Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,618
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa.

Hii ndio makala ya leo swali la wito kwa Watanzania wenzangu, jee jjifunze kujikubali kuwa hatuwezi kila kitu!, hakuna nchi yoyote duniani wanaweza kila kitu wao wenyewe!. Kuna vitu sisi Watanzania wenyewe hatuwezi!, na inapptokea kuna vitu hatuwezi, tunapojaribu tukashindwa, lazima tujikubali hili tumeshindwa, hatuwezi!. Swali ni unaposhindwa kuna ubaya wowote kubali kusaidiwa au tuendelee tuu kujitutumua tukomae tuu mpaka tuweze?

Kiukweli kabisa uamuzi wa kulipa kampuni ya Dubai kutuendeshea Bandari yetu ya Dar es Salaam, Dar Port, kwanza msiuamini upotoshaji wa miaka 100!, ni uzushi tuu!, lakini uamuzi huu ni uamuzi sahihi, na kwa maoni yangu, baada ya Bandari, hata ATCL peke yetu hatuwezi, lazima tongue ubia!. Tukija kwenye SGR ndio kabisa!

Kuna vitu Watanzania hatuwezi na tunashindwa sio kwasababu ni vilaza, au hatuna uwezo, tunashindwa kwasababu tuu hatujui kutazama mbali!

Mfano saa hizi tuko busy kujenga SGR, lakini hatuna mkakati wowote wa kujiandaa kwa mzigo wa kuendesha SGR kwa faida. Waona mbali hili tukaliona, tukashauri Reli ya SGR: Je, Tujifunze kwa wenzetu Kenya kuepusha SGR yetu kuwa ‘A White Elephant’? Wenzetu yameshawakuta..., sasa tusubirie SGR yetu ikamilike, tujaribu kuioparate tushindwe ndipo tutafute usaidizi?, au wakati ujenzi unaendelea, tutazame mbali kwa kujenga uwezo wa uendeshaji na maandalizi ya kutafuta mzigo wa kushiba wa kubebwa na SGR?.

Hivi tuu tuna reli ya TAZARA tumeshindwa kuiendesha!, Tunduma ndio the busiest border kwa mizigo ya Zambia inabebwa na malori, huku mabehewa ya Tazara yamelala bure!.

Reli ya kati tumeshindwa kuiendesha to it's full capacity!, nenda Bandari kavu ya Isaka!, ukiwa mzalendo mwenye machozi ya karibu, unaweza kutoa machozi!. Reli ya Tanga, Moshi, Arusha, almost zimetelekezwa!. Mtu aliyeshindwa kuendesha kidogo hiki uje umpe kukuendeshea li SGR!, nategemea nini?. Kuna ubaya kuwaita watu wenye uwezo wakuendeshee kwa kipindi fulani huku unajenga uwezo wa ndani kuendesha, ukiwa tayari ndipo uendeshe?.

ATCL, tushukuru Magufuli kwa kuwa bold kukimbilia kununua midege kwa cash kwa mtindo wa kupiga tanchi, bila kuwa na business plan!.

Tumenunua midege ya masafa marefu, long hauls, tunaizungusha Dar-Mwanza-Kia!, tunaichosha bure, wear and tear ni kubwa!, matokeo yake by now, tume ground midege 4 kwa uchovu wa engine, tutatengeneza kwa millions of dollars halafu tuje kuharibu tena!. Ukiangalia abiria wa Tanzania wanaokwenda Ulaya na America kwa ndege za mashirika mengine ni abiria wa kujaza a 7 day flights, lakini sisi wenyewe hatuwezi!, lazima tusaidiwe!.

Pale unaposhindwa kitu fulani, hakuna ubaya wowote kuomba msaada kwa wenye uwezo usaidiwe!.

Tuliwahi kujaribu kwa ATC, TTCL, Tanesco, Dawasco, tukaja kuvunja mikataba kwasababu tulikuwa kuzaliwa!. Ukitaka kula ni lazima uliwe!, hivyo hata huu mkataba wa Bandari, kwavile tunataka kula, ni lazima tuliwe!. You can't eat your cake and have it!.

