Tanzania ya Maridhiano ni Ushindi wa Watanzania

Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,649
2,911
Tupo katika kipindi cha kuliponya Taifa, kutafuta maridhiano ya kitaifa, kuujenga na kuumirisha umoja wa kitaifa. Katika kufika hapo, wapo majemedari wa mstari wa mbele. Katika kufika hapo, wapo walioumia, walioteseka, waliotoa uhai, waliopotezwa, n.k.

Lakini tukitaka kuwa washindi wa kweli, tusamehe bila kusahau, tuaminiane, kuna wakati pande zilizokuwa zinasigana, kila upande ujishushe ili kuwa katika level nzuri. Najua kuna hardliners pande zote - CCM na CHADEMA. Lakini ukweli ni kwamba, kama kila upande ukishikilia msimamo wake katika mambo inayoyataka, na kutaka kupata yote kwa 100% kwa muda unaotaka, kwa wakati unaotaka, na kwa namna uunavyotaka, hatushindi.

Nchi imefika katika hatua nzuri. Watanzania, kila siku tunazidi kupata points 3, na katika haya mapambano, tuna majemedari waliokaa mbele kutuongoza, ni Rais wetu Mh. Rais Samia na Mh. Freeman Mbowe (pole sana kwa mateso, lakini ufurahi kwa kuwa umeteseka kwaajili ya watanzania. Ni sawa na mama anayelia kwa uchungu wa operation ya uzazi, lakini umwonapo mtoto, huyasahau mateso yake, na kufurahia ujio wa mwanae. Mungu akujalie ujasiri ya kuyapokea uliyoyapitia kwa moyo wa hekima).

Mh. Rais Samia na Mh. Freeman Mbowe, ninyi ni dira. Mkisimama pamoja kwaajili ya lengo moja la kutaka kuijenga Tanzania ya ushindani lakini inayozingatia umoja, upendo, na uzalendo kwa Taifa na watu wake, walio nyuma yenu, nao hakika watatembea katika njia yenu.

Watanzania tumechoshwa na siasa zisizo na tija, siasa za kukomoana, siasa za hila, siasa za chuki, tunataka mawazo kinzani lakini yasiyoondoa upendo miongoni mwetu, umoja miongoni mwetu, na uzalendo kwa Taifa letu. Kwa upande wa Rais Samia na CCM,
nahitaji sana hekima kwa sababu mna dola. Ni rahisi sana kwenu kukosa hekima na kutumia nguvu za dola, kwa sababu mamlaka, hupofushwa, lakini mkiwa na hekima, dola itawapa nafasi nzuri zaidi ya kuyapata mawazo chanya ya kulijenga Taifa la mfano, na ndicho tunachokitaka tulio wengi.

Mungu aliye chanzo cha kila jema, tunakuomba uwajaze hekima waliopata nafasi ya kuwa viongozi ili walitazame zaidi Taifa kuliko vyama na nafsi zao. Viongozi wetu wanaposimama kwaajili ya yaliyo mema kwa Taifa letu, uwajaze ujasiri wa kutokubali kuyumbishwa na mawakala wa ibilisi, wanaofurahia Tanzania ya uonevu na utengano.
 
Unazungumza sana lugha ya upendo umoja na mshikamano lakini kamwe sioni haki,
Lazima tuanze kupigania mabadiriko ya sheria ovu na kuongeza thamani ya haki kwa kutunga sheria rafiki.

Ni vyema ukajua kwamba chama cha mapinduzi nia yao kuu ni kuona vyama vingine havikui na vinabaki havina uelekeo.

Lakini chadema sasa ni chama kilichokua ushahahidi ni namna wanavyo kitreat tofauti na vyama vingine.

Na namna gani kila kukicha ugomvi wao ni chadema? Huwezi kupigana na mnyonge siku zote utapigani na yule anayekutosha.

Na lengo la Chadema kama chama cha siasa sio kupamba magazeti kwa maridhiano ni kushika dola.
Kwa hiyo huo umoja na maridhiano haupo kama hakuna haki katika kuendesha vyama na chaguzi
 
Unazungumza sana lugha ya upendo umoja na mshikamano lakini kamwe sioni haki,
Lazima tuanze kupigania mabadiriko ya sheria ovu na kuongeza thamani ya haki kwa kutunga sheria rafiki.

Ni vyema ukajua kwamba chama cha mapinduzi nia yao kuu ni kuona vyama vingine havikui na vinabaki havina uelekeo.

Lakini chadema sasa ni chama kilichokua ushahahidi ni namna wanavyo kitreat tofauti na vyama vingine.

Na namna gani kila kukicha ugomvi wao ni chadema? Huwezi kupigana na mnyonge siku zote utapigani na yule anayekutosha.

Na lengo la Chadema kama chama cha siasa sio kupamba magazeti kwa maridhiano ni kushika dola.
Kwa hiyo huo umoja na maridhiano haupo kama hakuna haki katika kuendesha vyama na chaguzi
Umenena vema. Na wala sipo tofauti nawe. Ni suala la nini kinaanza, haki au upendo. Kwangu mimi, naamini dhuluma, fitina, sheria gandamizi, ni matokeo ya kukosekana upendo na umoja.

Kama mnapendana na mna umoja, mtatunga sheria zinaxozingatia haki kwa sababu unataka sheria hizo ziwaongoze watu kwa njia ya haki.

Kama hakuja upendo wala umoja, hila hutawala. Watu watajitahidi kuweka sheria zenye hila ndani yake ili kuwagandamiza wengine na kuwapendelea kundi fulani.

CCM wakiwa na upendo, wakaamini kuwa sote ni watanzania, wakaamini kuwa mtu yeyote anaweza kuwa kiongozi alimradi umma umetaka, hawatahangaika kutunga sheria gandamizi au kutengeneza mifumo ya uchaguzi yenye hila ndani yake kwa nia ya kudhulumu ushindi wa wapinzani wao.

Tukienda kutengeneza sheria, tukiwa na chuki miongoni mwetu, hatuwezi kutengeneza sheria nzuri za kusimamia haki, demokrasia na uhuru wa maoni wa kila raia.
 
Yaani CCM wafanye hivyo??????
Hakuja aliye na nadhiri ya uovu, usipokuwa shetani pekee yake.

Hawa watu waliokuwa wanateka,wanatesa na kuua wenzao, hawakufanya vile kama wao bali ni mashetani yaliyokuwa na sura za binadamu.

Hata haya ambayo yamekuwa yanashangilia mateso na mashambulio yenye lengo la kumwua Tundu Lisu, yale yote ni mashetani ambayo yanaishi katika maumbile ya wanadamu.

Shetani anayeishi ndani yao, akiwatoka, utashangaa watakavyoujutia uovu wao. Kumbuka kuna nyakati shetani alijishikamanisha kabisa na mkuu wa ikulu, nchi yote ikaishi katika ushetani.
 
Back
Top Bottom