Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye kampeni za Mgombea Urais Tundu Lissu kwenye Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara

Wakuu ikiwa hii ni wiki ya lala salama , bado yule mgombea anayependwa nchi nzima na anayekadiriwa kushinda kwa zaidi ya 70% Tundu Lissu anaendelea kuomba kura kwa wananchi wenzake , ambapo leo atafanya mikutano kadhaa kwenye maeneo mbali mbali ya mikoa ya Pwani , Mtwara na Lindi .

Endelea kubaki hapahapa JF kwa Taarifa za uhakika


==========
Mikutano ya Magufuli saa 12 watu wamejaa uwanjani!! Mikutano ya Tundu Lisu haijawahi kufata muda maana anabembelezea wapita njia!! Wapita njia wakijaa ndio na picha zinapigwa na ndipo mgombea anaingia. Chezea CCM weweeee!! Halafu mseme mmeibiwa kwa kuvizia wapita njia.

Queen Esther
 
Polepole alisema mikutano ya magufuli haijai kama ya Lissu kwa sababu wao wanafanya asubuhi Lissu anajaza kwa kuwa anafanya mchana na jioni
 
Asisahau kumchongea Jiwe, na hapa chini ni sehemu ya Kampeni Chonganishi!!!

Ndugu zangu wa Kusini, sisi tulio kwenye system ndio tunafahamu Rais Magufuli anawachukuliaje!!

Bila kupepesa ndugu zangu, Magufuli anawadharau sana watu wa Kusini na kuwaona ni watu msiojua chochote na ndio maana ndio maana hata kuja huku HAKUTAKA kabisa kuja!!

Magufuli hakutaka kuja kwa sababu anawaona nyie ndugu zetu ni kama watu msiojitambua na msiojua chochote na kwahiyo hata asipokuja mtampigia tu kura!!

Ndo maana Magufuli hakuona taabu kumwambia Majaliwa kwamba atakuja kuwapiga makofi shangazi zake... yaani kwa jinsi Magufuli alivyowadharau, anaona anaweza kuja hapa na kuwatwanga makofi na bado mkampigia tu kura!!!

Ni kutokana na dharau zake kwenu ndo maana wala hakuona taabu kuwapora pesa zenu za korosho ili zisiendeleze Kusini, na badala yake akaziingiza Hazina ili akajengee Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kijijini kwao!!

Lakini kafanya yote hayo kwa sababu amewadharau kwa kuona pamoja na kuwapora jasho bado anaamini mtampigia tu!!!

Ndugu zangu, umbali kutoka Dar es salaam hadi Kigoma ni zaidi ya 1200KM, na umbali kutoka Dar es salaam hadi Kagera ni zaidi ya 1000KM wakati Dar es salaam hadi Lindi ni 460KM tu na Dar es salaam hadi Mtwara, ni 560KM tu!!

Lakini Magufuli kwa kuwadharau watu wa Kusini, kuja huku ameona mbali lakini Kigoma na Kagera ambako ni mbali mara mbili ya huku ameenda!!!

Yaani ameona hawezi kuopoteza muda wake kwa kusafiri kilometa 500 hadi 600 kuja kuwaomba kura zenu kwa sababu anaona hamjitambui na hapa asipokuja, mtampa tu kura!!

Sasa ngoja niwaulize ndugu zangu... Je, niwaulize?

Raia: "NDIYOOOOOOOOOOOO"

Sasa mtu anayewadharau namna hii kweli anastahili kura zenu?!

Raia "HASTAHIIIIILI!"

Tena nimekumbuka... sijui nianzie wapi manake najisikia uchungu sana!!!

Ndugu zangu wa Kusini, pale Lindi kulikuwa na mpango wa kujenga kiwanda cha kuchakata gesi ambacho thamani yake ni karibu shilingi Trillion 70!!!

Hivi mnaijua Shilingi Trillioni 70 Ndugu zangu?! Ukitaka kujua wingi wa Shilingi Trillion 70, chukua biashara zooooooote Tanzania lakini thamani yake haifiki Shilingi Trillion 70!

Uza majengo yooooote yaliyopo Dar es salaam, bila kusahau ile mighorofa, bado huwezi kupata Sh Trilioni 70!!!

Watu wooooote wa Lindi Mtwara hamfiki 3 million. Ukitaka kujua Shilingi Trilioni 70 ni nyingi kiasi gani, watu wooooote wa Lindi na Mtwara, hadi waliokopo vijijini ndani ndani huko, kila mmoja anaweza kupewa Shilingi 20 million na bado chenji ikabaki!!!!

Magufuli kwa kuwadharau watu wa kusini, akaleta mizengwe na matokeo yake kile kiwanda hadi leo hakijajengwa, na katu hakitajengwa endapo ataendelea kubaki madarakani kwa sababu anaona watu wa kusini hamstahili uwekezaji mkubwa namna hiyo!!!

Ngoja niwaulize jambo lingine!

Raia: "ULIZA BABA....."

Hivi mnadhani hii gesi iliyojaa huku Kusini ingekuwa ndo ipo Chato, mnadhani hadi sasa ingekuwa kiwanda hakijajengwa?! Amini amini, hivi sasa ingekuwa kiwanda kimeshajengwa na maghorofa ingekuwa yanajengwa kwa kasi hivi sasa kule Chato lakini kwavile gesi ipo Lindi na Mtwara Magufuli kwa makusudi ameamua kuweka mizengwe kwa sababu hapendi maendeleo yenu, anataka mbaki kuwa maskini maisha yenu yote!!

Je, hiyo ni haki ndugu zangu?!

Raia: 'HAPANAAAAAA"

Sawa sawa, sio haki hata kidogo na ndio maana mimi kwa kuwajali na kuwathamini Watanzania wote nikaapa kwamba ingawaje Tume ya Uchuguzi wamesimamisha kufanya kampeni zangu lakini SITAKUBALI kuwaacha watu wa Kusini na upweke!

Nikaapa kufanya kila niwezalo ili nije kuwajulia hali na kuwaomba kura zenu za urais, wabunge na madiwani ili hatimae mpate serikali inayowajali watu wote kwa usawa!!!

Tena ngoja niwadokeze jambo!!! Si mlimsikia anavyohangaika kuipinga sera yetu ya majimbo kwavile tulisema kila jimbo litakula kutokana na wanachozalisha?!!!

Magufuli anajua tukileta hiyo sera Watu wa Kusini ndio mtanufaika zaidi kwa sababu mna gesi yenye thamani ya mabilioni kwa mabilioni!!!!

Magufuli lazima apinge hiyo sera kwa sababu anafahamu CHADEMA tukiingia madarakani na kuanza kuchimba gesi na watu wa Lindi na Mtwara kuwa ndio wanufaika wa kwanza, basi baada ya miaka michache uchumi wa Kusini utapaa wakati yeye na CCM yake wanataka muendelee kuwa maskini!

Sijui mmemkosea nini huyu baba!!

Niendelee ndugu zangu wa Lindi/Mtwara/Kilwa/Masasi?!
 
"CHADEMA ACTwazalendo hakuna kulala
CCM wameandaa Masive vote rigging machine ikiongozwa na NEC/ZEC" alisikika Sheikh Ponda
 
Wakuu ikiwa hii ni wiki ya lala salama , bado yule mgombea anayependwa nchi nzima na anayekadiriwa kushinda kwa zaidi ya 70% Tundu Lissu anaendelea kuomba kura kwa wananchi wenzake , ambapo leo atafanya mikutano kadhaa kwenye maeneo mbali mbali ya mikoa ya Pwani , Mtwara na Lindi .

Endelea kubaki hapahapa JF kwa Taarifa za uhakika


==========
Usisahau updates na clips muhimi muhimu. Tuko macho na maskio tumeelekeza huko Pwani kwa Mkombozi wa Taifa.
 
Mikutano ya Magufuli saa 12 watu wamejaa uwanjani!! Mikutano ya Tundu Lisu haijawahi kufata muda maana anabembelezea wapita njia!! Wapita njia wakijaa ndio na picha zinapigwa na ndipo mgombea anaingia. Chezea CCM weweeee!! Halafu mseme mmeibiwa kwa kuvizia wapita njia.

Queen Esther
Chama kina miaka zaidi ya 60 bado mnashindanisha kujaza watu.
 
Back
Top Bottom