Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,646
- 2,911
Kwa namna tunavyoenda, hakika nchi hii tutaendelea kunung'unika na kulaumiana milele na kuwataja wenzetu wa mahali pengine Duniani wanavyosonga mbele. Sababu mojawapo kubwa ni kwamba hatutaki kuishi kwa kufuata kanuni za maendeleo ya uchumi.
Ukitaka uchumi wa nchi au hata wa kwako binafsi uboreke, ni lazima uzingatie kanuni za uchumi, na facts ambazo zipo, na ambazo wakati fulani huna uwezo wa kuzibadilisha mara moja.
Kununi Kuu:
Ili uondoke kwenye umaskini/uwe tajiri ni lazima uzalishaji uzidi matumizi.
Hii ina maana kuwa unaweza kubakia na matumizi yako palepale lakini ukaongeza uzalishaji. Au ukabakia na uzalishaji wako ule ule lakini ukapunguza matumizi. Lakini utapiga hatua kwa kasi zaidi kama utaweza kuongeza uzalishaji na wakati huo huo ukapunguza matumizi.
Fact Specific kwa Tanzania
Tanzania ni miongoni mwa nchi 5 Duniani zinazoongoza katika ukuaji wa ongezeko la watu. Huu ni mtihani mkubwa. Hii ina maana, mathalani kama ongezeko letu kwa mwaka ni 3%, uchumi ukakua kwa 3%, hakuna mabadiliko yatakayoonekana. Kama uchumi utakua kwa 2.5%, kadiri miaka itakavyoenda ndivyo mtakavyozidi kuwa maskini zaidi. Kama tunataka kuwe na ongezeko halisi la maendeleo ya uchumi kwa maana ya maendeleo ya watu na ubora wa huduma kwa kiwango cha 5% basi ina maana uchumi ukue kwa 8%. Ikiwa na maana kuwa ongezeko la 3% litaliwa na ongezeko la watu, na ongezeko linaloenda kwenye kuboresha uchumi wa watu na nchi ni 5% tu. Hii hali ndiyo inayosababisha, mwaka huu mnajisifu tumejenga madarasa mengi ya kutosheleza wanafunzi wote, baada ya miaka 5, kuna crisis kubwa ya kukosekana vyumba vya madarasa.
NCHI IMEFUNGWA MSHIPI, SERIKALI INAOGELEA KWENYE ANASA
Kwenye kanuni ya kuondokana na umaskini, hapo juu nimeeleza kuwa ili kuweza kusonga mbele haraka ni lazima uongeze uzalishaji na upunguze matumizi, hasa ya anasa. Tujiulize:
1) Sisi, ukuaji wa uzalishaji wetu unaongezeka kwenye sekta zipi na ni kwa kiasi gani?
2) Kwa upande wa Serikali ni matumizi gani ya anasa mnayoyapunguza? Hivi Waziri akisafiri na gari aina ya prado ya sh milioni 100, na akasafiri kwa gari Landcruizer new model ya sh milioni 600, uwaziri wake unabadilika? Au akisafiri kwenye hilo gari la kifahari huko aendako atawapelekea maendeleo zaidi? Serikali inaonesha mfano mbaya kabisa kwenye matumizi, kwa kuendekeza matumizi ya anasa.
3) Kwa upande wa Serikali, katika muundo wake, kweli ni lazima kuwa na ofisi zote tulizo nazo? Hizo ofisi zinatuongezea matumizi kiasi gani tulinganishe na kile ambacho tutakikosa tukiziondoa, tukizipunguza au kuziunganisha? Hivi kamati za ulinzi na usalama zikiwa chini ya OCD pale Wilayani, na chini ya RPC pale mkoani, tukawaondoa wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa (pamoja na wasaidizi wao), ambao tunaambiwa kazi yao kubwa eti ni wenyeviti wa kamati za Ulinzi na usalama, tutapungukiwa na nini?
WITO
Kwa kuwa ni dhahiri Serikali inashindwa kudhibiti matumizi yake, ni vema sasa tupiganie kupata katiba mpya haraka, na kwenye katiba hiyo iwekwe wazi kuwa wakati wote, matumizi ya kawaida ya Serikali hayatazidi 50% ya mapato. Hii itamaanisha si chini ya 50% ya mapato itaenda kwenye maendeleo badala ya kwenda kwenye kununua magari ya kifahari, kulipana posho na kuongeza ofisi za utawala.
Kama mwananchi wa kawaida mwenye mshahara wa shilingi laki 5 anavyojibana ili ajenge nyumba yake, ni lazima na Serikali ya nchi maskini kama ya kwetu ifanye vivyo hivyo.
Uzalishaji hata kama utaongezeka kiasi gani, kama matumizi ya Serikali yasiyo ya lazima yatazidi na yenyewe kupaa, hakuna mabadiliko ya wazi ya haraka yatakayoonekana.
Katiba Mpya isiangalie tu mambo ya uchaguzi bali zaidi iangalie namna ya kuidhibiti na kuielekeza Serikali ili uwepo wake uwe ni kuisaidia nchi kusonga mbele haraka na kuwapa matumaini wananchi.