Mabadiliko Makubwa yanahitajika. Rais Samia 2025 apitishwe ili Kusimamia Mabadiliko

Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,649
2,911
Hakuna shaka hata kidogo kuwa Taifa letu hili linahitaji mabadiliko makubwa ya kutengeneza mifumo itakayoishi na kudumu, kwa kuanzia na katiba mpya.

Kwa Katiba yetu ya sasa, mtu mmoja aitwaye Rais, kwa madaraka makubwa kupindukia aliyopewa na katiba, asipotaka, hakuna kinachoweza kufanyika. Watanzania, kwa asili yetu, siyo watu wa kupigania kile tunachokitaka kwa dhamira na nguvu zetu zote.

Ukweli wa mamlaka ya Rais na uduni wa nafasi ya umma katika maamuzi ilidhihirika kwa uwazi zaidi wakati wa awamu ya 5, licha ya manung'uniko mengi lakini hakuna aliyekohoa. Wachache walio na ujasiri, kama Tundu Lisu, waliishia kupigwa risasi kama mnyama mharibifu. Watu waliporwa pesa zao, wakarundikwa magerezani, wengine walitekwa na baadaye kutupwa, wote tukabakia kimya.

Makubwa yaliyodhihirika katika madhira yale ni kuwa:

Rais yupo juu ya kila kitu. Yupo juu ya katiba, juu ya sheria na juu ya mihimili yote. Kwetu hapa, Rais kukutendea haki, zaidi ni kutokana na uungwana wake, siyo kwa sababu amelazimishwa na mifumo ya utawala.

HOJA KUU
Ili kutengeneza katiba mpya, na hata kuweza kuunda mifumo imara ya utawala, kusimamia demokrasia, uhuru wa maoni, uhuru wa vyombo vya habari, ni lazima Rais awe muungwana sana, mwenye mapenzi mema kwa Taifa lake na watu wake, mtu ambaye analiweka Taifa juu hata ya Urais wake.

Maadam Rais Samia ameonesha sifa hizi, ni vema Taifa likatamka kupitia asasi mbalimbali za kiraia, za kidini, vyama vya siasa, kuwa tunamtaka na kumwomba asimamie mabadiliko haya makubwa yatakayoweka misingi imara ya Taifa letu. Na sisi wananchi tusioangukia kwenye asasi yoyote, tuunge mkono. Kwa maneno mengine, tutamke kuwa Rais Samia aungwe mkono na asasi zote, pamoja na vyama vya upinzani kuwa, kwa mapenzi ya Mungu, Rais Samia aendelee kuwa Rais mpaka 2030, huku mwaka 2025 akipigiwa kura za ndiyo na hapana kwa lengo tu la kudumisha misingi ya demokrasia.

Tukikosa kufanya mabadiliko ya kuwezesha nchi kuwa na mifumo imara na mizuri katika kipindi hiki, huko mbeleni kutakuwa ni vigumu zaidi, na hasa tukija kuwapata marais wale wanaosema hawataki ushauri, na mkimshauri ndiyo mmeharibu kabisa.
 
Back
Top Bottom