PostGE2025 Samia anasema wapiga kura wa CHADEMA walimpigia yeye

PostGE2025 Samia anasema wapiga kura wa CHADEMA walimpigia yeye

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,773
Reaction score
6,904
Sikusikiliza hotuba nzima ya jana kwa hiyo kila ninapopata vipande vipya napata mshangao mpya.

Katika hotuba yake ya jana, Samia aliwakosoa watu wanaoshangaa na wanaosema 98% alizopata hawezi kuwa amezipata kwa sababu mwitikio wa wapiga kura ulikuwa mdogo sana. Akasema 98% ni ya kura zilizopigwa.

Kuna mfululizo wa sentensi alioutoa katika hoja hii, moja ni kweli ila zilizofuata mmmmh...embu tupitie hoja moja baada ya nyingine.

1. Alisema 98% alizopata si za wapiga kura wote waliojiandikisha bali ni za kura zote zilizopigwa. Embu tuchukulie labda hii ni kweli maana wachache waliopiga kura wengi ni CCM. Kwa hiyo hata kama kura zilizopigwa nchi nzima ni 2300, 98% walimpa Samia. Embu tumpe hii point ingawa Tume wakazingua kwa kutuambia actually zimepigwa kura milioni 31. Tuendelee....

2. Alisema alishinda kwa kishindo kwa kuwa hakuwa na wapinzani imara na akawataja kabisa kwamba CHADEMA na ACT hawakuwepo ulingoni. Kitendo cha kukiri hivi kilinishangaza sana maana yeye anahusishwa moja kwa moja na kutokuwepo kwao katika uchaguzi. Hapa IQ inahusika.

3. Alisema wapiga kura walipiga kura asubuhi na hao walioanzisha vibe lao la maandamano saa 5 walikuta kura zimeshapigwa. Mmmhhh. Ukiacha vituo kuwa vitupu ila kuna idadi ya kutosha ya vituo vilivyoharibiwa na kura kutupwa na kuchomwa moto. Hesabu za Tume ya Uchaguzi zinaanza kuharibika.

4. Akamaliza hoja yake kwa kusema kuwa kwa sababu wapinzani wake wakubwa hawakuwepo katika uchaguzi, basi wapiga kura ambao labda wangewapigia wapinzani kina Lissu wamempigia yeye. Nilivyosikia vile nikajisemea ile video inabidi niihakiki, inaweza kuwa ni AI.

Mwisho lakini siyo kwa umuhimu, kwa takwimu zilizotolewa na Tume ya Uchaguzi, Samia alishinda kwa 84.8% ya kura zote kama wapiga kura wote waliojiandikisha wangepiga kura. Hii asilimia bado ni kubwa sana kwa mwitikio ule tuliouona na joto la kisiasa lililokuwepo nchini. Hii figure ndiyo inakosa kabisa uhalisia kuliko hata ile ya 98% ya kura zilizopigwa.

Mchana mwema.
 
Sikusikiliza hotuba nzima ya jana kwa hiyo kila ninapopata vipande vipya napata mshangao mpya.

Katika hotuba yake ya jana, Samia aliwakosoa watu wanaoshangaa na wanaosema 98% alizopata hawezi kuwa amezipata kwa sababu mwitikio wa wapiga kura ulikuwa mdogo sana. Akasema 98% ni ya kura zilizopigwa.

Kuna mfululizo wa sentensi alioutoa katika hoja hii, moja ni kweli ila zilizofuata mmmmh...embu tupitie hoja moja baada ya nyingine.

1. Alisema 98% alizopata si za wapiga kura wote waliojiandikisha bali ni za kura zote zilizopigwa. Embu tuchukulie labda hii ni kweli maana wachache waliopiga kura wengi ni CCM. Kwa hiyo hata kama kura zilizopigwa nchi nzima ni 2300, 98% walimpa Samia. Embu tumpe hii point ingawa Tume wakazingua kwa kutuambia actually zimepigwa kura milioni 31. Tuendelee....

2. Alisema alishinda kwa kishindo kwa kuwa hakuwa na wapinzani imara na akawataja kabisa kwamba CHADEMA na ACT hawakuwepo ulingoni. Kitendo cha kukiri hivi kilinishangaza sana maana yeye anahusishwa moja kwa moja na kutokuwepo kwao katika uchaguzi. Hapa IQ inahusika.

3. Alisema wapiga kura walipiga kura asubuhi na hao walioanzisha vibe lao la maandamano saa 5 walikuta kura zimeshapigwa. Mmmhhh. Ukiacha vituo kuwa vitupu ila kuna idadi ya kutosha ya vituo vilivyoharibiwa na kura kutupwa na kuchomwa moto. Hesabu za Tume ya Uchaguzi zinaanza kuharibika.

4. Akamaliza hoja yake kwa kusema kuwa kwa sababu wapinzani wake wakubwa hawakuwepo katika uchaguzi, basi wapiga kura ambao labda wangewapigia wapinzani kina Lissu wamempigia yeye. Nilivyosikia vile nikajisemea ile video inabidi niihakiki, inaweza kuwa ni AI.

Mwisho lakini siyo kwa umuhimu, kwa takwimu zilizotolewa na Tume ya Uchaguzi, Samia alishinda kwa 84.8% ya kura zote kama wapiga kura wote waliojiandikisha wangepiga kura. Hii asilimia bado ni kubwa sana kwa mwitikio ule tuliouona. Hii figure ndiyo inakosa kabisa uhalisia kuliko hata ile ya 98% ya kura zilizopigwa.

Mchana mwema.
Kukaa na kufanya analysis ya data za kipumbavu nao ni upumbavu.
 
Ukimfuatilia unagundua kuwa watanganyika tumepigwa pakubwa sana.

Can you imagine anasema wafuasi wa chadema walilipigia kura ila hapo hapo kwenye spichi yake anadai kuwa alitaka aanze mchakato wa maridhiano ila kwa sasa hawezi kuanza hadi tufanye maridhiano kwanza kwa kuwa Kuna mvurugano

Sasa unajiuliza anafanya maridhiano na nani wakati wafuasi wa chadema na wale wapinzani uchwara walilipigia kura,bna hii Ina maana Kuna ana amani
 
She is confused! Yaani mimi raia wa Tanganyika, kirahisi tu nimchague mtu kutoka nchi nyingine! Kisa tu ameweka mabango yake nchi nzima, huku akitumia kodi yangu!! Huu ujinga siwezi kuufanya hata siku moja.
 
Ni sahihi Lissu mwenyewe kule gerezani alimpigia kura Samia
 
Hayo ndio madhara ya kutokukojozwa, wanaume tujitahidi kukojoza Wanawake zetu ili wasichanganyikiwe kama huyu manyonyo
 
Ccm walimkataa tangu uteuzi, akajiteua, wakamuonyesha vifungu vya katiba yao alivyovunja na kuvikiuka, akaitisha kikao kuvirekebisha mgombea awe yeye.

Wakasema wananchi wajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura, watu hawakujitokeza,.

Nida wakasema wananchi wakajiandikishe NIDA bure, na wale wenye number waende wapewe vitambulisho bure au waseme walipo wapelekewe vitambulisho, ikawa ngumu.

Nida wakasema wana sitisha matumizi ya number za nida wakaweka na deadline haikusaidia.

Siku ya kupiga kura, hata ccm hawakujitokeza kupiga kura, watu wakaandamana kumpinga na bado waka kusanya number wakasema ni kura wakamtangaza.

Hapo utasema anaongea yeye au AI?

Alitumwa na mtandao na katekeleza.

Huna haja kutafuta scientific reason kwenye hili.

Hili wale wa PhD za siasa hata ukiandika abstract tu, unapewa PhD yako huna haja kufanya utafiti wowote.
 
Ni sahihi Lissu mwenyewe kule gerezani alimpigia kura Samia
markup_1000203681.png

Acha njaa na utapeli kwanza
Ndo uanze kusifia mafisadi
 
Back
Top Bottom