chadema

CHADEMA (Chama cha Demokrasia na Maendeleo)
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha kiasiasa nchini Tanzania ambacho kilianzishwa tarehe 28 Mei 1992 na mwanasiasa mkongwe Edwin Mtei, aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha katika miaka 1997 hadi 1979.

Mwaka 2000 CHADEMA hakikuwa na mgombea wa Urais. Mwaka 2005 mgombea wa CHADEMA Freeman Mbowe alikuwa namba tatu kati ya wagombea kumi akapata asilimia 5.88 za kura.

Mwaka 2010 CHADEMA ilipata asilimia 27.1% na mgombea Urais wa chama Wilbroad Peter Slaa na kura 4,627,923 kwa 31.75%.

Hata hivyo CHADEMA imekataa matokeo mengi kutokana na mchakato mzima kuwa mikononi mwa Tume ya Uchaguzi isiyo huru.
  1. Allen Kilewella

    Nchi inaongozwa na CCM, kwanini wanalaumiwa CHADEMA?

    Kwa ufuatiliaji wangu niliofanya kwenye mambo mbali mbali, nimegundua kwamba CHADEMA imekuwa ikilaumiwa mara nyingi kwamba haitimizi wajibu wake hadi mambo yanaharibika. Kwamfano; Wakati wa Bunge la katiba CHADEMA iliongoza vyama vingine kutoka kwenye vikao vilivyokuwa vinaendelea vya Bunge la...
  2. J

    Sijawahi kuwasikia CHADEMA wakiambatana na Waganga wa Kienyeji

    Hawa ndugu zetu wa Ufipa st Chadema wao huwa hawajihusishi na "ndumba"? Sijawahi kuwasikia wakiambatana na Waganga wa mitishamba Hata wakati ule ilikuwa wao na askofu Gwajima au askofu Malone na hata sass wanaye askofu Mwamakula na Shehe Ponda. Isijekuwa hawa jamaa ni Mpango wa Mungu kweli...
  3. Allen Kilewella

    CHADEMA wanachukia maendeleo ya Tanzania?

    Mara kadhaa imesemwa na CCM kwamba CHADEMA hupinga kila kitu/jambo linalofanywa na serikali inayoongozwa na CCM. Ina maana CHADEMA hawataki nchi yetu ipate maendeleo? Na ni kweli pia kwamba huwa wanapinga kila kitu kinachofanywa na serikali inayoongozwa na CCM?
  4. Erythrocyte

    Mbeya: Wanachama 7 wa CHADEMA walioswekwa Rumande waachiwa huru

    Wanachama Saba wa Chadema wa Mkoani Songwe waliobambikiwa Makosa ya uongo wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020, yaliyotengenezwa kinafiki na watu waoga walioshindwa hoja za majukwaani, na kurundikwa Jela kwa uonevu KWA MUDA WA ZAIDI YA MIEZI 18, Leo wameachiwa huru kutoka Jela na Mahakama Kuu kanda...
  5. The Palm Beach

    Shauri Na. 36/2022 la Halima Mdee na wenzake 18 dhidi ya CHADEMA, Spika wa Bunge la JMT & NEC. Ni nini madai yao?

    ✓ Dai lao kuu ni kuiomba mahakama ipitie mchakato wote wa CHADEMA kuanzia ndani ya KK na kisha BK wa kuwafuta/kuwafukuza uanachama ili mahakama ijiridhishe iwapo CHADEMA walifuata taratibu na sheria (katiba yao) ama laa... ✓ Wanasema, mahakama ikiona hawakutendewa haki (utaratibu haukufuatwa)...
  6. R

    Tukimbilie wapi? Mtetezi wetu CHADEMA amekaa kimya!

    Bado nina Imani kubwa na Chadema. Toa neno Mh. Mbowe katika hizi vurugu za "kudanganywa "mishahara, Kingai (mbambikaji wa kesi kupanda cheo) and many other hot issues!
  7. The Sunk Cost Fallacy

    Waziri Mkuu wa Italy ajiuzulu kufuatia maandamano. Mbona hatuoni nyuzi zikianzishwa na CHADEMA kutolea mfano Viongozi wetu kama kule Sri Lanka?

    Nawasalimu kwa jina la JMT. Waziri Mkuu wa Italy amejiuzulu nafasi yake kutokana na Maandamano ya wiki zima Kuhusu ugumu wa maisha.. Mario Draghi amewasilisha hati yake kwa Rais Ili Mchakato wa kumpata PM mwingine uendelee.. Huyu ni Waziri Mkuu wa pili kuachia ngazi huko Barani Ulaya baada ya...
  8. F

    CHADEMA nendeni na moja Kichwani

    Kuna sehemu nahisi CHADEMA hawaendi na moja Kichwani zile hesabu za darasa la pili, tatu, nne hadi la tano. Bahati mbaya mkiambiwa Ukweli huwa mnapiga kelele bila logic. Hebu CHADEMA kwa unyenyekevu niwaombe mtumie logic bila kusahau hesabu za moja Kichwani. Moja ya jambo ninaloliona halina...
  9. J

    CHADEMA sasa wawe Watu wa kupenda amani na kutotenda uhalifu, vinginevyo watamlaumu sana Kingai bila sababu!

    Nikiuangalia utatu wa DCI, DPP na Jaji Kiongozi ni dhahiri nyakati za kutenda uhalifu wa namna yoyote kwa sababu zozote zimefika ukomo. Natoa tu tahadhari kwa BAVICHA waache mihemko na Lugha za kuudhi/matusi pia watii sheria bila shuruti. Namshukuru sana Mwenyekiti Mbowe kwa kuwaonya BAVICHA...
  10. J

    CHADEMA ni kama jini lililofungiwa mfano ya kidumu, siku likibahatika kutoka hapatatosha

    Nawaza tu kwamba kama BAVICHA bado inaishi na changamoto zote wanazokutana nazo siku wakiachiwa wajinafasi kisiasa hali itakuwaje? Ni hero kuilambisha asali hivi hivi hapo tunapoteza kodi zetu.
  11. S

    Tukubali tu sasa CHADEMA imewekwa kiganjani na CCM

    Wanachezewa masharubu, hawana ule mvuto wa mwanzo sasa ni waunga juhudi wakubwa wa CCM, kinachoonekana ni michezo ya kitoto tu wenye akili wanafahamu. Naamini siasa za Tanzania ni chukua chako mapema wengine watajiju, huo ndio ukweli, halafu kutishana kumezidi zidi ili kuwavalisha uoga waTz.
  12. Monica Mgeni

    Hali ya CHADEMA katika picha muundo wa Ngalawa

  13. M

    SI KWELI Tundu Lissu na Godbless Lema Kuhudhuria vikao vya Baraza Kuu la CHADEMA

    Kumeibuka dondoo kuwa Viongozi wa CHADEMA walio nje ya nchi Tundu Lissu na Godbless Lema wanatajwa kuwemo kwenye Vikao vya Baraza kuu la Chadema vitakavyofanyika 11/5/2022 Nchini Tanzania. Aidha, inadaiwa pia wawili hao mpaka sasa wanazo tiketi mikononi mwao kwa ajili ya kuanza safari za...
  14. M

    SI KWELI CHADEMA kupeleka majina mengine ya wabunge Viti Maalum Bungeni

    MADAI Taarifa zinaenea mitandaoni kuwa CHADEMA watapeleka majina ya wabunge Viti Maalum Bungeni pamoja na kuanza kuchukua ruzuku ambayo wameigomea kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Zaidi ya hayo inadaiwa Bunge litaridhia Halima Mdee na wenzake kuondolewa bungeni baada ya kikao cha Baraza kuu...
  15. kavulata

    Kesi ya Mdee na wenzake 18 yaitia aibu CHADEMA

    Sisi wanachama wa CHADEMA tunataka kuona, kusikia na kufanya mambo yanayosaidia kujenga, kukuza na hatimaye CHADEMA kuingia ikulu. Kwa mara nyingine CHADEMA imenasa kwenye mtego wa ulimbo wa CCM. CHADEMA Inahangaika na kuwaondoa wanawake wao bungeni kwenye uchaguzi ambao cHADEMA walikataa...
  16. M

    Hakuna haja ya kumsakama Nape juu ya kukamatwa Mwaipaya. CHADEMA tambueni kuwa hakuna jinai pasipo na sheria

    Kama kweli alizua uongo acheni sheria ifuate mkondo. Japokuwa Nape sio, lakini msimsakame kama vile amefanya kwa amri zake binafsi.
  17. Getrude Mollel

    Katiba Mpya haiwezi kupatikana kabla ya 2025 na CHADEMA haitosusia Uchaguzi Mkuu

    Niliwahi kusema hapa vyama vyama vyote vya siasa vimetokana na CCM. Ni kama vile madhehebu mengine ya dini ya kikristo yalivyomeguka kutoka Katoliki. CCM ni chama kikubwa sana barani Afrika, hivyo hakuna chama hata kimoja Tanzania kinaweza kukitingisha. CCM ni kweli wamesema kwamba wanategemea...
  18. J

    Hayati Magufuli aliwapenda sana CHADEMA, vinginevyo angekifutilia mbali. Ila kwa sasa kinaweza kufutwa na Msajili wa Vyama

    Kiukweli hayati Magufuli aliwapenda sana na kuwavumilia Chadema vinginevyo mh Mutungi angekifutilia mbali. CHADEMA na viongozi wenu msipofuata agizo la mwenyekiti Mbowe kwamba muache Mihemuko, Uzushi na Uchochezi basi chama chenu hakika kinaweza kufutwa kwenye daftari la Msajili wa vyama vya...
  19. Q

    CHADEMA waondoa pingamizi dhidi ya maombi ya kina Mdee ya zuio la muda

    Baada ya Chadema kuondoa pingamizi lao, kina Mdee nao wameamua kuondoa pingamizi ambalo walikuwa wameliweka dhidi ya kiapo kinzani cha Chadema. Sasa Mahakama itaanza kusikiliza maombi ya msingi ya ridhaa ya kufungua rasmi shauri la kupinga kina Mdee kuvuliwa uanachama. KIBATALA: Maombi ya...
  20. M

    CHADEMA hamna mandate ya kumlazimisha Rais kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa

    Lack of wisdom "Bavicha tunamtaka Mh. Rais @SuluhuSamia kupitia siku ya miaka 30 ya maadhimisho ya vyama vya siasa, afute zuio batili la vyama vya upinzani kufanya mikutano ya hadhara, asipofuta sisi kuanzia tar 30.7.2022 tutaanza kufanya mikutano ya hadhara kama noma acha iwe noma. Pambalu...
Back
Top Bottom