Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

i can't believe this is actually happening in the land of Nyerere! I've always suspected kwamba kuna great inequality huko kwenye machimbo lakini kusoma repoti na maelezo ya viongozi wa dini - inaleta a new perspective in this whole issue.

Sasa tujiulize ni kwanini Ken Sarowiwa alianzisha machafuko kule Nigeria? Ni kwa nini akina Castro walifanikiwa katika vita yao dhidi ya Baptista? Ni kwa sababu tabaka la viongozi (akina Kiwete, Makamba et al) wanalimbuka na madaraka na kujiona kama miungu na kuamua kuwanyanyasa wananchi wenzao, tena wale wanaowapigia kura kuwapa madaraka, na kuwasujudia wazungu huku wakiwapa hao wazungu kila kitu wanachotaka. Huu ni zaidi ya ukoloni mamboleo aliouzungumzia Nyerere, huu ni utumwa wa kiakili on the part of our politicians. Inatia hasira kichizi.
 
Ile ripoti ya kamati aliyounda Rais kuangalia mikataba ya madini imeishia wapi licha ya kamati kutumia mamilioni ya shilingi za walipa kodi. Ina maana rais alifanya hivyo makusudi kuzima moto wa Buzwagi uliokuwa umewashwa na Mh. Zitto?. Mbona baada ya kujumuishwa kwenye hiyo kamati hatumsikii Zitto akiongelea tena mambo ya madini?. Kwa nini Mh. Rais baada ya kukabidhiwa ile ripoti alimrushia Mh. Ngeleja bila kuangalia japo mapendekezo yaliyokuwemo kwenye hiyo ripoti?. Mh. Rais alikuwa na nia ya dhati ama ilikuwa ni ile staili ya "funika kombe mwendawazimu apite"!!!. Tumeshuhudia kamati/tume nyingi lakini ripoti zake hatujui zilikoishia pengine karatasi zake zilishafungia maandazi na vitumbua mitaani, Mungu saidia labda kupitia kwa watumishi wako pengine mamlaka ambazo hazijali maisha ya wananchi wake zitaweza kuongoka na kusikiliza maoni na ushauri wao.
 
Date::10/22/2008
Viongozi wa dini waonya nchi inaelekaa pabaya
*Washauri Rais apunguze safari za nje

Na Waandishi Wetu
Mwananchi

VIONGOZI wa dini wamesema kukithiri kwa migomo, maandamano, vitendo vya kikatili, na migogoro kati ya serikali na watumishi wa umma ni ishara tosha kwamba, mambo hayako sawa nchini.

Wakizungumza na Mwananchi nyakati tofauti jana, viongozi hao walisema hali hiyo inaipeleka nchi pabaya na kuitaka serikali kutafuta suluhisho la matatizo hayo haraka iwezekanavyo.

Walisema kuwa kinachotokea sasa ni matokeo ya ahadi zisizotekelezeka na kwamba njia pekee ni kuyashughulikia madai hayo ya wananchi.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Kanisa la Katoliki jijini Dar es Salaam, Mhashamu Methodius Kilaini alisema, iwapo hali hiyo haitashughulikiwa mapema itasababisha hali kuwa mbaya zaidi nchini.

Kauli hiyo imeungwa mkono na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ramadhan Sanze aliyesema kuwa, ili kuondoa mitafaruku iliyopo nchini serikali lazima iwe tayari kuwajibika kwa jamii kisheria, kisiasa.

Aliishauri serikali kuyashirikisha makundi mbalimbali ya kijamii na kisiasa katika kupanga na kubuni sera mbalimbali kiutawala na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Sanze alimwomba Rais Jakaya Kikwete kupunguza safari za nje na hasa Marekani, akidai kuwa nchi hiyo si marafiki wazuri kwa ustawi wa taifa la Tanzania.

“Sidhani kama rais safari hizi za Marekani anapanga mwenyewe au anapangiwa, kama anapangiwa basi itifaki hii sio nzuri, hivyo tunamwomba apunguze safari za huko,” alisema Sheikh Sanze.

