Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Mkandara mie na wewe ni wakristo lakini ukiangalia article ya Padri mwenzao Privatus hapo juu utagundua kuwa kuna ufisadi hata makanisani na ndio maana Lowassa alipokewa na askofu Laizer kwa mbwembwe kubwa kule monduli, ukiangalia kwa makini ukristo wetu na wa wenzetu wa ulaya kuna tofauti kubwa, hebu leo nenda mahali uwaambie nina katoto kachanga nataka kabatizwe uone utakavyozungushwa wee mara ulipe mchango wa kigango mwaka mzima, mchango wa Mapadri, michango ya mavuno na usishangae at the end ukaambiwa imeshindikana kwani hujafunga ndoa lakini hiyo inawezekana kwa siku chache kabisa kama una fedha, hivyo basi wao ni sawa na Nyani haoni kundule na si haki kuikoromea serikali

Naam umesema kweli tupu hata misikitini pia kuna ufisadi wa hali ya juu na udikteta. Katika maswala ya condom kujikinga na maradhi na pia kufuata uzazi wa majira mimi sikubaliani na kanisa au msikiti maana vyote hupinga matumizi ya condom. Halafu nashangaa hadi hii leo 2008 bado dini hizi mbili hazioni umuhimu wa kuwa na mapadri na masheikh wanawake. Hawana sababu yoyote ya muhimu inayowaunga mkono katika hili isipokuwa ni udikteta tu.
 
Vita dhidi ya Ufisadi: Maaskofu waonya

  • Kardinali Pengo: Taifa halina amani

Na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

VIONGOZI wa madhehebu ya Kikristo nchini, wameonya Watanzania kutoendelea kujidanganya kuwa nchi ina amani kutokana na kuibuka kwa matukio ya ufisadi na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (maalbino).

Viongozi hao wamesema matukio hayo yanadhihirisha kutokuwapo kwa amani na taifa kuingia katika hatari ya kugawanyika kutokana na matukio hayo.

Akitoa salamu za Sikukuu ya Krisimasi na mwaka mpya jana, katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, alisema kutokana na hali ilivyo nchini kwa sasa, imefanya kanisa lishtuke na kuamua kuandaa ibada maalumu ya maombi, kwa ajili ya kuliombea taifa amani.

Alisema ombi la Rais wa Baraza la Maaskofu (TEC), Askofu Yuda Thadei Ruwaich, kuliombea taifa, ili matukio hayo yaishe kwa amani, ni kuwaweka wananchi kuwa macho na matukio yanayoendelea kutokea.

“Tusiendelee kujidanganya kuwa bado Tanzania ni nchi ya amani wakati watu wanakufa kila siku. Tuondokane na hali inayoleta wasiwasi.

“Tumejisahahu, tumezoea kujiita kuwa tunaishi kwenye nchi ya amani hata tunaposikia kuwa kuna mauaji ya maalbino, vikongwe na ufisadi, hatushituki tunaona kuna utulivu, huo ni utulivu wa kujidanganya na kupotezana.

“Tujue kuwa hali yetu si salama, maaskofu wameamua kuwa na kauli moja na kuungana, ili kuweza kuwaepusha wananchi na hali inayoweza kutokea baadaye, watu wawe macho, waangalie namna ya kuzuia hali inayoendelea kutishia taifa letu,” alisema Kardinali Pengo.

Kardinali Pengo alisema matukio ya ufisadi na mauaji ya maalbino yanayotokana na imani za ushirikina ni dalili tosha kuwa kuna hatari ya kusababisha maafa makubwa kutokana na watu hao wanaoua kugeukia kundi jingine la watu na kuanza kuwaua.

Alisema kuna watu wanateseka hospitalini hawana dawa, lakini watu wachache wameachiwa nafasi na mwanya wa kutunisha mifuko kwa mabilioni ya pesa na kufanya watu wachache kuendelea kufurahia matunda ya nchi hii kiasi cha kuwafanya wengi kuiona dunia ni kama jehanamu.

Alisema wananchi wengi wanateseka hawana amani, lakini hakuna mtu mwenye huruma nao, kila mtu anataka kujikusanyia mali zaidi ili awe mbali, na maisha yake yazidi kuwa mazuri.

“Ukitaka kujua kuwa watu wamepoteza utu, ubinadamu na hata hakuna chembe ya nuru ya Mungu ndani mwao, unaona mtu mmoja anajikusanyia mali nyingi, mabilioni ya pesa peke yake wakati watu wengi maskini wanakufa kwa kukosa dawa katika hosipitali zetu, hii ndiyo Tanzania tuliyo nayo,” alisema.

Aidha, alisema hali inayoendelea kutokea nchini inasababishwa na ubinafsi wa kutaka kuwa na kila kitu mikononi mwa wachache huku mnyonge asiye na kosa wala hatia akitumika kama chambo cha kuwanufaisha wachache hao.

Alisisitiza kuwa watu wote walioko madarakani wanapaswa kuacha tabia ya kuthamini watu wanaowawezesha kupata mali, kwani wanapaswa kuwathamini fukara kwanza, kwani ndipo sauti ya Mungu ilipo.

Aidha, alisema hali inayoendelea ya mauaji ya maalbino nchini ni vita ya Watanzania wote na si ya kuwaachia maalbino wapigane peke yao.

“Kila mtu kwa nafasi yake anapaswa kuwa adui wa vitendo hivyo na serikali ikitia nguvu katika udhibiti na vyombo vya dola vikifanya kazi, ili kuokoa maisha ya watu hao,” alisema.

Alisema tabia ya kutumia ushirikina kujipatia fedha au utajiri imepitwa na wakati, hivyo watu wanapaswa kutumia akili zao, kwa kusoma, ili kupata maendeleo na si kutumia mbinu za kizamani zilizopitwa na wakati, ambazo zinaliletea taifa hili aibu.

“Mambo haya yalianza kwa kuwachuna ngozi watu, likasimama kwa muda, sasa wameanza kuua kundi la walemavu hawa, kesho albino wakiisha ni kundi gani litafuata? Hii ndiyo amani tunayojivunia? Tunapaswa kuamka haraka tutangaze mbinu za kupambana na matukio haya,” alisema Kardinali Pengo.

Pia alisema tabia ya watu kufikiri kutumia baadhi ya vitu ili kujipatia fedha au utajiri ilianza kuingia kanisani kwa watu hao kuiba sakramenti kanisani na kwenda kuzitumia au kuzipeleka migodini, ili wapate utajiri, lakini sasa umehamia kwenye uhai wa watu.

Mbali na hilo, Kardinali Pengo, alisema umefika wakati kwa Watanzania kuondokana na ujinga huo wa kukumbatia ushirikina mpaka kwenye karne hizi za maendeleo makubwa, na dawa pekee ni kupata elimu nzuri.

“Ili kuondokana na hilo, tuwekeze kwa nguvu kwenye elimu, tujenge shule nyingi watu wasome ujinga huu utaisha na kila mtu atastaharabika,” alisema.

Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa, amesema taifa linaelekea kugawanyika kutokana na mauaji ya maalbino.

Akihutubia katika Kanisa la Azania Front, Askofu Malasusa alisema mgawanyiko huo unaweza kuhatarisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa uliopo kama serikali haitachukua hatua za haraka dhidi ya wahusika wote.

“Wapendwa wakati leo (jana) tunaadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo… nawaambia kwamba taifa letu linaelekea kugawanyika vipande vipande kutokana na matukio ya mauaji, yakiwemo ya maalbino ambayo yanatokea sehemu mbalimbali za nchi yetu,” alisema.

Alisema kitendo cha watu wenye ulemavu kuuawa pasipo hatia kinapaswa kulaaniwa na waumini wa madhehebu yote bila ya kujali itikadi zao, ili kunusuru taifa kukumbwa na aibu kubwa.

“Wakati sisi tukikusanyika katika nyumba zetu na familia kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo… kuna wenzetu wenye ulemavu wa ngozi wao wanajiuliza wajijifiche wapi wasiuawe. Nawaambia maandiko matakatifu yanakataza unyama huu…fungueni maisha yenu kuwa sehemu ya mahubiri kila siku iendayo kwa Mungu,” alisema Askofu Malasusa.

Askofu Malasusa alisema maalbino wamekuwa wakiuawa kinyama kwa kichinjwa na kukatwa viungo katika sehemu mbalimbali za mwili na kuwafanya waishi maisha ya wasiwasi.

Alisema kama waumini watamgeukia Mungu, vitendo viovu havitakuwa na nafasi kama ilivyo sasa ambapo kila kukicha matukio mengi yamekuwa yakiripotiwa.

Aidha, Askofu Malasusa alisema hakuna jambo ambalo limekuwa likimnyima usingizi kama mauaji ya vikongwe yanayotokea katika mikoa ya Shinyanga na Mwanza.

“Sijui taifa letu linakwenda wapi, huko Shinyanga na Mwanza kumekuwa na mauaji ya vikongwe muda mrefu… hawa wanauawa kinyama pasipo hatia yoyote ile…. Hii ni changamoto ambayo inapaswa kuwagusa wote katika kuyakemea haya,” alisema.

Askofu huyo ambaye alitumia muda mwingi kuonya mauaji na kuwaasa waumini wake, alisema migogoro ya vita katika nchi mbalimbali na mapigano ya koo yanayotokea nchini ni dalili tosha ambayo nguvu ya Mungu inahitajika kwa ajili ya kunusuru hali hiyo.

“Wote tumekuwa mashuhuda, hivi sasa vitendo hivi vinatia aibu, mapigano ya koo katika sehemu mbalimbali za nchi yetu, mapigano katika nchi zingine zikiwemo jirani zetu zimekuwa na tatizo hili… umefika wakati wa kumgeukia Mungu, kuomba na kusali kwa bidii ili atuepushe na haya,” alisema Askofu Malasusa.

Aidha, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Augustine Shayo, amesema njia bora kwa vigogo wanaotuhumiwa kwa ufisadi nchini ni kutubu na kurejesha fedha za umma walizozichukua kutoka serikalini.

Akizungumza katika ibada ya mkesha wa Krismasi iliyofanyika katika Kanisa la Minara miwili, Shangani katikati ya Mji Mkongwe Zanzibar, askofu huyo alisema kurejeshwa kwa fedha hizo ni njia pekee ya kujisafisha wahusika kwa vile kutubu ndio njia muafaka kwa mafisadi na wala rushwa.

“Hawa wote Kristu anawaita na kuwapa matumaini ya kwamba amezaliwa kwa ajili yao na wanachopaswa kufanya ni kutubu na kurejesha mali hizo kwa manufaa ya wanyonge,” alisema.

Aidha, alisema imefika wakati shughuli za uongozi zisiendeshwe kwa usiri kwa vile ndiyo chanzo cha kukithiri kwa ufisadi nchini, ambao unawaathiri wananchi walio wengi hasa maskini.

Askofu huyo alisema inapokuwa viongozi wanawajibika kwa rais pekee na si wananchi, ni mwanzo wa watu kufanya wanayotaka, kwa vile rais hawezi kufahamu mambo yote yanayowakabili wananchi wake.

“Viongozi washughulikie wanyonge na wajifunze kujinyima kwa faida ya wengi,” alisema Askofu Shao.

Kauli ya askofu huyo ni ya kwanza kutolewa visiwani Zanzibar kuhusiana na masuala ya ufisadi yanayojitokeza katika serikali ya Jamhuri ya Muungano, hasa katika kipindi cha uongozi wa Awamu ya Tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa.

Hadi sasa viongozi watatu wa juu katika Serikali ya Awamu ya Tatu wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kutumia vibaya madaraka na kusababisha upotevu wa mabilioni ya shilingi.

Viongozi waliofikishwa mahakamani ni aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Aggrey Mgonja.

Wakati huo huo, Askofu Shao alisema tabia ya serikali kuwanyima mikopo wanayostahili wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini ni sawa na kufanya matayarisho ya kuiuza nchi kwa wageni.

Alisema taifa lolote linahitaji vijana wenye nguvu, ili liweze kudumisha uchumi wake kwa malengo ya kufanikisha mpango wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa wananchi wake.

“Suala la wanafunzi kudai mkopo wa kukidhi mahitaji yao ni haki, kwani kila serikali inayojali ni lazima ielimishe taifa lake kwa gharama yoyote na isipofanya hivyo ni matayarisho ya kuuza nchi kwa wageni,” alisema.

Alieleza kuwa serikali lazima ipime kwa umakini kwa kutofautisha maisha na kipato cha waziri, katibu mkuu wa wizara na kipato cha mkulima anayetumia jembe la mkono katika suala zima la kunufaika na mikopo ya elimu ya juu.

“Huwezi kulinganisha kipato cha waziri, katibu mkuu wa wizara fulani na mkulima kijijini anayetegemea jembe la mkono,” alisema askofu huyo.

Alisema kwa kuwa Krismasi ni mwanga kwa wananchi maskini walio wengi, basi ni wakati muafaka kwa wahusika kuangalia kwa makini suala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, ili kuwepo majadiliano kati ya mtoaji na mkopaji.

Aidha, Askofu wa Kanisa la Anglikana Mkunazini, mjini Zanzibar, John Ramadhan, alimsifu Rais Mstaafu Mkapa kuwa ni mtu aliyeheshimu haki za binadamu na uhuru wa mtu kuishi katika kipindi cha utawala wake.

Alisema Mkapa wakati wa uongozi wake pamoja na watu kupatikana na hatia za mauaji, lakini hakuthubutu kuidhinisha adhabu ya kifo na aliwaachiwa wahusika kuendelea kuishi.

Alisema pamoja na maamrisho ya dini kueleza anayeua naye auawe, na kutoa mfano wa jino kwa jino au jicho kwa jicho, lakini Mkapa aliendelea kuheshimu haki za binadamu juu ya suala zima la haki ya mtu kuishi.

Alieleza kuwa jamii inapaswa kuheshimu uhuru wa mtu na haki ya kuishi kwa vile hivi sasa mataifa mbalimbali yakiwemo ya Ulaya na Afrika yanapiga vita adhabu ya kifo.

Sifa za askofu huyo kwa Mkapa amezitoa huku baadhi ya wasomi na wanaharakati nchini wakitaka rais huyo mstaafu aondolewe kinga, ili aweze kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kutumia vibaya madaraka yake.

Wanasiasa wakongwe na wanasheria wamekuwa wakihoji sababu ya rais huyo mstaafu kutoshitakiwa, licha ya kuhusishwa na kashifa nzito ya mradi wa makaa ya mawe wa Kiwira, baada ya kutumia vibaya madaraka akiwa Ikulu.

Taarifa hii imeandaliwa na Kulwa Karedia na Deogratius Temba (Dar es Salaam) na Mwanne Mashugu (Zanzibar).
 
Tunaposema mafisadi wako humohumo makanisani kila siku wanawaona, wanachukua sadaka zao, wanakula nao, leo tunapoona matamko ya askofu mmoja kuwasema mafisadi wakati , wote kama kanisa hawajakaa chini na kue-valuate usafi wao inashangaza.

Anapotokea Nguri kama Privatus na kuandika nakala hii, hiyo siyo ndani ya ukatoliki ni makanisa mengi yao hivyo.

wanapowasema walokole wengi wametokea maanisa haya haya, walikosa kitu au waliona jambo wakaondoka kwa majina mengine mengi, lutheran n.k

Mtu unapokuwa ndani ya Katoliki na unaambiwa huwezi kuuliza swali , mtu mzima!!! msomi inashangaza.
Unapokuwa mkatoliki unaulizwa swali na unaishia kukasirika ni dalili ya udhaifu wa imani, na hawa wako wengi zaidi!

Kwa ujumla dini zetu hizi hapa Tanzania ni kuhakikisha kuwa tunajitahidi kupeleleza hata machimbuko ya dini zetu, tujue tumetoka wapi, mtu anapouliza imani zetu una uwezo wa kujibu.

Kuhusu katoliki , lazima we hivyo kanisa haliongozwi kwa mujibu wa biblia!, ila kwa mujib u wa katiba na hii siyo dini, wala ukristo, nao wanajiita wakristu!

Kama kuna kanisa linaloishi ambalo liko contrary na biblia ila liko kutimiza siasa basi ni katoliki, kila wanachofanya kinyume na biblia wao wana majibu ya mswali, na yote ni siasa tu.

kama kuna kanisa ambalo, lina criticism nyingi basi ni wakatoliki, na ndio maana wanayumba yumba, kutaka kumfurahisha kila mtu, sijui mpango wao wa kuungana na waislamu umeishia wapi?? interesting.

Haya niliyoyaandika hapa siyo kuwalaumu upande mmoja au wa pili, ishu ni kuwa imefika wakati wa sisi tunaojiita WAKRISTO KUKAA CHINI INTELECTUALLY NA KUJIULIZA TUNAISHI VIPI, MADHEHEBU SIYO YESU, YESU ANABAKI YESU HATA KAMA MADHEHEBU MTALETA SIASA

TUMFIKIRIE YESU, HIZI POLITICS, HAZISAIDII KUSIMAMIA UKWELI,
KARUGENDO,na wengine wote, siyo muda wa kulaumu dehebu fulani, ni muda wa kumwangalia Yesu kama Yesu na maandiko yake!

Hii kuwa mnywe pombe kidogo, ndiyo haya sasa, watu wanazini kidogo, ufisadi kidogo n.k, ndiyo maana SI AJABU KUMKUTA PADRE ANAFUNGISHA NDOA YA WATU WALIOISHA PEANA MIMBA KANISANI! kimungu huu ni UFISADI , ijapofikia kusimama na kuisema serikali , tuangalie hapa je tuko sahihi???

hii si kwa wakristo tu, hata dini zngine, tunapopigana misikitinikila siku na kugombaniana maiti, hii ni dalii ya jamii iliyoko gizani

Alama nzuri zaidi ya kidikteta ni mfano , unapomzaa mtoto, anafikisha mwezi mmoja unaenda kumbatiza, ni dalili ya udikteta mtoto anakuwa akijijua mkristo, kumbe hakuamnua toka ndani ya moyo wake, Biblia kwa kifupi(acha siasa) inaonyesha ubatizo ni kwa watu wazima, ''' mtu akiisha hubiriwa na akaamini, ndiyo abatizwe'' hii kulzaimisha vitoto vichanga , haiitaji degree tatu kujua kuwa ni ujinga, umbumbumbu, wa watu wasio kaa chni na wakafanya homewrok hata kutafakari kwa common sense. hawa akina John, na mary wenye majina mazuri ya kikristo ndio , machangudoa,mafisadi, wauaji,wezi n.k, kama kuna dini ambayo wangefuata mafundisho ya biblia na kuwa ingevutia wengine wengi duniani basi ni ukristo, kwa namna hii kwa nini watu wasiseme Katoliki ni mping kristo? I am apologetics I acn testfy this, siyo katoliki tu wote wanaondesha mafudisho kinyume na biblia ni mpinga kristo.

Athari za kulazimisha watoto kubatizwa, ni mbaya sana, kuliko maelezo, wengi wamekataa ukristo kwa sababu wale waliotakiwa kufanya mazuri, wanafanya mabaya, hawa wanaofanya mabaya hawajui dini, walibambikiziwa na wazazi wao tangu utotoni.

Tuna Taifa dhaifu kwa sababu tuna MAKANISA dhaifu, na kwa sababu viongozi wa makanisa wadhaifu, tuna viongozi wa kanisa dahifu kw sababu, tuna familia dhaifu, simply because we have weak parents.
Tusitegmee kiongozi wa nchi mzuri kutoka taasisi za dini dhaifu kama wakristo na waislamu Tanzania hivi sasa. Ndiyo maana huwa na wajoke waislamu kuwa mbona sioni waislamu wenye imani kali na kuishi kitakatifu, hizo mahakama za kadhi si zitawafukuza wengi kutoka uislamu??

Karugendo, nitakutumia article niliyoituma gazeti fulani mwaka, 2005 same story but different church!!!!!!!!

''Politics in church mbaya sana''

BIBLIA INASEMA

''NENO LITASIMAMA''

MERRY-XMASS
 
NA NASRA ABDALLAH

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maombi ya kuliombea taifa yanayotarajiwa kufanyika kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa kamati ya mandalizi ya mkutano huo, Askofu Godfrey Emmanuel, alieleza hayo jana katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO).

Alisema mbali na rais, pia watakuwapo mawaziri na manaibu waziri wao, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na wakuu wa wilaya zake tatu. Katika mkesha huo wa Mwaka Mpya, kutakuwa na dua maalumu kwa ajili ya kuliombea taifa. Dua hiyo itaanza saa 2 usiku hadi 12 asubuhi.

Kwa mujibu wa Askofu Emmanuel, mkutano huo umeandaliwa na makanisa mbalimbali na kuratibiwa na Kanisa la Tanzania Fellowship.

Akizungumzia mafanikio yaliyojitokeza tangu kuanzishwa kwa maombi hayo mwaka 1997, alisema wanaamini masuala ya ufisadi yanayojitokeza sasa hivi yametokana na maombi hayo.

“Kutokana na nguvu za giza ziliokuwa zimefunika macho ya watu kipindi cha hapo nyuma, sasa hivi nguvu hizo zinaonekana kutoweka na ndiyo maana tunaona masuala ya ufisadi yakiwa yanaibuliwa.

“Ieleweke kwamba serikali yenyewe haiwezi kufanya mambo yote isipokuwa na wananchi tunatakiwa tushiriki katika kuliombea taifa letu lisiangamie.

“Pamoja na kujua kuwa kila mtu kwa nafasi yake na imani yake inavyomtuma huwa anaomba, lakini tuliamua kutenga siku hii maalumu bila kujali itikadi za dini tulizo nazo. Tunashukuru Rais Kikwete amekuwa akituma salamu za kitu gani anataka taifa liombewe. Hii ni kutokana na kuthamini mchango wa maombi haya kwa taifa letu,” alisema askofu huyo.

Aliitaja mikoa mingine itakayofanya maombi hayo siku hiyo kuwa ni Mwanza (kiwanja cha CCM Kirumba), Arusha na Kilimanjaro (Uwanja wa Ushirika Moshi), Tanga (Uwanja wa Mkwakwani) na Tabora (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi).

CHANZO:- GAZETI LA TANZANIA DAIMA JUMANNE (DESEMBA 30, 200
 
Na hawa wapambe wa Rais wanafanya uchunguzi kabla ya kukubali mialiko kwa Mhe Rais? Suala la kuiombea nchi si baya lakini baada ya kusikiliza kauli za waandaaji ndipo pumba unapojitokeza. Kwa nini wanajibebesha mambo yasiyo yao kwani tangu 1997 hadi leo hayo wanayosema wamefanikiwa kuyafichua hawakuyasema wakati huo. Harakati za waandishi, wabunge na wananchi kwa ujumla sasa zinageuka kuwa hazina nafasi. Haya natuende kwani Muungwana ana tabia ya kuwapa madaraka watu wanaoonea huruma Taifa na hasa tukitilia maanani alishaanza kuwaona wa Kanisa (wanamaombezi)
 
Maaskofu Katoliki watoa tamko zito

  • Wasema ni jambo la hatari ukweli kupindwa

na Joseph Sabinus
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MAASKOFU 32 wa majimbo yote ya Kanisa Katoliki nchini, wametoa tamko la pamoja wakisema hali inayoendelea nchini, inawatia wasiwasi na kuwafanya wakose amani.

Miongoni mwa mambo waliyotaja kuwatia wasiwasi maaskofu hao ni pamoja na kuwapo kwa malumbano yasiyojenga taifa, vitendo vya kuwindana kwa hila za kisiasa na kasumba ya kupindisha ukweli kwa kupamba uovu kwa maelezo bandia.

Katika barua ya kichungaji yenye kurasa 13, maaskofu hao wakiwamo Rais wa Baraza la Maaskofu (TEC), Mhashamu Yuda Thadei Ruwa’Ichi pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, wamesema kashfa juu ya fedha, mikataba mibovu ya rasilimali za nchi na tume zilizoundwa kushughulikia masuala ya ufisadi, ni miongoni mwa mambo yanayowafanya wajiulize mengi kuhusu mustakabali wa nchi.

“Tumesoma juu ya tume zilizoundwa kushughulikia ufisadi. Wakati huo huo tunashuhudia watu wengi wanavyoteseka na kutaabika. Gharama za vyakula, matibabu na usafiri zinaendelea kupaa, ada za shule pamoja na huduma nyingine za kijamii zinakuwa ni mzigo mzito kwa Watanzania wengi,” imesema sehemu ya barua hiyo ya kichungaji ambayo Tanzania Daima ina nakala yake.

Wamesema yapo mambo mengi yanayowafanya kujisikia vibaya, likiwemo suala la baadhi ya viongozi kutotimiza wajibu.

Wameyataja baadhi ya matatizo hayo kuwa ni pamoja na kuwapo kwa mauaji ya watu wasio na hatia (maalbino na vikongwe), wizi, ujambazi, vitendo vya ufisadi, dhuluma na ukosefu wa uwajibikaji, hali inayosababisha watu kupoteza muda mwingi wakisubiri kupata huduma na haki zao na kutolea mfano wa mafao ya wazee na wastaafu, mishahara na malimbikizo.

“Watu wanabaki kutingisha mabega yao kuonyesha kukata tamaa, hawajui wafanye nini. Hii ni kasoro kubwa ya jamii yetu,” lilisema tamko hilo.

Walisema umefika wakati Watanzania wa kada zote wakiwamo viongozi, kuepuka kasumba ya kupindisha ukweli kwa kupamba uovu kwa maelezo bandia, huku wakificha ukweli au kutoa nusu ya ukweli.

Katika barua hiyo ya Janauri 4, mwaka huu iliyosambazwa nchi nzima, maaskofu hao wamesema: “Kuna mengi katika jamii yetu ambayo yanaonyesha kuwa hatujikubali, tunajikataa. Watu wanakataa kukiri makosa yao. Hayo tunayaona katika uwanja wa siasa, katika jumuiya zetu na katika biashara na utawala,” walisema.

Wametaka viongozi na watu wengine, wasiwawakie hasira watu wanapowakosoa kuhusu mienendo mibovu kwa kufikiri kuwa watu hao wanataka kuharibu sifa zao.

“Ni lazima tuhimize ukosoaji mzuri na hata ulio hasi katika jamii yetu. Kupima dhamiri yetu ni kuona mazuri na yale yaliyo hasi,” walisisitiza.

Maaskofu hao waliendelea kusema ni hatari watu kukosa imani kwa viongozi wao, kwani madhara yake ni makubwa kwa jamii.

“Matukio tofauti na kashfa zinazohusu baadhi ya watu wanaoshikilia nafasi za juu za uongozi yameyumbisha watu. Kugundua kwamba mambo haya yalipangwa, na kuwekewa mpango na kujulikana kwa watu wengi, ni jambo linalotisha,” wamesema.

Wakaongeza: “Kushughulikia haya kwa njia ya kuunda tume haitoshi. Hili ni suala la kimaadili ambalo linatupa mwaliko na kuangalia mienendo na fikra zetu za msingi.”

Makuhani hao wamesema kiburi, hasira, kujikataa, kusafisha maovu kwa siri ni kama kuyaficha, hali ambayo wamesema, ni njia angamizi ya kushughulikia matatizo na migogoro.

Mambo hayo wamesema, ni dhambi inayoua, kwani ni sumu inayotishia amani na maelewano katika nchi.

Wamesema viongozi wana wajibu mbele ya Mungu, kwani wao ni chumvi ya dunia na nuru ya ulimwengu, na kuhoji, baadhi ya viongozi wa Tanzania wanamtumikia nani?

Viongozi hao wa juu wa kanisa hilo, walisema katika barua hiyo kuwa hali ilivyo nchini ni mbaya kiasi kwamba watu maskini wanataabika kupata matibabu na elimu ya sekondari au zaidi kwa watoto, kwa kuwa hawamudu ada na gharama nyingine za maisha.

“Kinachotokea sasa ni kujenga na kudumisha mgawanyo wa matabaka katika jamii yetu; hakuna tena usawa kwa wote. Jamii yetu sasa si familia moja ambamo wote wanaangaliwa. Badala yake, tunatengeneza machungu mengi kwa wale ambao hawana fursa ya kunufaika na maendeleo ya kiuchumi yaliyofikiwa na nchi yetu,” walisema.

Kuhusu tatizo la rushwa, viongozi hao wa Kanisa Katoliki walisema wahusika wote wafikishwe mahakamani bila kuingiliwa na matakwa au masilahi ya kisiasa na kibiashara.

“Kinachohitajika sasa ni hatua za kurekebisha kwa kuwapeleka watu wanaohusika na rushwa katika asasi za kurekebisha kufuata vyombo vya sheria.

Haya yafanyike bila kuingiliwa kati na matakwa ya kisiasa, kibinafsi wala kibiashara,” wanasema maaskofu hao.

Kuhusu vyama vya siasa, viongozi hao walisema ni kosa kwa vyama hivyo kutokuwa na uwiano katika uwezo na nguvu, mali na kiwango cha kuenea nchini.

“Kunahitajika hatua za haraka sana kuangalia kasoro hii na kuishughulikia kabla ya Uchaguzi Mkuu wa kisiasa ujao,” wamesema na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa Ripoti ya Kamati ya Kufuatilia Mwenendo wa Uchaguzi Mkuu wa 2005 (TEMCO), katika Uchaguzi Mkuu uliopita, kulikuwa na ukosefu wa uwiano miongoni mwa vyama.

“Hili ni suala la kushughulikiwa na baraza linalojitegemea linaloundwa na viongozi wenye hekima, ambao wako juu ya vyama vya kisiasa. Msajili wa vyama vya kisiasa ameshaongea sana kuhusu suala hili, na inafaa naye asikilizwe,” walisema maaskofu hao ambao wamekuwa na rekodi ya kutoa matamko kila yanapotokea masuala makubwa kitaifa kila wakati.

Wameasa jamii na vyombo husika kuhakikisha kuwa malumbano yasiyojenga taifa hayaruhusiwi na kwamba, vitendo vya kuwindana kwa hila za kisiasa vikomeshwe.

Kanisa Katoliki nchini lina majimbo 31 chini ya maaskofu 32, kutokana na Jimbo Kuu la Dar es Salaam kuwa na maaskofu wawili, yaani Kardinali Pengo, ambaye ni Askofu Mkuu na msaidizi wake, Mhashamu Method Kilaini.
 
Wameasa jamii na vyombo husika kuhakikisha kuwa malumbano yasiyojenga taifa hayaruhusiwi na kwamba, vitendo vya kuwindana kwa hila za kisiasa vikomeshwe.
size]​
​

Vitendo vya kuwindana vikomeshwe? Ni vitendo vipi hivyo? Je kuna mifano yaweza kutolewa? Kuna Askofu yeyote aliyekuwemo kwenye hicho kikao atufafanulie jamani.Mimi naona hili tamko kama rubbish.

Nadhani si sahihi kwa watu wazito kama maaskofu kuongea vitu kwa mafumbo wanapoongea na wananchi pamoja na usomi wao inabidi waongee kwa lugha inayoeleweka kwa watu isiyokuwa na chembe ya uoga uliojificha nyuma ya porojo za kidini.

Mimi hili tamko silielewi kabisa au walikuwa wanapeana wenyewe kwa wenyewe? Kama lilikuwa linatolewa kwa serikali au wananchi naona ujumbe haujafika bado hatuelewi wamesema nini na walimaanisha nini.

Tanzania watu wanalalamika wanasiasa wakiongea hawaeleweki wanasema nini na sasa hata maaskofu na majoho yao hawaeleweki wanasema nini.Hivi nchi hii wasomi wakiwemo maaskofu hawa wa Katoliki wanahitaji Speech therapist wa kuwasaidia?​
 
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

​

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail:
ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz

​
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

ASKOFU Method Kilaini wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Kanisa Katoliki Tanzania amesifia mpango wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini, akisema kuwa mpango huo wa Tanzania hauna mfano kabisa katika nchi za eneo la Afrika Mashariki na kati.

Askofu huyo msaidizi wa jimbo hilo pia amepongeza uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sekta ya elimu, akisisitiza kuwa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma utabakia katika historia kama ishara na mfano wa pekee wa uongozi wa Rais Kikwete katika kujali na kuthamini elimu.

Aidha, askofu huyo amesisitiza kuwa maisha bora yanawezekana kabisa kwa Tanzania, ili mradi kila Mtanzania afanye kazi kwa bidii na nidhamu.

Askofu Kilaini ameyasema hayo leo, Jumamosi, Februari 14, 2009, kwenye sherehe za mahafali ya kwanza ya Chuo cha Uhandisi ya Teknolojia cha Mt. Joseph kilichoko Luguruni, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Chuo hicho kinamilikiwa na Kanisa Katoliki.

Akizungumza kwenye mafahali hayo ambako wanafunzi 45 wametunukiwa stashahada za uhandisi katika masomo mbalimbali na wengine 80 wametunukiwa shahada za uhandisi, Askofu Kilaini ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Utendaji la Chuo hicho amemwambia Rais Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo:

“Mpango wa Serikali yako kuchangia elimu kwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, Mhe. Mtukutu Rais, hauna mfano katika Afrika Mashariki na Kati. Kweli bado Bodi inayohusika inahitaji kuboresha taratibu za kutoa mikopo hiyo, lakini huu ni mpango mzuri sana.”

Kuhusu mchango wa Rais Kikwete katika sekta ya elimu, Askofu Kilaini amesema: “Hakuna shaka kuwa wewe ni Rais wa Elimu. Kile chuo kikubwa sana pale Dodoma, kitabakia ni ishara kuu ya uongozi wako katika elimu katika historia ya nchi yetu.”

Kuhusu maisha bora, Askofu Kilaini ametumia mafanikio ya kikundi cha akinamama kinachoungwa mkono na Chuo hicho ambacho kimejipatia mafanikio makubwa ya kipato kwa kushirikiana tu na kufanya kazi kwa bidii.

“Mheshimiwa Rais, nakubaliana na wewe na naamini fika kuwa Maisha Bora kwa Kila Mtanzania Yanawezekana, ili mradi tu kila mtu afanye kazi kwa nidhamu, kwa bidii, kwa jududi na maarifa, na kwa kushirikiana kama walivyofanya akinamama hao.”

Akizungumza kwenye mafahali hayo, Rais Kikwete amesisitiza kuwa Serikali yake itaendelea kuunga mkono kwa uwezeshaji wa kila aina vikundi vya Watanzania ambao wanaamua kuendesha shughuli za kuboresha maisha yao kwa pamoja.

Rais amesisitiza hilo baada ya kuwa ameambiwa kuwa mafanikio ya kikundi hicho cha akinamama yamechangiwa, miongoni na juhudi nyingine, na kiasi cha sh milioni 800 kutoka Serikalini.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Padre Dk. Arul Raj OMI amewataka wahitimu kubakia nchini na kusaidia kupanua nafasi za kazi na wala wasivutiwe na kishawishi cha kukimbilia nje ya nchi kutafuta kazi.

“Kaeni katika nchi hii iliyowasomesheni. Saidieni kutengeneza nafasi zaidi za kazi kwa sababu nyie ni wasomi wenye ujuzi. Msijiruhusu kushiriki katika shughuli ya kuhamisha bongo kutoka hapa kwenda nchi zilizoendelea. Msikimbilie nchi nyingine na badala yake saidieni nchi yenu katika maendeleo,” amesema padre huyo na kutoa ombi kwa Serikali.

“Tunashukuru kuwa wanafunzi wetu wote wa shahada wanapewa mikopo na Serikali. Tunaomba wakati nyenzo zikiruhusu tuanze pia kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaosomea stashahada. Ili kuendelea kuunga mkono vizuri wahandisi na kusukuma mbele maendeleo ya taifa, wahitimu wa stashahada ni muhimu sana. Hawa ndio watendaji kwenye mashine na teknolojia nyingine, wenye shahada ni mameneja.”

Ombi hilo pia lilitolewa na wazungumzaji wengine kwenye mahafali hayo, akiwamo Askofu Kilaini. Rais Kikwete baada ya kuwa amesikia maombi hayo auambia umati kwenye sherehe hiyo kuwa amesikia ombi hilo. “Sisemi nalikubali, wala sisemi nalikataa. Tupeni nafasi tutafakari.”

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano na Habari ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

14 Februari, 2009
 
"Mkuu wa Shirika la Masista la Mbeya, Immaculate Mirambo, alielezea kukosekana kwa uwiano wa matumizi ya rasilimali za taifa baina ya wazawa na wageni kuwa ni sehemu ya ufisadi unaolalamikiwa na jamii.

"Mimi siyo mtaalam, nazungumza kama mtu wa kawaida kwamba kwa nini kusiwe na uwiano wa matumizi ya rasilimali za nchi kati ya wazawa na wageni?" alihoji.

Alisema kwa muda mrefu serikali imekuwa ikizuia matumizi ya baadhi ya rasilimali kwa wazawa na kuruhusu rasilimali hizo zitumike na wageni jambo ambalo limesababisha umaskini kwa mwananchi wa kawaida."

Hapa Sister Immaculate ame hit the nail on the head. Malalamiko yote haya ya wananchi kuhusu madini, kiini chake ni nchi yetu kuliwa na wageni wakati sisi tunaangalia tu kama wajinga. Baya zaidi wanatumia na nguvu zetu katika kuzila mali zetu kwa kututumikisha katika migodi yao kwa mishahara duni.
 
Kero ya ufisadi yatawala Pasaka

WENGINE WAKEMEA UFISADI

Salma Said, Zanzibar

MAASKOFU wa Katoliki wametumia mahubiri yao ya siku kuu ya Pasaka kuzungumzia tatizo la ufisadi, mmoja akitaka watu wenye utajiri wasibatizwe majina hayo kabla ya kuhukumiwa na vyombo vya sheria na mwingine akitaka watuhumiwa wabadilike.

Wakati askofu wa jimbo la Njombe, Mhashamu Alfred Malunda akiwataka viongozi na watendaji wanaotajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi kubadili tabia zao ili kuliwezesha taifa kupata maendeleo ya kweli, askofu wa jimbo la Zanzibar, Mhashamu Augustine Shao alikemea vitendo vya baadhi ya watu kuwaita matajiri kuwa ni mafisadi hata kabla ya mahakama kuwapata na hatia.

Akihubiri katika misa ya mkesha wa Pasaka iliyofanyika kwenye Kanisa la Katoliki la Minara Miwili liliopo Mji Mkongwe mkoani Mjini Magharibi, Askofu Shao alisema:

"Ndugu waumini, kwa miaka hii ya karibuni kumezuka kitu kinachowaita wenye mali wezi na mafisadi. Kama kweli tunapenda kuendeleza ukweli aliofunua Kristu katika ufufuko wake, hatuna haki kuwaita wenye mali au matajiri kuwa ni wezi au mafisadi mpaka watakapohukumiwa na sheria kwamba kweli ni wezi na mafisadi kwa mapana yake," alisema Askofu Shao.

Alisema iwapo waumini hao wanaamini kwamba kifo na ufufuko wa Kristu ni matumaini, mwanga na upendo kwa wale wanaohisiwa kuwa wabaya, basi kuna kila sababu kuwa sauti na chombo cha matumaini kwa wanaodhulumiwa.

Kauli hiyo ya Askofu Shao imekuja wakati wanasiasa wakinyoosheana vidole wakituhumiana kwa ufisadi. Tuhuma hizo zimefikiwa kiwango ambacho wanasiasa wamerushiana maneno machafu hadharani kila mmoja akimtuhumu mwenzake kuwa anataka kumchafua.

Alisema kwamba kusema hayo hana maana kwamba wizi na udanganyifu ni kitu kizuri, lakini anapenda kuwafundisha namna ya kuishi kwa ukweli. Alisema kutenda haki ni jukumu la kila mwanadamu na dini zote zinafundisha juu ya heshima kwa utu wa mtu na mali au uwezo wa mtu.

Askofu huyo aliwaambia waumini wa kanisa hilo kwamba wakumbuke kinachopingwa takriban na dini zote ni njia mbovu za kujipatia mali na kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakifanya hivyo bila ya kujali maadili ya dini zao.

Alisema suala la rushwa nchini kwa sasa limekuwa kama kitu cha kawaida kwa kuwa halikemewi kiasi cha kutosha. Aliongeza kuwa tangu rushwa ilipotambuliwa kama kero, hakuna ushahidi kuonyesha watu wengi wamehukumiwa kwa kosa hilo, hali ambayo ingeonyesha kuwa rushwa ni kosa.

"Katika mazungumzo ya kawaida utamsikia mzazi akitetea kabisa ningependa mwanangu aajiriwe na Mamlaka ya Mapato (TRA), Wizara ya Fedha, Bandari, Polisi Trafiki na katika siku za karibuni wazazi wanataka watoto waajiriwe mahakamani au wawe madaktari," alisema.

"Ni vizuri kutamani kazi lakini matamanio haya si ya kutaka kazi bali ni kupata mahali pa kunyanyasa wengine kwa kupokea rushwa."

Naye Geofrey Nyang'oro anaripoti kuwa, Askofu Malunda amewataka viongozi na watendaji wanaotajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi kubadili tabia zao ili kuliwezesha taifa kupata maendeleo ya kweli.

Akizungumza kwenye sherehe za siku kuu ya Pasaka ambazo kitaifa zilifanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, jimbo la Njombe mkoani Iringa na kutangazwa moja kwa moja na TBC1, Askofu Malunda alisema kumekuwa na taarifa za viongozi na watendaji wengi wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kwamba hadi sasa zipo kesi zinazoendelea mahakamani.

"Vyombo vya habari vimejitahidi kutoa taarifa za kweli hadi hapo tulipofikia. Tuna haki ya kuvipongeza. Hata hivyo vyombo hivyo vinapaswa kutambua kuwa jamii inahitaji kujua ukweli kuhusu nchi yao, kama kiongozi ni fisadi atajwe kuwa ni fisadi, hii itakuwa njia pekee ya kuwataka wabadilike," alisema Askofu Malunda.

Malunda pia aliwataka wananchi kuacha tabia ya kukata tamaa kwani licha ya matatizo yanayolikabili bara la Afrika, bado kuna dalili za matumaini.

Alisema hata ziara ya Baba Mtakatifu Papa Benedikit wa XVI barani Afrika hivi karibuni, alisisitiza hilo la kuwataka Waafrika kuacha kukata tamaa kutokana na serikali za nchi hizo kutoonyesha matumaini.

Alisema suala la kukata tamaa limekuwa likiwakumba vijana ambao mara nyingi wamekuwa wakilalamika kukosa ajira na kuwataka vijana kutumia fursa zilizopo katika kukabiliana na matatizo yaliyopo.

Siku kuu ya Pasaka hutafsiriwa kama ushindi kwa waumini wa dini ya Kikristo dhidi ya mauti na kwamba kwa kifo na ufufuko wa Yesu Kristu umeiokoa dunia katika giza la dhambi na mauti.

Kutoka Serengeti, Anthony Mayunga anaripoti kuwa, Padri Aloysius Magabe ametaka kundi la mafisadi wanaolitafuna taifa hili na wale wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi (maalbino) wanahitaji kuombewa kwa kuwa wako katika mikono ya shetani na ni jukumu la Wakristo wote kubadilika na amani itawale nchini kote.

Akihubiri katika misa iliyofanyika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Fransisco wa Asizi mjini Mugumu wilayani Serengeti, Padri Magabe alisema kutokana na ufisadi amani na haki vinapotea.

Alisema kuwa kristo alipofufuka aliwaambia wanafunzi wake amani iwe kwao kwa maana na haki pia, lakini kutokana na tamaa za watu wachache, mafisadi wamefikia hatua ya kupora haki za watu na kuwaacha wanyonge wanajitafuna.

"Mafisadi na wauaji wa maalbino wanahitaji maombi ili wabadilike maana vitendo wanavyovifanya vinapingana na ujumbe wa Yesu. Hawa hata kufungwa hawatakiwi, bali tuwaombee wabadilike maana wanawatesa watu kwa vitendo na tamaa zao," alisema Magabe.

Akizungumzia wauaji wa maalbino alisema kuwa hao wamekuwa kama vipofu kwa kuwa wanadanganywa na waganga kuwa wakiua wenzao watakuwa matajiri. Upofu huo unahitaji kuondolewa kwa maombi kwa kuwa hawaoni roho zao zimetekwa na shetani.

Aliwataka waumini kushirikiana kukomesha vitendo vyote vinavyopora haki za wengine kwa kuwa chanzo cha watu kuumizana, kutafunana wao kwa wao ni matokeo ya kutotendewa haki.

NAFIKIRI IPO HAJA YA KUJADILI KAULI ZOTE MBILI ZA VIONGOZI WETU WA DINI. Nahisi kuna kasense fulani kwa mahubiri yao.
 
Kero ya ufisadi yatawala Pasaka

Paroko wa Parokia ya Maria Mtakasifu,Kimara jijini Dar es Salaam, Padri Fransis akiwasha mshumaa ikiwa ni ishara ya mwanga wa Yesu Kristo kabla ya kuanza kwa misa ya mkesha wa pasaka juzi

Kwa upande wangu wahubiri wote wamesema kitu kizuri. Shida ni kwamba wanasiasa wetu wameshajijengea 'immunity' kiasi kwamba mahubiri au ushauri wowote ule mzuri hauna maana kwao. Ni kama wamevaa 'bullet proof' au 'water proof' kwa chochote kinachosemwa.

Wangekuwa wanajifunza na kutaka kurekebisha namna yao ya utendaji, wangefanya hivyo kabla Mwalimu Nyerere hajafa. Mwalimu alijitahidi sana kuwaasa lakini hakuna aliyeufanyia kazi ushauri wake. Sasa je, viongozi wa dini wataweza kwa vile wanasiasa wetu hata wakienda nyumba za ibada huwa mioyo yao iko mbali?
 
Nilikuwa nasoma kijarida cha mwanakijiji hivi juzi kuna mahali aliandika kwa kusema hapa namnukuu moja kati ya makundi ndani ya CCM ni(Kundi ambalo limejikita katika sera za ubepari na wao neno ujamaa ni kinyaa kwao. Hawa wana nguvu moja kubwa nayo ni pesa. Wana uwezo wa kushawishi mtu yeyote wa makundi yale mawili ya mwanzo na wakiamua kutishia maslahi ya mtu huyo (aidha bungeni au vinginevyo) kundi hilo haliwezi kusita kufanya hivyo. Ni kundi ambalo kwa watu wengine tunaweza kusema ndilo lililoiteka nchi! )hapa binafsi naugana nae tumeshuhudia mara kwa mara watu wa aina hiyo kukimbilia nyumba za ibada. ukisoma maelezo ya maskofu hao utapatwa na hisia zitakazo kufanya kuamini hawa ni miongoni mwa wale rubuniwa kipesa au kimawazo, jinsi walivyo simama kidete kuwatete direct or indirect .kwa tarifa zenu ndugu wote hapa tusije tukashangaa siku moja kuona baadhi ya viongozi wa nyumba za ibada wakatowa kauli kama zile zinazotolewa na baadhi ya nchi za magharibi zinazowatete mashoga kuwa viongozi ndani ya majumba ya ibada na kusema madhali anamtumika mungu basi likubalike au kulifanya jambo hilo ni sehemu ya maisha yetu ,kusema hivyo inatoka na kile nilichokiita kubuniwa kwao kimawazo au kifedha, tuwe macho sio kila wanachokisema wao binafsi tukubaliano nao, hayo ni mawazo yao wenywe lakini jee ndani ya dini wanazozitumikia zinaamrisha nini inapofikia maswala kama hayo?
 
Wakati askofu wa jimbo la Njombe, Mhashamu Alfred Malunda akiwataka viongozi na watendaji wanaotajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi kubadili tabia zao ili kuliwezesha taifa kupata maendeleo ya kweli, askofu wa jimbo la Zanzibar, Mhashamu Augustine Shao alikemea vitendo vya baadhi ya watu kuwaita matajiri kuwa ni mafisadi hata kabla ya mahakama kuwapata na hatia.

Akihubiri katika misa ya mkesha wa Pasaka iliyofanyika kwenye Kanisa la Katoliki la Minara Miwili liliopo Mji Mkongwe mkoani Mjini Magharibi, Askofu Shao alisema:

"Ndugu waumini, kwa miaka hii ya karibuni kumezuka kitu kinachowaita wenye mali wezi na mafisadi. Kama kweli tunapenda kuendeleza ukweli aliofunua Kristu katika ufufuko wake, hatuna haki kuwaita wenye mali au matajiri kuwa ni wezi au mafisadi mpaka watakapohukumiwa na sheria kwamba kweli ni wezi na mafisadi kwa mapana yake," alisema Askofu Shao.

Malunda afadhali amesema ni "Viongozi na watendaji" Shao kasema ni "Matajiri" na kwamba wasiitwe mafisadi hadi hapo waakapohukumiwa na sheria,sasa mimi najiuliza,kama matajiri hao ni wanasiasa,je ni sheria gani hizo zitzkazotumika dhidi ya wanasiasa/matajiri/mafisadi/wezi hao?

Waumini waelewe kabisa kuwa hao viongozi wao si Miungu,waende kusikiliza neno la Mungu na mengine watumie akili zao wenyewe walizopewa na Mungu kufanya maamuzi....Kama mpango wa Mungu ni kulifikisha Taifa letu hapa lilipo,then ni kivipi maaskofu hao wako right? Wanaposema hao matajiri wanaoitwa mafisadi siyo mafisadi,kwanini wasitoe mfano halisi?

Kiufupi ni kwamba Shao anaamini kwamba, kwasababu hakuna mafisadi(zaidi ya kina Mramba na Liyumba) waliofikishwa mahakamani, basi hakuna mafisadi na wananchi wanyamaze...Suala ambalo haliwezekani kwasababu mwananchi atamuhisi nani kuwa ni mwizi na fisadi zaidi ya wale wanaosimamia mali na shuguli za Taifa?
 
Mahakama zenyewe za Bongo, zimejaa na kunuka rushwa. Mafisadi wanaweza kutumia pochi zao za kifisadi na kuonekana hawana hatia na hivyo kuachiwa huru. Juzi juzi tuliona yule fisadi wa BoT Liyumba alivyopewa dhamana pamoja na kutotimiza masharti ya dhamana ile. Hawa nao maaskofu na mapadri wakati mwingine kauli zao zinakatisha tamaa katika vita dhidi ya mafisadi. Sasa watu kama Chenge, Idrissa Rashid, Mkapa, Rostam, Yona na wengineo wengi tunahitaji kweli uamuzi wa mahakama ili kujua kama hawa ni mafisadi!? Mbona kuna ushahidi wa kutosha tu dhidi ya tuhuma zao!? Wakati mwingine Maaskofu na Masheikh ni bora mkae kimya kuliko kutoa kauli za kutaka kuwatetea mafisadi.
 
BAK,Hivi unafikiri ni kwanini mapinduzi hutokea? Ni kwasababu watu huwa wanaujuwa ukweli lakini hawana pa kukimbilia. Sio siri mkuu,kama wananchi wakigunduwa kuwa mafisadi wako kila mahali na kwamba hakuna msaada kutoka kwa viongozi wowote wale wa kijamii,viongozi ambao wameshindwa kuwaelewa wananchi na pia wameshindwa kusoma alama za nyakati,viongozi wenye kufikiri mambo ni yale yale na kwamba jamii hubaki vile vile na kwamba pia jamii huamini yale yale...Ni vyema wakatofautisha mambo ya dini vs siasa, mambo ya dini ndo kama hivyo,ni imani bayana ya mambo yasiyoonekana,ikija kwenye issue za ufisadi kwani wao hawaoni ufukuara na ufujaji wa mali za wabongo? Nadhani wanatumia nafasi yao kuzidi kuwafukarisha watanzania,wao ni viungo muhimu sana kwenye jamii kati ya watawala na wananchi,kwani wako nao karibu,ila hatua wanazochukua ama kauli wanazotowa zinalenga kuwadumaza wananchi kwani wengi wao uheshimu maneno ya viongoiz hao wa dini....Na hivyo wanaposema wananchi wasihoji ina maana kuwa ndiyo ukristo bora huo? Hata Jesus Christ mwenyewe ugomvi wake ulikuwa ni dhidi ya watawala wala rushwa,sasa hawa wanataka kutueleza nini? Ni lini walishakemea basi huo ufisadi ili tujue kama wanajali? Inakera sana.
 
Si kusudi langu kuwatetea mafisadi lakini nachukulia mahubiri ya Padri Shao kwa upana zaidi. Tayari tunao matajiri ambao tuna ushahidi wa vitendo vyao vya kifisadi lakini pia tuna matajiri ambao bado hatujapata ushahidi wa kuhusika na ufisadi. Hawa wa kundi la pili ni wale ambao wanapata baraka na mahubiri ya Padri Shayo.
Tumeshashuhudia harakati za kuwatisha na kuwarudisha nyuma baadhi ya Matajiri kwa kutumia hichi kigezo cha Ufisadi. Tukubali kuwa matajiri wana sehemu yake katika maendeleo ya Taifa na kuwakosa kunasababisha ukosefu wa muhimili mmoja wa maendeleo. Natujifunze na kipindi cha utawala wa Nyerere alipofanya utajiri kuwa ni adui kwa maendeleo ya Taifa. Hata tukikaa pamoja uwezo wetu wa kiakili na harakati za maendeleo si sawa na hapo ndipo panapotokea wale wanaowahi katika maendeleo na kuwazidi wenzao. Uhusiano wa makundi mawili haya hauepukiki na ili uwe mzuri lazima tuheshimiane.
Tuna mtizamo mbaya na hili neno ufisadi. Wengi wetu tunaamini kuwa ufisadi hufanywa na matajiri tu na kusahau kuwa ufisadi mkubwa hufanywa nasi watu wa matabaka ya chini. Hebu tufikirie masaa mangapi ya kazi huwa hatutekelezi kazi zetu na kupata vipato visivyo halali. Ni kiasi gani mwananchi wa kawaida tunavyoharibu miundo mbinu kwa kutofuata masharti ya mazingira? Ni kiasi gani wizi mdogo mdogo unaofanyika maofisini na sehemu nyengine za huduma? Ni mambo mengi tu ya kifisadi huwa tunayafanya na kwa vile tabaka letu ni wengi na tuyafanyayo ni ya kuendelea ni wazi kuwa gharama tunayoisababishia Taifa ni kubwa mno.
Baada ya kuangalia hayo ndipo ninapoona kuwa ule uhubiri wa Askofu wa pili unapochukua nafasi yake. Lazima mafisadi sote tubadilike na kuacha ufisadi na kuamuwa kuendeleza Taifa. Hili la kujaribu kujinufaisha nafsi zetu ndio linaloleta matatizo kwani sisi tuliochini pengine tunafisadi kwa kutapia roho lakini wakubwa wanafisadi kwa Uroho, wanavyo lakini hawatosheki na kila mmoja anaangalia wa juu yake badala ya kuangalia wa chini. Wangeliangalia wa chini wangeona kuwa hali za watu wao ni mbaya.
 
Mahakama zenyewe za Bongo, zimejaa na kunuka rushwa. Mafisadi wanaweza kutumia pochi zao za kifisadi na kuonekana hawana hatia na hivyo kuachiwa huru. Juzi juzi tuliona yule fisadi wa BoT Liyumba alivyopewa dhamana pamoja na kutotimiza masharti ya dhamana ile. Hawa nao maaskofu na mapadri wakati mwingine kauli zao zinakatisha tamaa katika vita dhidi ya mafisadi. Sasa watu kama Chenge, Idrissa Rashid, Mkapa, Rostam, Yona na wengineo wengi tunahitaji kweli uamuzi wa mahakama ili kujua kama hawa ni mafisadi!? Mbona kuna ushahidi wa kutosha tu dhidi ya tuhuma zao!? Wakati mwingine Maaskofu na Masheikh ni bora mkae kimya kuliko kutoa kauli za kutaka kuwatetea mafisadi.

......ah kaka mi ndio maana nimeona nijinyamazie tuu nisichangie hoja hii
 
Haya ndiyo maombi ya Kadinali Pengo wakati akizindua kitabu cha mama Lowasa nyumbani kwa Mh. Lowasa:

"Mungu Baba Mwenyezi wewe ni mpaji wa mema yote. Paji hilo ni zuri lakini kwa bahati mbaya sisi wanadamu badala ya kukushukuru paji hilo kulipokea kwa mikono miwili, tukamtendea mwanao kama tulivyomtendea, na bado wewe, kuonyesha kwamba bado unataka kutuokoa na kutufikisha mahali pa heri, ulimfufua mwanao kutoka wafu, yeye ambaye tulikuwa tumemuua. Naomba msamaha kwa utovu huo wa maadili.
Naomba mwanga wa ufufuko wa mwanao, uangaze zaidi ndani mioyo yetu, kusudi wale wote tunamheshimu Yesu tuweze kuuambia ulimwengu kwamba nyuma yetu ndiyo msingi wa hali bora katika maisha.
Tunakushukuru pia kwa kutukusanya jioni ya leo, kwa lengo maalumu mwanao anatenda kazi ndani ya wanadamu kwa njia mbalimbali., na mojawapo ni huu mwanga ambao anaweza kuwapa watu wakaweza kuwaelekeza wenzao mahali anapopatikana huyu mwanao.
Tunakuomba ubariki jumuiya hii, ubariki kila kilicho chema tutakachokifanya. Tunaomba hayo yote kwa njia ya Kristu Bwana wetu, Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina".

(Rai Nguvu ya Hoja)
 
Back
Top Bottom