Uongozi wa Rais Samia Usitiwe Najisi

Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,649
2,911
Kwa hakika, na bila mashaka, uongozi wa Rais Samia umeonesha ushupavu. Wakati viongozi waoga huwaogopa wapinzani wao wa kisiasa, Rais Samia, bila woga, anawaweka karibu.

Tangu mfumo wa vyama vingi uanze, ni Rais Kikwete ndiye aliyekuwa anashikilia rekodi ya kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani, lakini rekodi hiyo imevunjwa maradufu na Rais Samia. Wapo ambao daima walikosa usingizi, wakabakia kila siku kupanga njama chafu dhidi ya vyama vya upinzani kwa hofu kuwa vyama vya upinzani vikiwa huru kufanya kazi zao kwa mujibu wa katiba, watapata nguvu na kuwaondoa madarakani. Kinyume chake, Rais Samia amewaweka karibu wapinzani wake, huku akiwapa uhuru wa kumkosoa yeye na Serikali yake LAKINI inakuwa ngumu hata kumkosoa kutokana na umakini wake.

Unaweza ukambeza, au ukashindwa kumpa anachostahili, lakini hakika Rais Samia katika mtazamo wa kisiasa, amewashinda watangulizi wake wote walioongoza kwenye mfumo wa vyama vingi. Na huyu Rais ataongoza katika mazingira tulivu sana ya kisiasa kuliko watangulizi wake wote. Kwa ujumla, kwa kiasi kikubwa, anakubalika na makundi yote: ndani ya chama chake, kwenye vyama vya upinzani, nchi jirani na jamii yote ya kimataifa. Hali hii kwa vyovyote haijaja hivi hivi bali ni kutokana na ujasiri alioubeba. Wakati marais watangulizi wake waliona kuwapa wapinzani uwanja huru wa kufanya siasa kungewadhoofisha wao kwenye madaraka yao, Rais Samia, kuwapa nafasi wapinzani kufanya siasa kwa kadiri ya ruhusa ya katiba, kumemuimarisha zaidi.

Na wale wanaojiita wabunge, ambao walitegemea zaidi uovu kuupata ubunge, ni wakati wao wa kuanza kuaga. Hawa waliopo sasa, kwa vyovyote zaidi ya 75% hawatapitishwa hata na wajumbe ndani ya CCM kuwa wagombea wa ubunge kupitoa CCM. Hata hao watakaopitishwa, waliozoea mbeleko ya kupora ushindi, hawatakuwa na hiyo nafasi, kwa maana Rais Samia hatataka ushujaa wake utiwe unajisi na watu wasiotakiwa na wananchi.

Kwa hali ilivyo sasa na jinsi inavyokwenda, bila shaka Rais Samia atakuwa Rais pekee atakayepata kura nyingi halali kutoka makundi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wa vyama vya upinzani.

USHAURI MUHIMU KWA RAIS

Rais asikubali ushujaa wake utiwe najisi na baadhi ya watu ambao wamefunga pingu za maisha na uovu. Ili kujiweka mbali na unajisi, yatazamwe maeneo yote yanayoweza kutumia dhamana zao vibaya: Tume ya uchaguzi, Jeshi la Polisi na TISS, maRC ma maDC. Hawa ndiyo siku zote wamekuwa wa kusimamia uovu wakati wa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom