Mbunge wa Kahama mjini ndugu Kishimba ahudhuria mkutano wa Tundu Lissu (CHADEMA) uliofanyika kata ya Isaka

Uzima Tele

JF-Expert Member
Jan 20, 2023
1,101
2,344
Screenshot_20230827-233852.png

Huyu umwonaye hapo☝️☝️☝️katikati ya umati (mwenye kapelo) ni mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini [CCM] maarufu kama Prof. Jumanne Kishimba..

Leo (kama anavyoonekana pichani alikuwa miongoni mwa maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa mwisho siku ya leo wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa ndugu Tundu Lissu katika OPERESHENI +255 KATIBA MPYA, OKOA BANDARI ZETU..

Mkutano huo ndo tu umemalizika muda si mrefu katika kata ya Isaka - Kahama ilipo bandari kavu (dry port ya Isaka iliyo chini ya TPA) ambayo nayo ni miongoni mwa walizopewa DP World..

Pamoja na uwepo wake pale, Tundu Lissu hakumkopesha hata kidogo kuhusu ushiriki wake wa kupitisha mkataba wa ugawaji wa bandari za Tanganyika Kwa waarabu wa Dubai kupitia kampuni yao ya DP World..

Video nzima ya hotuba hiyo itakujia si muda mrefu🙏
 
View attachment 2730559
Ni ajabu lakini ni kweli.

Huyu umwonaye hapo ☝️☝️juu ni mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini maarufu kama Prof. Ramadhani Kishimba...

Leo amekuwa miongoni mwa maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa mwisho siku ya leo wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa ndugu Tundu Lissu katika OPERESHENI +255 KATIBA MPYA, OKOA BANDARI ZETU..

Mkutano huo ndo tu umemalizika muda si mrefu katika kata ya Isaka - Kahama ilipo bandari kavu (dry port ya Isaka iliyo chini ya TPA) ambayo nayo ni miongoni mwa walizopewa DP World..

Pamoja na uwepo wake pale, Tundu Lissu hakumkopesha hata kidogo kuhusu ushiriki wake wa kupitisha mkataba wa ugawaji wa bandari za Tanganyika Kwa waarabu wa Dubai kupitia kampuni yao ya DP World..

Video nzima ya hotuba hiyo itakujia si muda mrefu🙏
Hotuba hii hapa

View: https://www.youtube.com/live/3bUJoIyxiqU?si=a6tCcXwFvhgm28_Q
 
Bandari na Katiba mpya ni jambo la kitaifa,

Pia nani ajuaye kuwa alikuja kuomba hisani kiaina akijua nyumba Yao itabomoka soon!!
 
Ni ajabu lakini ni kweli.
Kahama ilipo bandari kavu (dry port ya Isaka iliyo chini ya TPA) ambayo nayo ni miongoni mwa walizopewa DP World..
Sii kweli DPW hawajapewa Bandari hata moja1. Watapewa gati 3 tuu za container terminals za Bandari ya Dar
Video nzima ya hotuba hiyo itakujia si muda mrefu🙏
Asante kwa taarifa hii, tunasubiria video
kuona ni kuamini!.
P
 
Uliandika humu kuwa IGA ni kishika uchumba, inawezekana kurekebisha,

Pia ukadai Nchi inaweza kurekebisha HGA ndo mkataba wenyewe,

Unajua kuwa HGA ni Siri, na IGA ilipatikana Kwa umma ilipovujishwa!!

Kama HGA ni Siri , kwann ulikuwa mstari wa mbele kupingana na umma kurekebisha IGA ambayo ndo framework ya mikataba yote?

Huoni kuwa Kwa uliyolifanyia Taifa unastahili kuingia ktk orodha Ile ya wanahabari wenye price tags?
 
Tusikae kimya sasa kusubiri miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari, tumkosoe mapema ili akija kuandika kitabu hicho aseme nilishauriwa ila nilikataa Ushauri"-Baba Paroko wetu leo 27/08/2023
 
Huyo 2025 anajunga na chama cha uhakika wa maendeleo. Leo tarehe 27 Agosti 2023 mheshimiwa Jummane Kishimba mbunge wa CCM ahudhuria mkutano wa CHADEMA uliofanyika mji mdogo wa Isaka kulipo na bandari kavu kupata elimu ya uraia kuhusu ubovu wa mkataba bandari na masuala mengine

View: https://m.youtube.com/watch?v=kqVYQk8YOGc

Mnataka TRA waanze kumpigia hesabu za malimbikizo ya kodi tangu Uhuru ??!!😅😅😂 natania tu ! 😅🙏🙏
 
Uliandika humu kuwa IGA ni kishika uchumba, inawezekana kurekebisha,
Ni kweli Mwenye dada hakosi shemeji, IGA ni posa tu. Je, tuendelee kupiga kelele kuzozania posa, au tutulie tupange Mahari ya maana kwenye HGA?
Pia ukadai Nchi inaweza kurekebisha HGA ndo mkataba wenyewe,
Ni kweli Wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu? Ndoa ya TPA na DPW, ni Ubakaji? Wajua ubakaji unaweza kuwa alali? IGA batili yaweza kuzaa HGA halali?
Unajua kuwa HGA ni Siri, na IGA ilipatikana Kwa umma ilipovujishwa!!
Ni kweli ndio maana nimewashauri Baada ya IGA ya DPW na Bandari zetu, licha ya mapungufu, HGA yake inakuja. Ombi kwa Serikali yetu sikivu, tunaomba Maximum Transparency kwenye HGA
Kama HGA ni Siri , kwann ulikuwa mstari wa mbele kupingana na umma kurekebisha IGA ambayo ndo framework ya mikataba yote?
Jambo likiisha pitishwa na Bunge kwa kuridhiwa halirekebishiki unless ni Bunge ndio litengue Wajua japo Rais ni sehemu ya Bunge, bado hana mamlaka ya kuliingilia Bunge? Ili kufuta IGA ya DPW, Rais anapaswa kulivunja Bunge?
Huoni kuwa Kwa uliyolifanyia Taifa unastahili kuingia ktk orodha Ile ya wanahabari wenye price tags?
I have never had a price tag, ila kosa langu kubwa ni kuwa mkweli daima, na kwenye hili la DPW na Bandari zetu ukweli ni huu Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?
na huu Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?
P
 
Back
Top Bottom