Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na wenzake. Shahidi wa 12 Luteni Urio kuendelea kutoa ushahidi Januari 31, 2022

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
580
1,683
Habari Wakuu,

Leo tena shahidi wa 12 Denis Urio anaendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3.

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakama Kuu Kesi ya Ugaidi ya Mbowe na wenzake: Kesi imeahirishwa hadi 28/01/2022, Luteni Denis Urio kuendelea na ushahidi wake

Fuatana nami kupata yatakayojiri

UPDATES:

Jaji ameingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili

 • Pius Hilla
 • Abdallah Chavula
 • Jenitreza Kitali
 • Nassoro Katuga
 • Esther Martin
 • Ignasi Mwinuka
 • Mawakili wa Serikali Waandamizi na Tulimanywa Majige, Wakili wa Serikali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ikikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili

 • Seleman Matauka
 • Alex Massaba
 • Paul Kisabo
 • Sisty Aloyce
 • Maria Mushi
 • Khadija Aron
 • Michael Lugina
 • Evaresta Kisanga
 • John Mallya
 • Nashon Nkungu
 • Dickson Matata

Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tupo Tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea

Shahidi anapanda Kizimbani

Jaji: Shahidi Jana Ulikuwa Unatoa Ushahidi Wako, Unaulizwa Maswali Chini ya Kiapo na Leo Utaendelea Kuulizwa Maswali Chini ya Kiapo

Wakili John Mallya: Shahidi tunaendelea tulipo Ishia Jana, Mheshimiwa Jaji Naomba Jibu lake la Mwisho

Jaji: ni Kwamba Asipotumia Jina Namba zake Jina lake halitoonekana...

Malya: hivi kazi ya VIP PROTECTION Inafanyikaje

Shahidi: Mheshimiwa Jaji kazi ya VIP PROTECTION Inafanyika kwa mtu yoyote, Kwa Kufuata Sheria na Kanuni za Nchi

Malya: Ni sahihi Kwamba kazi Wanazofanya VIP protection Ni lazima wawe naye Kwa Wajibu wa Kum' protect

Shahidi: Ni sahihi Malya: hawa VIP protection Ni sawa na Body guard?

Shahidi: Sijawahi Kusikia Body Guard mimi

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba 26

Malya: Umesema kuwa hawa VIP protection Wanakuwa pamoja na Wanayem' protect, sasa ni somee Meseji ya Tarehe 20 July 2020, Ya Saa Mbili Asubuhi

Shahidi: Hawa wawili Kuanzia Siyo Mbaya Hawawezi Kutelekezwa, Nitakuwa nao Full time

Malya: Kwa Kazi gani

Shahidi: Ulinzi Ndiyo

Malya: Je, kuna meseji nyingine yoyote kwamba kuna mahali Mbowe anasema nitawatuma Kufanya kazi nyingine au uhalifu?

Shahidi: kwenye meseji hazipo

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo Namba 35

Malya: Tumeletewa report kule ulikopeleka simu , Je hii namba ina Jina gani?

Shahidi: Imeandikwa FREE... Ambayo ni namba ya Freeman Aikael Mbowe

Malya: Very Good shahidi umeniongezea information nilikuwa sijui, sasa washa simu yako

Shahidi anabonyeza simu, anasema tayari

Malya: Unasema Ulikuwa Unawasiliana na Mbowe Kupitia Mtandao Wa Telegram

Shahidi: Ndiyo Mtandao Wa Telegram

Malya: Naomba usogee kwa Mheshimiwa Jaji pale kamuonyeshe namba unayosema ume-chat na Mbowe. Je, hapa kuna Jina FREE linaonekana, ukiwa umefungua meseji?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji HAKI YA MUNGU hii ni akaunti ya Mbowe siyo Group, nafungua

Malya: Jina Free Ukifungua Meseji linaonekana au halionekani?

Shahidi: Halionekani lakini ni Akaunti ya Mbowe

Malya: Je, ulitoa Ufafanuzi/Maelezo kuwa Jina FREE halionekani?

Shahidi: Si nilimjibu mimi Bwana, Mimi siyo Mtaalamu Wa IT, Sasa nitoe Maelezo Ya nini

Malya: Mheshimiwa Jaji naomba atoe jibu

Jaji: Umeelewa Swali? Kwamba Wakati Unasoma Ulitoa Ufafanuzi? Kuwa jina halionekani

Shahidi: Ufafanuzi huo sikutoa

Mahakama: (Kicheko)

Malya: Haya Ulisema Kwamba Mbowe alikuwa nakupa Wishes za Christmas na Mwaka Mpya, je Meseji zimeanza lini

Shahidi: Tarehe 20 July 2020

Malya: Alikuwa anakutakia Heri ya Mwaka Mpya Kupitia nini

Shahidi: alikuwa ananipigia Simu

Malya: Alikuwa anakupigia simu kwa njia ipi

Shahidi: Kwa Telegram

Malya: Je, unafahamu kwamba ukipiga Simu Telegram unabakia na Calls Record

Shahidi: Sina Utaalamu huo

Malya: Je Jana Wakati wa Ushahidi Wako Kama Ulituonyesha WhatsApp Calls na Meseji za Mbowe

Shahidi: aliyechunguza ndiye anafahamu

Malya: Kwa hiyo Mtaalamu anaweza Kuwa amepunguza au ameongeza?

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi hajasema hivyo

Malya: Nitauliza Upya Kuokoa muda, Kilichokufanya Jana usitoe Calls za WhatsApp

Shahidi: nilisema kwamba Mimi Nilikuwa na wasiliana na Mbowe Kwa WhatsApp, Meseji na Telegram

Malya: Sawa Jana Ulionyesha WhatsApp Call wakati wa Ushahidi Wako?

Shahidi: Sikuonyesha

Malya: Ulionyesha namba zingine ambazo Ulikuwa Mbowe alikuwa anakupigia Simu

Shahidi: Sikuonyesha

Shahidi: (Ghafla) Sikuonyesha Kwa sababu..

Malya: sitaki sababu hapa

Shahidi: Sikuonyesha Kwa sababu

Malya: Sijakuuliza kuhusu sababu

Jaji: Shahidi sikiliza swali ndiyo ujibu

Malya: Naomba Kielelezo Namba 28

Malya anamkabidhi shahidi

Malya: Jana ulishindwa Kuiwasha hii simu

Shahidi: Sikushindwa, haikuwaka

Malya: Ulitoa Explanation Kwanini ilishindwa Kuwaka

Shahidi: Nilieza Kwamba simu ina ibovu wa Display, Ukiwasha Hai Display Kitu chochote

Malya: Kama kuna Taarifa ya Muhimu ambayo Mbowe anataka Kujitetea Kutumia hiyo Simu atafanyeje, Utampa akatengeneze

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Wakati natoa Ushahidi Wangu Kuhusu Kukabidhi Simu, Nilisema, Nilienda na Simu moja, Sikujua Kama Nilitakiwa Kukabidhi Simu, Nikauliza kwa sababu gani wakasema sababu ya Uchunguzi, Tarehe 10 nilipeleka simu zingine, na Mimi nilipeleka Simu Ikiwa imedondoka haifanyi kazi

Malya: Aliyechunguza hajasema Kwamba Simu Mbovu, Isipokuwa wewe unaogopa kwa sababu unajua Kilichopo humo hutaki kionekane

Shahidi: Washa wewe

Malya: Mimi siwezi Kuwasha Simu yako

Shahidi: basi awashe hata Mheshimiwa Jaji

Malya: wewe Ndiyo Mwenye Simu Shahidi: basi hayo Mengine ni Maoni

Malya: Kuna report ya hii Simu, Je Jana Ulionyesha Call Logs za mbowe

Shahidi: Sikuonyesha

Malya: Calls za Khalfani Bwire Jana Ulionyesha

Shahidi: Sikuonyesha, Sababu sikuulizwa

Malya: Je, jana Ulionyesha Meseji za Ling'wenya Kuhusu Kuwasiliana nao wasikengeuke

Shahidi: Sikuonyesha sababu sikuziona

Malya: Ni sahihi unasema Kwamba a baada ya kuwapeleka Vijana Wanne Kwa Mbowe Mwisho wa Kuwasiliana naye ilikuwa Tarehe 24

Shahidi: Ndiyo

Malya: Wakati Mbowe anaacha Kupokea Simu yako alikuwa tayari na Vijana Wanne

Shahidi: Ndiyo

Malya: Soma hapa

Shahidi: Kaka Wale Mtu 3 au 4 Ni Muhimu

Malya: Sasa kama Umeshampa Mtu Nne ukitaka uwasiliane naye nini

Shahidi: Nilichokitaka Kwake baada ya kukikosa nikakipata kwa Bwire

Malya: Kwa hiyo Wakati anaacha Kuwasiliana na wewe Hitaji lake alikuwa ameshalimaliza

Shahidi: Ndiyo

Malya: Miji ya Arusha, Dar es Salaam, Mbeya na Mwanza ina masoko mangapi?

Shahidi: Mimi sifahamu anafahamu Mbowe

Malya: Miji niliyotaja ina vituo vya mafuta vingapi?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji najibu swali kama Ifuatavyo anayejua idadi ya vituo vya mafuta ambavyo alipanga kulipua ni Freeman Mbowe

Malya: Shahidi Miji hiyo ina Mikusanyiko Mingapi

Shahidi: Mheshimiwa Jaji mimi sijui ina mikusanyiko mingapi, Ila Mheshimiwa Mbowe ndiye anajua kwa sababu alipanga kulipua

Malya: Ulifika Ofisi za DCI Je Ulifika ukiwa na Simu zako

Shahidi: Ndiyo

Malya: Je, ulieleza Jana Kama Ulikuwa na Simu zako

Shahidi: Mheshimiwa Jaji nilifika kwa DCI nikampa Taarifa, akasema endelea nao

Malya: Maelezo Yako Mazuri ila siyahitaji, Swali langu Ulieleza Kama Ulimuonyesha DCI Simu zako na Mawasiliano ya Mbowe?

Shahidi: Sikueleza

Malya: Unafahamu kwamba DCI ana vifaa Vya Kurekodi?

Shahidi: Mimi sifahamu

Malya: Je, unafahamu kwamba DCI ana vifaa Vya Upelelezi

Shahidi: Mimi sifahamu Kwa sababu, Kazi yangu haikuwa Kufanya Upelelezi Bali Kutafuta Watu wa Kufanya Kazi

Malya: Wakati Khalfani Bwire, Je alikwambia Vifaa wanavyokwenda Kuvitumia

Shahidi: Hakuniambia

Malya: Wakati Unaingia Jeshini ulikuwa na Certificate ya Form Four na Certificate Ya Ufundi

Shahidi: Ni sahihi ya Diesel Engine

Malya: Bwire alikuja Nyuma yako

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Ulikwenda South Africa Kufanya Mafunzo lini

Shahidi: 2010

Malya: Ukawa Mwanafunzi Bora

Shahidi: Hapana

Malya: Kwanini ulipewa zawadi ya Bunduki

Shahidi: Mheshimiwa Jaji, Inaonyesha Jinsi gani Wakili anataka Kuniweka Maneno Mdomoni, Labda yeye ndiyo alipewa Bunduki baada ya kufuzu Law School, anataka Kuficha Uhalifu

Malya: Ulipewa award gani

Shahidi: Sikupewa Award

Malya: Lakini wewe Ulifuzu

Shahidi: Ndiyo

Malya: Wakati Unakwenda Darfur Mara ya kwanza ulikuwa koplo?

Shahidi: Ni sahihi

Malya: na kwenye Jeshi koplo siyo Afisa

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Wakili ananitaka nieleze Kamisheni ya Kijeshi

Jaji: amekuuliza koplo ni Afisa siyo Afisa

Shahidi: Ni Afisa

Malya: Wakati Unakwenda Darfur ulikuwa na Ling'wenya kinachokufanya umkane Ni Kitu gani

Shahidi: Sijamkana, Siwezi Kukumbuka kama Nilikuwa naye

Malya: Shahidi Wewe ni Luteni Wa Jeshi, Je una Degree?

Shahidi: Hapana

Malya: Huna Digrii lakini ni Luteni wa Jeshi

Shahidi: Ndiyo

Malya: Adamoo na Ling'wenya Mlipoachana Morogoro alikwenda Wapi

Shahidi: Walikwenda Dar es Salaam

Malya: Naomba Kielelezo D1, Maelezo aliyo andika Kingai ambapo anasema alimuhoji Ling'wenya akakiri, Soma hapa

Shahidi: Luteni Urio alitupa nauli TSh 87,000 nauli ya kwenda Moshi

Malya: na wewe Umesema Walitoka Kwako Walikwenda Wapi

Shahidi: Nimekwambia Dar es Salaam Siyo Moshi

Malya: Kwenye Nauli uliwapa TSh ngapi

Shahidi: TSh 199,000

Malya: hapo Wao Wameamdika uliwapa TSh Ngapi

Shahidi: Nauli TSh 87,000, Ndivyo walivyo andika wao

Malya: Ulielezea Shahidi Kwenye Ushahidi Wako namba Uliyotumia Kuwasiliana na Bwire ni Namba gani

Shahidi: Sikueleza

Malya: Wakati Mnaenda Kuonana na Swila Mara ya Kwanza Ilikuwa lini

Shahidi: Tarehe 11 August 2020

Malya: Ndiyo Siku hiyo ulitoa Maelezo Yako

Shahidi: Ndiyo

Malya: Nimesikia Siku Unakutana na DCI Mlikutana baadae akaja Kingai

Shahidi: sahihi

Malya: Ulielezea Kuna mtu Yoyote alikuja Kuwa Join Baadae

Shahidi: Kuwa Join wapi?

Malya: Kwenye Kikao cha Siku hiyo na DCI na Kingai

Shahidi: Hakuna Mtu yoyote alikuja Kutujoin Siku hiyo

Malya: Kwenye Meseji ya Mwisho ambayo Mbowe alikutumia, Ukasema Hukueleza, ni kwanini hukutuma Meseji Nyingine Kuuliza Una maana gani

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Baada ya Kupita Muda Hakuna Mawasiliano, Nilimuuliza Bwire Boss wako anajua, Sasa ningejibu Meseji ya Nini

Malya: Na ni Ushahidi Wako Kwamba Ofisi za Swila ni Ghorofa ya Nane Makao Makuu

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Mheshimiwa nafikiri Sina Swali la Ziada kwa Shahidi huyu

Anasimama Adv. Dickson Matata

Matata: Nikumbushe Ulionana na Mbowe Tarehe ngapi

Shahidi: Mwezi Wa Saba, 2020 Sikumbuki Tarehe gani

Matata: Na Ulipo Onana naye ndiyo alikwambia anahitaji Vijana Wa Kuambatana naye wa Kuchukua dola

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Kwa Maelezo yako Ndiyo alikwambia anahitaji Vijana hao Vijana Kwa ajili ya Kumsaidia Kuwashambulia Viongozi ambao hawaupendi Upinzani

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Na Ndipo alipokwambia Kwamba anataka Kuhakikisha anachoma Masoko na Vituo Vya Mafuta

Shahidi: Naomba Ni'refresh alisema Kwamba ataleta Taharuki Kwa Kufanya hayo Uliyo niambia

Matata: juzi Ulisema Kwamba Ulifanya Kitu kinaitwa Tactical appreciation, na Mimi Leo nataka tufanye Tactical appreciation ya Kisheria, Wakati anakwambia Mlikuwa Wawili

Shahidi: Ndiyo

Matata: Kwa Lugha Nyingine Hapakwepo na Watu wengine

Shahidi: Sahihi

Matata: tofauti na Siku hiyo, Kuna Siku yoyote aliwahi Kukwambia Jambo hilo au kukuandikia Barua

Shahidi: Hakuna

Matata: Kwa hiyo kwa tafsiri nyingine hatutopata ushahidi wa maandishi au wa sauti au meseji unaoweza kuthibitisha kuwa alikwambia hayo maneno?

Shahidi: Hakuna sauti

Matata: Baada ya Kukwambia Ukaona Inafaa ukatoe Taarifa, Ukaenda kwa DCI, Kwanza Ulimpigia Simu halafu akakupa appointment

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Na Kwamba Baada ya Kumueleza akamuita Kingai

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Utakubaliana na Mimi Kwamba DCI ni Mtu Mwenye Ujuzi Katika Upelelezi

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Kingai alikuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, Unafahamu Kwamba anakuwa na uzoefu wa Upelelezi

Shahidi: Kwanza Nilikuwa sijui kuwa ni Mpelelezi

Matata: Mtu akiwa Mpelelezi Wa Mkoa ana uzoefu au hana Uzoefu

Shahidi: anakuwa na Uzoefu

Matata: Wewe Kama Komandoo, Katika Kikao hicho na Baada ya Hapo, Hukuona wewe au DCI na Kingai, Hukuona Kuwa Kuna Umuhimu kuwa Msiridhike Kile ambacho umesema, Je Hukuona Kuwa Kuna Umuhimu Wa Kurekodi Voice Notes

Shahidi: Mamlaka labda Ndiyo haikuona Umuhimu

Matata: Wewe Uliona Kuna Umuhimu au Hakuna Umuhimu, Kwamba Usiridhike na Maneno Utengeneze Voice Record

Shahidi: Niliona Kuna Umuhimu

Matata: kwenye huo Umuhimu hukuona Kuna Umuhimu Wa Vinasa Sauti na Meseji ambao Vitasema Exactly Kuwa anataka Kulipua
Masoko

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Mbowe alikuwa alishaniambia Kwa Meneno, asingerudia

Matata: Narudia Swali langu, kwenye huo Umuhimu hukuona Kuna Umuhimu Wa Vinasa Sauti na Meseji ambao Vita, sema Exactly Kuwa anataka Kulipua Masoko

Shahidi: Sikuwa na Vifaa Vya kunasa Sauti

Matata: Freeman Mbowe akikataa leo hakusema, ni ushahidi gani unao mbele ya Mahakama Kwamba Mbowe alisema hayo maneno uliyosema?

Shahidi: Ni ushahidi wa meseji ya kusema "muda umeisha"

Matata: hiyo meseji inayosema muda umeisha ina sehemu inasema kulipua masoko

Shahidi: Hakuna mahali inasema

Matata: hiyo Meseji ina sehemu inasema kushambulia viongozi ambao hawapendi upinzani?

Shahidi: Hakuna mahali inasema hivyo

Matata: Hiyo meseji kuna sehemu inasema kulipua vituo vya mafuta

Shahidi: hakuna mahali inasema hivyo

Matata: Tutoke hapo, Unasema Ulienda Kwa DCI na Kabla ya kwenda Ulimpigia Simu,

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Ulielezea Mahakama Kwamba Ulikuwa Unafahamiana na DCI

Shahidi: Nilieleza, Kuna Mtu aliuliza Kama Nilienda Ofisi ya DCI Mara ngapi

Matata: Mimi Sitaki Habari ya Kwenda Ofisini, DCI Anabadirika, nakuuliza Kama Ulielezea Kwamba Unafahamiana na DCI

Shahidi: Sikueleza

Matata: Ulieleza Mahakamani hapa Kwamba Namba yake Ulipata Wapi

Shahidi: Sikueleza

Matata: Hata hiyo namba yenyewe Ulitaja

Shahidi: Sikutaja

Matata: Ushahidi gani Unathibitisha Kwamba Ulimpigia Simu

Shahidi: Ushahidi ninao kwa sababu nina namba zake na Nilifika Ofisini Kwake

Shahidi: Je ulivitaja hivyo Vitu Wakati Unahojiwa na Upande wa Mashitaka

Shahidi: Sikuvitaja

Matata: Unasema Kwamba Ulienda Kesho Ukasema Una Appointment naye Ukakutana na Secretary Wake

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Kwa Maana hiyo Ulifuata Utaratibu wa Umma Wa Jinsi ya Kuingia Ofisi Fulani

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Ulisema Kwamba Ulipofika Ulifuata taratibu za Ofisi za Umma

Shahidi: Nilieleza Kwamba, Nilionyesha Kitambulisho kama Askari

Matata: Ulisema Kwamba Askari apaswi Kufuata Utaratibu Wa Kuingia Ofisi Za Umma

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Mimi Nilieleza Kuwa ni Askari, yeye Ndiye alitakiwa aniambie Kufuata Utaratibu

Matata: Wakati Unahojiwa na Wakili wa Serikali Abdallah Chavula, Ulisema Kwamba Nyie Askari hamfuati Utaratibu

Shahidi: Sikueleza

Matata: Ulileta Visitors Book Kuonyesha Kweli Ulienda Ofisi Za DCI

Shahidi: Hapana Sikuleta

Matata: Shahidi Wewe ni Mwanajeshi, Ulitakiwa Kufuata Taratibu zote za Kijeshi

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Unapotoka Mkoa Mmoja Kwenda Mkoa Mwingine, unatakiwa Kuwa na Movement Order

Shahidi: Inategemea na Siku Ngapi, Kama Chini ya Siku Tatu unaweza Kwenda bila Movement Order kama zaidi ya Siku Nne Unatakiwa Kuwa na Movement Orde

Matata: Wakati Unahojiwa na Wakili Abdallah Chavula Uliyasema hayo

Shahidi: sikuyasema

Matata: Unapokuwa Askari Unapoenda Ofisi za Umma si lazima Uwe na Pass

Shahidi: Ni kwenye Kitabu Unachotaka,

Matata: Si lazima uonyeshe Pass

Shahidi: Ndiyo ni lazima

Matata: Umeleta Mahakamani hapa Pass Kwamba Umeruhusiwa Kutoka kazini Kwako

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Sijaleta Sikujua I nahitajika Mahakamani

Matata: Tarehe 11 ulienda kwa Inspector Swila na Tarehe 12 Ulimpelekea Simu

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Ulileta Mahakamani Hapa Pass za Umeruhusiwa

Shahidi: Sikuleta, Sikupewa Maelezo

Matata: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo Namba 20

Matata: Naomba Nikuonyesha Kielelezo namba 20 ambacho Kina Miamala yako ya namba ya Airtel

Matata: Jana Wakati Unahojiwa ulisema Freeman Mbowe alikurushia Kwa Mara ya Kwanza TSh 500,000

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Na Ukatoa TSh 499,000

Shahidi: Kweli

Jaji: Umeelewa Swali? Anasema Umetumiwa TSh 500,000, Swali Ukatoa kwenye hiyo Fedha kiasi gani?

Shahidi: Ni TSh 499,000

Matata: Kwa Mantiki Nyingine Hukutoa yote Kwa sababu Kuna Makato kidogo

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Kwa hiyo Ulichukua TSh 500,000 Ukatoa TSh 499,000 Je Makato TSh ngapi?

Shahidi: TSh 1000

Matata: Naomba Nikuonyeshe Kwa Siku hiyo, Mheshimiwa Jaji Namuonyesha Muamala Wa Siku hiyo ambapo anasema alitoa Muamala Wa TSh 499,000

Matata: Sasa Shahidi angalia Tarehe 20 July 2020, Kwenye Miamala sehemu ambayo Umeenda Kwa Wakala Ukatoa TSh 499,000

Jaji: anakuuliza Hapo Hapo hapo Kwenye hiyo Nyaraka

Shahidi: Hapa Kwenye Miamala Haipo hiyo 499,000

Matata: Mheshimiwa Jaji naomba ni Muonyeshe Hapo hapo, Kuna Majedwali ambayo Yanaonyesha Receiver Balance kabla ya kutumiwa TSh 500,000 kutoka Kwa Mbowe.. Utakubaliana na Mimi Kwenye akaunti yako palikuwa na TSh 49,646

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Baada ya Kuweka TSh 500,000 balance Ikawa TSh 549,646

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Na Tarehe hiyo hiyo Ukatoa TSh 300,000

Shahidi: Ni sahihi

Matata: Na Balance Yako Ikabakia 243,646

Shahidi: Ni sahihi

Matata: hebu chukua salio uliokuwa nalo la 549,646 Kutoa 300,000 ukabaki na 243,646 tuone Makato ni TSh ngapi

Amesimama Mmoja Wakili wa Serikali Robert Kidando

Wakili wa Serikali Robert Kidando: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Naona Hajajengewa Misingi Kwamba wakili anauliza ikiwa hayo Makato yapo au hayapo..

Matata: Mheshimiwa Jaji Mimi lengo langu nikutaka kujua kwanini Shahidi atoe TSh 499,000 akatwe TSh 1,000 na atoe TSh 300,000 akatwe Elfu Sita na usheeee..

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hicho ndicho alichopaswa Kuulizwa

Matata: Je Shahidi Utakubaliana na Mimi Kwamba Ukitoa TSh 300,000 ikibakia TSh 243,646 Je Elfu 6 inaenda Wapi?

Shahidi: Siwezi Kujua Kama ni Makato au imeenda wapi

Matata: Kwani hiyo Tsh 1000 Mwanzo Ulijuaje Kama ni Makato

Shahidi: (Kimya)

Jaji: Swali lako la Mwisho liasema Kuhusu Elfu 6 nimesharekodi

Mallya anasaidia kufafanua kidogo

Matata: Shahidi Ulitoa maelezo hii TSh 1,000 Ilienda wapi

Shahidi: Sijawahi Kutoa

Matata: Shahidi sasa ulitoa...sorry Mheshimiwa Jaji Kidogo

Matata anapekua Nyaraka hapa

Matata: Shahidi Umesema Freeman Aikael Mbowe alikuwa na Mpango Wa Kulipua Vituo Vya Mafuta, Je Wakati Unahojiwa ulitaja Majina ya Vituo Vya Mafuta

Shahidi: Hakuniambia Vituo Vya mafuta anavyoenda Kulipua Bali alitaja Mikoa tu

Matata: Kwa hiyo ukiulizwa Alitaka Kulipua Vituo gani Morogoro hutakuwa na Majibu

Shahidi: Sitokuwa na Majibu kwa kweli

Matata: Tukisema Utaje Vituo Vya Mafuta alivyo taka Kulipua Mkoa wa Mwanza Utakuwa na Majibu au hutakuwa na Majibu

Shahidi: Mimi sina Majibu, Majibu atakuwa nayo Freeman Mbowe

Matata: Ukiulizwa pia Kuhusu Mkoa wa Dar es Salaam Vituo Vipi Vya Mafuta alitaka Kulipua

Shahidi: Mimi sina Majibu, Majibu anayo Freeman Mbowe, Mimi alinificha

Matata: Ukiulizwa ni eneo gani alipanga Kukata Miti kati ya Mkoa wa Morogoro na Iringa

Shahidi: Hakuniambia ni Eneo gani

Matata: Ukiulizwa, Ukiachana Na Sabaya ni Viongozi gani wengine Walipanga Kuwashambulia

Shahidi: Sikutaja Jina la Kiongozi Yoyote, Hakuniambia Kiongozi Yupi

Matata: Mpaka anakushirikisha bila Shaka alikuwa anakuamini

Shahidi: Ndiyo

Matata: Ukiachana na suala la Kumtafutia Vijana, Je alikueleza kuhusu kumtafutia vilipuzi

Shahidi: Hakunieleza

Matata: Kuhusu kumtafutia silaha za kuwashambulia viongozi

Shahidi: Hakunieleza

Matata: Naomba Kurejesha Kielelezo cha simu .. Ahsante

Mallya: Mheshimiwa Jaji, hata hivyo haiwaki.

Matata anaketi..

Anasimama Wakili Peter Kibatala

Kibatala:
Shahidi Nikikuita baba Careen ni sawa?

Shahidi: Ni sawa

Kibatala: Baba Junior

Shahidi: Ni Sawa

Kibatala: Baba Jackson

Shahidi: Ni sawa

Kibatala: Jackson amezaliwa Lini

Shahidi: 17 December 2020

Kibatala: Hospitali gani

Shahidi: Hospitali Ya Mkoa Morogoro

Kibatala: Nani na nani alikwepo

Shahidi: Mke wangu na Jirani

Kibatala: Wewe ni Mkristo

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: unasali Kanisa lipi

Shahidi: Parokia Ya Ngerengere, Kigango cha Kizuka

Kibatala: Paroko wako Unamfahamu

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Kwani Kanisani Umeenda Mara ya Mwisho lini?

Shahidi: Juzi juzi

Kibatala: Paroko anayehudumu Ngerengere Unamfahamu

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Katekista anayemsadia Paroko

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: narudia tena Mara ya Mwisho Kanisani Umeenda Lini

Shahidi: Sikumbuki Kusema Kweli

Kibatala: Una Gari ya silver

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Aina gani

Shahidi: Rav 4

Kibatala: Namba zake zipi

Shahidi: T 114 DHL

Kibatala: Toka Mwaka 16 August 2020 hiyo Gari ipo Wapi

Shahidi: Kazini Kwangu Ngerengere

Kibatala: Toka Tarehe 16 August 2020 Gari hii ilikuwa parked Wapi

Shahidi: Nilikuwa natumia, Kila Nilipo ipo

Kibatala: Baada Tarehe 16 August 2020 Gari hii umeitumia

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Umekuja kutoka Morogoro kutoa ushahidi kwenye hii Kesi, na kwamba siyo kutoka kambi fulani ya Jeshi ulikokuwa umetekwa?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji (Shahidi kamuita Jaji hapa ana jambo gani?)

Kibatala: Ndugu shahidi RELAX..