Alifafanua kuwa, ni vema kwa sasa rais akabakia nchini kuwatumikia Watanzania na kutuliza mitafaruku iliyopo badala ya kusafiri safiri tu huku nchi ikiwa inateketea kwa kuzongwa na migogoro ya kijamii.

Sheikh Sanze alionya kuwa, ikiwa hali itaendelea kama ilivyo sasa bila hatua madhubuti kuchukuliwa, basi kwa mara ya kwanza historia inaweza kubadilika kwa kuwa na rais wa kipindi kimoja.

Awali, Askofu Kilaini alisema ingawa tatizo la migomo linaonekana kuwa ni la miaka mingi, lakini ishara ya sasa inatia mashaka kwani serikali imekuwa ikitoa ahadi nyingi kwa wananchi na mambo machache tu ndiyo yanatekelezwa

“Hatuwezi tukasema kuwa mambo haya yanayoendelea kujiri ni ishara ya kukua kwa demokrasia, bali inatubidi tufahamu kuwa, serikali isipotekeleza ahadi zake kwa wananchi tutaendelea kushuhudia vitendo hivi kila mara.

Alisema uchumi wa dunia unapotikiswa, nchi zinazoendela ndizo zinazoathirika zaidi, hivyo ni vema serikali kupitia wizara zake ikatafuta mbinu zaidi za kuhakikisha kuwa suala la mfumuko wa bei unadhibitiwa ili mwananchi wa kawaida aweze kumudu maisha.

Alisema watu wanapochoka, na kukata tamaa na serikali yao, hutafuta njia nyingine kujinasua na matatizo yanayowakabili.

“ Ukizingatia kuwa suala la maandamano au migomo ni haki za msingi za wafanyakazi, hivyo kama serikali inataka kupunguza masuala haya ni vema ikabeba gharama na siyo kukwepa,” alisema Askofu Kilaini na kuongeza:

“Ninawaomba wananchi wenzangu watafute madai yao kwa kufanya mazungumzo na si kushiriki kwenye vurugu na migomo na pia serikali inapaswa kuwajibika kwa ahadi zake na si kuwayumbisha Watanzania.”

Hata hivyo, Askofu Kilaini alipoulizwa kwamba alishawahi kutamka kuwa Rais Jakaya Kikwete ni chaguo la Mungu na hivi sasa ana maoni gani, alisema kuwa kiongozi yeyote anayechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi ni chaguo la Mungu.

“Ni vema nikaeleweka kuwa maandiko ya Mungu yanasema uongozi na mamlaka yote hutoka kwa Mungu, hivyo basi rais aliyechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi wenyewe ndilo chaguo la Mungu na sisi tutaendelea kuwa na msimamo huo,” alisema Askofu Kilaini.

Alisema pamoja na kwamba Rais Kikwete ni chaguo la Mungu, anahitaji kusaidiwa katika kutekeleza sera na kutimiza ahadi zote zilizoahidiwa katika serikali yake, kwa sababu viongozi wengine wakimwachia na kushughulikia zaidi maisha yao binafsi, hakuna jambo litakalotekelezeka.

Aliwataka mawaziri na watendaji wengine serikalini wakawa mstari wa mbele kumshauri Rais mambo mema na si kumpotosha ili aweze kutekeleza.

Naye Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Salum Fereji na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Padri Charles Kitima walisema jana kwenye semina ya waandishi wa habari toka mikoa mbalimbali nchini inaendelea katika Hoteli ya Isamo mkoani hapa kuwa sera na sheria na madini vimetungwa kwa masilahi ya watu wachache walafi ambao wanajali masilahi yao na hivyo lazima vibadilishwe sambamba na mikataba yote ambayo makampuni ya wawekezaji yameingia katika uchimbaji wa madini hapa nchini.

Sheikh Ferej alisema ni lazima serikali kuamka kwa kuwa sasa nchi inaelekea pabaya kutokana na rasilimali muhimu kama madini kuachiwa watu toka nje ya nchi kuwaacha Watanzania kuendelea kuisha katika umaskini uliotopea.

