Wachina waja na maji haya, wanaliteka soko mdogo mdogo

Wachina waja na maji haya, wanaliteka soko mdogo mdogo

Nilikuwa nafikiria hili suala tangu zamani kwamba akija mwekezaji mmoja akatumia akili kidogo tu ya kuongeza ujazo wa maji katika chupa basi wateja wote watakimbilia kwake,na kweli maji ya jambo yalithibitisha ndoto yangu maana aliongeza ujazo kutoka 1.5 mpaka 1.6 na 0.5 mpaka 1.6 na kweli alisepa na Kijiji Kanda ya ziwa yote ni JAMBO sijajua sehemu nyingine.Wafanyabiashara wajifunze kuacha tamaa ya kupata faida mara dufu,hivi ukiongeza ujazo wa maji wewe ukapanda Hadi litre 2 Kwa bei ile ile ya lt 1.6 utapungukiwa nini!??? Mbona maji yamejaa tele unit Moja ya maji ni 1100 ina maana unatoa chupa kibao
 
Jana nipo Kariakoo nikaagiza maji nikaletewa maji haya muuzaji akinambia yanaitwa “Mshangazi” ikabidi nicheke.

Nikaambiwa wengine wanayaita “Bonge la Dada”

Mchina kaja na maji mengi kwa bei ileile nafuu, yaani 1.8L

Wazawa wamelala, wakija kushtuka hawana chaoView attachment 3532995View attachment 3532997
Hawa jamaa ni wale wa kamari.. Wamevuna mtaji wamebadili gia angani baada ya biashara ya kamari kudoda
 
Kwa nini Wachina ni wawekezaji kutoka nje ila wanauza vitu bei rahisi kuliko wazawa??
Naona wazawa wanaweka margin kubwa zaidi
Fikra tu
Wachina viwanda vinatoka kwao na wanajua wapi pa kuvipata na huenda hata hitilafu ilitokea wana vijana wao wa kutengeneza pia.
Sisi ujanja mwingi sana

Nakumbuka hata Nairobi Wasomali walishika soko la vyombo na kuwatoa wahindi wazoefu kwenye biashara kwa sababu ya unyonyaji na bei kubwa wakajisahau sana
 
Kila mtu na mteja wake. Wanaofuata bei wapo,wanaofuata jina wapo,wanaonunua kilichopo wapo. Mimi binafsi hata angeuza tzs 100 sinunui maji ya mchina.
Na hili nalo neno
Hawa wajanja pia wanaweza kuwa wanajaza maji ya Dawasa kwenye machupa hili nalijua kuna watu UK walikamatwa wakijaza maji ya bomba kwenye chupa za glass na kuyauza bei mbaya
 
Watu walidhani mgogoro na mchina utaishia kkoo tu.

Sasa hatimae wafanyabiashara wakubwa wamefikiwa.


Na hii ishu haitoishia hapo tu, ndani ya miaka 6-10 ijayo, tutakua na wachina kwenye siasa.

Vyama vyote vitakua na wagombea wachina

Waheshimiwa wabunge mjiandae vizuri, miaka 6-10 ijayo utakua jimboni unapambana na mchina, wewe unahonga yeye anajenga.

Nyie mkichaguliwa mnahamia dar, chenyewe kikichaguliwa tu,kinalowea huko huko jimboni.

Jinping anacheza draft kwa akili sana.

Trump hakukosea kusema Africa inahitaji kutawaliwa tena.
NI bora iwe hivyo kwani siasa ya chukua chako mapema ni pasua kichwa.
 
Back
Top Bottom