Kuna vitu vingi tuu tunashindwa lakini hatusemi!. Juzi kati Tundu Lissu kashambuliwa kwa kupigwa risasi mchana kweupe, Ben Saanane wetu humu, kakosoa kitu, kayeyuka!. Azory Gwanda kaandika kitu, kafuatwa na Toyota Land cruiser ya mkonga, kapotezwa!.

Serikali yetu imeshindwa kufanya uchunguzi kwasababu hatuna uwezo huo wa.... Watu tumejitokeza humu tukasema tuna uwezo kusaidia, tunachotaka ni serikali ijitokeze tuu na kukiri imeshindwa, na kuomba msaada kwa wenye uwezo!. Tumewasaidia kupata pa kuanzia Taifa linahangaika na wasiojulikana waliomshambulia Tundu Lissu! Je, ni hawa?! Mhe. Mwigulu, IGP, anzieni hapa! bado wakashindwa!. Tumejitokeza tena live Mubashara kupitia kwenye TV, tukasema tunaweza kusaidia Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija lakini wapi!.

Kuna watu wanadhani Scotland Yard, wanazaliwa na uwezo huo!, no!, Scotland Yard wanafanya scouting kuwapata watu wenye uwezo huo!, hapa Tanzania watu hao tunao lakini hatuwatumii!.

Niliwahi kuuliza WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?.

My Take:
Rais Nyerere japo alitupatia uhuru, lakini kulikuwa na watu wengine wenye uwezo kuliko Rais Nyerere, wangeweza kutututawala vizuri zaidi na kutufikisha mbali zaidi, ila ni Nyerere ndiye aliyechaguliwa na Mungu kuwa rais wetu!. Vivyo hivyo kwa Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia, haina maana kuwa ndio they are the best, but the chosen ones!, lakini the best wapo wanajijua wanaangalia tuu huku wamejinyamazia kwasababu hawajaombwa au kushirikishwa!.

Wito kwa serikali yetu Tukufu, mkishindwa jambo lolote, kabla hamjakimbilia huko nje kuomba msaada, exhaust the local remedies!. Serikali ijitokeze kwa uwazi kabisa very transparently iseme wazi kabisa kuwa hili limetushinda, kama kuna Mtanzania au kampuni ya Kitanzania inaweza kusaidia, na ina uwezo huo, ijitokeze isaidie.

Ikitokea hakuna hakuna Mtanzania au kampuni ya Kitanzania ina uwezo huo, ndipo tutafute wabia kwa kutangaza kwa uwazi kabisa, mabingwa wa uendeshaji wa Bandari ni Bandari kama ya Rotterdam wangejitokeza!.

Kuna kushindwa na kushindwa, kushindwa kungine ni aibu!. Sherehe zote za ndoa za kiasili na kidini, zilikuwa zinasherehekewa ndoa inapokuwa ndoa na sio ndoa inapofungwa!, ma bi harusi lazima awe sealed!. Sasa ikitokea ndoa imefungwa, ikakutikana ndugu ameshindwa kufungua seal ili sherehe iendelee!, ili kuepuka aibu, huyo ndugu anasaidiwa in a very closed guarded secret, kwa kaka mtu, and some tribes hata baba mtu!.

Hivyo Watanzania tunaposhindwa jambo fulani, tusione aibu kusema tumeshindwa!, tuanze kuomba msaada kwa Watanzania kwanza, tukikosa ndio twende kwa wageni kutafuta msaada kwa uwazi na ushirikishwaji.

Paskali
 
Tumekuwa mfano wa kuigwa, kwa Uzalendo tuliokuwa nao. National pride!
Tunatakiwa tuendelee kuwa hivyo.
=================
Wachaneni na hizi non-sense kuwa hatuwezi.

Bora ungeshauri wale wanaojisikia hawawezi wahamie huko, baadala ya kushawishi ukoloni Mamboleo.

ikiendelea tutasahihisha!

Chini ni matokeo ya mawazo na fikra zilizonipeleka kuweka niliyoyaweka huko juu
=================
imekuwa dhahiri jamvini kusikia na kuona utetezi ambao, kwa namna moja au nyingine unatetea muendelezo wa Ukoloni mamboleo, mfano Utasikia Serikali iingie ubia na Raia au kwa lugha ya kigeni kuwe na uwepo wa "Private/Public partnership" na watetezi wa hoja hio huwa wanafunika hoja za wapingaji, yaani watetezi wa Serikali kuendesha mashirika.

...na utakuta kuna sehemu huwa wanakubaliana,(where there is harmonization au ndoa za hoja zinazokinzana kukutana) napo ni Ujengaji wa Miundombinu kwa kutumia nguvu za Serikali-ambayo ina maana fedha ya mlipa kodi au Mtanzania ndiyo inayotumika-hata ikiwa ni ya Mikopo;bado ni mzigo wa Mtanzania, hapo utasikia "uwekezaji huo" au Investment hiyo ni nzuri na itazungusha fedha mtaani, kweli hilo linatokea, ila baada ya mradi kuisha na wakandarasi kulipwa fedha hiyo hutoweka na kuwepo kwenye mifuko ya wachache., including, fedha nyinginre za kigeni kubakia katika nchi zilipotoka wakandarasi.....hapa unajiuliza, kwanini hawa wawekezaji wasije kujenga barabara au madaraja, au mtandao wa mawasiliano wakope wenyewe, walipe hao wafanyakazi wenyewe, halafu ndio waje waombe watoe ubia kwa Serikali au kwa lugha nyepesi a true Public Private partneship -yaani sasa waingie ubia na Wananchi wa Tanzania kutafuta hela za uendeshaji kama vile inavyotokea katika Nchi nyingi za Magharibi....Kwanini isiwe hivyo? Badala ya Watanzania kunyonywa hela, halafu tunaingia Ubia na makampuni ya Nje tena mengine yasiyokuwa na Fedha kwa kuwawezesha na kuwatwisha, mfano hapa Bandari halafu wao waende nje na kutafuta ipos wake huko nje...ikiwa ina maana wanalazimika kuwarudishia wawekezaji wao wa Capital makwao kabla hawajarudisha kwetu....wakati huohuo tushapoteza mabilioni kwa kuwekeza fedha za walipa kodi! Na bado tunakuwa hatujarudisha the initial Investments.... it is absurd

Hakika tuna uwezo wa kujiwezesha, na hilo jambo ni Uamuzi tu.

Tuache Ulimbukeni
 
ATCL, TRC, TTCL, na mashirika mengine lukuki huko nyuma yalishawahi kubinafishwa kwa wageni! Na matokeo yake kila mtu aliyaona. Kwa hiyo watu wanapotikia shaka huo uwekezaji, wana sababu za msingi.

Viongozi wengi wenye dhamana kwenye hii nchi siyo wazalendo! Mara nyingi wamekuwa wakiingia mikataba tata yenye manufaa binafsi zaidi kuliko Taifa.
 
Kwa nini tushindwe are we sub humans?

We need major reforms ambayo itawaondoa kabisa wanasiasa kwenye kuendesha mambo ya kitalam.

We need to have a fair political system itakayozaa checks and controls kwenye mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi.

Tunahitaji whole legislation overhaul tukianza na katiba.

This country is so blessed but is run by rotten system
 
Unashindwaje kwenye mazingira tuliyopo leo miaka 60 baada ya kupata uhuru?

Wasomi tunao wa kila aina, teknolojia ya mawasiliano imekuwa, mfano internet kutafuta information ipo, lugha kwetu sio tatizo, rasilimali za kila aina tunazo..

Sisi hatujashindwa kusimamia mali zetu, tatizo letu ni kuwa na viongozi wavivu kufikiri, wabinafsi, wasio na uzalendo, walioweka maslahi yao binafsi mbele zaidi ya taifa.

Matokeo yake hata hiyo mikataba watakayoingia hao wezi, bado hawawezi kutuacha salama, kwa nje tutabaki kudanganyana tunasaidiwa kuendesha, kumbe kwa ndani ya hiyo mikataba, wezi wameshachukua chao, huku sie huku nje tunaimba tu tumewapa wawekezaji.
 
Mie sina imani na huo sijui uwekezaji mpya wa waarab bandarini.

Hii serikali awamu ya 6 imejaa upigaji sawa na awamu ya JK, ngumu mnoo kuwaamini.

Nna uhakika hata Sa100 huo mkataba hajausoma, na kama ameusoma sidhani kama ameuelewa!!.
Nendeni Mkalitazame!
 
Back
Top Bottom