimamizi wa kituo.
Nilipiga picha fomu hizo zote za matokea ya kubumba na za matokea halisi (wale 32 kati ya 439 waliopiga kura kwenye kituo chetu) na ninayo kwenye simu yangu. Siku yakihitajika na mazingira kuruhusu kuyatoa kama ushahidi, nitakuja kuyatoa. Katika zile kura za kweli, kura halisi baada ya kuzihesabu, Samia wa CCM alipata kura 08 tu na 24 ziligawanwa na wagombea wengine.
Kwa hiyo unaweza kuona kuwa,hata waliokuja kupiga kura wengi walimkataa kabisa huyu mama na bila shaka ni CCM wenzake. Hiyo ndiyo mbinu na mkakati waliotumia wahuni hawa na kusema nchi nzima wapiga kura 32,000,000 ndio walipiga kura. Ndugu Ngurumo, huo ulikuwa uchafu na uhuni mtupu na kamwe haukuwa uchaguzi. Inaumiza na kuudhi sana.
Na sielewi wao wenyewe (Emmanuel Nchimbi na Samia Suluhu Hassan) wanajisikiaje kuwa hapo walipo kwa matokeo ya uchaguzi wa uongo na udanganyifu huku wakiwa na damu za watoto, kinamama na kinababa wasio na hatia waliowaua kuhalalisha upuuzi wao. Hawa hakika, wanatembea na kuishi katikati gadhabu ya hukumu ya Mungu na ni lazima iwamalize hapa hapa duniani!..."