Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Tanzania imepata ugeni kutoka Misri ukiongozwa na Waziri wa Uchukuzi wa Misri, Luteni Jenerali Kamel Alwazeer kwa lengo la kujifunza fursa za uwekezaji zilizopo Nchini
Akizungumza wakati wa kuwakaribisha wageni hao, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema “Sekta ya Uchukuzi, Serikali ya Tanzania imeweka fedha nyingi kwa ajili ya kuhakikisha sekta inakua.
“Sekta hiyo ikikua na Uchumi wa Nchi yetu utakua, kwani wenzetu wameendelea sana na tumewaeleza miradi mbalimbali wanayoweza kuwekeza, mfano pale Bandari ya Dar, tuna mradi wa ujenzi wa bandari katika namba 13, 14 na 15 katika mfumo wa PPP.”
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema pamoja na maboresho yaliyofanywa katika bandari ya Dar es Salaam, kuna haja ya kuongezwa gati namba 13 hadi 15.
Profesa Mbarawa amesema tayari, Serikali imefanya maboresho makubwa katika bandari hiyo lakini bado kuna msongamano wa meli bandari hapo.
Akizungumza katika kikao cha Wizara ya Uchukuzi ya Tanzania na Misri kilichohusu ushirikiano wa uwekezaji katika sekta ya uchukuzi Profesa Mbarawa amesema kuna haja ya kuongeza magati katika bandari hiyo, ili kupunguza msongamano wa meli zinazohudumiwa.
"Pamoja na maboresho ya bandari yaliyofanywa na Serikali hivi karibuni bado kuna meli 18 zinasubiri kuhudumiwa,"amesema Profesa Mbarawa.
Ameongeza "Kule Misri wana reli iliyojengewa katika Mfumo wa SGR, wana reli ya kawaida na nyingine ya ‘express’. Tumewaomba vijana wetu kutoka TRC watembelee wajifunze jinsi ya kuendesha Reli ya SGR na Waziri (wa Misri) amekubali bila tatizo, kilichobaki ni wataalam kukaa pamoja kuangali jinsi inavyoweza kutekelezwa."
Kuhusu ushirikiano kati ya Misri na Tanzania, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema utawezesha watu wa Tanzania na Misri kubalilishana ujuzi na hatimaye kukuza uchumi huku akieleza manufaa katika ajira.
Katika maombi yake Profesa Mbarawa amemuomba Waziri wa Uchukuzi wa Misri kuridhia kuwapokea watanzania watakaokwenda kujifunza uendeshaji wa Mradi wa Reli ya Kisiasa (SGR).
Katika hatua nyingine, Profesa Mbarawa amezikaribisha kampuni za Misri kuwekeza katika miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), maboresho ya bandari za Tanzania.
Upande wake Waziri wa Uchukuzi wa Misri, Luteni Jenerali Kamel Alwazeer ameeleza kuridhishwa na fursa za uwekezaji katika sekta ya uchukuzi nchini na kwamba wapo tayari kuwekeza.
Amesema hatua ya mwendelezo wa kikao hicho, amemkaribisha Profesa Mbarawa kwenda Misri kwa mazungumzo na kujifunza zaidi.
"Sisi tupo tayari kuwekeza na kubadilishana uzoefu tulionao kwa watendaji wa Tanzania ili kuongeza ushirikiano," amesema.

Last edited: