ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,042
- 49,726
Kusema ukweli kama unafikiria kiuchumi na kimkakati huwezi fanya maamuzi ya kuchagua vipaombele kama hivyo ambavyo Kwa maoni yangu ni vipaombele vya hovyo kabisa.
Kwamba Tumetukia Trilioni 3.6 Kwa Ajili ya kununua ndege 15 Kwa kile kinachoitwa kufufua Shirika la ATCL.Pesa hii inaweza kuongezeka zaidi.
Pili tumetumia Trilioni 23.3 Kwa Ajili ya ujenzi wa Sgr,vichwa vya treni na mabehewa yake lakini hadi Sasa hakuna kinacholeta faida na Wala faida haitokaa ije Kwa sababu tumejenga Kwa kubahatisha tukitegemea eti faida itakuja baadae.
Ukiacha kwamba ni miradi ya kupigia picha ila Haina impacts yeyote ya maana inayoweza kuondoa umaskini Kwa watu ila bahati mbaya hatuna watu wenye akili wanaoweza kufikiria na kuona hasara ambayo Nchi imeingia.
Ukweli ni kwamba ukilinganisha tulichopata na ambacho tungepata ni kama Tumepigwa na tumepata hasara kubwa sana kama Taifa.Hizo Trilioni 27 Kwa pamoja zingeweza kufanya mambo makubwa yafuatayo.
1.Kufungua Barabara Mpya za lami Nchi nzima zaidi ya km 10,000.=10.0T
2.Kupata Uhakika wa Umeme Kwa zaidi ya megawatt 5,000=6T
3.Kupeleka Maji ya uhakika Kila Kijiji na Kila Mji Tanzania nzima (Water Grid)=2.5T
4.Kuanzisha Mashamba Makubwa ya Kilimo Cha Umwagiliaji=1.5T
5.Kujenga Kituo Cha Afya Kila Kata,Zahanati Kila Kijiji na Hospital Kila Wilaya,Mkoa na Kanda.=1.5T
6.Kujenga Miundombinu ya Shule kuanzia za awali Hadi Vyuo Vikuu Kila Mkoa.=1.5T
7.Kufanya Upanuzi wa Bandari zote kubwa za Bahari na Maziwa Pamoja na Kununua Meli=2.5T
8.Ku upgrade reli ya Kati kutoka meter Gage na kuwa Cape kama ya TAZARA.=1.5T
Swali.
Hivi kweli hizo Trilioni 27 Zingetumika kwenye Maeneo hayo hapo Juu Nchi ingekuwa hivi ilivyo saizi na umaskini huu?
My Take
Tunaangamia Kwa kukosa Akili na Maarifa.Tutaendelea kuwa Maskini Kwa sababu ya Maamuzi ya hovyo na vipaombele vya Maonesho kama hivyo.
Inauma Sana ,hapo ndio kwanza Sgr Bado haijafika Kigoma Wala Mwanza,Hadi inatoboa huko pesa inaweza kufika Trilioni 35 au zaidi.
View: https://www.instagram.com/reel/C48biH-u8Wq/?igsh=a3FsNG9pM202Y2w3
Pia Soma Serikali imetumia Trilioni 3 Kununua Ndege 13 Badala ya Kujenga km 3,000 za Lami.Je Tanzania tumenyimwa akili au Tumerogwa?