Wachina waja na maji haya, wanaliteka soko mdogo mdogo

Wachina waja na maji haya, wanaliteka soko mdogo mdogo

Jana nipo Kariakoo nikaagiza maji nikaletewa maji haya muuzaji akinambia yanaitwa “Mshangazi” ikabidi nicheke.

Nikaambiwa wengine wanayaita “Bonge la Dada”

Mchina kaja na maji mengi kwa bei ileile nafuu, yaani 1.8L

Wazawa wamelala, wakija kushtuka hawana chaoView attachment 3532995View attachment 3532997
acha mchina awapge bao wazawa maana mfano mi npo kanda ya ziwa kampuni ya jambo jamukaya anatengeneza maji, juice nk lakn bei anayouza uku kanda ya ziwa ni sawa na juice na maji ya azam uhai, wkt jambo yeye gharama za usafiri zko chini tofauta na bidhaa za azam znatoka dsm ilitakiwa ili ateke soko kanda ya ziwa maji ya buku auze hata jero tu, halafu uko dsm ndo auze bei kubwa, azam nae ilitakiwa kwa dar na pwani na morogoro,tanga, mtwara, lindi angeshusha bei sbb gharama za usafiri si kubwa.
 
Kwa nini Wachina ni wawekezaji kutoka nje ila wanauza vitu bei rahisi kuliko wazawa??
wachina wanakuja na tech cheap sn ambayo haina gharama kubwa ya uendeshaji, unakuta hcho kiwanda kpo eneo dogo sn na machine ndogo za ksasa umeme kdogo sn, znasafisha maji, znatoa chumvi maji yanakuwa safi kwa gharama ndogo mno, unakuta machine zpo kwny kachumba kamoja tu na znahtaji watu 4 wa kuziongoza, mmoja wa computer, mwngne wa kuweka dawa na wawili wa kupanga na machine zko faster.
 
Hawa Wachina wanaokamatwa na mabilioni kwenye viroba hawana la kuambiwa na TBS.

Na tatizo sio kwa TBS pekee, machimbo ya madini kule kanda ya ziwa (ambayo nayo siku hizi yamevamiwa na Wachina) yanamwaga mercury kwenye vyanzo vya maji, unakutana na kesi nyingi za kansa uko Shinyanga na Simiyu. Tatizo ni serikali nzima kuanzia wanaosimamia uwekezaji, manufacturing, biashara, exports na imports, sera za uchumi, mikopo na kila kitu.
Ok.
Kwa hiyo kimsingi tatizo sio wachina na biashara zao. Ni mifumo ya serikali ndio imefeli. Pia tufahamu kuwa magumashi hayafanywi na watu wa nje tu, ni pamoja na wabongo wenzetu. Mfano ni wanaoingiza bidhaa zisizo na viwango na wakijua hazina viwango ni watz wenzetu. Na mara kadhaa waswahili wamekamatwa wakitengeneza pombe feki huko Manyara.
Kwa hiyo lawama ziende kwa serikali.
 
Jana nipo Kariakoo nikaagiza maji nikaletewa maji haya muuzaji akinambia yanaitwa “Mshangazi” ikabidi nicheke.

Nikaambiwa wengine wanayaita “Bonge la Dada”

Mchina kaja na maji mengi kwa bei ileile nafuu, yaani 1.8L

Wazawa wamelala, wakija kushtuka hawana chaoView attachment 3532995View attachment 3532997
WaBongo atakuja na propaganda kwamba yanapunguza nguvu za kiume ili kuharibu soko la Mchina😁😁Acha tuone!!
 
Ok.
Kwa hiyo kimsingi tatizo sio wachina na biashara zao. Ni mifumo ya serikali ndio imefeli. Pia tufahamu kuwa magumashi hayafanywi na watu wa nje tu, ni pamoja na wabongo wenzetu. Mfano ni wanaoingiza bidhaa zisizo na viwango na wakijua hazina viwango ni watz wenzetu. Na mara kadhaa waswahili wamekamatwa wakitengeneza pombe feki huko Manyara.
Kwa hiyo lawama ziende kwa serikali.
Kwahiyo Wachina ni wasafi, ila Watanzania ndio wenye makosa na serikali ilaumiwe?
 
Kwahiyo Wachina ni wasafi, ila Watanzania ndio wenye makosa na serikali ilaumiwe?
Hujanielewa. Nisome tena.

Kunya anye kuku, akinya bata kaharisha!

Mchina na uchafu wake ameruhusiwa na serikali.
Mtanzania na uchafu wake ameruhusiwa na serikali.
Kuwepo kwa uchafu huo, ilaumiwe serikali. Na kama unalaumu watu, basi mchina na mtanzania wanaofanya magumashi walaumiwe wote wawili bila kujali uraia wao.
 
Sio kweli mchina kaja mkomboa mwafrika katika swala zima la uchumi kwa sababu kwa miaka yote hii toka uhuru mzungu bidhaa zake ameweka ngumu kwa afrika ikiwa ni pamoja na bei kubwa hakutaka muafrika anyanyuke kiuchumi.Kwa hivyo mchina amekuja kama mkombozi kwani wewe leo hii wamkataa mchina wakati 90% unatumia bidhaa zake kuanzia hiyo simu uliyokua nayo.
 
Kwani ni bidhaa ngapi zinatoka ulaya leo hii kulinganisha na china?So tusimkatae mchina bali awe chachu ya kutuamsha usingizini sisi waafrika katika maswala mazima ya uchumi.Wazungu tunao washabikia wametunyonya kwa miaka yote na hawakutaka tuinuke kiuchumi walitaka tuendelee kua tegemezi kwao lakn mchina kaja fanya mapinduzi ya kiuchumi,leo hii kandarasi nyingi kapewa mchina na sio mzungu kwanini mzungu ni mnyonyaji hataki afrika iendelee
 
Naona wazawa wanaweka margin kubwa zaidi
Fikra tu
Wachina viwanda vinatoka kwao na wanajua wapi pa kuvipata na huenda hata hitilafu ilitokea wana vijana wao wa kutengeneza pia.
Sisi ujanja mwingi sana

Nakumbuka hata Nairobi Wasomali walishika soko la vyombo na kuwatoa wahindi wazoefu kwenye biashara kwa sababu ya unyonyaji na bei kubwa wakajisahau sana
China wanakopeshwa mikopo Kwa annual interest ya aslimia 3

Unataka alingane bei na mtanzania anaekopeshwa na bank za Tanzania Kwa interest ya 20%+ ?

Acheni unafiki na roho mbaya.

Hao wachina wanakuja kuchota Hela wanapeleka kwao
 
Kila mtu na mteja wake. Wanaofuata bei wapo,wanaofuata jina wapo,wanaonunua kilichopo wapo. Mimi binafsi hata angeuza tzs 100 sinunui maji ya mchina.
Wewe bhn upo kama mimi. Nlivyoyaona tu nikamwambia sister wangu "hapa hakuna maji." basi akacheka 😅😅 namskia anasema "maji yenyewe Mengi 1.8L khaa kama ya bule." 🤣🤣
 
Nimekunywa hayo maji niseme tu yametulia na yanakuja kwa kasi balaa wachina ni nuksi kwenye biashara kupambana nao jipange hata siko la sabuni za unga washalinyakuwa tafuta omo,azania,foma gold mitaani zimepotea kwa sasa zimezagaa nice one za kichina tu na ile ya kupima yaani biashara ya mchina anakupa kingi kwa bei kitonga
 
Wayalete sasa na huku vijijini maana akina kilimanjaro sametuzoea vibaya.
 
China wanakopeshwa mikopo Kwa annual interest ya aslimia 3

Unataka alingane bei na mtanzania anaekopeshwa na bank za Tanzania Kwa interest ya 20%+ ?

Acheni unafiki na roho mbaya.

Hao wachina wanakuja kuchota Hela wanapeleka kwao
Hapo ndio tunaita kukosa elimu ya Biashara
Biashara haifanywi kulipa mkopo bali inafanywa kwa standard profit margin ili mtu atumie sehemu ya faida kulipa mkopo; Au unataka kutuambia; ukisha maliza kulipa mkopo utashusha bei kama wachina?

Mbona takribani nusu ya bishara kariakoo hawana mikopo lakini hatuoni hizo bei nafuu kama za wachina?
Mtanzania analeta bidhaa kutoka china anasema tu bei 280,000 hata ukimuuliza ametumia hesabu gani kupata hiyo bei hajui? unategemea nini

Mfano: Mtanzania anaweka fridge moja faida ya shs 200,000 anauza moja kwa siku
Mchina anaweka fridge moja faida ya shs 100,000 anauza 5 kwa siku
Ukilinganisha hapo, nani mwenye akili ya biashara na aliyepata faida nyingi?
 
Hawana tamaa kama wazawa. Halafu kingine wanatumia technolojia yenye high productivity. Kwahiyo unakuta average cost yao ni ndogo kuliko makampuni ya wazawa.

Halafu kwenye biashar kuna kitu tunakiita predatory pricing--unauza bidhaa kwa bei ya chini ili uuwe ushindani na baadae uweze kuliteka soko.
Hiyo PREDATORY PRICING ndio unyama wenyewe
 
Hawana tamaa kama wazawa. Halafu kingine wanatumia technolojia yenye high productivity. Kwahiyo unakuta average cost yao ni ndogo kuliko makampuni ya wazawa.

Halafu kwenye biashar kuna kitu tunakiita predatory pricing--unauza bidhaa kwa bei ya chini ili uuwe ushindani na baadae uweze kuliteka soko.

Wabongo wanaweka faida kubwa huku wakiwaachia mawinga waweke faida mara mbili; halafu wanasingizia wachina. Wachina wana elimu ya biashara.....hela ya winga mwenye duka ndiye analipa sio mteja
Siku wafanyabiashara wakitoka usingizini watajua kuwa, Mawinga ni tatizo kubwa kuliko Wachina
Kuhusu Predatory pricing, wala haiko applicable hapo.....kwa sababu wachina wanauza kwa profiti magin kubwa tu...
 
Back
Top Bottom