Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,649
- 2,911
Katika baadhi ya mataifa, serikali ndiyo huwa sababu ya biashara na uchumi kushamiri. Kwa Tanzania, serikali huwa ni chanzo cha biashara na uchumi kusinyaa. Na hayo husababishwa na sera, sheria na usimamizi usio rafiki wa uchumi na biashara. Tatizo ni nini? Huenda nisiwe sahihi kwa 100% lakini ninaamini kwa kiasi kikubwa kuwa uchumi na biashara kwa tanzania unasimamiwa na watu wasioujua uchumi wala biashara.
Kwa Tanzania, anayeujua uchumi na biashara ni mtu mwenye vyeti vingi au hata PhD za kusomea uchumi na biashara. Hii inaweza pia kuwa ni sababu kubwa hata Rais wetu leo hii kuwajaza maprofesa na madaktari kwenye serikali yake akiamini kuwa atapata ufanisi. Kitu ambacho amesahau kuwa unaweza kuwa na maprofesa na madaktari wenye vyeti vingi vya biashara na uchumi lakini wasiojua uchumi wala biashara. Kuna watu wanaujua uchumi na biashara, kwa vile wanauishi uchumi na biashara, wanatenda/wanafanya shughuli za uchumi na biashara, wanauchunguza uchumi na biashara kila siku, na maisha yao yamejaa mafanikio katika uchumi na biashara. Ili kuyajua wanaoyajua hawa wanauchumi na wafanyabiashara halisi, wataalam nadharia wa uchumi na biashara (professors na PhD holders), wanalazimika kuingia darasanai kujifunza nadharia ambayo wachumi na wafanyabiashara halisi wanaishi na kuifanyia kazi.
Serikali ya Tanzania haijawahi kufanikiwa kwa lolote katika miradi ya uchumi na biashara lakini bado inaamini ina uwezo thabiti katika nyanja hizo. Serikali kwa kipindi kirefu imethibitisha pasipo hata chembe ya mashaka kuwa haiwezi kusimamia na kuendesha mradi wowote wa kibiashara na kiuchumi.
Serikali ya Tanzania inatakiwa iache masuala yote ya kibiashara na kiuchumi kwa sekta binafsi, na wasiingilie kama wanavyofanya hivi sasa. Hii inatokana na ukweli tuliopata kwa kipindi kirefu. Baadhi hapa chini ni mifano tu:
1) Migodi
Serikali ya Tanzania iliitafisha migodi ya madini yote toka kwa makampuni binafsi miaka ya sitini baada ya Azimio la Arusha. Baada ya hapo migodi ya dhahabu, Mica, Lead, Copper na Zinc, chini ya STAMICO, yote ilikufa. Mpaka miaka ya 1990, Tanzania ilikuwa inauza dhahabu inayochokonolewa na wachimbaji wadogo tu. Migodi ya serikali ilikuwa haizalishi hata kilo 1 ya dhahabu. Ni makampuni binafsi walioitoa Tanzania kutoka uzalishaji sifuri wa dhahabu mpaka kuwa nchi ya 3 kwa uzalishaji wa dhahabu barani Afrika mwanzoni mwa miaka 2000. Mgodi wa Bulyanhulu pekee, kwa wakati ule uliweza kutoa makusanyo ya kodi mbalimbali 98% ya makusanyo yote ya kodi katika mkoa. Ikumbukwe nyuma kidogo serikali ya Tanzania ilikuwa inashindwa hata kulipa mishahara ya wafanyakazi wake kwa wakati.
2) Kilimo
Kabla ya mashamba makubwa ya mkonge kutaifishwa, Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza kwa uzalishaji wa katani, na huku ikiwa mzalishaji mkubwa wa pamba, kahawa, chai, n.k. Utaifishaji wa mashamba hayo uliifanya Tanzania kupotea kabisa katika ramani ya Dunia katika uzalishaji wa mazao mbalimbali
3) Biashara za Bidhaa Muhimu
Miaka ya 1980 mwanzoni serikali iliamua kuendesha biashara ya maduka yenyewe, maduka ya RTC. Kwenye maduka haya, ukiritimba wa ajabu ulijengeka na kusababisha kushamiri kwa rushwa. Wenye kauli kwenye biashara hizi waligeuka kuwa ni mawaziri, wakuu wa mikoa, n.k. Wakazi wa maeneo, majina yao yaliandikwa kwenye daftari, na wewe kama siyo mkazi wa eneo husika, huwezi kupata bidhaa muhimu kama sukari, sabuni, sembe, bia, kanga, n.k. Na hata hao wakazi wa maeneo walipangiwa kiasi cha mwisho cha kuweza kununua. Ni sekta binafsi ndiyo iliyosababisha, siyo kupatikana kwa bidhaa hizo tu, bali kutoka kusukumwa kwenye foleni ya kununua sabuni mpaka hatua ya kushawishiwa ununue sababuni au nguo fulani kwa kuwa ina ubora, tena ukiwa nyumbani kwako ukitazama TV.
4) Huduma za Simu
Wakati biashara ya simu ikiendeshwa na serikali, ili kuunganishiwa tu simu upate kuongea, kuna wakati ilihitajika kufahamiana na operator au ilihitaji kumpa chochote. Kuna wakati pamoja na yote hayo, ilihitajika kukaa nje ya kiboksi cha TTCL zaidi ya masaa 12 kusubiria kuunganishiwa simu. Sekta binafsi ilipoingia, leo yamejaa matangazo tele ya kutushawishi wakati wote tutumie simu, na TTCL ikiendelea kufaidi uzoefu wa serikali katika kuendesha biashara ambao ni kuua biashara
5) Viwanda
Serikali hii iliwahi kutaka kufanya biashara ya viwanda. Tukawa na viwanda vya kuunganisha magari na matrekta, viwanda vya baiskeli, bia, sigara, soda, sukari, chumvi, viatu, matairi, nguo, zana za kilimo, sabuni, mafuta ya kupikia, majiko ya kupikia, maturubai, redio, n.k. Mafanikio ya viwanda hivyo yanafamika, lakini baadhi ni pamoja na watu kukamatwa na kusweka ndani kwa biashara ya magendo ya kuuza pakiti ya sigara au kreti la bia. Leo watu siyo tu wanaweza kupata sabuni, bia, sukari, kwa kiasi chochote, wakati wowote na mahali popote, lakini pia wametoka kutoka kwenye foleni za kugombania bidhaa mpaka kubembelezwa wanunue bidhaa. Nilishangaa sana niliposikia eti serikali inataka kuanza kufufua baadhi ya viwanda ili vijiendeshe. Nikasema kweli sikio la kufa halisikii dawa!
Nimeandika haya machache kuthibitisha tu kuwa serikali hii ya Tanzania haina uwezo hata chembe wa kuendesha uchumi wa kibiashara. Tunaposema serikali haina uwezo wa kuendesha biashara maana yake ni kuwa maofisa wa serikali kwa umoja wao hawana uwezo wa kuendesha uchumi wa kibiashara. Na ndiyo maana hata wengi wao wanapokoma kuwa maofisa wa serikali, wanapoanzisha biashara, hazifiki popote. Laiti kama maofisa wa serikali wangekuwa na uwezo wa kuendesha uchumi wa kibiashara, basi miradi inayosimamiwa na taasisi za serikali ndiyo ingekuwa miradi ya mfano kwa ustawi. Lakini ukweli ni kuwa miradi ya serikali ndiyo imekuwa mifano mizuri kwa ubovu wa uendeshaji na utengenezaji hasara. Tazama ufanisi wa kampuni kama:
1) TANESCO
Hawa wanapewa ruzuku, ni watoaji huduma pekee wa bidhaa muhimu ya nishati ya umeme, hawana mshindani. Shirika hili halijawahi kutengeneza faida wala halijawahi kuwa na ufanisi hata katika huduma yenyewe. Leo hii nchi nzima, TANESCO hawawezi kumuunganishia mteja mpya umeme hata angalao ndani ya mwezi mmoja tangu alipokamilisha malipo. Karibuni nimeongea na Meneja wa umeme Ilemela, Mwanza anasema wamesimama kuwaunganishia umeme wateja wapya kwa sababu hawana nguzo, na nguzo zikija wataanza kuunganisha wateja walioleta maombi mwezi wa nane, mwakajana. Ukienda katika uhalisia, watu wnaoshindwa hata kupata nguzo tu za miti, wanaweza kuendesha uchumi wa kibiashara? Hivi ingekuwa TANESCO ni kampuni binafsi, ingeweza kutokea hata siku moja ya kukosa nguzo? Mimi nina imani TANESCO ingekuwa ni kampuni binafsi, wanaojenga nyumba huenda wangekuwa wanafuatwa tangu nyumba ikiwa katika hatua ya msingi, na wasingelipia hata pesa ya nguzo. Kama serikali inashindwa kuisimamia tu TANESCO iliyoachiwa soko lote, itaweza kusimamia biashara mathalani ya anga ambako kuna washindani binafsi? Sitarajii kabisa.
2) TTCL
Hii kampuni kwa miaka mingi ilifurahia soko lisilo na ushindani lakini halina dalili ya kutembea. Ni shirika mfu. Serikali imeshindwa kuliendesha shirika hili kibiashara lakini serikali hiyo hiyo inaamini ina uwezo mkubwa sana wa kusimamia miradi ya wawekezaji.
UJUMBE KWA SERIKALI
1) Serikali kama inataka ifanikiwe kujenga uchumi wa Tanzania ni lazima iingie darasani kujifunza uchumi wa kibiashara. Na walimu wazuri siyo watu waliojaza makaratasi ya nadharia ya uchumi bali ijifunze kwa wanaouishi uchumi wa kibiashara, watu au taasisi zilizofanikiwa. Tuna wasomi wa nadharia wengi ambao hawawezi hata kuendesha biashara ya genge kwa faida. Ukitaka kuendesha biashara ya genge, mwalimu mzuri ni yule aliyefanikiwa kuanzisha genge, likapata faida, na baadaye likageuka kuwa duka au hoteli. Wataalam wa nadharia ya uchumi na biashara watumike tu kukusanya na kuyaweka pamoja mawazo na ushauri wa wanaouishi uchumi.
2) Serikali ikubali na itambue kuwa haina uwezo wa kusimamia uchumi. Kukosa uwezo huo ndio uliofanya miradi yote ya kibishara chini ya serikali kufa. Uliyeshindwa kuendesha miradi yako huwezi kuwa msimamizi mzuri wa miradi ya wengine, bali unaweza kuwa mwanafunzi mzuri maana unaujua uchungu wa kushindwa.
3) Serikali ijue namna ya kulinda mazingira ya uchumi wa kibiashara. Kauli tu ya serikali na hasa Rais ina uwezo wa kuua uchumi. Wanaofuatilia masuala ya uchumi wanafahamu. Siku ile tu Rais aliposema anazuia mchanga wa dhahabu wa kampuni ya Acacia kwenda nje, hisa za kampuni ya Acacia kwenye masoko ya fedha zilianguka kwa 20% (mamilioni ya dola yalipotea kwa usiku moja), makampuni yote ya madini yaliyowekeza Tanzania, hisa zao kwenye masoko ya fedha zilianguka. Makampuni yanayojenga miradi ya graphite, na yale yanayofanya utafiti wa madini ya Nickel, nayo yaliathirika sana maana na yenyewe yanategemea kusafirisha unfinished products yatakapoanza uzalishaji. Lakini pia kwa kiongozi mkuu kusema kampuni inaliibia Taifa, ni kauli nzito sana, na hasa inapotolewa wakati hakuna hata utafiti au uthibitisho maana kamati za kuchunguza zimeundwa baada ya kauli.
4) Uchumi ni Sayansi yenye miiko yake, ambayo kwa kiasi kikubwa serikali ya tanzania inaonekana kutokutambua lakini ikiamini kuwa inafahamu sana. Serikali ya Tanzania haijajua bado kuwa hela ya serikali (kodi) ni pesa ya wananchi, siyo ya serikali. Wananchi ndiyo walioitafuta, wakaigawia serikali kwa utaratibu/sheria zilizokubaliwa kwa njia ya kodi. Serikali ni lazima iitumie fedha hiyo kwa faida ya aliyeitoa ili aweze kuendelea kutoa zaidi. Ni loop ambayo haitakiwi kukatika. Mwananchi atoe kodi, kodi iende serikalini, serikali irudishe fedha kwa walipa kodi, walipa kodi wazalishe, sehemu ya faida waipatie serikali; mzunguko unaendelea. Kuchukua fedha kwa walipa kodi na kwenda kuifungia BOT, ni serikali kuamua kujinyonga yenyewe na kuwanyonga walipa kodi kiuchumi.
Serikali kila mara inaomba ushauri, huu ni sehemu ya ushauri, na kuonesha wanashaurika, wanastahili kutupa mrejesho ili tujue kuwa ushauri unapokelewa au hapana. Tunafanya hivi kwa kuamini kuwa kauli za Mh. Rais kuwa urais ni wa kwake, fomu alichukua mwenyewe bila ya kushauriwa na mtu, na hivyo halazimiki kufuata ushauri wa mtu, ilikuwa ni kauli ya kuteleza maana tukiizingatia hasa kauli hiyo kimantiki, ni kuwa hatuhitajiki kushauri lolote.