Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

1.
Mkuu katiba inasema kuwa kila mtu atahesabika hana hatia mpaka mahakama itakapothibitisha vinginevyo.Kwahiyo wao na heshima yao unataka waanze kuropokaropoka Mkapa mwizi kama sisi wengine hapa kabla ya huo wizi kuthibitishwa mahakamani?

- Mkuu kumbe unaropoka ropoka hapa JF bila ya kuwa na ushahidi? Sisi tunao dhidi ya Mkapa, na tulimkabidhi rais wa sasa ambaye aliamua kumsamehe apumzike, kwa hiyo next time hakikisha una ushahidi kama tuliompa rais dhidi ya Mkapa, badala ya kuropoka ropoka kama nyinyi wengine hapa!

2.
Hawana uwezo wa kumchagua mtu kuwa Rais wa Tanzania.Lakini kumbuka kwamba linapokuja swala la uchaguzi basi kila mtu atakuwa na mtu wake ambaye angependa kuona anakuwa kiongozi wa ngazi fulani hata kama mwisho wa siku lile chaguo lake litashindwa.Kwahiyo wao nao wako katika mkondo huo na ndiyo mana hata wanasiasa nao wanajaribu sana kuwa karibu yao wakitafuta kuungwa mkono kwa nguvu yao waliyonayo kwa wale waumini wanaowasimamia.

- Hiyo nguvu yao ya waumini wanaowasimamia, waliwahi kuitumia kumchagua rais gani kati ya waliowahi kutawala Tanzania?
 
1.

- Mkuu kumbe unaropoka ropoka hapa JF bila ya kuwa na ushahidi? Sisi tunao dhidi ya Mkapa, na tulimkabidhi rais wa sasa ambaye aliamua kumsamehe apumzike, kwa hiyo next time hakikisha una ushahidi kama tuliompa rais dhidi ya Mkapa, badala ya kuropoka ropoka kama nyinyi wengine hapa!

2.

- Hiyo nguvu yao ya waumini wanaowasimamia, waliwahi kuitumia kumchagua rais gani kati ya waliowahi kutawala Tanzania?

Wanaoropoka ni wana JF na wengine wote wanaodai Mkapa mwizi bila ya mahakama kusema hivyo.Kama kuna post yangu yoyote niliyosema Mkapa mwizi basi niwe katika hilo kundi na kama hakuna basi wale wote wanaodai hivyo bila ya uthibitisho wa mahakama ni waropokaji mkuu.
Point yangu ya pili kama hujaielewa peace out mkuu!
 
Wanaoropoka ni wana JF na wengine wote wanaodai Mkapa mwizi bila ya mahakama kusema hivyo.Kama kuna post yangu yoyote niliyosema Mkapa mwizi basi niwe katika hilo kundi na kama hakuna basi wale wote wanaodai hivyo bila ya uthibitisho wa mahakama ni waropokaji mkuu.

- Mkuu acha matusi, maovu yote ya Mkapa, tumeorodheshewa na rafiki yake wa zamani mpenzi Mengi, kwenye magazeti yake, na rais wa sasa alipopewa hakusema ni uropokaji au ni uongo, ila alisema tumuache apumzike, kwa maana hii uropokaji wetu unaweza kuwa ni ule unaokubalika na mzuri kwa taifa,

- Kwa mfano, look lets say kwamba sisi ni waropokaji, maana tulisema Mramba, Yona, na Mgonja ni mafisadi na wezi na leo wapo kwenye mahakama kama tulivyoropoka huko nyuma bila ya wewe kushiriki, maana wewe unasubiri mahakama kwanza, sasa huoni kwamba tuna uropokaji ulioenda shule? na ni mzuri kwa taifa letu?

- Sasa wewe subiri mahakama, sisi wacha tuendelee kuropoka kuhusu mafisadi waliobaki, halafu vipi na blaza Mwakyembe naye mropokaji maana uropokaji wake haukuenda mahakamani lakini waziri mkuu na mawaziri wawili wa jamhuri walikimbia kazi zao bila kuambiwa na mahakama kama unavyotaka, sasa unasema na blaza naye ni mropokaji au?
 
Wakuu wa dini zote Tanzania ni wanafiki. Wanataka kujionyesha wapo pamoja na Watanzania katika vita ngumu dhidi ya mfisadi na wakati huo huo wanataka pia waonekane wema kwa mafisadi!!! Mfano ni pale moja ya makanisa yetu walipomkaribisha fisadi Rostam Aziz kanisani na kupokea mchango mkubwa wa pesa zake za kifisadi.

Hili kamwe haliwezekani mkawa pande zote mbili kwa wati mmoja!!!! Lazima muache unafiki na kuungana na upande ambao unatetea maslahi ya nchi. Kamwe nchi haiwezi kuingia kwenye machafuko kwa kuwatia hatiani mafisadi waliojivisha ngozi ya uongozi ili kuwafisadi Watanzania.

Naam mimi ni mmoja wa waropokaji kuhusu mafisadi ndani ya nchi yetu, sihitaji kusubiri mahakama ili kujua nani ni fisadi ndani ya nchi yetu maana ushahidi unaibuliwa kila kukicha na wananchi mbali mbali wenye mapenzi ya kweli na nchi yetu.
 
Wanafiki tu siku zile walisema Muungwana ni zawadi toka kwa Mungu, mimi nitakubaliana nao ikiwa yeye Muungwana atasafisha na kufanikisha kurudi kwa mamilioni yaliyotumika katika kampeni za uchaguzi.

Bubu ulisema kweli kuwa hawa jamaa ni wanafiki wakubwa, nakumbuka kabla ya uchaguzi wa kenya uliopita nilikutana na Padri mmoja Mtanzania lakini yupo Nairobi kama makazi yake ya kudumu, nilishangaa sana aliponiambia kuwa angependa Kibaki ashinde na nilipoendelea kumdadisi niligundua kuwa serikali ya Kenya wakati huo (Kibaki) ilikuwa na fungu la fedha lisilokuwa rasmi kwa makundi makubwa ya kidini ili wawapigie debe wakati wa uchaguzi, na yule Padri alikuwa ana wasiwasi kuwa endapo serikali itabadilika basi atakosa michuzi, sasa hebu angalia wanavyofanyiana wenyewe ndani ya kanisa, kwa mfano mkeo anaenda ungama kwa Padri kuwa kazini nje ya ndoa halafu Padri huyo baadaye anatumia maungamo yake ambayo ni weakness yake anamwomba na yeye kula vitu, kuna imani hapo?

Padri Privatus Karugendo Disemba 24, 2008

NIANZE kwa kuwatakia wasomaji Krismasi njema na Mwaka Mpya 2009 wenye mafanikio.

Wote watakaofanikiwa kusherehekea Krismasi ya mwaka huu na kupata bahati ya kuuanza Mwaka Mpya wa 2009, wana wajibu wa kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kuwaruhusu kuendelea kuishi.

Tunaishi na kuwapo kwa huruma na upendeleo wa Mwenyezi Mungu. La msingi ni kukumbuka kwamba tunaishi ili kutekeleza mpango wa Mwenyezi Mungu, wa kusimika ufalme wa Haki, Wema na Huruma duniani.

Katika makala iliyopita nilitoa ahadi ya kuiendeleza kwa kutoa mifano hai ili kuonyesha jinsi viongozi wetu wa dini na hasa wakatoliki, wanavyotutawala badala ya kutuongoza. Mtu anayeishi chuki, hawezi kukemea chuki, mtu anayeshindwa kutenda haki, wema na huruma, hawezi kuwakemea wanaoshindwa kama yeye.

Ni lazima mtu kutoa kibanizi ndani ya jicho lake ndipo atoe vibanzi kwenye macho ya wengine. Ni lazima kwanza viongozi wetu wa dini wajifunze kuongoza na kuonyesha njia, ndipo waingize ushawishi wao ndani ya jamii yetu. Wakikazania kutawala hawawezi kutoa mchango wowote!

Siandiki makala hii kutafuta haki, siandiki makala hii kumshitaki mtu yeyote, siandiki makala hii kutafuta kushinda ama kushindwa, siandiki makala hii kushindana na mtu yeyote yule.

Nijuavyo mimi, katika mfumo wa Kanisa Katoliki, mnyonge hawezi kupata haki wala kusikilizwa. Haki ni ya wakubwa: Maaskofu, Makardinali na Baba Mtakatifu. Hivyo kufikiri utamshinda Askofu, hata kama amekukosea ni ndoto. Ninaandika makala hii kuelezea ukweli. Nina imani kubwa kwamba ukweli hata ukipindishwa namna gani, kuna siku utajitokeza. Ukweli ni ukweli siku zote. Na hasa kama ukweli umeandikwa, inasaidia zaidi, maana kuna msemo: “Kilichoandikwa kimeandikwa!”.

Ninaandika makala hii kuwashawishi waumini, ili waanze kuwashinikiza viongozi wao, kuachana na utawala. Wajifunze kuongoza, wajifunze majadiliano, wajifunze kushirikisha, wajifunze kusikiliza na kutoa haki bila upendeleo, waache tabia ya uchu wa madaraka, waache tabia ya kupenda utukufu – wajifunze kutumikia, maana Bwana Yesu hakuja kutumikiwa bali kutumikia. Marekani na Ulaya wamefanikiwa kufanya hivyo na kuliweka Kanisa mikononi mwa waumini, kwanini sisi Afrika tusifanikiwe?

Lakini pia ninaandika makala hii kujibu maswali mengi ninayoulizwa kila siku. Ninapokea simu, ujumbe mfupi na barua pepe, watu wakitaka kujua kama kweli mimi ni padri wa Kanisa Katoliki au ni kujipachika tu kama wale wanaojiita madaktari bila kuisomea fani ya udaktari.

Nilipadrishwa Desemba 27, 1981parokiani Itahwa-Bukoba. Marehemu Askofu Christoher Mwoleka, ndiye aliyenipatia daraja la upadri, maana nilipadrishwa kulitumikia Jimbo Katoliki la Rulenge. Kati ya watu walioshuhudia upadrisho wangu ni (sasa) Askofu Severine NiweMugizi, wakati huo akiwa bado mwanafunzi. Wengine walioshuhudia upadrisho wangu ni waumini, mapadri wa Bukoba na Rulenge na Askofu Nestory Timanywa, wa Jimbo Katoliki la Bukoba.

Nilipadrishwa baada kumaliza masomo yote ya upadri, falsafa nilisomea Seminari ya Ntungamo, Bukoba (1975-1976) Rector wangu alikuwa Askofu Damian Kyaruzi, Askofu wa Jimbo Katoliki la Sumbawanga. Askofu Anthony Banzi, wa Jimbo Katoliki la Tanga, alikuwa mwalimu wangu pale Ntungamo. Teolojia, nilisomea Kipalapala Tabora (1977-1981). Rector wangu alikuwa Padre Alfons Ndekimo, wa Jimbo Katoliki la Moshi. Mwadhama Policap Kardinali Pengo, alinifundisha mwaka wa kwanza wa Teolojia. Askofu Agapitus Ndorobo, Askofu wa Mahenge, alikuwa mwaka mmoja mbele yangu. Askofu Thadeus Ruwaichi, Askofu wa Dodoma; Askofu Almachius Rweyongeza, Askofu wa Kayanga; tulikuwa darasa moja. Askofu Msonganzila, Askofu wa Musoma, alikuwa nyuma yangu miaka miwili. Mimi ni padri, sikujipachika upadri.

Nilisimamishwa huduma tangu mwaka 2000, baada ya kutumikia miaka 19. Kusimamishwa kwangu ni mfano mzuri wa wanavyotutawala badala ya kutuongoza. Askofu Severine NiweMugizi, aliwekwa wakfu kuwa Askofu wa Rulenge Februari 16, 1997. Tarehe hii ni muhimu sana kuelewa ninachotaka kuelezea.

Askofu Severini, akiwa bado padre na anafundisha Seminari Segerea, wakati wa likizo yake ya mwaka 1993, alilizunguka jimbo zima la Rulenge, akiwahoji mapadre kuhusu maisha yao kwa kile alichokiita yeye “Matatizo ya mapadre”.

Kama alikuwa ametumwa na TEC au na Balozi wa Baba Mtakatifu au kwa juhudi zake binafsi –haina maana yoyote kwangu. Ninalotaka kueleza ni kwamba alizunguka na kati ya watu aliowahoji mimi ni mmoja wao. Alinikuta Bushangaro-Karagwe, kwa vile nilishapata habari zake na kazi yake nilijiandaa vilivyo kumpokea.

Ushahidi wa maongezi yetu hayo - mimi na Padre Severini, wakati huo- haukanushiki kwa lolote lile. Ushahidi unatosha na ni mzito!!

Niliongea na Padre Severini na kujifunua kwa yote aliyotaka kuyajua juu yangu: maisha ya kiroho, misimamo yangu juu ya ukristo na teolojia na mambo mengi tu. Nilijifunua bila woga wowote maana yeye alikuwa rafiki yangu wa karibu sana. Katika kitabu ninachokiandika kuelezea tukio hili, nitaweka barua alizokuwa akiniandikia tulipokuwa marafiki. Baada ya maongezi yetu hayo ya Bushangaro, nilimwomba maongezi yetu tuyafanye maungamo. Niliungama kwake na akaniondolea!

Jambo la kusikitisha sana na kukatisha tamaa na kupunguza imani ni kwamba baada ya Askofu Severini, kupata daraja la Uaskofu wa Jimbo la Rulenge Februari 17, 1997, hata kabla ya miezi miwili kupita nilipata barua kali kutoka kwake ikiwa inataja pamoja na mambo mengine yale tuliyoongea pamoja siku za nyuma kule Bushangaro, wakati akizungukazunguka kuwahoji mapadre na maungamo yangu kwake.

Barua hiyo ya Machi 29, 1997, kumbukumbu 0037/27 yenye kichwa cha habari : KUTOKUAMINI UKRISTU. Akinitaka kuthibitisha au kukana mambo ambayo niliungama kwake mwaka 1993. Jambo hili sikulielewa kabisa na lilinivuruga na kupunguza imani yangu kwake. Niliijibu barua yake kwa unyenyekevu mkubwa. Yeye akajibisha tena kwa Onyo la kwanza nililolipata Aprili 18, 1997 - miezi miwili kamili baada ya Uaskofu wake!

Askofu wangu kwa vile ni mtawala aliamua kutumia maungamo yangu kuninyanyasa, kuharibu imani yangu na wito wangu.

Canon Law, inamzuia kiongozi wa Kanisa kufanya hivyo: Can.984:1 . “The confessor is wholly forbidden to use knowledge acquired in confession to the detriment of the penitent, even when all danger of disclosure is excluded.”

2. “A person who is in authority may not in any way, for the purpose of external governance, use knowledge about sins which has at any time come to him from the hearing of confession.” Unaweza kuangalia pia na Can 1388!!

Mimi ninasema alitumia maungamo yangu. Anaweza kukataa kwa kujitetea. Lakini hoja kubwa ni je, alifahamu vipi mwenendo wangu kwa muda wa mwezi mmoja akiwa ofisini? Sheria ya Kanisa inamzuia kiongozi kutumia “Previous knowledge” ya watu walio chini yake anapoingia madarakani.

Baada ya onyo hili la kwanza ambalo lilitokana na maungamo yangu, maonyo mengine yaliendelea kunyesha kama mvua. Yalikuwa yamepangwa vizuri, ili kila mwaka nipate onyo moja, ili apate msingi wa kunisimamisha huduma za upadri.

Onyo la pili ni kichekesho. Padre Emmanuel Mutabazi, kaka yangu, mwalimu wangu, msomi na mtaalamu wa Biblia, na leo hii bado anafundisha Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki kule Nairobi, aliingia chumbani mwangu pale Bushangaro, na kuiba kutoka chumbani kwangu kitabu nilichokuwa ninakisoma kwa wakati huo chenye jina : “Jesus The Man” kilichoandikwa na “Barbara Thiering”, na kukipeleka kwa Askofu, kunishitaki kwamba ninasoma vitabu vinavyopotosha. Mtaalamu wa biblia badala ya kunielekeza ananishitaki kwa Askofu, kwa kosa la kusoma kitabu.

Hivyo onyo la pili nililolipata Mei 7, 1998, kumbukumbu 0037/31, ni la kusoma kitabu cha “Jesus The Man”. Hii sheria ya kuwazuia watu kusoma vitabu inatumika wapi katika Kanisa Katoliki?!

Onyo la tatu nililipata kwa sababu ya kuchelewa Ujerumani. Nilikwenda Ujerumani kumwangalia Mzee Mwoleka, wakati anaumwa. Askofu Severini, anadai alinipatia ruhusa ya juma moja! Juma moja kwenda Ujerumani kumwona mgonjwa! Lakini hata kabla juma moja alilonipatia kumalizika alishaniandikia barua ya onyo kana kwamba alijua nitachelewa. Onyo liliandikwa Machi 29, 1999, kumbukumbu 0037/37 na kutumwa parokiani kwangu wakati ruhusa yangu ilikuwa inakwisha Aprili 4, 1999! Ushahidi upo maana maandishi hayafutiki.

Kama nilikosa kwa kuchelewa na kwa vile alikuwa anajua kwamba nilikwenda kumwona mgonjwa basi angenisubiri nilirudi nijieleze. Badala yake nilikuta barua ya onyo juu ya kitanda changu!

Kisa cha kusimamishwa huduma (suspension): Askofu Severini, aliniandikia hivi: “On the 13th of June 2000 you wrote to me just informing me about your plans to meet the doctors from the USA and a friend from Holland coming to visit you. It is a fact beyond doubt that for more than two months up to the day I passed by the parish premises on the 7th of August, you were out of your place of work without permission......

I am now suspending you from the priestly ministry for one year from the day you receive this decree..”

Hivyo suspension, kisa chake ni kuwapokea wageni na kuwa nje ya kituo kwa kipindi cha mwezi, ingawa yeye labda kwa kupitiwa anasema miezi miwili. Ushahidi upo na wageni waliokuwa wamenitembelea wapo na watanisaidia kulieleza hili vizuri .

Ukiangalia kosa na adhabu unaona kuwa hakuna uwiano. Nikumbushe kwamba maonyo yote matatu na suspension ni vitu nilivyopokea bila majadiliano wala kuzungumza na Askofu Severini. Hakunipatia nafasi ya kujieleza. Ni mambo ambayo inaonekana wazi alikuwa ameyapanga hata kabla ya kushika utawala wa Jimbo la Rulenge.

Hivyo nimekuwa kwenye suspension miaka kumi. Bila matunzo ya kimwili na kiroho kutoka kwa Askofu wangu. Nimenyimwa haki za msingi za binadamu:Chakula, malazi na matibabu, vitu ambavyo hata majambazi, magaidi wanapofungwa wanavipata.

Niliandika barua kwa rafiki yake mkubwa Mheshimiwa Askofu Methodius Kilaini, kulalamikia uonevu wa Askofu Severine, lakini sikupata jibu hadi leo hii. Niliandika barua tatu kwa Balozi wa Baba Mtakatifu Tanzania, kulalamikia uonevu wa Askofu wangu, lakini sikupata jibu. Niliandikia barua mbili kule Roma na kuhakikisha kwamba zimefika, lakini sikupata jibu lolote. Huu ni ushahidi wa kutosha kwamba ndani ya mfuno wa Kanisa Katoliki, wanyonge hawasikilizwi. Nimetoa mfano wangu, ili kulielezea vizuri hili, lakini mifano iko mingi sana, na nitaendelea kutoa mmoja baada ya mwingine.

Swali la kujiuliza ni je, kwanini mtu aliyekuwa rafiki wa karibu, anigeuke kiasi cha kutumia maungamo yangu kuninyanyasa na kuniharibia imani yangu na wito wangu? Haya ndiyo nitakayoyaeleza kwenye makala inayofuata. Lengo kubwa likiwa ni kuonyesha jinsi viongozi wetu wa dini wanavyotutawala badala ya kutuongoza.

Mgeni Rasmi ameandikwa ni Waziri Mkuu Edward Lowasa. Lowasa ni Waziri Mkuu Mstaafu. Waziri Mkuu ni Mizengo Pinda. I just need clarification mgeni rasmi alikuwa nani. Hii barua ya Padri Karugendo kali. Mimi ni Mkatoliki na naelewa Kanisa Katoliki linaendesha mambo yake kidiktator, kkwa amri na utekezaji tuu bila maswali. Na mimi ni mmoja wa wakatoliki wanaosoma sana vitabu vya criticism ya Ukatoliki lakini bado nipo na imani kali zaidi.

Niliwahi kufanya mahojiano na Askofu Kilaini kuhusu matumizi ya kondom kwa mwanandoa mkatoliki ambaye amegundua mwenzake ameathirika na yeye yuko salama. Askofu alijibu suala la Kondom ni no. Akasema ukigundua mwenzako ni muathirika huo ndio mwisho wenu kushiriki tendo hilo mpaka mwisho wa maisha yenu. Muishi kama Matowashi. Hivi hii ni haki kweli kwa Mkatoliki?. Sisi ni Wakatoliki ni lazima kupokea amri na kuzitekeleza bila kuuliza. Huu ndio utii na unyennyekevu kwa kanisa letu.
 
tatizo la viongozi wa kikatoliki ni vigeugeu haohao mafisadi wanakuwa wageni rasmi kwenye sherehe zao
 
Hii habari haikukaa sawa kabisa!...bila shaka sio ya jana wala juzi.
Kisha jamani naomba kuuliza. Hivi Askofu fulani akitoa mawazo yake ni lazima ichukuliwe kama ni Tamko la kanisa Katoliki1 au mimi ndio nachanganya misingi ya Uongozi wa kanisa!..
 
Mkandara mie na wewe ni wakristo lakini ukiangalia article ya Padri mwenzao Privatus hapo juu utagundua kuwa kuna ufisadi hata makanisani na ndio maana Lowassa alipokewa na askofu Laizer kwa mbwembwe kubwa kule monduli, ukiangalia kwa makini ukristo wetu na wa wenzetu wa ulaya kuna tofauti kubwa, hebu leo nenda mahali uwaambie nina katoto kachanga nataka kabatizwe uone utakavyozungushwa wee mara ulipe mchango wa kigango mwaka mzima, mchango wa Mapadri, michango ya mavuno na usishangae at the end ukaambiwa imeshindikana kwani hujafunga ndoa lakini hiyo inawezekana kwa siku chache kabisa kama una fedha, hivyo basi wao ni sawa na Nyani haoni kundule na si haki kuikoromea serikali
 
Mimi nafikri habari hii jamaa wenda hajaelezea mambo mengine.Yawezekana kabisa huyo askofu alimfanyia mtima nyongo kwa kumlima barua mfululizo ili atakapochukuliwa hatua ionekana kama hakuonewa.

Nabado siamini kama askofu anaweza pekee kumsimamisha bila kupata ruhusa maalumu kutoka kwa askofu mkuu na vatican.

Na kama sikosei huyu padri alishaanza makombora yake juu ya ukatoliki miaka mingi tu iliyopita hata kabla ya kusimamishwa na bado huyu nahisi anataka mambo yaende kwa kunegotiate mambo ya Imani.Nakubaliana naye kabisa kuwa Imani ni UDIKTETA maana kama hukubaliani na imani hiyo hakuna jinsi nyingine ya kusikiliza mawazo yako.

Mfano nikisema YESU ni MUNGU no way out ya kukusikiliza wala hakuna jinsi ya kusema vinginevyo.
Mfano nikisema QURAN ilitoka mbinguni Ndivyo hivyo ilivyo hakuna tena hoja ama mawazo yako mbadala ,Sana sana utakachosaidiwa kujuwa ni kukufundisha jinsi YESU alivyo MUNGU ama Jinsi QURAN ilivyoshuka kutoka mbinguni.Kama hukubaliani na hilo basi wewe si mwezetu hakuna jinsi nyingine ya kusikiliza mawazo yako tofauti na commands hizo kuwa YESU ni MUNGU ama QURAN ilitoka mbinguni.

Kwenye Imani ni Commands hakuna namna nyingine ya kukusikiliza mfano kama wanasema ili uwe padri hakuna kuoa na wewe unasema ahaa unajuwa mimi nina wito lakini bado nawakwa tamaa kwa mwanamke hivyo ninahitaji kuoa ,mawazo kama haya hakuna kunegotiate jibu ni moja tu.

Ila kama kweli alisimamishwa na Askofu kwa sababu alizozitoa mwenyewe hapo basi binafsi naona alionewa.
 
Kiongozi yoyote wa ngazi ya juu, iwe serikalini, chama ama taasisi fulani kauli yake inachukuliwa kuwa ndio msimamo wa taasisi hiyo vinginevyo taasisi husika itoe tamko rasmi ya kukana kilichosemwa na kupelekea kubaki kuwa ni tamko binafsi la muhusika.

Hii ni sawa sawa na ile issue ya personality na institution. Nilitolea mfano urais ni taasisi inayoongoozwa na rais.
Lakini huyo huyo rais anayeongoza taasisi ya urais ni binadamu at personal capacity kama binadamu wengine wote na ana utashi wa kutenda yale ya urais kama rais na ya kwake kama binadamu.

Tamko la Askofu ni la Kanisa Katoliki ila kama kanisa watalikana ndipo linakuwa la Askofu husika katika binafsi yake.
Makanisa sio wanafiki bali ni miradi kama ilivyo miradi mingine. Yanajitahidi kuchunga kondoo wa bwana ili wasipotee lakini wakati huo huo wanawaangalia kwa makini wale kondoo 'walionona' kwa sababu wataleta mavuno zaidi wakati wa mavuno.
Utaona wenye fedha wanakumbatiwa na makanisa yote hata ya wokovu hao mnaowaona wako safu za mbele na masuti ni wale kondoo walionona na wale waliokondeana wanasweka katikati ama nyuma ili wasionekane sana. Kuna mpaka wanaohubiri umasikini ni laana. Ukusoma noval ya God Father na vitabu vya mwandishi Malachi Martin utapata picha ya inside Vatican. Ni fedha za Mafia zimetumika kuendesha kanisa!.
 
Mkandara mie na wewe ni wakristo lakini ukiangalia article ya Padri mwenzao Privatus hapo juu utagundua kuwa kuna ufisadi hata makanisani na ndio maana Lowassa alipokewa na askofu Laizer kwa mbwembwe kubwa kule monduli, ukiangalia kwa makini ukristo wetu na wa wenzetu wa ulaya kuna tofauti kubwa, hebu leo nenda mahali uwaambie nina katoto kachanga nataka kabatizwe uone utakavyozungushwa wee mara ulipe mchango wa kigango mwaka mzima, mchango wa Mapadri, michango ya mavuno na usishangae at the end ukaambiwa imeshindikana kwani hujafunga ndoa lakini hiyo inawezekana kwa siku chache kabisa kama una fedha, hivyo basi wao ni sawa na Nyani haoni kundule na si haki kuikoromea serikali

Nchi za ulaya za wapi hizo mkuu? Kwa macho yangu tena juzi tu kuna bwanamdogo kafa kwa ajali ya gari yani gharama ya mazishi tu ilikuwa kama Laki tano padre alizodemand.

kufunga ndoa hapa padre anataka fedha,kubatiza tu mtoto lazima umlipe padre.Wewe unasema huko ulaya ulaya wapi?
 
Mimi nafikri habari hii jamaa wenda hajaelezea mambo mengine.Yawezekana kabisa huyo askofu alimfanyia mtima nyongo kwa kumlima barua mfululizo ili atakapochukuliwa hatua ionekana kama hakuonewa.

Nabado siamini kama askofu anaweza pekee kumsimamisha bila kupata ruhusa maalumu kutoka kwa askofu mkuu na vatican.

Na kama sikosei huyu padri alishaanza makombora yake juu ya ukatoliki miaka mingi tu iliyopita hata kabla ya kusimamishwa na bado huyu nahisi anataka mambo yaende kwa kunegotiate mambo ya Imani.Nakubaliana naye kabisa kuwa Imani ni UDIKTETA maana kama hukubaliani na imani hiyo hakuna jinsi nyingine ya kusikiliza mawazo yako.

Mfano nikisema YESU ni MUNGU no way out ya kukusikiliza wala hakuna jinsi ya kusema vinginevyo.
Mfano nikisema QURAN ilitoka mbinguni Ndivyo hivyo ilivyo hakuna tena hoja ama mawazo yako mbadala ,Sana sana utakachosaidiwa kujuwa ni kukufundisha jinsi YESU alivyo MUNGU ama Jinsi QURAN ilivyoshuka kutoka mbinguni.Kama hukubaliani na hilo basi wewe si mwezetu hakuna jinsi nyingine ya kusikiliza mawazo yako tofauti na commands hizo kuwa YESU ni MUNGU ama QURAN ilitoka mbinguni.

Kwenye Imani ni Commands hakuna namna nyingine ya kukusikiliza mfano kama wanasema ili uwe padri hakuna kuoa na wewe unasema ahaa unajuwa mimi nina wito lakini bado nawakwa tamaa kwa mwanamke hivyo ninahitaji kuoa ,mawazo kama haya hakuna kunegotiate jibu ni moja tu.

Ila kama kweli alisimamishwa na Askofu kwa sababu alizozitoa mwenyewe hapo basi binafsi naona alionewa.

MkamaP nakubaliana nawe kuwa huyu PK huenda alianza makombora yake angali ndani ya kanisa lakini ni uhalali upi uliofanywa kumsulubu kwa kutumia maungamo yake aliyotoa kwa Askofu? Hili linafanya tufikirie sana uadilifu wa viongozi wetu wa dini kama wana ethics na kazi zao, angalia ni wao waliotuambia kuwa JK ni chaguo la Mungu lakini leo hii watanzania wanalia na kusaga meno na wao wamekaa kimya, mimi naona hivi sasa tusiwaabudu sana hawa viongozi wa dini bali tusikilize neno la mungu kutoka midomoni mwao na linapokuja suala la kijamii tuwaone wao ni binaadamu na wana mapungufu kama mie, Issa, au Juma
 
Pasco,
Mkuu nimekusikia isipokuwa naomba zaidi ufahamisho toka kwa watu wengineo maanake nashindwa kuamini..Labda kwa sababu ya ukubwa wa Taasisi nzima ya Vatican kwani nashindwa kuona wazo la Askofu mmoja toka kitongoji kimoja kuwa ndio maamuzi ya Taasisi nzima. Kanisa moja la katoliki linaweza kuwa tofauti na kanisa jingine jirani yake tu ktk maamuzi ya kisiasa kwani hata hao maaskofu wana msimamo tofauti kuhusiana na viongozi wa Kitaifa...na wengine ni wanachama wa vyama pinzani, hapa nashindwa kuunganisha kabisa.
Kisha sidhani hata Vatican wanajua kinachoendelea Tanzania kuhusiana na Ufisadi.. Pengine Ndivyo Nilivyo!
 
Nchi za ulaya za wapi hizo mkuu? Kwa macho yangu tena juzi tu kuna bwanamdogo kafa kwa ajali ya gari yani gharama ya mazishi tu ilikuwa kama Laki tano padre alizodemand.

kufunga ndoa hapa padre anataka fedha,kubatiza tu mtoto lazima umlipe padre.Wewe unasema huko ulaya ulaya wapi?

Hapa lugha gongana?
 
Interesting article. Hivi vitu havipaswi kuwa hivi maana haya makanisa hayapo kwetu tu. Huu udikteta ni reflection ya udikteta katika mazingira mapana zaidi katika jamii yetu kuliko kanisa.
 
MkamaP nakubaliana nawe kuwa huyu PK huenda alianza makombora yake angali ndani ya kanisa lakini ni uhalali upi uliofanywa kumsulubu kwa kutumia maungamo yake aliyotoa kwa Askofu? Hili linafanya tufikirie sana uadilifu wa viongozi wetu wa dini kama wana ethics na kazi zao, angalia ni wao waliotuambia kuwa JK ni chaguo la Mungu lakini leo hii watanzania wanalia na kusaga meno na wao wamekaa kimya, mimi naona hivi sasa tusiwaabudu sana hawa viongozi wa dini bali tusikilize neno la mungu kutoka midomoni mwao na linapokuja suala la kijamii tuwaone wao ni binaadamu na wana mapungufu kama mie, Issa, au Juma

Mkuu
Hayo maneno ya Jk kuwekwa na Mungu sio maneno ya askofu wala kiongozi wa dini.
Ni maneno yanayopatikana moja kwa moja kutoka kwenye Biblia yani ya kwamba waheshimu viongozi wa serikali kwani wanatoka kwa Mungu.Na hata ukifuatilia majibishano ya Yesu na Pilato utaona Yesu anabainisha mamlaka aliyokuwa nayo pilato alipewa na Mungu.

Mkuu hatuheshimu Paroko,padre, ama nani tunachoheshimu ni imani lile ni fumbo la imani.
Huyu jamaa nakubaliana naye kama aliadhibiwa kwa hoja alizozitoa lakini nawasiwasi naye sana na maelezo yake pia ni vigumu kujuwa mkweli nani maana haya ni maelezo ya upande mmoja tu.
 
Hapa lugha gongana?

sio gongana mkuu hizi hoja zakuwa sisi tufanye kwa sababu watu wa ulaya wanafanye vile ni mwendelezo wa fikra mbaya.Na hata hivyo ulaya hawafanyi hivyo kama anavyosema labda atuambie nchi fulani inafanya hivi na sio ulaya kama ripota anavyo ripoti.
Kwana namna hiyohiyo kwa vile agrican ya marekani inaruhusu ushoga na sisi turuhusu ndoa za ushoga??
 
Back
Top Bottom