Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,829
Mkurugenzi wa hospitali ya Muhimbili, Profesa Mohammed Janabi amesema mpaka sasa wanawake 100 wamewekewa puto na wanaume wachache. Prof ameongeza kuwa puto ni kitu kimoja lakini nidhamu kwenye chakula ni kitu kingine.
Janabi amesema kitu hatari zaidi kwenye mwili ni sukari na wanga na wala si mafuta kwasababu mwili hautunzi wanga wala sukari bali huvibadilisha kuwa mafuta. Ametaka watu kupunguza matumizi ya vitu vyenye sukari, utamu mkubwa na sukari yenyewe.
Prof Janabi amesema matatizo ya kushindwa kupata watoto, moyo, kiharusi, magonjwa ya kupumua, vifo vya ghafla asilimia mkubwa vinachangiwa na uzito usio sahihi na kula mara kwa mara. Profesa amesisitiza kutopeleka mwili kwa utaratibu wa chakula bali wale chakula wanapohisi njaa.