Waliobadilisha Maisha yangu....

Waliobadilisha Maisha yangu....

Mwita Maranya mkuu wangu pia umekuwa wa maana sana kwangu hasa mara zote linapokuja suala la siasa ndugu yako Nyambala yupo wapi asee na yeye kabadili ID kama MTM sijui??
Pamoja sana mkuu jouneGwalu tunajaribu ku-engage kwenye siasa ili tuweze kutumia taaluma zetu na maono yetu kujaribu kuisaidia jamii yetu na nchi yetu kwa ujumla.

Sina uhakika alipo huyo mkulu Nyambala kwa sasa hata mimi sijakutana nae jamvini muda mrefu kidogo. You never know bana hii JF ina mambo mengi labda yumo humu kwa jina la ubatizo. lol

Ila mwita hilo jina linakuathiri sana nadhani mambo ya nyumbani na mizizi, kuna siku ulinichenjia asee ila kwasasa ni raha tu kukumbuka....
Mkuu nilifundishwa ati mwacha mila ni mtumwa. Mimi ni mkurya orijinale, baba mkurya mama mkurya sasa unategemea nijivunge? nadhani pia hiyo inanisaidia pia kwa upande mwingine watu kunielewa kirahisi!!

Brother PakaJimmy na dadangu WiseLady wanaweza kukusimulia siku ya kwanza tunakutana nao ilikuwaje.:smile::smile::smile: Mweeeeee
 
Last edited by a moderator:
Nipo kuandaa mawakili nipeleke malalamiko yangu kamati ya mahusiano kule chitchat..mwaka huu laza kieleweke.. Asprin aachie ngazi au atangaze
ndoa.....tukutane mahakamani soon

Mmmh,,, yaani natamani nikuweke kwenye ignore list ili nisione hizi comments zako, mambo gani haya ya kulazimishana ndoa hadi kupelekana kwa pilato? hivi unategemea nini kesi yako akikabidhiwa jaji wa Tundu Lisu?
 
Wee! wee! wee! Mwita Maranya usinitafutie kesi nisiyoweza kuijibu! Wakeze babu Asprin watazuka hapa patakuwa hapatoshi! Babu alikuwa hanibughudhi maana mie ni mjukuu wake mpendwa!

Babe achana na huyo babu Asprin na wake zake. Hata yeye ananitambua nilivyo makini na ndio maana hakuona tabu kukukabidhi kwangu.
Weekend hii tunaonana wapi vile? (babu asprini atakesha hapa kusubiria jibu lako)
 
Last edited by a moderator:
Hahhahaha kaka Mwita Maranya......karibu nikuambukize upako si unaona MTM?TIMING kanipaisha hapo kati hahahha.
Aksante sana Babu sasana wewe unakagua sio? Ndio usharithishwa kimfuko cha uganga eh?

Aksante sana kaka nashkuru kama nimekugusa pamoja na kuwa threads zangu zinakuwaga na malalamiko mengi!

Trust me MwanajamiiOne inawezekana hayo malalamiko ndiyo yanatufumbua macho wengine na kutusaidia kuimarisha familia zetu.
Ingawa pia sina uhakika kama yote unayoyaandika huwa yamekutokea ama unawakilisha wadau wengine waliofikwa.
 
Last edited by a moderator:
Rafiki yangu sakapal kwa niaba ya pacha wangu snowhite kokote kule aliko naomba kusema ..'WE ARE HUMBLED''..
Always you are my friend and please take it from me!!!...A friend in Need is A friend Indeed!!!

.....Ni wengi kwa kutaja nitajaza karatasi kama kumi ila sitoweza kusahau michango ya mapacha wawili ambao ni Snowhite na SnowBall.....
 
Last edited by a moderator:
Mwanangu Snowball sikujua kuwa ningebadili maisha yako. Shukrani kwa kulitambua na kulisema hilo.
 
Astakhf'lahi....

Hii imekubeba sheikh, vijana hawana nidhamu kabisa hawa yaani wameshindwa kupima kuwa una hoja za kishebabi kabisa lol!!

Namsaidia erick kukutaka radhi!

Hii imenichekesha sana, na nikicheki Avatar yako hapo, yaani napata picha ulivyolalamika....

Huyu Chalii amenionea kweli aisee!!
 
Waliobadilisha maisha yangu hapa JF ni

The Boss, Mnama,BAK, Mahmetkic, Mute na Asprin.

Hawa nawakubali kwa michango yao Mtambuzi, Kiranga, Ashadii na Mwali.

Kwenye vichekesho hawa hunichekesha na hufanya nitabasamu siku nzima Boflo, Excy zamani Excellent na Ndallo.

Ni wengi kwa kutaja nitajaza karatasi kama kumi ila sitoweza kusahau michango ya mapacha wawili ambao ni Snowhite na SnowBall.

Mbarikiwe wote, pamoja sana.

Ever Remaining,

Sakapal.
asante sana my wee!
ubarikiwe mwaya
 
Mmmh,,, yaani natamani nikuweke kwenye ignore list ili nisione hizi comments zako, mambo gani haya ya kulazimishana ndoa hadi kupelekana kwa pilato? hivi unategemea nini kesi yako akikabidhiwa jaji wa Tundu Lisu?

ha ha ha..basi dady nitamuacha kisirisiri...lkn naomba uache kudai mahari za serengeti ili asilete vurugu....aniache nisepe zangu
 
Babe achana na huyo babu Asprin na wake zake. Hata yeye ananitambua nilivyo makini na ndio maana hakuona tabu kukukabidhi kwangu.
Weekend hii tunaonana wapi vile? (babu asprini atakesha hapa kusubiria jibu lako)

Nimeamua kujibu kwa njia ya posta!
 
dah! am very humbled madame...............
but ukweli siwez kuliongelea hili jamvi pas kumtaja Kongosho, King'asti Blaine boss, mwaJ na Mtambuzi napenda sana michango yenu wapendwa ingawa yahitajika sana akili kuweza kung'amua nondo za Kongosho na King'asti manake waweza kukuta jicho ukadhan pua lol! wewe boss yaani unaniachaga hoi kwa vijicoment vyenye harufu ya sintofahamuuuuuuuu nyingiiiiiiiii kuliko kufaham lol! sijuagi huwaga mnawaza nn mnapotoa comment and nataman sana niwaone siku moja.
Mtambuzi wewe stor zako zinatupa akili ya maisha, Blaine u mdogo but you have brain especially ktk social life, mwaJ wewe sijui ni wa tandale ama wa tandika manake lol! kuliko nikutane na mnango mmoja wakwako heri kugongwa na semi trela hahahha!


YOU are welcome anytime
siku moja will have lunch together..
 
@Mamndenyi, natoa asante nyingi kwa jf members kwa ujumla wao,
kipekee sana kwa :-

(1) jukwaa la Business & Economic Forum kitengo cha Ujasiriamali ambapo imenisaidia kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa kisasa, pia nimeweza kuanzisha mradi wangu wa kutengeneza sabuni.

(2) jukwaa la Matangazo madogo limenipa rafiki walionisaidia kupata shamba la kupanda miti huko mafinga (Love you more my sons), na kupata marafiki walionishauri namna ya kuendeleza shamba langu huko kibaha (more respect lecturer wa OUT), pia kwa kusoma postings za marafiki wengine nikapata ushawishi wa kuanzisha biashara ambayo inasonga vizuri. na mengi mengine nimepata kutoka kwenye hili jukwaa,

(3) Kupitia jf niliweza kumfahamu TBJoshua na kwa kupitia masomo yake nimepona mambo mengi sana.

(4) Ninapata shangamoto nyingi kupitia jukwaa la wakubwa japo sitoi comment.

(5) Naomba niweke haya majina mara zote nayakumbuka hata nikiwa nje ya jf

theboss, @RR, Mtambuzi, AshaDii, Kongosho, Arushaone, Bishanga, Boflo, mia, @Ruhazwe (my son), Asprin, Erickb52, Katavi, zomba, charminglady, @nugu mamaya, Mwanakijiji, Ruttashobolwa, BadiliTabia, gfsonwin, @Mkiruwa, Mkuu rombo, Baba V, Dena Amsi (Mjukuu), @Saint Ivuga, @Superman (Asante kwa 'like'), Cantalisia, Pdidy na wengine wengi nawapenda sana.

Nimeandika hivi ili wengi wajue kuwa jf siyo mahali pa kupoteza muda bali ni zaidi ya darasa la mafanikio.






i am so humbled
thanks a lot
nafurahi kutajwa na wewe
much respect
 
I'm humbled (source AshaDii) for your appreciation.
Kwakweli sikuwa natambua kwamba ninaweza kuwa na mchango mkubwa katika maisha yako, ubarikiwe sana mamito.

Kusema kweli hapa JF watu ni wengi sana waliochangia mimi kuwa hapa nilipo leo na kuwa hivi nilivyo leo kwa namna moja ama nyingine.
Kwakuwa siwezi kuwataja wote lakini kwakweli niwataje wachache kama Mtambuzi, Zion Daughter, WiseLady, Asprin & Filipo (hawa tumetoka nao mbali sana!!), Preta, PakaJimmy, zumbemkuu, Mungi, LiverpoolFC, Mzee wa Rula, Dena Amsi, Maxence Melo na Dark City.

Lakini pia kuna watu ambao sijawahi kuonana nao lakini nimekuwa nikiwasiliana nao mara kwa mara aidha kwa simu ama kwa PM hapa JF, nao pia wamechangia sana kunifikisha hapa nilipo kwani najifunza vitu vingi toka kwao; Nguruvi3, Mag3, Mkandara, Mchambuzi, Mtumishi Wetu, Mohamedi Mtoi, Thanda, AshaDii, Matola, Molemo, Michelle, carmel na Riwa.

Na mwisho kabisa ningeomba niwatambue marafiki wanaonifanya nilipende jukwaa la MMU na kulitembelea mara kwa mara tofuti na siku za mwanzo; Madame B, Kongosho, Ciello, gfsonwin, Kaizer, Kabakabana, The Finest, The Boss, lara 1, cacico, mwaJ, mdida, nivea, platozoom, snowhite, SnowBall, Boflo, King'asti, MwanajamiiOne na MziziMkavu.

ahsante sana Mwita Maranya nafurahi kuwemo kwenye list yako!
 
Last edited by a moderator:
Naomba radhi nimechelewa kwenye huu uzi maana MKOLONI WANGU KANIBANA SANA MWEZI HUU (Source: Asprin)

Kuna watu watatu humu ambao kwa kweli walinisaidia sana kunishauri namna ya kuweka post na kuifanya iwe na changamoto mpaka sasa najivunia kuona kwamba wapo watu leo hii wanakiri kwamba kile ninachokifanya kimesaidia kubadili maisha yao.

Naomba niwalete kwenu Da' AshaDii, kaka yangu The Boss na dada yangu gfsonwin.

Nakumbuka nilijiunga na Jamii forum mwaka 2008, wakati huo ikiitwa Jambo Forum, lakini nilipokuwa nikiweka post zangu watu wanalaumu kuwa ni ndefu na zikawa hazisomwi sana. Nikaacha kuweka post na kuendelea na maisha.

Siku moja nadhani mwaka 2011, nikajiambia hebu nijaribu tena, nakumbuka nilikuwa naweka post nyingi kwa siku tena ndefu tu kama zamani... Hali ikawa ni ile ile. Siku moja baada ya kusoma post ya AshaDii, nikavutiwa nayo na nikawasiliana na yeye kwa PM kwa ajili ya ushauri.

Alinisaidia sana kunielimisha namna ya kuweka post na kushiriki mjadala katika post niliyoweka na pia kushiriki mijadala mbalimbali katika majukwaa tofauti tofauti kwani itasaidia kutambuliwa kama mchangiaji mzuri wa JF... nashukuru kwamba ushauri huo umenisaidia sana. The Boss na yeye alinisaidia sana namna ya ya kujenga hoja na kuitetea, pia alinisaidia sana kwenye maeneo ya IT.......... kwa mfano ku-quote, kuweka picha na vitu kana hivyo...

Dada yangu gfsonwin sina la kusema, wewe mwenyewe unajua ni kiasi gani umekuwa msaada wangu kwa ushauri wa mambo ya kifamilia hususan kumjua Mungu na maombi. (SUGUA GOTI SANA...!)

Lakini pia yupo mama yangu Mamndenyi, nilipopata ajali tarehe 25/10/2011, ulijitahidi sana kunitumia asali na mdalasini kama dawa, leo nimepona na nina bofya keyboard kama kawa, ubarikiwe mama.

Nitafanya kosa kubwa kama nisipowataja wanangu wawili ambao kupitia changamoto zao za ulinzi shirikishi zimenisaidia sana kuniepusha na kifo cha UKIMWI maana wamejitahidi sana kunibana kila kona mpaka nimesalimu amri...

Big up sana kwa mwanangu Cantalisia popote ulipo na dada yako mkubwa King'asti......

Naomba niwatambue wana MMU wooote jamani ngoja tu nitambue uwepo wa SnowBall, jouneGwalu, Eiyer, Mwita Maranya, Asprin, mwanjamiione, BADILI TABIA na nyumba kubwa .......

Mwisho ni wana CHIT CHAT, hapa naomba niwataje Madame B, lara 1, cacico, snowhite, charminglady, sweetlady 1, @Smail, Kongosho na wengine ambao sikuwataja, lakini wamekuwa wakichagiza mijadala mbalimbali hapo chit chat kwa mipasho na kujishetua mpaka raha jamani.............. Loooooooh!!!!!!!!!!!
Mtambuzi Iam so humbled ..
Uwepo wako Jf umeongeza kitu kikuubwa sana
jf imekuwa na mature contents nyiingi zaidi
na age group ya wana jf iliyokuwa inakosa vingi vya kujadili imefaidika

Nashkuru kwa kutambua mchango wangu pia
 
Last edited by a moderator:
AshaDii.
AshaDii many thanks for having me in your list, much appreciated really i didnt know if anyone thought anything of whatever i write here, so am actually speechless and really thankful...

my list goes

1. AshaDii ( not returning favour but you are one JF sweetheart, atleast to me and many when you see the tags you are getting, i dont know how to tag a name yet )
2. Michelle......miss you big !
3. FaizaFoxy...as i was just getting to know you ....
4. Miss Judith....ever wondered what happened to huyu Mpendwa ?
5.Kaizer,The Boss, EMT, BAK, Kiranga, Nyani Ngabu
6. Reverend Kishoka...where @ thou ?




wengine woooote, nawapenda jamani Lara1 na wengineo


Thanks a lot Engineer...
much respect
 
Back
Top Bottom