Kwa hakika, na bila mashaka, uongozi wa Rais Samia umeonesha ushupavu. Wakati viongozi waoga huwaogopa wapinzani wao wa kisiasa, Rais Samia, bila woga, anawaweka karibu.
Tangu mfumo wa vyama vingi uanze, ni Rais Kikwete ndiye aliyekuwa anashikilia rekodi ya kukutana na viongozi wa vyama vya...
Hakuna shaka hata kidogo kuwa Taifa letu hili linahitaji mabadiliko makubwa ya kutengeneza mifumo itakayoishi na kudumu, kwa kuanzia na katiba mpya.
Kwa Katiba yetu ya sasa, mtu mmoja aitwaye Rais, kwa madaraka makubwa kupindukia aliyopewa na katiba, asipotaka, hakuna kinachoweza kufanyika...
Kwa namna tunavyoenda, hakika nchi hii tutaendelea kunung'unika na kulaumiana milele na kuwataja wenzetu wa mahali pengine Duniani wanavyosonga mbele. Sababu mojawapo kubwa ni kwamba hatutaki kuishi kwa kufuata kanuni za maendeleo ya uchumi.
Ukitaka uchumi wa nchi au hata wa kwako binafsi...
Watanzania kwa kiasi kikubwa inaingizwa hasara kubwa na makampuni ya China.
Kwa asilimia kubwa barabara nyingi zimejengwa na makampuni ya Kichina. Barabara hizi hazieleweki kama ujenzi wake haujakamilika au ulikwishakamilika, maana huku zinaendelea kujengwa, walikoanzia tayari zinakuwa kwenye...
Tanzania, kiuhalisia, tumekuwa tukifanya demokrasia ya maigizo, demokrasia iliyokosa ingridients za demokrasia. Mfumo mzima unakosa uhalali wa demokrasia ya kweli:
1) Tume ya uchaguzi inateuliwa na kiongozi wa chama, yaani Tume ya uchaguzi inateuliwa na kiongozi wa chama kimojawapo...
Kuna nchi zina kodi moja tu. Halafu kuna nchi zina sheria iliyoweka ukomo wa kodi.
Bahati mbaya sana kwa Tanzania, tuna mfumo laghai wa kodi. Serikali huweza kuwadanfanya wananchi eti imepunguza kiwango fulani cha kodi wakati kiuhalisia inakuwa imeongeza kodi.
Kwa mfano inaweza kutamka kuwa...
Hakuna mtu anayeweza kuhoji umuhimu wa sensa. Wakristo wanakumbuka, kwa kadiri ya maandiko matakatifu ya Biblia, Mama Maria na Mt. Joseph walienda Betlehem kwaajili ya sensa, ni katika tukio hillo, Yesu Kristo Masihi ndiyo anazaliwa.
Hivyo umuhimu wa sensa ulionekana hata kabla ya nyakati za...
Msingi wa kodi, tozo au ushuru ni mapato. Kutokana na mapato uliyoyaingiza, sehemu ya hayo mapato, wewe uliyeingiza unastahili kutoa sehemu ya hayo mapato kama kodi, ushuru, tozo au jina jingine lolote utakalopenda kuita lenye lengo la makato yanayyoenda kwenye mamlaka za serikali. Hii ni kanuni...
Tupo katika kipindi cha kuliponya Taifa, kutafuta maridhiano ya kitaifa, kuujenga na kuumirisha umoja wa kitaifa. Katika kufika hapo, wapo majemedari wa mstari wa mbele. Katika kufika hapo, wapo walioumia, walioteseka, waliotoa uhai, waliopotezwa, n.k.
Lakini tukitaka kuwa washindi wa kweli...
Ukiyatazama yaliyofanyika wakati wa Samia, ukiacha doa kubwa la kesi ya inayoaminika ni ya kumbambikia Mbowe na makomandoo, kuna nafasi nzuri zaidi ya kuijenga Tanzania ya haki na demokrasia, katika utawala huu wa Samia, pengine kuliko utawala wa mwingine yeyote.
Kuna mengi positive yamefanyika...
Hivi karibuni, hata bila ya kutumia ufahamu mkubwa, kuna mambo yaliyo dhahiri:
1) Polepole haamini kama Mama Samia ni mtu sahihi kwa nafasi yake kama Rais. Ukosoaji wake mkubwa ameuelekeza kwa Rais.
2) Polepole ana mashaka makubwa kuwa ama kuna siku atafikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu...
Katiba yetu inasema wazi kuwa Rais atakoma kuwa Rais mara anapofariki. Dakika ile anapofariki tu, Urais wake umeishia pale. Hafi, akiwa umeubakiza Urais nyuma kiasi cha kuweza kukasimisha kwa mtu mwingine.
Rais akifa, Katiba yetu inasema kuwa aliyekuwa Makamu wake, ataapishwa kuwa Rais. Atakuwa...
Maendeleo ya nchi yoyote na hata mtu binafsi ni mabadiliko chanya ya wakati husika, ukilinganisha na ilivyokuwa kabla ya kipindi kinachofanyiwa tathmini. Maendeleo kwa Taifa, huangalia uchumi (wa nchi na wananchi wake), demokrasia, haki na uhuru (huangaliwa sheria, mifumo na utekelezaji wake)...
Mtu mnafiki amelaaniwa Duniani na Mbinguni. Na amtegemeaye mnafiki kamwe hawezi kufanikiwa.
Kwa mujibu wa katiba, chombo cha kwanza cha kumshauri Rais ni Baraza la Mawaziri. Rais anatakiwa kujiuliza, hawa wanaounda Baraza la mawaziri ni watu wa namna gani?
Rais ili afanikiwe katika uongozi...
Katika ujenzi wa uchumi, ili uweze kufanikiwa na kusonga mbele kwa haraka ni lazima uzitambue:
Sekta wezeshi
Sekta muhimu
Sekta kipaumbele
Ukikosa uelewa huo, unaweza ukawa unapanga mipango yako, ukiamini umepanga ili kusonga mbele kumbe umepanga ili kurudi nyuma, kubakia mahali ulipo, au...
Katika Taifa moja, kuna wakati watu waliambiwa, "Taifa hili ni tajiri. Ninyi ni matajiri". Wengi wakaamini.
Wakaamini kuwa ghafla wamekuwa matajiri. Japo wengine hata kupata milo miwili ni shida, waliamini kuwa labda matajiri ndivyo wanavyoishi. Wengine japo kununua nguo mpya ni shida...
Umadhubuti wa Taifa unatokana na kukamilika kwa jamii. Ukamilifu wa Taifa unatokana na uwepo wa watu wenye fikra, uwezo, vipaji na weledi wa aina mbalimbali.
Kila mmoja katika mchanganyiko huo wa wananchi, akitumika na kuchangia kikamilifu, mchango wake ndiyo huleta maendeleo katika Taifa. Na...
Kuna hatua/kauli kadhaa ambazo Mh Rais Magufuli alizifanya/alizitamka, wengi zilitukwaza. Hazikutukwaza kwa sababu hatupendi kuzisikia bali tulijua athari zake katika uchumi wetu na maisha yetu kama wananchi tunaoipenda nchi yetu.
Sina sababu ya kuzirejea hizo hatua au zile kauli ambazo...
Sikumbuki tarehe wala kikao gani cha chama lakini nakumbuka wakati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere akisisitiza dhana ya kukosoana ndani ya chama, aliwahi kutamka, 'Kukubali upungufu huu siyo kujidhalilisha bali ni kujiimarisha'.
Mheshimiwa Rais ukitaka kuwa kiongozi mzuri, imarisha na kuikubali...
Katika baadhi ya mataifa, serikali ndiyo huwa sababu ya biashara na uchumi kushamiri. Kwa Tanzania, serikali huwa ni chanzo cha biashara na uchumi kusinyaa. Na hayo husababishwa na sera, sheria na usimamizi usio rafiki wa uchumi na biashara. Tatizo ni nini? Huenda nisiwe sahihi kwa 100% lakini...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.