Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,504
- 113,620
Wanabodi hii Makala ya Nipashe ya leo 11/06/2023
Makala ya leo ni wito kwa Watanzania wenzangu, tujifunze kujikubali kuwa hatuwezi kila kitu!, hakuna nchi yoyote duniani ambayo wanaweza kila kitu wao wenyewe!. Hivyo hakuna ubaya wowote kwa mtu yoyote, taasisi yoyote, ana nchi yoyote kusaidiwa pale inaposhindwa.
Kuna vitu sisi Watanzania wenyewe hatuwezi!, na inapotokea kuna vitu hatuwezi, tunapojaribu kuvifanya na tukashindwa, lazima tujikubali hili tumeshindwa, hatuwezi!.
Swali ni unaposhindwa kuna ubaya wowote kukubali kusaidiwa au tuendelee tuu kujitutumua tukomae tuu mpaka tuweze?
Kiukweli kabisa uamuzi wa kulipa kampuni ya Dubai kutuendeshea Bandari yetu ya Dar es Salaam, Dar Port, ni uamuzi sahihi, kwasababu sisi tumeshindwa, tena kwa maoni yangu, sio Bandari pekee, hata kuiendesha ATCL kwa faida sisi wenyewe peke yetu hatuwezi, lazima tongie ubia!. Hata tukija kwenye SGR ndio kabisa!, lazima tushirikiane na wajuvi wenye uzoefu, wakati tukijenga uwezo wetu wa ndani.
Kuna vitu Watanzania hatuwezi na tunashindwa sio kwasababu ni vilaza, au hatuna uwezo, tunashindwa kwasababu tuu hatujui kutazama mbali!.
Mfano saa hizi tuko busy kujenga SGR, lakini hatuna mkakati wowote wa kujiandaa kwa mzigo wa kuiendesha hiyo SGR kwa faida ndio tukaja na Bandari ya Bagamoyo.
Kuendesha Reli ya SGR kwa faida sio mchezo!. Wenzetu Kenya yameshawakuta, wanaiendesha SGR yao law hasara. Jee sisi tusubirie SGR yetu ikamilike, tujaribu kuioparate tushindwe ndipo tutafute usaidizi?, au wakati ujenzi unaendelea, tutazame mbali kwa kujenga uwezo wa uendeshaji na maandalizi ya kutafuta mzigo wa kushiba wa kubebwa na SGR?.
Hivi tuu tuna reli ya TAZARA tumeshindwa kuiendesha!, Tunduma ndio the busiest border kwa mizigo ya Zambia inabebwa na malori, huku mabehewa ya Tazara yamelala bure!.
Reli ya kati tumeshindwa kuiendesha to it's full capacity!, nenda Bandari kavu ya Isaka!, ukiwa mzalendo mwenye machozi ya karibu, unaweza kutoa machozi!. Reli ya Tanga, Moshi, Arusha, zimetelekezwa!. Mtu aliyeshindwa kuendesha kidogo hiki uje umpe kukuendeshea li SGR!, unategemea nini?!. Kuna ubaya kuwaita watu wenye uwezo wakuendeshee kwa kipindi fulani huku unajenga uwezo wa ndani kuendesha, ukiwa tayari ndipo uendeshe?.
ATCL, tushukuru Magufuli kwa kuwa bold kukimbilia kununua midege kwa cash kwa mtindo wa kupiga tanchi, bila kuwa na business plan!.
Tumenunua midege ya masafa marefu, long hauls, tunaizungusha Dar-Mwanza-Kia!, tunaichosha bure, wear and tear ni kubwa!, matokeo yake by now, tume ground midege 4 kwa uchovu wa engine, tutatengeneza kwa millions of dollars halafu tuje kuharibu tena!. Ukiangalia abiria wa Tanzania wanaokwenda Ulaya na America kwa ndege za mashirika mengine ni abiria wa kujaza a 7 day flights, lakini sisi wenyewe hatuwezi!, lazima tusaidiwe!.
Pale unaposhindwa kitu fulani, hakuna ubaya wowote kuomba msaada kwa wenye uwezo usaidiwe!.
Tuliwahi kujaribu kwa ATC, TTCL, Tanesco, Dawasco, tukaja kuvunja mikataba hiyo.
Kuna msemo wa Kiswahili usemao, "Ukitaka kula ni lazima uliwe!", hivyo hata huu mkataba wa Bandari, kwavile tunataka kula, ni lazima tuliwe!. Wazungu wanasema "You can't eat your cake and have it!".
Kuna vitu vingi tuu tunashindwa na tunaomba msaada tunasaidiwa. Jengo la BOT lilipoungua, polisi wetu walishindwa kufanya uchunguzi, tuliomba msaada wa polisi wa Uingereza, The Scotland Yard, wakatusaidia.
Juzi kati Tundu Lissu kashambuliwa kwa kupigwa risasi mchana kweupe, Ben Saanane wa JF, kakosoa kitu, kayeyuka!. Azory Gwanda wa gazeti la Mwanamke kaandika kitu, kafuatwa na Toyota Land cruiser ya mkonga, kapotezwa!.
Serikali yetu imeshindwa kufanya uchunguzi wa matukio hayo kwasababu hatuna uwezo huo, lakini tumeona aibu kuomba msaada ili tusaidiwe!. Matokeo yake watu wasiojulikana bado wapo wanajivinjari tuu.
Kuna watu wanadhani Scotland Yard, wanazaliwa na uwezo huo!, no!, Scotland Yard wanafanya scouting kuwapata watu wenye uwezo huo!, hapa Tanzania watu hao tunao lakini hatuwatumii!.
Niliwahi kuuliza WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?.
Ushauri:
Rais Nyerere japo alitupatia uhuru, lakini kulikuwa na watu wengine wenye uwezo kuliko Rais Nyerere, wangeweza kutututawala vizuri zaidi na kutufikisha mbali zaidi, ila ni Nyerere ndiye aliyechaguliwa na Mungu kuwa rais wetu!. Vivyo hivyo kwa Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Samia, haina maana kuwa ndio they are the best, but the chosen ones!, lakini the best wapo wanajijua wanaangalia tuu huku wamejinyamazia kwasababu hawajaombwa au kushirikishwa!.
Wito kwa serikali yetu Tukufu, tukishindwa jambo lolote, kabla hatujakimbilia huko nje kuomba msaada, lets exhaust the local remedies!, yaani tuwaulize kwanza Watanzania wenye uwezo kusaidia.
Serikali ijitokeze kwa uwazi kabisa very transparently iseme wazi kabisa kuwa hili limetushinda, kama kuna Mtanzania au kampuni ya Kitanzania inaweza kusaidia, na ina uwezo huo, ijitokeze isaidie.
Ikitokea hakuna Mtanzania au kampuni ya Kitanzania ina uwezo huo, ndipo tutafute wabia kwa kutangaza kwa uwazi kabisa, mabingwa wa uendeshaji wa Bandari duniani washindane kwa ushindani wa wazi tumpe mshindi.
Hivyo Watanzania tuache nongwa, tunaposhindwa jambo fulani, tusione aibu kusema tumeshindwa!, tuanze kuomba msaada kwa Watanzania kwanza, tukikosa ndio twende kwa wageni kutafuta msaada kwa uwazi na ushirikishwaji.
Huu mpango wa kumpa Mwarabu wa Dubai kutuendeshea Bandari yetu, ni mpango wenye maslahi makubwa kwa taifa la Tanzania, tuunge mkono ila tuwe makini na huyu Mwarabu wa Dubai maana...!.
Paskali