Nikiwa jirani wa Zitto Kabwe hapa Mwandiga Kigoma mahali alipozaliwa sijashangaa kabisa kuona upuuzi anaouandika huyu bwana mdogo kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo jana ambapo ameshinda siku nzima anaibeza siku ya Watanzania kuadhimisha miaka 58 ya yangu Uhuru.
Hili suala naona kama halitiliwi mkazo inavyopaswa lakini ukweli ni kuwa Zitto hana asili ya Tanzania. Baba yake aliyekuwa Dereva wa Taxi ni mzaliwa wa DRC
na Mama yake ni Mzaliwa wa Burundi
.
Kwa hiyo Zitto sio mtu anayeguswa na Tanzania na ndio maana kila kitu kizuri kwa nchi hii yeye hupinga na amekuwa akiendesha harakati za kuichua Tanzania ndani ya nchi na kimataifa.
Jana kashupalia kumshambulia Mbowe kwa kuhudhuria sherehe za Uhuru kule Mwanza, sasa mjiulize kuna ubaya gani kwa viongozi wa vyama vya upinzani kuhudhuria sherehe za uhuru? Kwa sababu zile sio sherehe za CCM ni sherehe za nchi.
Ndio maana viongozi wetu wote walikuwepo Rais, Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu, Makamu wa Pili wa Zanzibar, Maspika wote hadi wastaafu, Majaji wakuu na Marais Wastaafu wote ispokuwa Rais Mstaafu Kikwete ambaye sote tunajua yupo Marekani kwa majukumu muhimu ya kimataifa.
Mawaziri na Wabunge wenzake walikuwepo, Mabalozi wa nchi mbalimbali, viongozi wa dini nakadhalika.
Kwa tunaomjua na ajenda zake haki hii haiwezi kumpendeza hata kidogo, na mimi nimeamua leo niuseme huu ukweli ili Watanzania mjue.
Mnamuona anavyopambana kupinga miradi mikubwa ya maendeleo, yaani Zitto anatamani Watanzania wakose umeme, kwa hiyo anauchukia kabisa mradi wa bwawa la Nyerere utakaozalisha megawati 2,115 za umeme, anasikia raha kuona watu wanavyohangaika kusafiri kwa treni na ndege na hivyo hapendi kabisa kuona reli inajengwa na ndege zinanunuliwa, hapendi kuona vituo vya afya na hospitali zinajengwa, anafurahishwa kuona Watanzania wanakosa dawa hospitali, wanakosa mahali pa kupata matibabu na hivyo wanakufa. Anachukia kabisa kusikia Tanzania inapata mikopo nafuu kwa ajili ya kuwajengea wananchi miradi ya barabara, maji nakadhalika, na ndio maana anawatisha wananchi kuwa deni la Taifa kubwa mno wakati Wataalamu wa uchumi wanasema ni deni stahimilivu na fedha zinakopwa kwa mambo ya msingi kwa wananchi.
Kwake yeye Zitto taarifa za kuwa uchumi wa Tanzania ni mzuri hazifai, anashupalia shingo na kusikia raha kuwaaminisha Watanzania kuwa hali ya uchumi ni mbaya sana na yupo tayari kupika takwimu za kuonesha uchumi umezorota ili kuwatisha wawekezaji wasije kujenga viwanda na watanzania wakapata ajira na nchi ikapata kodi.
Na mengine mengi, naifahamu vizuri familia ya Zitto. Nashangaa kwa nini mmoja wa viongozi wa Kigoma ambaye baada ya Mama yake kukosa maziwa alipelekwa kunyonya kwa Mama yake Zitto hasemi ukweli huu kuwa huyu dogo hawezi kuguswa na mazuri ya Tanzania.
Zitto Kabwe pengine anaweza kufurahia uhuru wa DRC alikotoka Baba yake au Burundi alikotoka Mama yake. Na kama Watanzania mmesahau alipokuwa Chuo Kikuu Zitto alishaitwa mara kadhaa na Idara ya Uhamiaji kuhojiwa kuhusu uraia wake, kwa tunaofahamu hapa ndio palikuwa pa kupata ukweli wote na kama idara yetu ya uhamiaji ingekuwa shapu ingeumwaga ukweli huu ili Watanzania wajue.
Ndio maana kwa sisi majirani zake hapa Mwandiga hatushangai kuona jinsi anavyotumiwa na wazungu kuivuruga Tanzania, wazungu wanafanya hivyo kwa Zitto kwa sababu wanajua michezo hiyo hiyo ndio wanayoifanya DRC na Burundi ambako hakujatulia miaka na miaka na kila uchao ni mauaji tu. Wanatamani waivuruge Tanzania ili waje kuvuna rasilimali zetu kama wanavyovuna madini kule DRC.
Nampongeza Rais Magufuli na serikali yake kwa jinsi alivyombana Zitto, endelea hivyo hivyo na mwakani iwe ndio mwisho wa huyu mtoto mpuuzi. Alizoea huko tulikotoka walikuwa wanamkweza na kumfanya aonekane wa maana wakati ni kibaraka mkubwa na mtu asiyetakia mema Tanzania. Ni mpinzani asiye na faida kwa nchi. Muda wote anawaza machafuko tu.
Mbowe kazungumza maridhiano yeye anaona Mbowe kakosea, anataka fujo? Anataka vita? Hapo sasa watanzania ndio mnaweza kupata picha ya aina ya mtu huyu. Anachukizwa sana na hali ya amani ya Tanzania kwa sababu anajua hiyo ndio silaha kubwa inayomkwamisha.
Nawasihi watanzania wenzangu mpuuzeni, tujenge nchi yetu, wakati ni huu na kwa bahati nzuri tumepata Serikali ambayo inamwelekeo wa kututoa katika lindi la umasikini, ufukara na uombaomba. Tushike hapo hapo.
Mwananchi wa Mwandiga
Kigoma
Disemba 10, 2019