Tanganyika ya 1958 Ilikuwa na Demokrasia zaidi ya Tanzania ya leo

Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,449
2,000
Maendeleo ya nchi yoyote na hata mtu binafsi ni mabadiliko chanya ya wakati husika, ukilinganisha na ilivyokuwa kabla ya kipindi kinachofanyiwa tathmini. Maendeleo kwa Taifa, huangalia uchumi (wa nchi na wananchi wake), demokrasia, haki na uhuru (huangaliwa sheria, mifumo na utekelezaji wake).

Tanganyika ilifanya uchaguzi wake wa kwanza kuwapata wajumbe wa Legislative council (sawa na Bunge la leo) mwaka 1958 kule Tabora. Uchaguzi ule, kwa jina maarufu, uliitwa uchaguzi wa Kura Tatu. Uliitwa uchaguzi wa Kura Tatu, kwa sababu kila mjumbe alitakiwa kupiga kura 3. Alitakiwa kumpigia kura mgombea mzungu, mhindi na mwafrika.

Ili kuhakikisha, wanapatikana wajumbe wanaofaa kuingia kwenye hilo Bunge la mwanzo, kwanza kuliwekwa sifa za mtu anayeruhusiwa kupiga kura:

1) Asiwe anayeweza kuhongwa au kuhongeka kiurahisi (maana yake asiuze kura). Hivyo ni lazima awe na kipato kisichopungua pauni 400 kwa mwaka.

2) Awe ni mtu mwenye uelewa wa kumtambua mgombea mwenye uwezo, anayeweza kuwakilisha vizuri. Hivyo mjumbe wa kupiga kura alitakiwa kuwa na elimu siyo chini ya darasa la 12.

3) Awe ni mtu ambaye hawezi kuhongwa kwa ahadi ya kutafutiwa kazi kama mgombea atakayempigia kura akachaguliwa. Hivyo mjumbe wa kupiga kura lazima awe na ajira rasmi. Maana yake asiwe mbangaizaji.

Kwa kutazama sifa za wajumbe wa kupiga kura, unaweza kuona kukikwa na ubaguzi wa aina fulani. Lakini kwa upande mwingine ni kwamba ulikuwa ni ubaguzi wenye dhamira njema. Ni ubaguzi uliolenga kuwapata wawakilishi wanaofaa kwa sababu anayewachagua ana uelewa wa kutosha. Leo tuna wapiga kura wanaohongwa mpaka kilo ya sukari, ubwabwa, sh 5,000, na wengine kudanganywa kuwa mgombea akichaguliwa atamtafutia kazi. Leo tuna wapiga kura ambao hawajui hata kusoma na kuandika lakini tunaamini wana uwezo wa kutambua kuwa mgombea fulani anafaa kuwa Rais au hafai!

Jambo la pili ni kwamba uchaguzi uliangalia uwakilishi wa makundi ya kijamii, kuhakikisha hakuna jamii inayoachwa kwenye uongozi. Unaweza kusema uchaguzi ulipalilia kuimarika kwa makundi ya kijamii na pengine kujenga fikra za ubaguzi wa rangi. Lakini leo, tuna ubaguzi ulio mbaya zaidi kuliko huu uchaguzi ulioendeshwa na mkoloni. Leo, kiuhalisia, ili ushiriki uongozi, ni lazima uwe mwanaCCM. Ukiwa wa chama kingine, halafu unataka kuwa kiongozi, utatengenezwa kila aina ya mizengwe na tuhuma mbaya za ajabu. Utabambikiwa kesi za uchochezi (Sugu, Lisu, Mdee, Mbowe, Zito, n.k.), wote wamewahi kubambikiwa kesi na baadaye mahakama kuthibitisha kuwa ni uwongo, na walionewa. Utabambikiwa kesi za madawa ya kulevya (Mbowe na Lisu ni mfano mzuri), kesi za ugaidi (sote tunajua). Wapo wagombea wa vyama vya uoinzani waliowahi kushambuliwa na kujeruhiwa wakati wa vipindi vya uchaguzi. Yote hiyo, indirectly ni kuambiwa hawatakiwi kushiriki kwenye uongozi. Kwa taswira hii, na kwa vigezo vya ushahidi uliopo, ina maana mkoloni mwingereza alikuwa na unafuu katika kuheshimu misingi ya demokrasia kuliko watawala wa leo ambao ni waafrika wenzetu na waafrika wenzetu.

Kwa kumbukumbu zilizopo, hakuna mgombea aliyeenguliwa na Tume ya uchaguzi mwaka 1958. Hakuna aliyepita bila kupingwa. Chaguzi za Tanzania ya leo, ni vituko, ni uchafu, ni vurumai, ni matukio ya aibu na yanayotia kinyaa kwa watu wastaarabu, wenye akili na utashi wa kibinadamu. Tume ya Mahera ilichofanya mwaka 2020, ni maajabu ya Dunia. Hakuna nchi yoyote Duniani iliyowahi kufanya uchafu wa kiwango hicho kwenye uchaguzi. Tume ya uchaguzi ya Mahera iliengua zaidi ya 50% ya wagombea wote kutoka vyama vya upinzani. Tamisemi chini ya Jafo, iliengua zaidi ya 90% ya wagombea wote kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa na vijiji. Halafu mtu bila aibu wala kinyaa, anasimama na kusema chama tawala kimepata ushindi wa kishindo. Yaani mambo ya aibu ndiyo kwayo tunasimama kujivunia na kutamba.

Kufanya matukio yanayofanyika hapa Tanzania kwenye demokrasia na haki , kwa kuzingatia mifano michache niliyoitoa, ni lazima uwe ni mtu uliyekosa ustaarabu wa kibinadamu, lazima uwe na roho ya kiharamia, lazima uwe mbumbumbu usiyejua Dunia inaenda wapi, lazima uwe ni mtu ambaye huna uzalendo kwa Tanzania na Watanzania wenzako, lazima uwe na chuki kubwa dhidi ya Watanzania wenzako.

Kwa ujumla, Taifa letu, japo watu wanafikiri tunaenda mbele, kiuhalisia kwenye maeneo mengi tumerudi nyuma:

1) kwenye demokrasia tumeporomoka ajabu. Mifano imetolewa

2) kwenye viwanda tumeporomoka. Miaka ya nyuma tulikuwa tunaunganisha malori aina ya scania pale Kibaha, leo hatuunganishi gari lolote. Tulikuwa tunaunganisha matrekta imara na ya ubora wa hali ya juu, matrekta ya Valmet, hatuunganishi hata trekta moja. Wanunuzi wa magari, zamani, karibia wote walikuwa wanaagiza magari mapya, leo karibia wote wanaonunua magari used. Zamani kuvaa nguo ya mtumba (ilikuwa inaitwa kafaulaya) ilikuwa ni aibu, leo ni ufahari. Zamani ufahari ilikuwa ni kuvaa kitenge na kanga bora zilizotengenezwa Tanzania, ukiwa na hela pungufu unavaa kanga ya India au China (za ubora duni), leo kuna bidhaa ambazo kiubora unaweza kuita takataka, kutoka China zimezagaa kila mahali. Kulikuwa na kiatu 100% leather cha Bora Shoes, leo tuna plastic za China kila mahali, halafu tunaamini kuwa tumeendelea.

3) kwenye uongozi, ndiyo balaa kabisa. Zamani ukimsikia mtu ni kiongozi, kweli ni kiongozi hasa, kuanzia haiba yake, uelewa, akili na maadili. Ukisikia DC au RC, unajua ni mtu mweledi hasa, leo tuna mpaka majambazi ni maDC, na wala sina shaka mpaka maRC, maWaziri, watakuwepo. Leo tuna maDC, maRC, maWaziri, ambao kazi yao kubwa ni kumsifia Rais. Zamani, ukisikia kesi ipo kwa Jaji, basi unajua haki itatendeka. Nani leo wa kumlinganisha na Jaji Lugakingira, Nyalali, Samatta, Augustino Ramadhani, n.k. Hawa walikuwa ni wajuzi wa sheria, wenye maadili na weledi wa hali ya juu. Kila mtu alikuwa akisikia majina yao, anataka kusikia kitakachotoka vinywani mwao. Bungeni huko, ilikuwa ukisikia Spika leo ataongea, unarekebisha ratiba yako ili usikose kusikia Spika atasema nini. Leo, wapo watakaozima TV au tu hawana hata muda wa kusikiliza kwa maana wanajua kuwa Spika zaidi ataongelea kuwasuta watu badala ya kuelezea weledi wa taasisi yake. Jaji Mkuu, alikuwa Jaji mkuu hasa. Leo unasikia Jaji mkuu akiwaagiza majaji eti wahukumu kwa kuangalia mihimili mingine inataka nini!aana yake nini? Yaani wasiangalie sheria wala misingi ya haki, bali waangalie mihimili mingine inataka nini? Maajabu makubwa!