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Mawakili Uliwakataza Kutoa Mawazo yao Bali Kuulizwa maswali

Kibatala: Shahidi hiyo Gari Ipo wapi

Shahidi: Kambini Kizuka

Kibatala: Umepeleka lini hiyo Gari

Shahidi: Ijumaa Wiki Iliyopita

Kibatala: Utaratibu gani Umetumika kupark hiyo gari

Shahidi: Park at Your Own Risk

Kibatala: Kwa hiyo wewe Kama afisa wa Jeshi unataka Kuniambia Kuwa Una park Gari at Owner's Risk Kambini, Upo serious kweli wewe?

Shahidi: Lipo Katika Parking ya Staff

Kibatala: Bado Kwamba Unaendelea Kusema Gari ipo Parking Owner's Risk?

Shahidi: Hapana Nimeliondoa jibu la Owner's Risk

Kibatala: Jibu lako la Kwanza kwamba Uli park Chini ya Owner's Risk Ulilitoa Chini ya Kiapo?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: haya, Turudi tena Kwamba Gari Umei' park Kwa Utaratibu gani

Shahidi: Pale Hakuna Ku'Register, Nilitoka Kwenye Oparation Nikaambiwa Nije kutoa Ushahidi

Kibatala: hapo Maana yake ni Owner's Risk

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: si Ndiyo umeliondoa hilo Jibu

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Naiachia Mahakama Twende Eneo Lingine

Kibatala: Mwanzo Ulisema Ulikuwa unapanda Tax huna Gari

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Basi Ujue kwanini Nimekuuliza Kuhusu Gari

Kibatala: Shahidi Fungua Yohana Sura ya 8, Mstari wa 31 Mpaka 39

Shahidi anasoma biblia hapa..

Amemaliza..

Kibatala: Unafahamu Maan ya hilo Neno

Shahidi: Ndiyo Nafahamu

Kibatala: Maana yake ni nini

Shahidi: Tusiogope, Tuseme Kweli

Kibatala: Soma pia Waefeso Sura ya 4 Mstari Wa 25 Mpaka 32

Shahidi anasomeshwa Biblia tena

Kibatala: Je, unafahamu Maana ya hilo Neno

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Maana Yake ni nini

Shahidi: Tusiseme Uongo na tupendane

Kibatala: Kwa Hiyo Unafahamu Kwamba Maisha ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya yapo Mikononi Mwako

Shahidi: Ndiyo najua

Kibatala: na Ulisema Kwamba Mara Ya Kwanza Ulikutana na Mbowe Lini

Shahidi: JULY 2020

Kibatala: Tarehe Ngapi

Shahidi: Sikumbuki ni Tarehe za Kati kati

Kibatala: zipi hizo

Shahidi: Tarehe 10 Mpaka 15

Kibatala: Hizo ndiyo Tarehe za Katikati

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: na wewe ni Luten wa Jeshi la Wananchi Tanzania tunalolipenda wote

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Elimu yako ni Form Four

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ulipata Divisheni Ngapi

Shahidi: Three ya Point 25

Kibatala: unajua Division Four Inaanza point ngapi

Shahidi: Point 28 ila Sikumbuki Vizuri

Kibatala: Kwa hiyo Unakumbuka au hukumbuki

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Umesoma wapi.?

Shahidi: King'ori Sekondari

Kibatala: Headmaster Wako ni nani

Shahidi: Simkumbuki

Kibatala: Graduation Mlifanya lini

Shahidi: Hatukufanya Graduation

Kibatala: Ukimaliza Form Four lini

Shahidi: Mwaka 1999

Kibatala: Yule Mchungaji Wako anayefundisha Mzumbe Mara ya Mwisho Kuwasiliana naye ni Lini

Shahidi: Sina Mchungaji

Kibatala: Na Nabii Tito anayefundisha Mzumbe Umeacha Kusali Kwake lini

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Habari Nzito ya Mbowe Ulimshirikisha Paroko au Mchungaji

Shahidi: Sikumshirikisha Mtu

Kibatala: lakini Ulishindwa kulala

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: lakini Ukaenda Kumshirikisha nani

Shahidi: DCI na Kingai

Kibatala: Mwingine Je?

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Msemo wa Kwamba Askari hawezi Kuwa Raia ila Raia anaweza Kuwa Askari Maana yake nini

Shahidi: Kwamba Ukishakuwa Askari huwezi kuwa Raia, Ila Raia anaweza Kwenda kujifunza Kuwa Askari

Kibatala: Jeshi la Wananchi Tanzania Mnafundishwa Kuwa Jeshi la Polisi ni Jeshi Kweli au si Kweli

Shahidi: Kweli

Kibatala: Raia Akiona Uhalifu unatendeka anaweza Kuzuia Uhalifu

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwamba Mwajeshi Akiona Uhalifu Unatendeka anaweza Kuzuia au anaacha utokee alafu ana report Taarifa Polisi

Shahidi: Anazuia Uhalifu

Kibatala: ila wewe Ulikuwa na Mbowe anakwambia Mambo ya Kigaidi ukamuacha

Shahidi: Ndiyo Maana Nilienda Ku report Polisi

Kibatala: Kwani Jeshini si Kuna sehemu ya kwenda Kutoa Taarifa za Kihalifu

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Jeshi la Wananchi Tanzania Kuna Kitengo Kina shughulika na Ugaidi

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kuna Jeshi la Navy ambalo kazi yao Ni Kushughulika na Ugaidi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: na bado wewe ni Luteni wa Jeshi kabisa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwani kwa ufahamu wako wewe Jeshi halishirikiani na Jeshi la Polisi

Shahidi: Kama ikihitajika

Kibatala: Kwani Shahidi Kwa Mfano Mbowe angelipua Kituo cha Mafuta Puma pale Mwenge, Jeshi Pale Jirani Wangedhurika au Wasingedhurika

Shahidi: Wangedhurika

Kibatala: Bado Ukaona Usiwaambie Jeshi

Shahidi: (Kimya)

Kibatala: unasema Kwamba Mbowe alikwambia Kukata Miti wapi

Shahidi: Kukata Miti Kwenye Barabara zote zinazo ingia Mjini

Kibatala: pale Kambi ya Jeshi Lugalo Kuna Barabara ya Kuingia Mjini au Hakuna

Shahidi: Ipo

Kibatala: Kama Wangekata Miti pale Barabara ya Lugalo Jeshi lingedhurika au lisingedhurika

Shahidi: Lingedhurika

Kibatala: Lakini Bado wewe Ukaona Usiwaambie Jeshi

Shahidi: Nilipeleka Taarifa Polisi Kwa sababu wao Wana husika na Uchunguzi

Kibatala: Kati ya Wewe Ulipo pale Mgulani Kambini na Ofisi za DCI, Wapi Ilikuwa Rahisi Kwako Ku report?

Shahidi: Kambini Mgulani

Kibatala: Unafahamu Kitu kinaitwa Logic na Common sense

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: haya pale kwa DCI umesema Kwamba Kuna Scanner, Umejitambulisha Kuwa wewe ni Luteni na ukafanyeje

Shahidi: Nikatoa Kitambulisho

Kibatala: Baada ya Pale Ulimwambia Jaji Kwamba Jina lako liliingizwa Kwenye Register

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Unafahamu Kwamba sisi tumefika Kwa DCI Mara ngapi

Shahidi: Hapana, Sijui

Kibatala: Nikikukwambia Kwamba pale kwa DCI Nilifika Kumsindikiza Edward Lowassa Mwaka 2017

Shahidi: Ndiyo nitakubali

Kibatala: Unafahamu Kuwa DCI ni Mwanajeshi

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Ulimwambia Jaji Kwamba Kuna Mtu alipiga Simu Kwanza Kuhakiki appointment Yako

Shahidi: Hapana Sikumwambia

Kibatala: Unafahamu Kwamba Wanajeshi hasa DCI ambaye ndiye Kama WAZIRI Mkuu wa Jeshi la Polisi ni watu wa tahadhari kwa sababu ni Watu wana deal na Uhalifu Nchi Nzima?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je, Umemwambia Jaji Kwamba Kuna Kitambulisho Ulipewa cha Kuvaa

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Unafahamu Kwamba Kwa DCI Kuna Askari Kwa ajili ya Kimsindikiza Wanaenda Kwa DCI

Shahidi: Sikumwambia Jaji

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kuna Askari Wa Kukusindikiza Mpaka Kwa PS wa DCI

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Waiting Area ya Ofisi za DCI Makochi ni Rangi gani

Shahidi: Ya Brown

Kibatala: Unauhakika Kwamba Siyo Mekundu

Shahidi: (Kimya)

Kibatala: Ukifika kwenye Ofisi za DCI PS anakuwa Upande Upi

Shahidi: Upande huu, (anaonyesha Kushoto)

Kibatala: Umebadilsha Sasa hivi eeh?

Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba niilipokuwa Ulipokuwa wait Area Kwa DCI iwapo Body Guard Wake Ukiwa Una subiri Kuingia

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Je Jana wakati wa Ushahidi Ulizungumzia Meza na Viti, Je Ulizungumzia DCI kuwa Ni Mnene, Mfupi, Mwembamba au Lah

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Je Ukaona ni Muhimu tufahamu Viti na Meza na siyo DCI ambaye Ulimfuata

Shahidi: DCI SI anajulikana

Kibatala: anajulikana na nani

Shahidi: Watanzania wote

Kibatala: Je Ulimwambia Jaji Kwamba Utaratibu gani Ulitumia Kutoka

Shahidi: Sijamwambia

Kibatala: Ulimwambia Jaji Kuwa Ulipokuwa Unatoka Ulisaini Out

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Unasema Ulifika Ofisi ya DCI Saa ngapi

Shahidi: Nimefika Majira ya Saa Mbili au Saa Tatu

Kibatala: Je Unafahamu Kwamba Huo Ndiyo Muda wa Kufika DCI

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Kwamba Chini ya Kiapo hapo Luteni Kwamba Siku hiyo DCI alipanda Ngazi Kwa Mguu Mpaka Ghorofa Ya Saba

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kwa hiyo ufahamu Kwamba DCI alikuwa na Umri Miaka zaidi ya 50 na Sasa amestaafu Kwamba alipanda Ngazi

Shahidi: Sifahamu alifikaje Juu

Kibatala: kwa hiyo Wewe Unasema Kwamba DCI Kiongozi Wao Kama. Waziri Mkuu, Kuwa Lift yake Ilikuwa bovu

Shahidi: Hapana, Sifahamu

Kibatala: Jana Ulionyeshwa Simu zako, na Moja ilikuwa na Display ya Mke Wako

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Wakati Simu zako zote Nne Umepewa, Je Ni wakati gani Uliomba nafasi ya Kungalia Simu yako Namba ya Kingai Kama Kweli uliwasiliana naye?

Shahidi: Hapana Sikumwambia jaji

Kibatala: Je Kwa DCI pia ulimuomba Jaji nafasi ya Kungalia namba ya DCI Kwenye Simu yako?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Sasa Ni saa Saba Kamili, Kama Wenzetu wataridhia Twende Health Break na naomba Niependekeza Kwako Dakika 45

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi

Jaji: Kwa Maana hiyo tuta' break Kwa Muda wa Dakika 45 na Saa Saba na Dakika 45 tutarudi

Jaji amerejea

Kesi imetajwa

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wa Jamhuri tumetimia Kama Ilivyo kuwa Mwanzoni tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Quorum yetu ipo Kama Mwanzo, Wakili John Mallya amepata Udhuru atarejea Baada ya Dakika 10 badala yake naomba Wakili Michael Lugina awakilishe Ingawa ni wakili wa Mshtakiwa Wa Nne

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Naona italeta Shida, Kwa sababu Wakili Michael Lugina Tayari ameshaingia Kwenye Quorum, Mshtakiwa Wa Pili anahitaji Kupata Full representation..

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa Maoni yangu Mimi, Mimi Ndiyo Nina Cross Exermine, Ila Ooohh Kwa Bahati Nzuri ndiyo anaingia... Huyu hapo.. Ikupendeze Kurekodi kuwa Sote Tupo na tupo tayari Kuendelea

Jaji anaandika Kidogo, Mahakama ipo Kimya wakati huu

Jaji: Shahidi nakukumbusha kuwa Ulikuwa Chini ya Kiapo wakati Unatoa Ushahidi Na Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo Wakati Unatoa Ushahidi

Jaji: Shahidi nakukumbusha kuwa Ulikuwa Chini ya Kiapo wakati Unatoa Ushahidi Na Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo Wakati Unatoa Ushahidi Wakili

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kwa Hisani ya Mwisho Nikumbushwe Swali lake

Jaji: Kama Iwapo Alikuwa na Simu zake na Kama Aliomba Mahakama atoe humo namba za DCI Akasema Hapana

Kibatala: Unafahamu Kwamba Utambulisho Wa su Moja dhidi ya Nyingine ni IMEI, Je unafahamu

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Wakati Unaongozwa na Mawakili Wenzetu wa Somi waliluomhoza Kutoa Nyaraka fulani hivi

Shahidi: Ndiyo Nakumbuka

Kibatala: Kwahiyo Nyaraka Ile Ilikuwa ni Kuthibitisha Kuwa palikuwa na Makabidhiano kati yako wewe na Inspector Swila

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Inaitwa Techno nini Vile

Shahidi: Tecno CAMMO

Kibatala: Niambie Kama wakati Unaonyeshwa Simu zako zote Nne, Je ulitambua Simu Moja Moja Kwa kutumia IMEI namba Shahidi Hapana, Nilitambua Moja tu

Kibatala: Kwahiyo Kama tuna Simu Nne, Tatu hukuzitambua kwa IMEI namba ya Simu Moja Moja

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: kwa hiyo hii Tecno CAMMO ulitambua Kwa IMEI namba

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwa Ushahidi Wako wote hapa umesema Kwamba Unaishi Ngerengere, Je Kuna sehemu Umesema Kwamba unaishi kihonda

Shahidi: Nina Makazi Mawili Ngerengere na Kihonda

Kibatala: Je Ulisema Jana na Leo Kabla Sijakuuliza

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Je Kuna Mahala Popote Ulitambua Maneno CAMMO Kama Yapo

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Kuna Maneno gani badala yake

Shahidi: Tecno tu

Kibatala: Je, Wakati Unaongozwa na Wakili Wa Serikali Abdallah Chavula Ulimfafanulia Mheshimiwa Jaji Kwamba hiyo Tecno ndiyo Tecno CAMMO

Shahidi: Sikufafanua

Kibatala: Wakati Wa Ushahidi Wako Wote Unaongozwa na Wakili Wa Serikali Abdallah Chavula, Uliongozwa kutoa Betri na Kusoma IMEI namba na Kumwambia Mheshimiwa Jaji Kama IMEI zinafafana na Inspector Swila Wakati wa Makabidhiano?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Soma Hapa Pameandikwa Kwamba wewe Luteni Urio unaishi Wapi

Shahidi: Kihonda

Kibatala: Je, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kwenye Kielelezo Kuwa wewe Luteni Urio Unaishi Kihonda Shahidi anatikisa kichwa hapa, namna gani..

Kibatala: Mahakamani, Usijibu kwa Kichwa

Shahidi: Sikumwambia Mheshimiwa Jaji

Kibatala: Soma Hapa

Shahidi: CD/IR/2097/2020

Kibatala: Ni nini hiyo

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je Ulifafanua ni nini hicho

Shahidi: Sikufafanua

Kibatala: Kuna IMEI namba Ngapi hapo

Shahidi ameshika Kielelezo cha karatasi moja

Shahidi: Sijui ni IMEI namba ngapi

Kibatala: Unafahamu Inspector Swila alikozitoa hizi IMEI namba au hufahamu

Shahidi: Kwenye Simu yangu

Kibatala: Je, Zipo ngapi hizo IMEI namba zipo ngapi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Hiyo ni Standard Form Document

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Soma hapo chini

Shahidi: Jina na Sahihi ya anayekabidhiwa

Kibatala: Wakati unatoa Ushahidi Jana Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba hiyo ni sahihi yako

Shahidi: Nilimwambia

Kibatala: Soma Hapo Chini ya Mstari Uliochapwa

Shahidi: 11 August 2020 Imeandaliwa Chini ya

Kibatala: ulifafanua Kuwa Kwanini hayo Maelezo Yapo Chini ya Nyaraka

Shahidi: Siku fafanua

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Nyaraka inasema Mimi Luteni Denis Urio Wa Kihonda Morogoro, Na mkabidhi Vitu ambavyo Vimekamatiwa Tarehe Deshi, Kutoka Kwa Mtuhumiwa Deshi, Vitu aina ya Deshi, Ushahidi Wako wewe Tukiangalia Kwenye Deshi tunaweza Kujua ni nini

Shahidi: Sijui ni nini

Kibatala: Mkumbushe Mheshimiwa Jaji Ulisema Simu yako wewe Ulikabidhi sababu ya

Shahidi: Uchunguzi

Kibatala: ambapo Wewe Unaamini ilikuwa Mawasiliano ya wewe na nani

Shahidi: Mheshimiwa Mbowe

Kibatala: Tuache Simu, Turudi Ofisini Kwa DCI

Kibatala: Lengo la Kutaja Meza na Viti Kwa DCI Lengo ilikuwa Kuonyesha Kwamba Ulifika kwa DCI, Mwambie Mheshimiwa Jaji kama Ulimwambia kuwa Meza ni ya Rangi gani

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Kwakuwa Lengo lako lilikuwa Kuonyesha Unaifahamu Ofisi ya DCI Je Ulisema Juu Palikuwa na nakshi gani

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Kwa kuwa Lengo lako lilikuwa Kuonyesha Unaifahamu Ofisini ya DCI Je Ulisema Juu ya Rangi ya Viti

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Je Umwambia Jaji Details zingine Kuhusu ile Ofisi

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Unafahamu Kama Ofisi Ya DCI Kuna Bendera ya Taifa

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Sasa Ulimwambia Detail hiyo Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Unafahamu Kwamba Ofisini Kwa DCI kuwa Kuna Picha ambazo zinaonyesha Matukio Mbalimbali ya Utejelezaji Wa Majukumu Yake

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Je, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuhusu hilo

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Je, ofisini kwa DCI kuna kalenda zaidi ya Tatu

Shahidi: Niliona moja

Kibatala: Ulimwambia kuhusu hiyo kalenda moja

Shahidi: Sikumwambia, na pembeni ya Kiti chake kuna kiti kingine pia sikumwambia Mhe Jaji

Mahakama: (Kicheko)

Kibatala:
ahsante kwa taarifa

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa Ofisini Kuna Beseni la Kunawa Mikono

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Je, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Ofisini Kwa DCI palikuwa na Askari Wangapi Wa zamu

Shahidi: Walikuwa wawili Ila Sikumwambia

Kibatala: Kwamba Pale Reception Kuna Magari ya Viongozi Mazuri Mazuri, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Hapana Sikumwambia

Kibatala: Pale Nje Kuna Gari ya Rapid Response, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Umeliona

Shahidi: Sikumwambia, Ila siku hiyo halikuwepo

Kibatala: Unakumbuka Juu ya somo letu la TRUTH SHALL SET YOU FREE?

Shahidi: Ndiyo nalikumbuka

Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kwanini ulishindwa Kumweka Mheshimiwa Mbowe Chini ya Ulinzi?

Shahidi: Hapana Sikumwambia

Kibatala: Ni nini cha Ziada Kilichoongezeka kutoka Tarehe July 2020 Mpaka Leo hapa Mahakamani

Shahidi: Tuna Amani tu Tanzania

Kibatala: Tarehe ya Katikati ya July 2020, Toka Kipindi Kile Mpaka Leo ni zaidi Ya Mwaka sasa, Je Kuna Kitu cha Ziada ambacho wewe Binafsi Moyoni Mwako ulipata Taarifa ya ziada

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Swali hilo lime Ulizwa na kujibiwa, Amani.

Kibatala: Twende Eneo Lingine, Unasema Baada ya Kupata Taarifa za Freeman Mbowe Kupanga Uhalifu, Bado Unasema hukumbuki Tarehe?

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Swila anasemw alifungua Faili lake Tarehe 18 July 2020, Unaweza Kukumbuka Siku Uliyoenda Kwa DCI

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: sisi shida yetu ilikuwa ni Kutaka Kujua Kama Ulifika kwa DCI lini Tujue kuwa Faili lilitungwa au la

Shahidi: Siwezi Kukumbuka Tarehe

Kibatala: Kwa Mujibu wa Bando Kitita la Commital hata DCI hajui Wewe Ulifika Lini Ofisini Kwake

Shahidi: Siwezi Kumsemea

Kibatala: Je Unakumbuka Tarehe Uliyokutana na Khalfani Bwire

Shahidi: Sikumbuki ila ilikuwa Mwenzi Wa Saba

Kibatala: Je, Khalfani Bwire Uliwasiliana naye lini akiwa Tunduma

Shahidi: Sikumbuki ila Katikakati ya Mwezi Wa saba

Kibatala: Na Adam Kasekwa Uliwasiliana naye lini

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Kwa Mujibu Wa Mohammed Ling'wenya katika Maelezo Yake anasema Kwamba Tarehe 24 July 2020 Mkakutana Morogoro Shahidi Ndiyo

Kibatala: Siku Sita Tangu Inspector Swila aseme alifungua Faili Tarehe 18

Shahidi: Sijui

Kibatala: Si upige Hesabu Kutoka Tarehe 18 July 2020 Mpaka 24 July 2020 ni Siku ngapi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Umeanza Kuwakusanya hawa baada ya Tarehe 20 July 2020

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Na wewe ndiyo Ulikuwa Unawafahamu hawa wala Siyo Mbowe

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unaweza Kutuisaidia Kuwa Kwanini Inspector Swila alifungua Faili la Kula Njama Tarehe 18 July 2020 Wakati Wakati Umekutana hawa Vijana Tarehe 20 Mpaka 24

Shahidi: Sijui sasa

Kibatala: Je wewe Ulikula Njama na Mbowe.

Shahidi: Sijala Njama na Mbowe

Kibatala: Kwani Shahidi suala hili Kuna Mtu Zaidi Yako alienda Kutoa Taarifa Kwa DCI

Shahidi: Ni Mimi Pekee Yangu ndiye niliye Mwambia DCI Kibatala Kwani wewe Ulimueleza Jaji Kwamba Mbowe alikuwa tayari ana vijana Wengine

Shahidi: Sikumwambia Mheshimiwa Jaji

Kibatala: Baada ya Kutoka Kwa DCI ulienda Wapi

Shahidi: Morogoro

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Ulitumia Usafiri gani Kurudi Morogoro

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Je, baada ya Kutoka Kwa DCI Ulifika Nyumbani Kwako Usiku

Shahidi: Nilifika Jioni Jioni

Kibatala: Tuambie nani alikwepo Nyumbani Kwako ulimkuta Siku hiyo

Shahidi: Mke wangu

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba alikwepo Mtoto wako Careen Nyumbani kwako

Shahidi: Alikwepo Mke wangu na Watoto

Kibatala: Unabadilisha Enheeeee

Kibatala: haya Ulitumia Basi gani Kurudi Morogoro

Shahidi: Abood bus Service

Kibatala: Je Unayo ticket

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mimi na Malya tunafahamu CASA Motel, na Kila Gari Inayoingia pale inasajiliwa

Shahidi: Sijui

Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Gari yako Tax ile Ilisajiliwa pale Mlangoni

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba CASA Motel ni Nyumba ya Chini au Ghorofa

Shahidi: Ni Ghorofa

Kibatala: Ndiyo hiyo si Taarifa Muhimu

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji sasa

Shahidi: Hapana Siku Mwambia

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba mlilaa sehemu gani, Nje au Ndani

Shahidi: Hapana Siku Mwambia

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba mlikaa kwenye Makochi ya namna gani

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Ushahidi Wako Kuwa Mbowe Mwenyekiti Wa Chadema Taifa, alikuwa CASA Motel Bila Dereva wala Mlinzi

Shahidi: Nilisema Alitupokea Kijana Mmoja akasema Chairman Yule Pale

Kibatala: Sasa Ulimwambia Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Hapana Siku Mwambia

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba aliyekuwa anaye wahudumia ni Mwanamke au Mwanaume

Shahidi: Hapa Sikumwambia

Kibatala: Je wewe Luteni Wa Jeshi Moja ya ulichojifunza ni Kufanya kazi Katika High Pressure, Si Ndiyo

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Moja ya Ulichojifunza ni Kuongeza umakini

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Sasa Afisa wa JWTZ nimesoma tangu Wakati wa Willy Gamba, Luteni Unaitwa sehemu na Mtu ambaye humjui unaenda tu?

Shahidi: Nilikuwa namsikia kwenye TV tu

Kibatala: Mtu akakupigia yeye ni Peter Kibatala akakuita Goba Unakuja tu

Shahidi: Alikuwa anawasiliana Siku nyingi

Kibatala: Ulipokuwa Pale Kwa Mhe Freeman Mbowe, Nani alilipa Chakula

Shahidi: Freeman Mbowe

Kibatala: Nani alilipa Tax Yako

Shahidi: Freeman Mbowe

Kibatala: Pamoja na Kukwambia Taarifa za Ugaidi bado Ukapokea Fadhila zake

Shahidi: Siyo Taarifa za Ugaidi, Ni Uhalifu tu

Kibatala: Kwa hiyo Baada ya Kukwambia Mipango hiyo ya Uhalifu, Bado alilipia Tax Yako

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je, wewe Kama Luten wa Jeshi, Ulimwambia Mtu yoyote Kuhusu Swala hilo

Shahidi: Nilimwambia CEO wangu

Kibatala: Ulimwambia lini

Shahidi: Tarehe 05 August 2020

Kibatala: hayo Mambo Uliyo enda Kumwambia CEO wako, Yapo Katika Maelezo Yako Uliyo andika Kwa Inspector Swila

Shahidi: Hayapo Katika Maelezo yangu

Kibatala: hayo Unayosema Kwamba Ulienda Ku report Kwa CEO wako, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji

Shahidi: Sikumbuki Kama nilimwambia

Kibatala: Mimi Nikikwambia hujamwambia?

Shahidi: No, Sikumbuki nilitamka Kwenye situation gani

Kibatala: Mlikaa na Mbowe pale CASA Motel akakwambia Masuala Kadhaa wa Kadhaa

Shahidi: CASA Motel Siyo Wakati wa hiyo Mipango, CASA Motel ni Wakati wa 2012

Kibatala: Baada ya Kujua Mbowe ana mipango ya Kigaidi Uliendelea Kuwasiliana naye

Shahidi: Ndiyo nilikuwa naendelea Kuwasiliana naye ili Kumtafutia Watu wa Kutekeleza Mipango yake

Kibatala: Ni kweli Kwamba Ulishiriki Mipango ya Kigaidi

Shahidi: Sikushiriki

Kibatala: Nani aliyemuwezesha Mbowe Kupata hao Vijana Kutekeleza Mipango ya Kigaidi

Shahidi: Ni Mimi

Kibatala: Wewe ni Afisa Wa Jeshi, Je Unafahamu Sheria yoyote Inayoruhusu wewe Kutafuta Vijana Kutekeleza Mipango ya Kigaidi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Wewe si Ulikuwa Darfur

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kilichokufanya Mpaka Muende Darfur ni Janja Weed na SPLM

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je Ingewezekana Wewe Askari Umeenda Darfur Chini ya Chapter Seven Ukawa Unafanya Mawasiliano ya Simu na Kiongozi wa Janja Weed?

Shahidi: Nisingeeleweka

Kibatala: Ni Kwa Sababu Yule alikuwa Mhalifu wa Amani?

Shahidi: Ndiyo alikuwa Mhalifu Wa Amani

Kibatala: lakini huku Tanzania ulikuwa Unawasiliana na Freeman Mbowe

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Je Kule Darfur Ungemuita Kiongozi Wa Janja Weed "Bro" Ungeeleweka?

Shahidi: Nisingeeleweka

Kibatala: Kwani Kule Darfur Si palikuwa na Askari Wengine Wa Chapter Six Wanaofanya Peace Keeping wapo armed na wanafanya Demining?

Kibatala: na Kwamba Wewe Kabla ya Tarehe 05 August 2020 Hakuna Uliyekuwa Umempa Taarifa Ndani ya Jeshi Kuwa Umepewa Kazi na DCI na Kingai

Shahidi: Sikumwambia Mtu

Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba huyo Dogo Adam Kasekwa anajina lingine anaitwa Adamoo

Shahidi: Hapana

Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Mohammed Ling'wenya anajina Lingine anaitwa DOYI

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Unafahamu Moses Lijenje Yupo wapi

Shahidi: Nilimkabidhi Kwa Freeman Mbowe

Kibatala: Moses Lijenje Yupo Hai au amekufa

Shahidi: Nilimkabidhi Freeman Mbowe

Kibatala: ulimkabidhi Wapi

Shahidi: Nilimpigia Simu akasema Kwamba ameshafika

Kibatala: Nikuonyeshe Meseji zako utanionyesha sehemu ambayo ina meseji Kuwa Mbowe anasema Umemkabidhi?

Shahidi: Hakuna. Alinipigia Simu

Kibatala: Jana Ulionyesha Sauti zako za Kukabidhiana Kwa Mbowe Moses Lijenje

Shahidi: Hapana

Kibatala: Wewe Mpaka Unaonana na Moses Lijenje, alikuwa anafahamu Masuala ya Ugaidi

Shahidi: Hapana, Masuala ya Ulinzi

Kibatala: Wewe Ulionana Lini tena na Moses Lijenje Baada ya Tarehe 21 August 2020

Shahidi: Sikuonana naye tena

Kibatala: Walicho ongea Na Mbowe Huko Hai au Popote unakifahamu

Shahidi: Sikifahamu

Kibatala: Unaweza kuonyesha chochote kile au sauti ukionyeshe kwa mheshimiwa Jaji kwamba Freeman Mbowe alimwambia Lijenje wakafanye ugaidi?

Shahidi: Sijawahi kusikia mimi

Kibatala: Ni sahihi kwamba hakuna Pesa iliyotoka Moja Kwa Moja kutoka kwa Mbowe Kwenda Kwa Moses Lijenje

Shahidi: Hakuna

Kibatala: badala yake Shahidi Unasema Mbowe alituma Laki Tano ambayo iingia Kwenye Simu yako, halafu wewe Ukatoa ya kwako
Mfukoni

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Nakuuliza tena, Kuna Pesa unazo Mfukoni Mwako, na Mbowe katima. Pesa za Kwenye Simu, Je pesa uliyompa Moses Lijenje, ulitoa Kwa Wakala Ukampa au Ulitoa za Kwako Mfukoni

Shahidi: Nilitoa Laki 3 kwenye muamala, Nikachanganya na za Kwangu Mfukoni

Kibatala: Unasema Kwamba Moses Lijenje Ulikutana naye Morogoro Tarehe ngapi

Shahidi: Tarehe 21 August 2020

Kibatala: na hiyo Fedha Ulipokea Lini Kwenye Miamala

Shahidi: Tarehe 20 August 2020

Kibatala: Na hiyo 500,000 ulipokea Kutoka Mbowe Moja kwa Moja?

Shahidi: Hapana Kwa Wakala

Kibatala: Wewe Ulitumiwa TSh ngapi

Shahidi: 500,000

Kibatala: Kwa Wakala Ulitoa TSh Ngapi

Shahidi: TSh 300,000, na Mfukoni nilikuwa na 199,000

Kibatala: Lijenje na Khalfani Bwire Uliwapa TSh ngapi

Shahidi: Niliwapa hiyo Tsh 300,000, Wagawane

Kibatala: Ile Laki 499,000 sasa Ilitoka Wapi

Shahidi: Siwezi Kutoa Pesa yote, Nilikata TSh 1000 la Makato

Kibatala: Kwa hiyo Wewe Ulimkata Mbowe TSh 1000 katika ile TSh 500,000

Shahidi: Ndiyo Mbowe alikatwa Juu Kwa Juu, TSh 1000 nilijikata Mimi

Kibatala: Ulijikata wewe Kwa Sababu ipi

Shahidi: Ilienda Katika Deposit Ya Kampuni

Kibatala: Kwa hiyo Ile TSh 1000 hujui Imeenda Wapi?

Shahidi: (Kimya)

Jaji: Kuna sehemu Mnashindwa Kuelewana, Wewe Ulitumiwa TSh 500,000, Ukaenda Kutoa 300,000, na Mfukoni Kwako Ukatoa 199,000, Anzieni hapo.

Kibatala: Swali langu hiyo 499,000 Imetoka Wapi, ambayo Ulimwambia Malya.. Na assume Kuwa ile Laki 5 haiwezi Kutoka Yote, Laki 3 nilitoa Kwa sababu Nilikuwa na Balance Yangu

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Mfukoni Kwako Ulikuwa na Laki 2 ni nani aliyekata TSh 1000, Ni wewe au Wakala?

Shahidi: Ni Wakala

Kibatala: Ile Laki 2 Iliyobakia katika Simu yako Ulitoa lini?

Shahidi: Nilitoa Walipo Kuja...... Sikumbuki

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Naomba Nipewe Kielelezo namba 20

Kibatala: Shahidi Tafuta Ile Laki Mbili ambayo ilibakia katika simu yako Ulitoa Tarehe Ngapi, Ukipata wewe tuambie..

Shahidi aanaendelea kutafuta Miamala...

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Shahidi ile Nyaraka siyo yake, na Shahidi hajajengewa uwezo Wa Kusoma Ile Nyaraka, Kuokoa Muda, Shahidi aelekezwe Maeneo hayo na wakili..

Kibatala: Sawa Fair enough, Wacha Twende Kwa namna Nyingine

Kibatala: Shahidi Kwani Wewe Unakumbuka ulitoa lini hiyo pesa Kibatala anamfuata Shahidi, Na Kumueleza Kwenye Nyaraka ya Airtel, Ili Kuokoa muda Shahidi ANATUTA TENA..

Shahidi: Kuna Laki Mbili na Nusu

Kibatala: Miye Nimekuuliza Laki Mbili

Shahidi: Laki 2 Hakuna

Kibatala: Baadae Unasema Freeman alikutumia Laki 2 na Tisini na Tisa Je Ilikuwa Tarehe Ngapi

Shahidi: Ilikuwa Tarehe 22 july 2020

Kibatala: Namba Iliyo Ingiza ni 0780900244 Hiyo namba ya nani

Shahidi: Sijui ya nani

Kibatala: Siyo namba ya Mbowe?

Shahidi: Siyo Namba ya Mbowe

Kibatala: Pesa Uliyompatia Ling'wenya na Adamoo ulitoa Mfukoni na yenyewe au Ulitoa kwa Wakala

Shahidi: Nilitoa Kwa Wakala

Kibatala: Ulitoa TSh Ngapi

Shahidi: TSh 170, 000

Kibatala: Tafuta Tarehe 24 July 2020 Mahala ambapo unasa Ulitoa TSh 170,000

Shahidi: Haipo Katika Kielelezo Namba 20

Kibatala: lakini wewe Unasisitiza ulitoa Kwa Wakala

Shahidi: Ndiyo Kwa sababu nilitoa Kwa Serial Namba

Kibatala: Lakini Haipo Katika Kielelezo namba 20

Kibatala: Hiyo namba hapo 0782 237913 ni Namba ya nani

Shahidi: Siwezi Kukumbuka Mpaka niangalie Kwenye Note Book

Kibatala: Hiyo Notebook ipo wapi

Shahidi: Hotelini Kwangu

Kibatala: Hotel Yako Inaitwa Je Vile

Jaji: Kuna ulazima Wa Kutaja Hotel aliyofikia?

Kibatala: Ndiyo Kwasababu Tangu Mwanzo Case Theory Yetu ni Kwamba Hatokei Nyumbani Wala Hotelini sababu amewekwa sehemu

Jaji: Ndiyo Nauliza Kuna Ulazima Wa Kutaja Hotel ambayo anatoka Kuja Kutoa Ushahidi

Kibatala: Sawa Mheshimiwa Jaji Wacha Niendelee

Kibatala: hiyo Namba 0787 555200 ilituma TSh 190,000 Kwenda 0782 237913

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Huo Mhamala unafahamu

Shahidi: Ndiyo lakini Sikumbuki

Kibatala: Hiyo namba Iliyotuma ni Ya Kwako

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Namba Unaye Mtumia Unaifahamu

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji, Je ni maJukumu gani Moses Lijenje alipewa Kutekeleza Majukumu ya ugaidi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu Wewe Binafsi Exactly ni wapi Moses Lijenje alikuwa anaishi Moshi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Tunakweda Kwa Bwire Mheshimiwa Wa Kwanza, Wakati anatoka Tunduma Kuja Morogoro alikuwa anajua anakuja Kufanya Ugaidi

Shahidi: alikuwa Hajui

Kibatala: Na Yeye huyu Khalfani Bwire Una Ushahidi Wowote Wa Kimaandishi Ambao Ulimsainisha Bwire

Shahidi: Sina Ushahidi Wowote

Kibatala: Unayo Meseji ambayo Khalfani Bwire ana acknowledge Brother Asante kwa TSh 150,000 nimepata?

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Kuna Majukumu Yoyote Mahususi ambayo unayafahu Kuwa alipewa na Freeman Mbowe Kwenda Kufanya Ugaidi

Shahidi: Khalfani Bwire aliniambia Kwenye simu Tarehe 04 kuwa Bro Samahani tumesha Kengeuka, Wakati huo anasema Yupo Moshi

Kibatala: Khalfani Bwire alipewa Jukumu gani Mahususi la Kutekeleza Ugaidi

Shahidi: alisema Kwamba tumepewa Jukumu la kwenda Kumdhuru Sabaya

Kibatala: alikwambia Kwamba wanaenda Kumdhuru Sabaya Tarehe Ngapi

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: namna Mahususi ambayo Bwire alikuwa anaenda Kumdhuru Sabaya Unaifahamu

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Bwire Alikwambia Chochote Kuhusu chochote Kuhusu Bastola aina ya Luger A5340

Shahidi: hajawahi Kuniambia

Kibatala: Bwire aliwahi Kukwambia lolote Kuhusu na Madawa ya Kulevya

Shahidi: hajawahi Kuniambia

Kibatala: Bwire alishawahi Kukwambia Kwamba walikutana Popote Kupanga Mipango Ya Ugaidi

Shahidi: Hakuniambia

Kibatala: Bwire alikuwa informer Wako

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ulimwambia Taarifa hiyo DCI Shahidi: Hapana nilimwambia Kingai

Kibatala: Kwa hiyo Wewe Bwire Ali confess Kwako

Shahidi: Ndiyo Kibatala Je Ulimwambia Kingai Kwamba Bwire ka' Confess Kwako

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: DCI alikwambia Umwambie Kingai Kila Kitu au Vingine Umfiche

Shahidi: Nimwambie Vyote

Kibatala: Taarifa Muhimu Ka hizo kwanini Hukumwambia Kingai

Shahidi: Taarifa za Muhimu Nilimwambia Kingai

Kibatala: Tarehe 11 August 2020 Ulikutana na Inspector Swila

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Jeshini Kule Kuna Mtu yoyote Ulimwambia Kuwa Bwire ame Confess

Shahidi: Sikumwambia Mtu , Sababu siyo Mahala Sahihi

Kibatala: Kwa hiyo wewe ulimruhusu Bwire Waendelee na Mipango yao, Mipango ipi

Shahidi: Waendelee na Mipango yao ya Kumdhuru Sabaya, Kama Wakiweza

Kibatala: kwa hiyo Baada ya Kumdhuru Sabaya Walitakiwa Kuriport Kwako tena

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwa hiyo Wewe Luteni Wa Jeshi la Wananchi Tanzania, uliwaruhusu Kwamba wakatekeleze Mpango wa Kumdhuru Sabaya Kwa sababu wapo Ground?

Shahidi: Ningefanyaje sasa na Watu wapo Ground

Kibatala: Kwani Wakati huo walikuwa weshamdhuru au Bado

Shahidi: Walikuwa Bado, Ndiyo Wapo Kwenye Mpango

Kibatala: Je Baada ya Bwire Ku Confess Kwako, Ulimwambia Afande Kingai

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Kwani Shahidi Wakati wa Tarehe 11 August 2020 ulipoenda kwa Inspector Swila alikwambia Kuwa Bwire alikamatwa

Shahidi: Hakuniambia

Kibatala: Je Kingai alikwambia Kuwa Bwire amekamatwa

Shahidi: Hakuniambia

Kibatala: Je Maelezo yako si Uliandika Tarehe 12 August 2020

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Katika Maelezo Yako Uliandika Kwamba Bwire Ali Confess

Shahidi: (Kimya)

Kibatala: Mimi bado nipo Tarehe 11 na Tarehe 12 August 2020

Kibatala: Wakili alikwambia Wakatinakabidhiana Simu mlisainiana Makaratasi Ma ngapi

Shahidi: Makaratasi Manne

Kibatala: Jana Ulitoa Makaratasi Mangapi

Shahidi: Nilitoa Karatasi Moja

Kibatala: Ulitoa Ufafanuzi Kuhusu Makaratasi Matatu

Shahidi: Siku toa kwa sababu Sikupewa

Kibatala: hukupewa na nani

Shahidi: Na Wakili ambaye alikuwa akiniongoza

Kibatala: Unakumbuka ulikuwa Unafanya Mawasiliano na Simu ipi Mara kwa Mara kwa Mara Shahidi: Kwa Samsung ya Torch

Kibatala: Hiyo Samsung ya Torch ndiyo Sumsumg Duo

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kuna Mahala Popote ambapo Umefafanua kwa Jaji Kuwa hiyo Samsung Duo

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mara ya Mwisho Kufanya Mawasiliano na Kingai Ulifanya Mara ya Mwisho ni lini

Shahidi: 10 August 2020

Kibatala: Nikukuombea Upewe Samsung DUO utaweza Kuonyesha Call Record zako na Kingai

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Namba ya Kingai Unaifahamu

Shahidi: Mpaka Nisome Kwenye Notebook Yangu

Kibatala: Mbayo Ipo wapi

Shahidi: Ipo Hotelini

Kibatala: Sawa Nitakuombea Mahakamani Ruhusa Ya Kufuata Notebook yako

Kibatala: Je Unafahamu hata Basic za Intelligence Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Je Wakati Mbowe amajiachia Kuongea na wewe Kwenye simu Kuhusu Mipango hiyo ya Ugaidi

Shahidi: Hakunipigia Simu alisema Kwamba Tuonane

Kibatala: Na Ni simu ipi pia itaonyesha Call Record za Simu Ya Bwire Tarehe 04 August 2020

Shahidi: Ni hiyo Simu ya Samsung Duo

Kibatala: Hivi Ile simu Yako ya Jana Ulikabidhi Simu Lini

Shahidi: Tarehe 11 August 2020

Kibatala: Ulimfafanulia Jaji Kwamba Simu yako inauwezo Wa Kukaa na Chaji zaidi Ya Mwaka Mmoja na Nusu

Shahidi: Hapana

Kibatala: Simu Yako Ilikuwa na Kiasi gani Cha charge Wakati Unamkabidhi

Shahidi: Ilikuwa Chini Kidogo ya Nusu

Kibatala: Ulimfafanulia Jaji Kwanini Simu hii ni tofauti na zile Tatu Kwamba Ina Kaa Na Chaji Mwaka Mmoja na Nusu

Shahidi: Siku fafanua

Kibatala: Ulisema Kwamba Pia Mbowe alikuomba Makampuni yanayo Install Mawasiliano Ya Jeshi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ulisema Kwamba Pia Mbowe alikuomba Makampuni yanayo Install Mawasiliano Ya Jeshi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Hilo Ombi ni kwamba wewe Ulilichukuliaje, La Kawaida au?

Shahidi: Niliona la kawaida tu

Kibatala:
na wewe ni Afisa wa Juu

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ni sahihi Kwa wewe Afisa Kuwa na Mahusiano na Mawasiliano na Watu Waliofukuzwa Jeshi Kwa Utovu Wa Nidhamu

Shahidi: Kuna Maisha Nje ya Jeshi, Siyo Hawa tu wapo wengine Wengi tunaishi nao Mtaani

Kibatala: Kanuni za Kijeshi Inaruhusiwa Kuwa na Mahusiano na Junior officer kupeana pesa na Kutafutiana kazi

Shahidi: Uraiani inaruhusiwa

Kibatala: Hawa Wangekuwa Watu wabaya au Majambazi usingekiwa na Mahusiano au Mawasiliano nao?

Shahidi: Hawa siyo Majambazi, Ni watu Wazuri

Kibatala: Baada ya Kubadilishana Pesa na Ma' junior Wako wewe Kama Prudent Officer, Ulikuwa na Jukumu la Kijeshi ku' report hilo Jambo

Shahidi: Siku report Ila Kuna sehemu lilikuwa linafanyiwa Uchunguzi

Kibatala: Nilisikia Kuwa umefahamiana na Mbowe tangu 2008

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala:
Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba wewe Ulishawahi Kutumiwa Pesa na Mbowe

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Je ilikuwa Muhimu Kwa Jaji Kujua Kama Alikutumia au Hakukutumia

Shahidi: Haikuwa Muhimu

Kibatala: Hii Namba ya 0754612525 ni Namba ya nani

Shahidi: Ya kwangu

Kibatala: Walikwambia Upande wa Mashitaka Kwamba report inaonyesha Namba hii Katika Taarifa Ya Chunguzi

Shahidi: Sikuambiwa

Kibatala: Unasema Bwire Unamfahamu Vizuri, unajua Bwire alishawahi Kuwa Body Guard Wa Kiongozi Fulani Jeshini

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: unasema Ulionana na MBOWE sehemu Nyingine zaidi ya CASA Motel, Ulimwambia Jaji sehemu nyingine inaitwaje

Shahidi: Nilimwambia ni Mikocheni

Kibatala: Ni kweli Ulikuwa, hujui Identity ya Viongozi waliokuwa wanaenda kudhuriwa

Shahidi: Nilikuwa siwajui

Kibatala: Hata Sabaya ulikuwa humjui?

Shahidi: Nilikuwa simjui

Kibatala: Shahidi CDF ni Kiongozi Wa Kitaifa au Siyo Kiongozi Wa Kitaifa

Shahidi: Kiongozi wa Kitaifa

Kibatala: lakini wewe Hukuona sababu Ya Ku report Jeshini

Shahidi: Kimya

Kibatala: Chief of staff Wa Jeshi ni Kiongozi Wa Kitaifa au siyo Kiongozi Wa Kitaifa

Shahidi: Ni Kiongozi Wa Kitaifa

Kibatala: Waziri Wa Ulinzi ni Kiongozi wa Kitaifa au Siyo

Shahidi: Ni Kiongozi Wa Kitaifa

Kibatala: Na Swala lake linaweza Kushughulikiwa Jeshi?

Shahidi: Linaweza Kushughulikiwa na Jeshi

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kuhairisha Cross Examination Sababu Ya muda Nitaendelea Jumatatu Kama Wenzangu Wataridhia..

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi

Jaji: Kufuatia Muda na Ombi la Wakili Kiongozi Wa Jopo LA Utetezi, Nahairisha Mpaka Jumatatu Tarehe 31 January ambapo Shahidi Namba 12 ataendelea Kuwa Kizimbani Kutoa Ushahidi Washtakiwa Wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Jumatatu Saa 3 Asubuhi

Jaji anatoka
 
Urio ndiyo kabeba kesi yenyewe - na ndiyo maana alikumbushwa kwamba baada ya ushahidi wake anaweza kuwa Shujaa ama mtu wa hovyo kabisa kutokea hapa duniani.

Wacha tuone leo maana jana hakutoka hata na point moja..alishidwa kabisa kumshawishi achilia mbali Jaji lakini mtu yoyote anayefuatilia hii kesi.
 
Urio ndiyo kabeba kesi yenyewe - na ndiyo maana alikumbushwa kwamba baada ya ushahidi wake anaweza kuwa Shujaa ama mtu wa hovyo kabisa kutokea hapa duniani.

Wacha tuone leo maana jana hakutoka hata na point moja..alishidwa kabisa kumshawishi achilia mbali Jaji lakini mtu yoyote anayefuatilia hii kesi.
Mtu asiye na thamani duniani.
 
Hakuna kitu kinaniumiza kama kumuonea mtu! Ni dhahiri hata nikigundua ninemuonea hata mke wangu, huwa najuta sana.

Tuendelee kumwombea Jaji awe fair, kuwaombea akina Adamoo, Ling'wenya na Bwire pamoja na Mh.Mbowe kwa Mungu ili kuwanusuru na dhuluma.

Wote tuseme kwa Ujasiri Waebrania 13:6
" Bwana ndiye Msaidizi wangu, sitasita, wanadamu (Bibi Michele, Siro, Kingai, Boaz & co) wanaweza kufanya nini kwangu"
 
Acha leo luteni muongo muongo akutane na spana za kina kibatala..

Njia ya muongo huwa ni fupi sana.
Na akitoka hapo anaenda kula ban jeshini kwa kuwadanganya makomando wenzake na kuwauza kwa watesi wao kina kingai kwa thaman ya laki5.
 
84 Reactions
Reply
Back
Top Bottom