Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,772
- 7,881
Mwanaume ni kiumbe ambaye ni raising kumteka kimapenzi. Na ndio maana matukio ya Wanaume kupotea na kukutwa kafungiwa ndani kwa mwanamke fulani ni mengi, ilibidi hata Mbosso aandike nyimbo ya "Amepotea" kuonesha ni namna gani mwanaume ni rahisi kuuiba mutima wake.
Ni tofauti na kuuteka moyo wa mwanamke, hapa sizungumzii binti wadogo ambao balehe zinawasumbua, unakuta kamengangania kwenye ghetto. Hapa nazungumzua kuuteka moyo wa mwanamke mtu mzima ni ngumu sana, na ndio maana watu utumua udhaifu kama fedha au ahadi mbalimbali hili kuushinda moyo wa mwanamke. Na bado sio guarantee ya yeye kukupenda.
Kuuteka Moyo wa Mwanaume haiitaji ufundi wala nini cha Kwanza uwa ni Kupitia tumbo lake yani Msosi. Mwanamke unanafasi kubwa sana ya kupendwa kama unajua kupika chakula kizuri na kitamu. Kuna msemo unosema "If you want to reach a Man's heart, go through his stomach". Ukiwa na mkono mzuri wa mapishi unakuwa umejihakikishia ufaulu wa 50% kuushinda moyo wake. 50% nyingine zilizobaki inatakiwa uzikamilishe kupitia mambo hayo hapo chini.
Vidokezo kwa wanawake – namna ya kuuteka moyo wake kwa 50% zilizobaki.
Kumshika mwanaume si kwa uchawi wala mbinu za kumfunga kamba.
Ni kwa jinsi anavyojisikia akiwa na wewe.
Upendo ni mzuri, ngono ni muhimu. Lakini Heshima ndiyo inamfanya akae.
👉 Mwanaume anayehisi kuheshimiwa, atapigania mahusiano yadumu.
Kama nyumbani ni kelele, drama na lawama kila siku… moyo wake utaanza kutoka taratibu.
💡 Wanaume ujikuta wameingia kwenye mahusiano na mwanamke anayewapa amani haraka kuliko mwanamke mwenye uzuri. Hapa ndipo matajiri wengi unakuta kaoa mwanamke wa kawaida.
👉 Wanaume wanatambua hali ya kujifanyisha au kuwaigizia haraka sana.
Mwambie:
⚠️ Usizidishe sana shukrani utaharibu, lakini usimnyime shukrani.
Badala ya: ❌ “Wewe hunijali kabisa!”
Sema: ✅ “Najisikia mbali pale hatuzungumzi.”
Hii inafungua moyo wake, haimfanyi ajitetee hili kujilinda. Lakini ukitumia lugha ya kushambulia lazima atataka kujitetea kwa kujilinda na si kufungua moyo wake kwa uwazi.
Ni:
Huwezi kumshika mwanaume asiyetaka kushikwa.
Upendo hautabadilisha misimamo yake kama:
Ni tofauti na kuuteka moyo wa mwanamke, hapa sizungumzii binti wadogo ambao balehe zinawasumbua, unakuta kamengangania kwenye ghetto. Hapa nazungumzua kuuteka moyo wa mwanamke mtu mzima ni ngumu sana, na ndio maana watu utumua udhaifu kama fedha au ahadi mbalimbali hili kuushinda moyo wa mwanamke. Na bado sio guarantee ya yeye kukupenda.
Kuuteka Moyo wa Mwanaume haiitaji ufundi wala nini cha Kwanza uwa ni Kupitia tumbo lake yani Msosi. Mwanamke unanafasi kubwa sana ya kupendwa kama unajua kupika chakula kizuri na kitamu. Kuna msemo unosema "If you want to reach a Man's heart, go through his stomach". Ukiwa na mkono mzuri wa mapishi unakuwa umejihakikishia ufaulu wa 50% kuushinda moyo wake. 50% nyingine zilizobaki inatakiwa uzikamilishe kupitia mambo hayo hapo chini.
Vidokezo kwa wanawake – namna ya kuuteka moyo wake kwa 50% zilizobaki.
Kumshika mwanaume si kwa uchawi wala mbinu za kumfunga kamba.
Ni kwa jinsi anavyojisikia akiwa na wewe.
1. Mheshimu (HILI NI MUHIMU SANA)
Upendo ni mzuri, ngono ni muhimu. Lakini Heshima ndiyo inamfanya akae.
- Heshimu mawazo yake hata kama unayapinga
- Usimdhalilishe mbele za watu
- Zungumza nae kama Mwenza, na si kama mtoto au mtu baki
👉 Mwanaume anayehisi kuheshimiwa, atapigania mahusiano yadumu.
2. Mpe amani, na sio msongo
Maisha tayari yanawapa wanaume presha—mfano kazi, kutafuta pesa, matarajio ya jamii.Kama nyumbani ni kelele, drama na lawama kila siku… moyo wake utaanza kutoka taratibu.
- Fanya nyumbani au mahali pa kukutana pawe eneo tulivu au lenye amani
- Zungumza kwa busara na unyenyekevu, sio kwa mashambulizi
- Chagua muda sahihi wa kuzungumza (na sio wakati akiwa amechoka au mwenye hasira)
💡 Wanaume ujikuta wameingia kwenye mahusiano na mwanamke anayewapa amani haraka kuliko mwanamke mwenye uzuri. Hapa ndipo matajiri wengi unakuta kaoa mwanamke wa kawaida.
3. Kuwa na uanamke ambao ni halisi, sio wa kuigiza
Kuwa na tabia za kike zaidi si udhaifu. Ni:- Mawasiliano yenye upole
- Akili ya kihisia au ujasusi wa kihisia
- Utulivu hata wakati wa presha (Wakati ambao kuna lawama au mambo hayaendi vizuri)
👉 Wanaume wanatambua hali ya kujifanyisha au kuwaigizia haraka sana.
4. Mthamini kwa maneno
Wanaume wengi hawahisi kama wanathaminiwa au wenye kupata shukrani au Asante. Ni wachache sana wanaopongezwa na wenza wao kwa moyo mmoja kutokana na jitihada wanazofanya. Hata kama hafanyi kwa ubora wewe mtie moyo tu kwa maneno yenye kuthamini hata kidogo anachofanya.Mwambie:
- “Ninakuthamini.”
- “Najisikia salama nikiwa na wewe.”
- “Ninapenda jinsi unavyoshughulikia mambo.”
⚠️ Usizidishe sana shukrani utaharibu, lakini usimnyime shukrani.
5. Kuwa na maisha yako
Hii inaonekana kinyume au tofauti na mitazamo ya wengi, lakini inafanya kazi. Mwanamke ukiwa na maisha yako inakuwa bora zaidi kuliko kuwa tegemezi kwenye kila kitu.- Kuwa na ndoto zako
- Marafiki wako
- Shughuli zako
6. Mruhusu ajisikie ni mwanaume
Wanaume hujenga mapenzi kupitia kuhisi wanafaa.- Mruhusu akusaidie
- Usikatae kila anachojaribu kufanya
- Muda mwingine Amini kwenye uwezo wake wa kuongoza mambo mbalimbali hata kama ana udhaifu
- Tambua mafanikio yake, hata madogo au makubwa
7. Wasiliana bila kumshambulia
Badala ya: ❌ “Wewe hunijali kabisa!”
Sema: ✅ “Najisikia mbali pale hatuzungumzi.”
Hii inafungua moyo wake, haimfanyi ajitetee hili kujilinda. Lakini ukitumia lugha ya kushambulia lazima atataka kujitetea kwa kujilinda na si kufungua moyo wake kwa uwazi.
8. Kuwa mwaminifu kwa vitendo, na si maneno
Uaminifu si kutosaliti tu.Ni:
- Kutocheza na hisia za wanaume wengine au kujitongozesha
- Kulinda mahusiano yenu mbele za watu wengine
- Kumchagua hata siku ambazo si mkamilifu
9. Dumisha ukaribu (kihisia na kimwili)
Faragha si kufanya ngono tu.- Migusano (Touch)
- Utani na michezo ya kimapenzi
- Kuangaliana machoni
- Vicheko vya
10. Chagua mwanaume sahihi
Huu ni ukweli ambao wengi hawaupendi:Huwezi kumshika mwanaume asiyetaka kushikwa.
Upendo hautabadilisha misimamo yake kama:
- Tabia na hisia za kitoto
- Kukosa maadili
- Hofu ya kujitoa kwa ajili yako
Ukweli wa mwisho ❤️
Mwanaume hukaa pale anapohisi:- Anaheshimiwa
- Anathaminiwa
- Ana amani
- Anatamaniwa
- Anaeleweka