Mpita Njia
Platinum Member
- Mar 3, 2008
- 6,999
- 1,189
Wana kazi zao hao, achana nao, utapoteza muda wako bure
Ukiiunganisha dots utajua nini kinaendelea kwenye media za Tanzania.....wengi tuliisha soma magazeti yao ie majira, rai, Nipashe etc etc wacha tuwe addicted na JF habari za uhakika na sahihi
Mugasa
Ingekuwa wamesema ROstam anaenda kujisafisha kanisa mngepinga tu?mnaona vyama vingine ni vya kuvionea tu siyo?
CHADEMA is untouchable here always
Ingekuwa wamesema ROstam anaenda kujisafisha kanisa mngepinga tu?mnaona vyama vingine ni vya kuvionea tu siyo?
CHADEMA is untouchable here always
What do you mean?
Ushirombo just what I was telling!
JF kuna kila aina ya watu!Sijui ni uwezo wangu mdogo wa kuelewa ila sijaona ambapo tayari CHADEMA wametetewa!
Ingekuwa wamesema ROstam anaenda kujisafisha kanisa mngepinga tu?mnaona vyama vingine ni vya kuvionea tu siyo?
CHADEMA is untouchable here always
VIONGOZI wa dini za Kiislamu na Kikristo nchini wametoa ripoti ya safari yao waliyoifanya katika maeneo ya machimbo ya madini mkoani Mwanza na kuanika hadharani mambo mbali mbali, ikiwemo hali mbaya ya maisha inayowakabili wachimbaji wadogo katika migodi hiyo.
Wakizungumza katika uzinduzi wa ripoti na mkanda wa video wa safari yao kwenye hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam jana, viongozi hao walisema hali ya wakazi wa maeneo hayo inatisha na kusikitisha sana.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la African Evangalist, Grace Masalakulangwa alisema walishuhudia watu "wanapanga foleni katika vidimbwi vya maji machafu huku juu yao kunatoka tani nyingi za dhahabu".
Alisema watu wamekosa imani na kamati zinazoundwa na serikali hadi kufikia wanakataa kuongea na viongozi wa dini kwa madai kuwa wanaendeleza usanii wa serikali.
"Hali ni mbaya hadi mtu anathubutu kumwambia kiongozi wa dini kwamba usiwe msanii kama kamati zinazoundwa na serikali," alisema Grace.
Grace alisema walishuhudia watoto wa baadhi ya familia miongoni mwa familia 86 zilizohamishiwa katika nyumba ya iliyokuwa mahakama ambayo haitumiki tena wakitambaa katika maeneo machafu huku wazazi wao wakiwa hawana hata sehemu ya kujisaidia.
Alisema familia hizo zilihamisha na askari wenye silaha za moto kwa amri ya mkuu wa wilaya kutoka katika eneo alilopewa mwekezaji majira ya saa 9:00 usiku na kupelekwa hapo kwa madai wao hawapaswi kukalia eneo lenye madini.
"Mpaka leo nakosa amani na utulivu kichwani na akilini mwangu... labda kwa kuwa ni mwanamke, lakini wale akina mama hawana hata sehemu ya kufulia nguo," alisema Grace huku machozi yakimtoka.
Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Salum Fereji alisema kitu pekee kilichomsikitisha na kukishudia katika safari hiyo ni kule kushuhudia watoto waliotenganishwa na ukuta huku hali zao za maisha zikiwa tofauti.
Alifafanua kwamba akiwa ndani ya ukuta huo anakula mkate kutoka Afrika ya Kusini na kuogelea ndani ya mabwawa ya kutengeneza, huku aliye nje ya ukuta huo anakula mchanga na kukaa zaidi ya siku tano hajaoga.
Sheikh Fereji alisema walishuhudia watu wanaoishi katika maeneo ya madini wanahamishwa kila siku na amri za kuwahamisha watu hao zinatoka katika vinywa vya viongozi wa nchi.
"Wanaowambia kaeni pale ni viongozi na wanaowambia hamieni pale pia ni viongozi wetu," alisema Sheikh Fereji.
Naye Askofu Dk. Valentino Mokiwa kutoka Kanisa la Kianglikana Dayosisi ya Dar es Salaam alisema walishuhudia uwanja wa ndege ambao unaweza kutua ndege yoyote duniani.
Alieleza kwamba walipouliza waliambiwa kuwa ndege zinazotua humo zinaleta mikate kutoka Afrika ya Kusini ambayo haipatikani Tanzania na kuongeza kuwa kwa tafsiri yake ndege hizo haziwezi kurudi tupu bali zinarudi na madini ya dhahabu kwa sababu haziwezi kurudi tupu.
Alisema walihisi kuwepo kwa serikali katika migodi ya madini, lakini hakuiona kwa sababu hawakuona ofisi za Mamlaka ya Mapato (TRA) wala dola, licha ya kuwa kuna mali nyingi inayozalishwa maeneo hayo.
"Nilishangaa sana, kwani katika vibanda vya wamachinga vinaweza kupitiwa na maafisa wa TRA zaidi ya mara tatu kwa siku wakidai kodi mbalimbali kwa nini isiwe kwa wawekezaji," alihoji Dk Mokiwa.
Alisema nchi inaimba ujinga katikati ya utajiri wa madini na kuongeza kuwa serikali zinakuwa za kijinga kwa kumtoa kafara wa kwake na kumtukuza mzungu kutokana na kumpa ardhi na kumuacha Mtanzania akidhalilika.
Aidha alisema walishuhudia mashimo makubwa matupu ambapo alidai kuwa udongo wake wenye dhahabu husafirishwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi kwenda katika nchi za Japan na kwamba makontena hayasimamishwi hata sehemu moja yanaposafirishwa.
Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Suleiman Gorogosi alihoji aina ya mkate ambayo haipatikani Tanzania mpaka iagizwe kutoka Afrika ya Kusini na kuongeza kuwa huo ni ujanja tu lakini ndege hizo zinakuja zikichukuwa madini.
Naye Askofu Peter Kitula kutoka Kanisa la African Inland Church (AIC) aliisihi serikali na wabunge watumie nafasi yao waliyopewa na Mungu kuwachukulia hatua za haraka wawekezaji hao ikiwa ni pamoja na kusitishwa kwa mikataba yote halafu uchunguzi ufanyike juu ya matukio mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binaadam.
Akisoma mapendekezo hayo Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislaam Tanzania (BAKWATA) Sheikh Ali Mzee alisema wanaitaka serikali kushughulikia kesi zote na kumaliza mateso kwa waathirika wa migodi hiyo na kusimamia ulipwaji wa fidia na kupatiwa matibabu wote waliothirika katika kuhamishwa maeneo yao.
Mengine ni kuchunguza ukiukwaji wa haki za Binaadamu na kuwaadhibu wahusika na kuunda kamati huru ya kuchunguza upya tuhuma za mauaji ya makusudi ya watu 50 katika machimbo ya Bulianhulu na ripoti yake kuwasilishwa bungeni na kwa wananchi.
Pamoja na mapendekezo hao pia viongozi hao walizindua mkanda wa video unaonyesha mateso ya watu wa machimboni.
Kwa upande wake mtafiti na mwanasheria, Tundu Lissu alisema serikali inapaswa kusoma na kuelewa alama za nyakati na mabadiliko yake kwa kuwa inapofikia viongozi wa dini kufanya utafiti na kuzungumzia hali mbaya ya nchi mambo ni mabaya.
Viongozi wa dini nchini wamecharuka na kudai kuwa rasilimali ya madini haijainufaisha nchi kutokana na kuibwa na wawekezaji wa nje hivyo wameitaka serikali kuandaa upya mikataba ya uwekezaji yenye manufaa kwa taifa.
Hayo yamo katika ripoti ya Madini kwa Maisha ambayo imeandaliwa na viongozi wa dini waliokwenda kutafuta ukweli kwenye maeneo ya migodi waliyoizindua Dar es Salaam jana baada ya kutembelea migodi ya Geita, Nzega, Kahama na North Mara.
Viongozi walioandaa ripoti hiyo ni kutoka Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC), Jumuiya ya Kikristo (CCT) na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata). Wamesema katika ripoti hiyo kuwa wachimbaji wadogo wamezidi kuwa masikini baada ya wawekezaji kuingia.
Wamesema watawasilisha ripoti hiyo kwa viongozi wa serikali akiwamo Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Nishati na Madini, wabunge na kuihubiri misikitini na makanisani.
Tumeshuhudia kule migodini hakuna watu wa TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) lakini kuna viwanja vya ndege vinavyohamisha rasilimali yetu kila siku. Wawekezaji hawa wanalalamika kuwa wanapata hasara, huu ni uongo, alisema Askofu Valentino Mokiwa wa Kanisa la Anglikana.
Viongozi hao pia wamesema wananchi ambao wanaishi katika maeneo ambako kuna migodi wameachwa masikini huku wawekezaji wakiishi maisha ya kifahari kama wako Ulaya.
Walisema hata miradi inayojengwa na wawekezaji hao huko vijijini haifanani na thamani ya mabilioni ya fedha wanayovuna kwenye migodi hiyo. Kwenye ripoti hiyo pia viongozi wamesema wananchi wananyanyaswa na wawekezaji hasa suala la kuhamishwa hali inayowafanya wananchi wageuke kuwa kama watumwa au wakimbizi ndani ya nchi yao.
Walitoa mifano ya kaya 86 za Kijiji cha Mtakuja, wilayani Geita, zinazoishi kwenye jengo la mahakama baada ya kuhamishwa kwa nguvu hali inayowafanya wageuke kama wakimbizi. Pia walitoa mfano wa wakazi wa Katoma ambao nao wamehamishwa kwa nguvu na kulipwa fidia kidogo.
Mokiwa alisema walipotembelea jengo hilo ambalo limetelekezwa walikuta makazi ya watu 250 ambao wanaishi katika mazingira magumu huku wakiilaumu serikali kwa kuyafanya maisha yao kuwa magumu kiasi hicho.
Jamii nyingi zinazozunguka migodi zimeathirika hawana ardhi ya kulima na hawana mahali pa kuchimba madini wanaishi kwa kuombaomba, alisema Mokiwa. Katika ripoti hiyo viongozi hao wa dini wamependekeza kesi zilizoko mahakamani zilizofunguliwa na wananchi waliohamishwa zishughulikiwe haraka.
Kuhusu haki za binadamu, ripoti hiyo imejikita zaidi katika mgodi wa Bulyanhulu ambako wamekiri kupokea malalamiko ya watu ambao wanadai ndugu zao walifukiwa wakiwa hai hivyo kutaka kuundwa kwa kamati huru ya kuchunguza upya tuhuma hizo na ripoti yake iwasilishwe bungeni na kwa wananchi.
Viongozi hao walisema hali inayoonekana Geita na Nyamongo ni ya wananchi kuwa na hasira kwa kuichukia serikali kuwa ndio chanzo cha umasikini wao kutokana na kuwahamisha katika maeneo waliyokuwa wanachimba dhahabu na kuwapa wawekezaji. Hili ni bomu kuna siku lazima litalipuka, alisema Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Salum Fereji, wakati akizungumza kuhusu safari yao.