MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,239
- 22,318
Wakuu kwa mara nyingine nipo hapa kwenye jukwaa la michezo kushea mawili matatu kuhusu mambo ya michezo na mazoezi. Kuna mwamko mkubwa sana wa wananchi kupenda michezo na kujihusisha na matukio yote ya kuweka mwili fit. Ni jambo la kujipongeza kwa kweli. Vikundi vya jogging vinazidi kuongezeka.
Binafsi siku za karibuni nimeanza mazoezi ya kukimbia kivyangu na kwa sasa nimefikia uwezo wa kukimbia 2.3km kwa dakika 15. Hakika hiki ni kishindo cha awamu ya 6. Changamoto niliyopata ni ile ya kisaikolojia kuona vibonge wakikata 13km huku mimi nikishindwa kufika hata 3km kwa kukimbia. Ila tayari nimepata jibu kuwa suala la mazoezi ni pana sana. Mtu anaweza kuonekana ana mwili mkubwa ila akawa fit kuanzia mwilini hadi pumzi.
Ila kama kichwa cha uzi kinavyosema ni kuwa wananchi waelewe kupunguza mwili kuna uhusiano mdogo na kuondoa kitambi au kitumbo flani hivi kisichoeleweka. Mchakato wa kuondoa tumbo na kupata six packs sio mdogo. Ni mchakato unaohitaji uvumilivu kwasababu inabidi ufanye mazoezi makali ya kuondoa kitambi na kupata six packs. Kupunguza mwili ni rahisi kwa sababu waweza tu kufanya jogging na ku-control misosi. Vijana wa umri mdogo wana nafasi kubwa ya kuondoa vitambi na kupata six packs ila wale wakubwa shughuli ni pevu.
Kama huwezi kupitia kwenye maumivu makali ya kutafuta six packs hata wajiunge kukuombea kina Mwamposa, Kakobe, Kadinali Pengo, Sheikh Kipozeo, Zumaridi, Dokta Manyaunyau, wazee wa kimila na viongozi wengine wa kiimani hutaweza kuondoa kitambi.
Nawatakia kila la heri.