Leo hata ile miiko ya kimaadili haipo. Majaji wanapandishwa vyeo katikati ya kesi, kesi ambayo serikali ndiyo mlalamikaji. Mlalamikaji anampandisha cheo jaji anayesikiliza kesi yake. Siyo ajabu, siku hizi mtu akiwa na kesi, haijalishi ana haki au hana, unasikia ndugu wanasema, wachangishane ili wakamwone hakimu. Na inaonekana ni jambo la kawaida.

Kama Taifa, tunapoelekea kwenye kumbukumbu ya Uhuru wa Tanganyika, tunastahili kujitafakari tunakoenda. Mungu alitupendelea, akatupatia rasilimali nyingi, tulichokosa, kwa uhakika wa 100%, ni uongozi wenye maono, uongozi unatoa njia ili watu watembee kwenye njia zilulizo sahihi. Njia za ubunifu, njia za haki, njia za demokrasia sahihi na utawala/uongozi shirikishi.

Ukiwa kiongozi haina maana una akili kuliko watu wote, una uwezo kuliko watu wote, una maono kuliko watu wote. Utambue kuwa nje ya utawala na nje ya Serikali, kuna watu kila nyanja, wapo wanaokuzidi. Kazi yako kubwa ni kutengeneza uwanja wezeshi ili hawa watu wenye uwezo mbalimbali, fani mbalimbali, vipaji na karama mbalimbali, waweze kuutumia uwanja huo kuchangia maendeleo ya jamii na Taifa. Kama hili litaendelea kutofanyiwa kazi, Tanzania, kila wakati tutakuwa watu wa kuongelea namna mataifa mengine yalivyofanikiwa.
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,728
2,000
Tupo katika zama za giza. Wakati wengine wanaenda mbele, sisi tunarudi nyuma.
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,728
2,000
Viongozi wa Tanzania, sijui ni ushetani, ujinga au uharamia maana wanayoyatenda, unaweza kuona wazi ni aheri mnyama wa pori amestaarabika kuliko hawa watawala wetu.

Sijawahi kusikia chatu kameza mwanae au chatu mwenzake. Sijawahi kusikia simba kala mwanae au simba mwenzake, sijawahi kusikia watoto wa mamba wakiliwa na mamba wakubwa. Lakini viongozi wa Tanzania wanaua watanzania wenzao, wanabambikizia kesi watanzania wenzao, wanawafunga kwa uonevu watanzania wenzao, wanawashambulia kwa risasi watanzania wenzao. Kama ni hivyo, viongozi wa Tanzania wakilinganishwa na hawa wanyama niliowataja, nani kastaarabika zaidi?
 

pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
13,385
2,000
Lakini viongozi wa Tanzania wanaua watanzania wenzao, wanabambikizia kesi watanzania wenzao, wanawafunga kwa uonevu watanzania wenzao, wanawashambulia kwa risasi watanzania wenzao. Kama ni hivyo, viongozi wa Tanzania wakilinganishwa na hawa wanyama niliowataja, nani kastaarabika zaidi?
Hii kitu ndio inatuumiza sana sana Tz kiasi kwamba hatuamini kama hawa wenzetu ni binadamu wa kawaida!
 

Ushindi victory

JF-Expert Member
Dec 11, 2018
775
1,000
ni heri ya mkoloni mweupe kuliko mweusi
we mwehu kwel, hv u awajua watu weupe ww? ama unaandika takataka hum sabbu ya chuki, mkolon mweupe unamjua wew? unajua madhira waliyotendewa babu zetu mpka uone hao weups wana ubora, hizo chuki zenu ztakuja kuwaponza
 

Ushindi victory

JF-Expert Member
Dec 11, 2018
775
1,000
wananch wanahitaj maendeleo na sio hayo mademokrasia yakipuuzi, demokrasi mnazihitaji ninyi wanasiasa kwaajil ya maslahi yenu na kugombea keki ya taifa kwenye nyazifa mbalimbali.

demokrasia si kigezo cha maendeleo na haitowai kuwa kigezo cha maendeleo, bali ni chachu ya usawa kwa wanasiasa ktk vyama tofaut kupata chance ya kufaid mema ya nchi pekeyao, ndiomaana utawasikia wale wanaodai katiba na tume huru ya uchaguz, haya yote wanayadai ilkupata nafasi serkalin wakatumbue kodi za wananchi

nyie wapuuzi mnaosifia utawala wa kidemokrasia kabla ya uhuru mtakuwa hna akil na hamjui jinsi gan babu zetu waliteseka mpka kugombania uhuru, hiyo demokrasia ingekuwa bora, wasingeutaka uhuru,

Asili ya afrika ni uongoz wa kidicteta&kifalme tu, ili kuleta matokeo chanya, hizo demokrasia mnazolilia ni mifumo ya hao weupe sio waafrika
 

Nas Jr

JF-Expert Member
May 15, 2018
5,347
2,000
Sijawahi kusikia chatu kameza mwanae au chatu mwenzake. Sijawahi kusikia simba kala mwanae au simba mwenzake, sijawahi kusikia watoto wa mamba wakiliwa na mamba wakubwa. Lakini viongozi wa Tanzania wanaua watanzania wenzao, wanabambikizia kesi watanzania wenzao, wanawafunga kwa uonevu watanzania wenzao, wanawashambulia kwa risasi watanzania wenzao
Nchi hii bhana.
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
2,728
2,000
wananch wanahitaj maendeleo na sio hayo mademokrasia yakipuuzi, demokrasi mnazihitaji ninyi wanasiasa kwaajil ya maslahi yenu na kugombea keki ya taifa kwenye nyazifa mbalimbali.

demokrasia si kigezo cha maendeleo na haitowai kuwa kigezo cha maendeleo, bali ni chachu ya usawa kwa wanasiasa ktk vyama tofaut kupata chance ya kufaid mema ya nchi pekeyao, ndiomaana utawasikia wale wanaodai katiba na tume huru ya uchaguz, haya yote wanayadai ilkupata nafasi serkalin wakatumbue kodi za wananchi

nyie wapuuzi mnaosifia utawala wa kidemokrasia kabla ya uhuru mtakuwa hna akil na hamjui jinsi gan babu zetu waliteseka mpka kugombania uhuru, hiyo demokrasia ingekuwa bora, wasingeutaka uhuru,

Asili ya afrika ni uongoz wa kidicteta&kifalme tu, ili kuleta matokeo chanya, hizo demokrasia mnazolilia ni mifumo ya hao weupe sio waafrika
Wewe sijui utaenda kujielimisha wapi! Maana hata elimu ya watu wazima siku hizi imefutwa. Huelewi hata maana ya maendeleo. Huelewi components za maendeleo, unafikiri ukila tu kisamvu na ugali ukashiba, ukanywa maji, basi umeendelea. Kama ni hivyo, basi nyani wa kule Selou, ana maendeleo kukuzidi wewe. Anakula nyasi mpaka anasaza, anakunywa maji ya mto Rufiji hata asijue yaliyobakia afanyie nini. Nyasi anazokula nyingine ni tiba kwake. Mapori na vichaka vyote ni mali na nyumba zake. Huyo, kwa tafsiri yako ya maendeleo, si ameendelea kuliko wewe?
 

dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
5,358
2,000
we mwehu kwel, hv u awajua watu weupe ww? ama unaandika takataka hum sabbu ya chuki, mkolon mweupe unamjua wew? unajua madhira waliyotendewa babu zetu mpka uone hao weups wana ubora, hizo chuki zenu ztakuja kuwaponza

babu yako alifanywa nini ? una ushahidi wowote? acha kukariri ndugu, tuishia kwenye uhalisia, CCM wanatutesa, wanatuua, wanatunyanyasa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom