Tozo zinaweza kugeuka na kuwa wizi wa dola dhidi ya Wananchi

Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,649
2,911
Msingi wa kodi, tozo au ushuru ni mapato. Kutokana na mapato uliyoyaingiza, sehemu ya hayo mapato, wewe uliyeingiza unastahili kutoa sehemu ya hayo mapato kama kodi, ushuru, tozo au jina jingine lolote utakalopenda kuita lenye lengo la makato yanayyoenda kwenye mamlaka za serikali. Hii ni kanuni mama ya kodi.

Kanuni kuu ya pili, mapato yaliyokwishalipiwa kodi, tozo au ushuru hayastahili kulipishwa tena kwa mara ya pili. Double taxation inazuiwa.

Wizi ni kuchukua kitu chochote ambacho siyo stahili yako. Wizi huu unaweza kuwa wa mtu mmoja dhidi ya Serikali, taasisi, mtu mwingine au kikundi au serikali dhidi ya wananchi wake au dhidi ya mwananchi mmoja.

Serikali inapomtoza mwananchi kodi zaidi ya kiwango halali au zaidi ya mara moja kwa mapato yale yale, huo ni wizi wa dola dhidi ya mwananchi.

Maswali muhimu ya kujiuliza:

1) Kwa mfano, mfanyakazi au mfanya biashara amepata mshahara au pesa ya mauzo, ameilipia kodi tayari, ikawekwa benki, benki amelipia gharama ya huduma, na benki inalipa kodi kwa mapato yanayotokana na utoaji huduma, huyu mteja anapotaka kuichukua pesa yake, akatozwa tena na serikali, ni mapato gani ameyapata kule benki?

2) Kwa mfano, mfanyakazi, kwenye mshahara wake amekatwa PAYE, pesa imeenda benki, anatoa kwenye ATM, anakatwa kodi kwa mara ya pili, anaweka kwenye simu, pesa ile ile anaituma kwa mama yake kijijini anakatwa kodi, mama yake anaenda kwa wakala kuchukua ile pesa, anakatwa kodi.

Pesa siyo chakula, lazima huyu mama ataitumia, anaenda kununua chumvi anakatwa kodi. Yaani makato mara 5 kwa mapato yale yale, hii ni halali? Lakini ikumbukwe kwamba, benki kutokana na mapato yake yanayotokana na utoaji huduma imekatwa kodi, mtandao wa simu kutokana na mapato ya utoaji huduma ya usafirishaji fedha, nao umekatwa kodi, na muuzaji wa chumvi naye amekatwa kodi.

Tax regime ya Tanzania ni lazima iangaliwe upya. Siyo regime rafiki kwa wananchi wala wawekezaji.

Siku zote kodi utitiri au kubwa huua uwekezaji. Hakuna nchi hata moja duniani iliyokuwa maskini ambayo iligeuka kuwa tajiri kwa haraka kwa kuwa na kodi utititiri au kodi kubwa.

Dubai, ilipata maendeleo makubwa, na kubadilika kabisa ndani ya miaka 15 tu kwa kufuta kabisa kodi nyingi na kubakia na kodi chache sana. Mpaka leo Dubai ni kituo cha biashara duniani.

Anayehamasisha Tanzania kuwa na kodi utitiri na kodi kubwa ni adui mkubwa wa maendeleo ya nchi yetu.

Nchi hii inahitaji sana uwekezaji ili watu wetu wapate ajira, na serikali iwe na vyanzo vingi vya mapato, na siyo kuongeza kodi kwa vyanzo vile vile.

Wazalendo wa nchi hii, wanaoitakia mema Tanzania tukatae mambo yote yanayoua uwekezaji katika taifa letu.

Tukiwa na sera na sheria ambayo inachochea uwekezaji kivitendo, kama uwekezaji utasababisha japo watanzania milioni 15 kupata ajira za uhakika, na hao milioni 15 angalau kila mmoja kwa wastani akalipa kodi ya sh milioni 4 kwa mwaka, PAYE pekee yake itaipatia Serikali 4,000,000×15,000,000 = 60,000,000,000,000 (trillion 60).

Haya ni mapato ambayo ni karibu 50% ya makusanyo ya serikali kwa sasa. Na haya ni mapato ambayo serikali itayapata, na huku mlipa kodi akifurahi kwa kuwa ana ajira inayompa kipato cha uhakika.
 
Mkuu umenena vyema kabisa, just imagine;
Pesa ukipata inakatwa kodi na TRA
Ukipeleka bank inakatwa kodi ya banki.
ukitoa unakatwa kodi
Ukimtumia baba yako kijijini unakatwa kodi (hapa zipo utitiri wa kodi)
B
aba yako akienda kwa wakala kutoa anakatwa kodi!
Hivyo hivyo kwa wafanyakazi
Mshahara unatwa kodi (PAYEE)
ukipelekwa bank unakatwa kodi!
akienda kutoa unakatwa kodi!
Wanachi "tusipoamka" tutarajie hadi kodi ya kupumua
 
Msingi wa kodi, tozo au ushuru ni mapato. Kutokana na mapato uliyoyaingiza, sehemu ya hayo mapato, wewe uliyeingiza unastahili kutoa sehemu ya hayo mapato kama kodi, ushuru, tozo au jina jingine lolote utakalopenda kuita lenye lengo la makato yanayyoenda kwenye mamlaka za Serikali. Hii ni kanuni mama ya kodi.

Kanuni kuu ya pili, mapato yalikwishalipiwa kodi, tozo au ushuru hayastahili kulipishwa tena kwa mara ya pili. Double taxation inazuiwa.

Wizi ni kuchukua kitu chochote ambacho siyo stahili yako. Wizi huu unaweza kuwa wa mtu mmoja dhidi ya Serikali, taasisi, mtu mwingine au kikundi au Serikali dhidi ya wananchi wake au dhidi ya mwananchi mmoja.

Serikali inapomtoza mwananchi kodi zaidi ya kiwango halali au zaidi ya mara moja kwa mapato yale yale, huo ni wizi wa dola dhidi ya mwananchi.

Maswali muhimu ya kujiuliza:

1) Kwa mfano, mfanyakazi au mfanyabiashara amepata mshahara au pesa ya mauzo, ameilipua kodi tayari, ikawekwa benki, benk amelipia gharama ya huduma, na benki inalipa kodi kwa mapato yanayotokana na utoaji huduma, huyu mteja anapotaka kuichukua pesa yake, akatozwa tena na Serikali, ni mapato gani ameyapata kule benki?

2) Kwa mfano, mfanyakazi, kwenye mshahara wake amekatwa PAYE, pesa imeenda benki, anatoa kwenye ATM, anakatwa kodi kwa mara ya pili, anaweka kwenye simu, pesa ile ile anaituma kwa mama yake kijijini anakatwa kodi, mama yake anaenda kwa wakala kuchukua ile pesa, anakatwa kodi. Pesa siyo chakula, lazima huyu mama ataitumia, anaenda kununua chumvi anakatwa kodi. Yaani makato mara 5 kwa mapato yale yale, hii ni halali? Lakini ikumbukwe kwamba, benki kutokana na mapato yake yanayotokana na utoaji huduma imekatwa kodi, mtandao wa simu kutokana na mapato ya utoaji huduma ya usafirishaji fedha, nao umekatwa kodi, na muuzaji wa chumvi naye amekatwa kodi.

Tax regime ya Tanzania ni lazima iangaliwe upya. Siyo regime rafiki kwa wananchi wala wawekezaji.

Siku zote kodi utitiri au kubwa huua uwekezaji. Hakuna nchi hata moja Duniani iliyokuwa maskini ambayo iligeuka kuwa tajiri kwa haraka kwa kuwa na kodi utititiri au kodi kubwa.

Dubai, ilipata maendeleo makubwa, na kubadilika kabisa ndani ya miaka 15 tu kwa kufuta kabisa kodi nyingi na kubakia na kodi chache sana. Mpaka leo Dubai ni kituo cha biashara Duniani.

Anayehamasisha Tanzania kuwa na kodi utitiri na kodi kubwa ni adui mkubwa wa maendeleo ya nchi yetu. Nchi hii inahitaji sana uwekezaji ili watu wetu wapate ajira, na Serikali iwe na vyanzo vingi vya mapato, na siyo kuongeza kodi kwa vyanzo vile vile.

Wazalendo wa nchi hii, wanaoitakia mema Tanzania tukatae mambo yote yanayoua uwekezaji katika Taifa letu.

Tukiwa na sera na sheria ambayo inachochea uwekezaji kivitendo, kama uwekezaji utasababisha japo watanzania milioni 15 kupata ajira za uhakika, na hao milioni 15 angalao kila mmoja kwa wastani akalipa kodi ya sh milioni 4 kwa mwaka, PAYE pekee yake itaipatia Serikali 4,000,000×15,000,000 = 60,000,000,000,000 (trillion 60). Haya ni mapato ambayo ni karibu 50% ya makusanyo ya Serikali kwa sasa. Na haya ni mapato ambayo Serikali itayapata, na huku mlipa kodi akifurahi kwa kuwa ana ajira inayompa kipato cha uhakika.

Wizi plus uporaji uliopitiliza
 
Hiyo dola ikiiba then pesa inazipeleka wapi? Kununua wapinzani njaa au?
 
Kwahiyo sasa hivi mmeacha kuwaibia matajiri ili kuendesha miradi na sasa mnawaibia masikini?
Kodi ya miamala ni ya haki kwa wote uwe Tajiri au uwe maskini na infact tajiri ndio analipa zaidi maana ana transact zaidi kuliko maskini..

Kanuni ya Kodi ni fairness
 
Sasa maoni yako ni yapi kutokana na mada ya kwenye huu uzi.
Kodi au tozo haziwahi kuwa wizi ndio maana nilikuuliza kama ni wizi hizi pesa zinaenda kutumika wapi? Hukujibu..pesa inatumika kuboresha huduma mbalimbali kama hizi 👇
 
Attachments

  • 20220801_081022.jpg
    20220801_081022.jpg
    89.1 KB · Views: 5
  • 20220801_081121.jpg
    20220801_081121.jpg
    58.1 KB · Views: 4
  • Screenshot_20220818-190357.png
    Screenshot_20220818-190357.png
    93.1 KB · Views: 4
  • Screenshot_20220816-203211.png
    Screenshot_20220816-203211.png
    87.3 KB · Views: 5
Back
Top Bottom