Waliobadilisha Maisha yangu....

Waliobadilisha Maisha yangu....

Nipo mchumba. Kuna mtu alining'ata sikio kwamba tuko watatu kwenye waiting list bado unatufanyia utafiti kujua nani anakufaa kuwa mwenza wa maisha. Sasa nikaona nitulie kidogo kupisha utafiti. Kama ilikuwa ni kweli unijulishe ili nijue naanzia wapi.
Afu nimekumisije!? babu yako Asprin nae siku hizi hasomeki sijui amevurugwa na nani!?

Leo yamefika kwa mama.....halafu huyu Asprin ndo mbaya wetu...anataka kutuvurugia familia..
 
Last edited by a moderator:
Leo yamefika kwa mama.....halafu huyu Asprin ndo mbaya wetu...anataka kutuvurugia familia..

Hahahaha.., kweli waswahili walisema kuzaa si kazi, kazi ni kulea!!
Kila kona anakopita dady nawe huchezi mbali? usifanye hivyo bana ntakununulia zawadi nzuuuuri, usimwambie mama yako yaishie hapa hapa.
by the way i'm please to meet you here.
 
Leo yamefika kwa mama.....halafu huyu Asprin ndo mbaya wetu...anataka kutuvurugia familia..

We zuga tu. Nshakubadilishia maisha yako we umekomaa kunimenshen. Mbona Mwita Maranya kanitaja, kwani kapungukiwa na nini?

Hebu nimenshen bana, mtoto wa mwanamke mwenzio nipate apetaiti ya kumzalisha mwanamke mwenzio.
 
Last edited by a moderator:
watu wangu sita, japo zamani niliwahi kuwa acknowledge watu kadhaa kwenye uzi mmoja kwenye chitchat, lakini how can i not mention watu wafuatao ambao wamenibadili in one way or another in real life au virtually: 1. Mtambuzi 2. chief-mkwawa (huyu ni shujaa wa jukwaa la science and tech) 3. Elizabeth Dominic 4. Young Master 5. nyasiro 6. charminglady
 
Last edited by a moderator:
Kuna wa kutafuta lakini si wewe. Nikikutaka si nakupigia mluzi tu unakuja mwenyewe? Ila nisipokuwa makini huchelewi kunigomea manake siku hizi umekuwa mkaidi kama mke wa Mwai Kibaki.

Hahahha naona kabisa jinsi ulivyonivua cheo changu cha Mjukuu Mtiifu bila idhini ya Bibi!
 
Naomba radhi nimechelewa kwenye huu uzi maana MKOLONI WANGU KANIBANA SANA MWEZI HUU (Source: Asprin)

Kuna watu watatu humu ambao kwa kweli walinisaidia sana kunishauri namna ya kuweka post na kuifanya iwe na changamoto mpaka sasa najivunia kuona kwamba wapo watu leo hii wanakiri kwamba kile ninachokifanya kimesaidia kubadili maisha yao.

Naomba niwalete kwenu Da' AshaDii, kaka yangu The Boss na dada yangu gfsonwin.

Nakumbuka nilijiunga na Jamii forum mwaka 2008, wakati huo ikiitwa Jambo Forum, lakini nilipokuwa nikiweka post zangu watu wanalaumu kuwa ni ndefu na zikawa hazisomwi sana. Nikaacha kuweka post na kuendelea na maisha.

Siku moja nadhani mwaka 2011, nikajiambia hebu nijaribu tena, nakumbuka nilikuwa naweka post nyingi kwa siku tena ndefu tu kama zamani... Hali ikawa ni ile ile. Siku moja baada ya kusoma post ya AshaDii, nikavutiwa nayo na nikawasiliana na yeye kwa PM kwa ajili ya ushauri.

Alinisaidia sana kunielimisha namna ya kuweka post na kushiriki mjadala katika post niliyoweka na pia kushiriki mijadala mbalimbali katika majukwaa tofauti tofauti kwani itasaidia kutambuliwa kama mchangiaji mzuri wa JF... nashukuru kwamba ushauri huo umenisaidia sana. The Boss na yeye alinisaidia sana namna ya ya kujenga hoja na kuitetea, pia alinisaidia sana kwenye maeneo ya IT.......... kwa mfano ku-quote, kuweka picha na vitu kana hivyo...

Dada yangu gfsonwin sina la kusema, wewe mwenyewe unajua ni kiasi gani umekuwa msaada wangu kwa ushauri wa mambo ya kifamilia hususan kumjua Mungu na maombi. (SUGUA GOTI SANA...!)

Lakini pia yupo mama yangu Mamndenyi, nilipopata ajali tarehe 25/10/2011, ulijitahidi sana kunitumia asali na mdalasini kama dawa, leo nimepona na nina bofya keyboard kama kawa, ubarikiwe mama.

Nitafanya kosa kubwa kama nisipowataja wanangu wawili ambao kupitia changamoto zao za ulinzi shirikishi zimenisaidia sana kuniepusha na kifo cha UKIMWI maana wamejitahidi sana kunibana kila kona mpaka nimesalimu amri...

Big up sana kwa mwanangu Cantalisia popote ulipo na dada yako mkubwa King'asti......

Naomba niwatambue wana MMU wooote jamani ngoja tu nitambue uwepo wa SnowBall, jouneGwalu, Eiyer, Mwita Maranya, Asprin, mwanjamiione, BADILI TABIA na nyumba kubwa .......

Mwisho ni wana CHIT CHAT, hapa naomba niwataje Madame B, lara 1, cacico, snowhite, charminglady, sweetlady 1, @Smail, Kongosho na wengine ambao sikuwataja, lakini wamekuwa wakichagiza mijadala mbalimbali hapo chit chat kwa mipasho na kujishetua mpaka raha jamani.............. Loooooooh!!!!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
We zuga tu. Nshakubadilishia maisha yako we umekomaa kunimenshen. Mbona Mwita Maranya kanitaja, kwani kapungukiwa na nini?

Hebu nimenshen bana, mtoto wa mwanamke mwenzio nipate apetaiti ya kumzalisha mwanamke mwenzio.

Teh Teh ..nimekuambia unipe rushwa nikumensheni ume-mute....Ngoja basi nikaedit post kwa ajili yako...
Halafu tabia yako ya kumfundisha dady wangu ukaguzi sio nzuri uiache....
 
can say nothing, i got no friends in my list but i do appreciate those who contribute with facts, evidence, those who are serious, ain't say i've bn here for long, i'm new to most of ya guys
 
DA anasema asanteni sana woooooteeeeeeee nianze kwa kusema hivi:

1. Waliobadilisha maisha yangu wa kwanza kabisa naomba nikutaje kwa msisitizo Kaizer wewe ndio uliniondolea mawazo na kunishauri vyema kama kaka mkubwa (Thank you so much)

2. Naomba niwataje hawa watu kwa msisitizo maalumu kwa mchango wao kwangu wakati nilipokuwa na matatizo MwanajamiiOne (Dada mkubwa) Asprin (Babu) RR AshaDii (wifi wa ukweli) Teamo WiseLady paka Jimmy Mzee wa Rula Mwita Maranya (shem wa ukweli) Kimey The Finest (Kijanaa sisemi kitu hapa) afrodenzi (Mdogo wangu mpenzi) Baba_Enock Tall Bigirita FirstLady1 Michelle (Mdada mdogo) Husninyo (Mdogo wangu wa ukweli) Bishanga Maty Dark City Nyamayao (big mama) Chauro Chapakazi BAK FP Lily Flower Elia kokudo Mr Rocky (My Huby) Fidel80 (Mzee wa Manzese) sweetlady zion Daugher mamadenyi (Bibi mwenyewe wa ukweli) (nawashukuruni sana kwa ushauri wenu na michango yenu) Kuna wengi nimewasau lakini nawapenda sana woooteee

3. Hawa ni marafiki wangu wakubwa iwe tumeonana au kupigiana simu au kutumiana PM kwa ushauri wa mambo mbali mbali KakaKiiza Ndahani Bujibuji Kimweka (mzee wa jukwaa pendwa) figganigga Kipipi Likasu Kaka Sam Mkwaruzo Sinziga Boflo jouneGwalu VUVUZELA Thomas Odela List ni ndefuuuuuuu kuna wale najua nimewasahau msijali sana nawapenda woooote

4. MMU imeniondolea stress kwa asilimia 99.9 kama sio 100 thank you wooooteee

DA
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi asante sana kwa kunitambua uwepo wangu.
"Lakini pia yupo mama yangu Mamndenyi, nilipopata ajali tarehe 25/10/2011, ulijitahidi sana kunitumia asali na mdalasini kama dawa, leo nimepona na nina bofya keyboard kama kawa, ubarikiwe mama".
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Mi nawashukuru wengi sana kila mmoja kwa namna yake ila kwa leo namshukuru baba yangu MziziMkavu karibu ananirithisha u doctor wake nimekuwa addicted na matumizi ya dawa na vyakula vya asili kwa sababu yake
 
Kuna vyeo vifuatavyo ambavyo ni vya kudumu na hakuna mwenye mamlaka ya kuvijadili
1. Mjukuu Mtiifu - MwanajamiiOne
2. Mjukuu Mteule - afrodenzi
3. Mjukuu Mwaminifu - Cantalisia.
4. Fellow Tablet - klorokwini
5. Dada mnoko - Nyamayao
6. Hommie - Kaizer
7. Shem wa ukwee AshaDii
8. Mchumba - Zion Daughter
9. Asali ya ODM Kongosho

I demand the tittle to change Asap...uchumba gani huu mpaka sasa tunakuwa wazee.nataka UNIOE au kieleweke rasmi..
Copy kwa wake zako.. cacico Yummy na wenzao
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom