Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,625
Akizungumza kupitia mjadala kwenye mtandao wa kijamii, Tundu Lissu amesema CCM wamekataa maridhiano, kwasababu CHADEMA ilipeleka mapendekezo mazuri juu ya kila kitu kinachohitajika kufanyika ili kupatikana kwa katiba mpya kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025, mapendekezo ambayo yalikataliwa yote kwa maandishi tar 30/5/2023. Tar 31 Mei CHADEMA ilitoa msimamo kuwa mazungumzo yataendelea tu iwapo Rais atabadilisha msimamo wa chama chake.
Akiongeza kuwa jambo hilo lilithibitishwa na kauli ya Waziri Ndumbaro juzi kuwa CHADEMA watakiwa kufundishwa katiba ya sasa kwa miaka mitatu ndio wazungumze habari ya katiba mpya. Akisema CCM hawataki kufanya mabadiliko yoyote wala hawataki maridiano na hivyo inabidi watafute njia nyingine za kufanya mabadiliko.
Akijibu swali kutoka kwa mchangiaji kwanini taarifa hii haijatolewa rasmi na uongozi wa chama, Lissu alisema kuwa; baada ya CCM kuwakatalia Kamati Kuu ya CHADEMA ilikaa kikao cha dharura na kuzungumzia juu ya hali hiyo, na kutoa maadhimio ya Kamati Kuu, ambapo kwenye mkutano uliofanyika Dar Mbowe aligusia kuhusu jambo hili na aliashiria juu ya maamuzi yatakayokuja kutolewa, na pia kama chama walishatoa msimamo wao kutokana na uamuzi wa CCM kukataa maridhiano na kwamba msimamo huo utangazwe na mwenyekiti wa chama kwa wananchi, hivyo Mwenyekiti akipata nafasi atato taarifa rasmi kuhusu jambo hilo.