"Ndugu zangu, sisi kama viongozi wa dini tulitembelea maeneo ya migodi yote, kule hali ni mbaya Watanzania wanaishi maisha ya dhiki, wamefukuzwa katika maeneo yao na watu toka nje ya nchi ndio wananufaika na madini haya kwa kupeleka kwao," alisema Sheikh Fereji.

Alisema wao kama viongozi wa dini wamebaini serikali imefanya makosa katika kuingia mikataba na wawekezaji toka nje ya nchi kwa sababu Watanzania hawanufaiki na madini hayo ambayo miaka michache ijayo yatakuwa yamekwisha na kuacha mashimo.

Naye Padri Kitima alisema bila serikali kufanyika marekebisho sheria na sera za madini Tanzania itaendelea kuwa maskini na siku zijazo yanaweza kukatokea mapigano kama ilivyo katika nchi nyingine barani Afrika ambapo kulikuwa na madini.

Alisema mikataba mingi ya wawekezaji ni mibaya na inatakiwa irekebishwe, lakini inavyoonekana hakuna wa kubadilisha hadi vyombo vya habari na wananchi washikamane na kudai mikataba hiyo ivunjwe au kurekebishwa.

Padri Kitima alisema katika mazingira ya sasa angependa yafanyike mabadiliko makubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kabla ya mwaka 2010 na kuwa na kundi la wafuasi wa Nyerere ambao watatetea rasilimali za nchi hii.

"Mimi binafsi kwa hali ilivyo ningependa CCM igawanyike najua kuna watu wazuri ndani ya CCM, lakini wanashindwa kuifanya nchi hii kuwa mikononi mwa Watanzania badala yake kundi la watu wabinafsi ndilo lina nguvu na hata katika kambi ya upinzani kuna matatizo makubwa ya ubinafsi na kuwepo viongozi wasio na sifa," alisema Padri Kitima.

Alisema nchi imepoteza agenda muhimu alizoziacha hayati Mwalimu Julius Nyerere alipounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sasa ubinafsi umetawala hadi kutishia kuvunja Muungano.

Habari hii imeandaliwa na Salim Said, Peter Edson na Mussa Juma
 
Wenye macho hawahitaji kuambiwa tazama. Viongozi wa dini hawakutaka tu kuwaambia CCM kuwa mchawi wao ni Kikwete. CCM wakiachana na JK na siasa zake za kulindana na kupendeleana, nchi inaweza ikawa na serikali ya kuwajibika na kuiepusha na mabalaa.

Please, Please CCM or Bunge, get rid of JK sooner than 2010 to rescue the country from self destruction.

Viongozi wa dini waonya nchi inaelekaa pabaya
*Washauri Rais apunguze safari za nje

Na Waandishi Wetu, Mwananchi

Topic zote zinazohusiana na makemeo, ushauri n.k kwenda/kutoka kwa viongozi wa dini tumeziunganisha. Natumaini mtu akisoma kuanzia mwanzo akafuata mtiririko atagundua mengi waliyokwisha yagusia.

Ahsanteni
 
INASIKIKITISHA kuona kuwa viongozi wa dini wanaweza wakaipinda na kuitafsiri visivyo katiba ya Jamhuri ya Muungano kwa lengo la kutaka kuwanyima watu Watanzania wengine haki zao za msingi.

Viongozi hao wajue kwamba sio wao tu wanaosma theolojia, saikolojia, falsafa, lojiki na argumentation. Kuna vijana wa Kitanzania tena wa dini zote ambao ni moto wa kuotea mbali kwa hilo.

Viongozi kama hawa tayari wameanza kushabihiana na wale wa Burundi na Rwanda ambao baadhi yao [huku Waislamu wahutu wakihifadhi watutsi] wao yaani viongozi wa dini hizo walikuwa wakiwadanganya watu na kuwakusanya katika makanisa yao na kisha kuwasakazia wauaji!

Janja hii ya nyani kwa kifupi haitawafikisha mbali. Viongozi wa dini muogopeni Mwenyezi Mungu na mtambue hakauna dini ambayo siku zote itakuwa juu ya mwenzake na apendapo Manani basi wa chini huja juu tena kwa ulaini tu-! Shikeni lenu, la wenzenu waachieni wenyewe. Na msimsakazie nyau mtu mzima na akili zake hatoogopa katu.

Penda msipende, uamuzi utakuwa ni kuwapa haki yao wale wanaodai haki yao tena kwa njia za amani. Na sio kwa namna mnayotaka nyie eti muwaone wakigombana kwanza na serikali na Watanzania wengine mpate justification ya hilo mnalolificha!

Pengine wanaojidai walikuwa wakimya ndio wazungumzaji wakubwa wa wakati wetu. Huenda mechi ilikuwa ikichezwa kirafiki lakini sasa inatakiwa rafu itawale. Na yapo mengi tu ya kufichua kwa sababu upande wa pili haujaonesha kabisa nia ya kutaka kuonesha upendo, uwazi, ukweli na haki kwa wote! Tuanze na yale yhnayotokea kule Rombo, Kilimanjaro ambayo tumeyafumbia macho kwa muda hivi sasa . Hili litawashtua wakajua tunajua mengi wasiojua hata wao wenyewe!
 
Huyo Askofu Kilaini asikwepe swali, hayo ya kusema JK ni chaguo la Mungu kama sikosei alilisema kabla Kikwete hajachaguliwa kuwa Rais wa nchi!

Bora sisi wengine tulikaa kimya, hatuhudhuria hata mkutano mmoja wa hadhara, wala kushabikia ushabiki usio na kichwa wala miguu. Sana sana nilikuwa nahoji kwamba hayo maisha bora kwa kila Mtanzania yatatokana na nini? Je atatumia rasilimari za ziada kutoka wapi ili alete hayo maisha bora kwa kila Mtanzania?

Hivi mnajua kwamba Makamba alipewa u Katibu Mkuu wa chama kwa kuwa tu ndiye aliyetunga ile kauli mbiu ya Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya!!!!? Kalaghabaho!!
 
Kanisa Katoliki sasa latishituka

Waandishi Wetu Disemba 10, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

  • Askofu Kilaini asema nchi inahitaji maombi isiangamie

KUYUMBA kwa mshikamano wa kitaifa kutokana na kuibuka kwa mgawanyiko katika jamii, ufisadi na mauaji ya watu wasio na hatia ni miongoni mwa mambo yaliyolishitua Kanisa Katoliki nchini na sasa limeamua kufanya ibada maalumu nchi nzima kumuomba Mungu ainusuru nchi isizidi kuangamia, imefahamika.

Tayari waraka maalumu umekwisha kusambazwa na kuanza kufanyiwa kazi nchi nzima na waumini wote wa kanisa hilo kubwa lenye waumini wengi kuliko madhehebu mengine ya Kikristo nchini.

Hali ilivyo sasa imeelezwa kulitikisa Taifa katika nyanja mbalimbali na kutishia mustakabali wa amani na utulivu uliodumu kwa miaka 47 tokea kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika. Jana Jumanne Tanganyika ilikuwa inaadhimisha miaka 47 tangu ipate Uhuru Desemba 9, 1961.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini ameliambia Raia Mwema wiki hii kwamba silaha kuu ya Kanisa ni ibada kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mwenye uwezo wa kuwaongoza binadamu kuhimili majaribu yanayowakabili.

“Kwa kweli tunaipongeza Serikali kwa hatua inazochukua lakini tuna kawaida ya kuombea taifa mara kadhaa na tumekuwa tukifanya hivyo katika serikali za awamu zote. Sasa siku hizi kuna mambo mengi yamelikumba taifa letu kama vile hii vita ya rushwa na ufisadi na hivyo kama viongozi wa kiroho kazi ya kwanza ni kuongoza waumini wetu kusali na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunasaidiana na Serikali,” alisema Askofu Kilaini katika mahojiano maalumu na Raia Mwema.

Alisema misa inafanyika kila mahali nchi nzima kuanzia ngazi ya kaya hadi kanisani kwa waumini wote wa Kanisa Katoliki ili kuhakikisha nchi inakuwa katika hali nzuri.

“Tumeanza misa maalumu kila mahali kuliombea taifa, viongozi na wananchi wetu. Tunamuomba Mungu tuwe na amani, atuepushe na mpasuko wa kidini na kikabila ambayo imeanza kuikumba nchi yetu,” alisema na kuongeza;

“Tumesikia sasa kuna mambo mazito kama haya ya ufisadi mkubwa wa kutisha wa mabilioni ya fedha na tunaambiwa ya kuwa kuna mabilioni mengine hayajatajwa. Pia hivi sasa kuna haya mauaji ya binadamu wenzetu maalbino kwa kuwa kuna watu wanatafuta viungo vyao kupata utajiri. Hatuna silaha ya kukabiliana na matatizo haya ndiyo maana sasa tunamuomba Mungu.”

Alisema wanaoua albino wanasukumwa na nguvu ya shetani na upumbavu na kuongeza kwamba watu hao wakiachwa wataanza kutaka kuwaua watu wenye maumbile tofauti ama hata wenye rangi tofauti na wao.

Tayari Baraza la Maskofu wa Katoliki Tanzania (TEC) limetangaza utaratibu mpya wa sala maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa na kuziamuaru Parokia na waumini wote wa kanisa hilo nchini, kufuata utaratibu huo ambao umekwishaanza kutekelezwa nchi nzima na katika ngazi zote.

Waraka maalumu wa Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadhama Polycarp Kardinali Pengo kwa maparoko, mapadre na waumini wa jimbo lake, umekariri agizo la Rais wa TEC kwa waumini wa kanisa hilo nchini.

Waraka huo umenukuu agizo la Rais wa TEC, Askofu Thaddeus Ruwaichi la kusali kwa ajili ya kuliombea Kanisa nchini na kuliombea Taifa kwa kuelemea zaidi hali na mwelekeo wa Taifa kwa sasa.

“Sisi kama wana kanisa na jumuiya nzima ya waamini hatuna budi kujiweka chini ya ulinzi wa Mungu zaidi katika kipindi hiki kigumu kwa kanisa na Taifa letu,” imeeleza sehemu ya waraka huo ukitoa utaratibu maalumu wa jinsi ya kuendesha ibada.

Sehemu ya sala hiyo ambayo imekuwa ikiendeshwa katika kila Kanisa Katoliki nchini inaanza kwa kusema, “-Baba yetu, Salamu Maria, Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, Tunaukimbilia ulinzi wako, Bikira Maria Malkia wa Amani, Utuombee”.

Mbali ya sala hiyo maalumu agizo hilo limewaelekeza waamini wote wa kanisa hilo iwe mtu binafsi au katika vyama vya kitume, jumuiya ndogondogo au parokia kuwa na sala ya Rozari Takatifu maalum kwa ajili ya nia hiyo.

Pamoja na Askofu Kilaini kubainisha kwamba ibada kama hiyo imekuwa ikiendeshwa mara kadhaa na hata katika kipindi cha serikali zilizopita, ibada ya sasa inedhihirisha nchi kukumbwa na mtikisiko mkubwa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo, hali ambayo si ya kawaida.

Miongoni mwa mambo yaliyoitikisa nchi ni pamoja na kuzidi kushamiri kwa tuhuma za ufisadi zinazowakabili viongozi na wafanyabiashara wakubwa nchini, baadhi wakiwa ni wale wenye uhusiano wa karibu mno na watawala wa sasa na wa zamani.

Miongoni mwa tuhuma zimesababisha hata kutikisika kwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kwa mara kadhaa ikiwa ni pamoja na sakata la umeme wa dharura uliokabidhiwa kampuni tata ya Richmond Development LLC ya Marekani, sakata lililowaangusha mawaziri watatu akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Mbali ya Lowassa mawaziri waliowahi kuongoza Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi, nao walianguka na wote walilazimika kujiuzulu mbele ya Bunge mjini Dodoma.

Sakata la ununuzi wa rada ya kijeshi nalo liliitikisa serikali baada ya Rais Kikwete kulazimika kufanya mabadiliko ya baraza lake, siku chache baada ya kumrudisha katika serikali yake, Andrew Chenge, mwanasiasa ambaye kwa miaka 10 alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Benjamin Mkapa.

Wakati sakata la Richmond likiwa halijapoa, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilitikisika kwa kuibuka kwa kashfa za mfululizo ambazo hadi sasa hazijapoa ikiwamo kashfa maarufu ya wizi katika Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) huku aliyekuwa Gavana wake, Marehemu Dk. Daudi Ballali, akiondoka nchini kwa utata mkubwa na baadaye kuondolewa katika nafasi yake huku akiwa ameandika barua ya kujiuzulu. Wakati hayo yakitokea Dk. Ballali alikuwa mgonjwa nchini Marekani na hatimaye alifariki dunia.

Mbali ya sakata la EPA, Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikitajwa kuguswa na upotevu mkubwa wa fedha za umma, ikiwa ni pamoja na zile zilizokwenda katika kampuni kadhaa tata ikiwamo Meremeta Gold, Tangold na Deeo Green, kashfa ambazo hadi sasa zinaendelea kufukuta.

Hali hiyo imesababisha hata wananchi kuanza kupoteza imani na serikali yao pamoja na kuwa sehemu kubwa ya kashfa zilizoibuka sasa ni zile zilizotokea wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya tatu ya Rais Benjamin Mkapa, ambaye yeye binafsi pamoja na familia yake wametajwa moja kwa moja kuhusika na baadhi ya kashfa hizo.

Tayari serikali imekwisha kuwafikisha mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka mawaziri wawili ambao Mkapa alikuwa akiwaamini, Basil Mramba aliyekuwa Waziri wa Fedha na Daniel Yona aliyewahi pia kuongoza Wizara ya Fedha na pia wizara nyingine nyeti ikiwamo ya Nishati na Madini, Makamu wa Rais na Mipango.

Baadhi ya wanasiasa na wanasheria wamekwisha kuweka bayana nia yao ya kutaka kuondolewa kinga kwa Mkapa ili naye ashitakiwe kwa tuhuma zinazomkabili ikiwa ni pamoja na kujihusisha na biashara kwa kutumia madaraka yake na hata rasilimali za umma ikiwamo majengo ya Ikulu.

Wakati watuhumiwa 20 wakiwa wameburuzwa mahakamani kujibu mashitaka kwa tuhuma za kuhusika na wiza wa fedha za EPA, bado hali ni tete baada ya wahusika wa kampuni nyingine kadhaa kutajwa kuwa katika za hatua ya mwisho za kushitakiwa.

Matukio mengine yaliyoitikisa nchi ni pamoja na migomo na maandamano kutoka kwa wanafunzi, waalimu, madaktari na hata maandamano ya wastaafu wa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977.

Hatua ya wastaafu hao kulala barabarani imeelezwa kuwa ilivitisha hata vyombo vya dola kutokana na jinsi walivyojikusanya bila kufahamika na kwamba serikali ilishitukizwa kukuta wazee hao wakiwa wamefunga barabara katika eneo la daraja la Selender, huku wengine wakivua nguo.

Hii si mara ya kwanza kwa Kanisa Katoliki kushitushwa na hali ya nchi, kwani gazeti hili liliwahi kuandika maoni ya Askofu Kilaini, aliyetahadharisha kwamba kwamba baadhi ya viongozi wa Serikali wanapokea pesa kutoka kwa wawekezaji wa nje, na hivyo kumfanya Rais Kikwete kuwa na wakati mgumu katika kuongoza vita dhidi ya ufisadi wa kimataifa.

Askofu Kilaini aliliambia Raia Mwema katika toleo hilo la miezi kadhaa iliyopita kwamba anamwonea huruma Rais Kikwete kwa kuwa lengo lake jema, la kupambana na rushwa kubwa au ufisadi wa kimataifa, linahujumiwa na baadhi ya viongozi walioko chini yake.

"Wanakuja na vitu vyao na mapesa mengi sana. Sasa wanapofika hapa wanayatumia mapesa haya kuwapa viongozi walioko madarakani. Viongozi wa aina hii, ambao ndio walipaswa kumsaidia Rais Kikwete, ndio hao hao wanakuwa wa kwanza kumkwamisha.

"Hao ndio wanaofanya dhamira nzuri ya Rais Kikwete, ya kupambana na rushwa hii kubwa, iwe ngumu kuitekeleza," alisema.

Askofu Kilaini anasema suala la ufisadi wa kimataifa lilianza kujitokeza wakati wa utawala wa Awamu ya Tatu pale milango ya uwekezaji ilipofunguliwa wazi ikigusa zaidi michakato ya mikataba.

Mara kadhaa wabunge wamekuwa wakilalamika ndani ya Bunge, kwamba mikataba hiyo ingekuwa inawekwa wazi mbele yao, lakini Serikali imekuwa ikipinga dhana hiyo kwa madai kuwa mambo mengi ni ya siri baina ya wale wanaoingia kwenye makubaliano ya mkataba.
 
na Deogratius Temba

MLOLONGO wa matukio ya kufikishwa mahakamani kwa waliokuwa viongozi waandamizi katika Serikali ya Awamu ya Tatu pamoja na watuhumiwa wa wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), unaonekana kuwatisha viongozi wa Kanisa Katoliki na sasa wameanza kupanga mikakati ya kuliepusha taifa na hali ya machafuko.

Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini, juzi aliiambia Tanzania Daima Jumatano katika mahojiano maalumu yaliyofanyika ofisini kwake kuwa, matukio yanayotokea sasa hapa nchini yanatisha kwa sababu yanaweza kuhatarisha amani iliyopo.

Alisema matukio ya kukamatwa kwa baadhi ya Watanzania wakiwa na mabilioni ya fedha zinazoweza kununua vijiji au mkoa, kufikishwa mahakamani kwa viongozi wastaafu wa serikali wakihusishwa na ufisadi na matumuzi mabaya ya madaraka wakiwa watumishi katika ofisi za umma, viongozi wa juu serikali kujiuzulu na matukio mengi ya mauaji ya kikatili, ni mambo yasiyokuwa ya kawaida na ya hatari.

Alisema kwa kutambua hali inayolikabili taifa, Kanisa Katoliki limeamua kuweka mikakati ya kulinusuru taifa na machafuko, itakayoongozwa na sala maalumu ya kuomba amani iendelee kutawala nchini.

“Kutokana na mambo haya mazito kutoka hapa nchini, tuna jukumu la kuhakikisha tunaiombea nchi yetu ili amani iliyopo iimarike kwa vile mlolongo wa matukio haya yasiyo ya kawaida yanaweza kuhatarisha amani iliyopo.

“Sisi Kanisa Katoliki tumepiga kelele tumechoka, wenye jukumu la kuongea sana ni viongozi wa vyama vya siasa na mashirika ya kijamii. Sasa tumeamua kuanza na silaha kubwa zaidi ambayo ni sala, tumewaambia waumini wetu waanze utaratibu maalumu uliotolewa na Baraza la Maaskofu (TEC) wa kusali sala maalumu ya kuliombea taifa amani, ambao utafuatwa na waumini wote Wakatoliki,” alisema Askofu Kilaini.

Alisema pamoja na kusali, kanisa lina jukumu la kuishauri serikali juu ya mwenendo wa mambo nchini, pamoja na kukemea maovu, uvunjaji wa maadili, tabia za ushirikina zinazokithiri, mauaji ya kikatili ya mtu mmoja mmoja na ya koo na mambo mengine ya kifisadi yanayofanywa na baadhi ya viongozi ambao ni waumini wa makanisa au misikiti.

Hata hivyo, alisema si wajibu wa kanisa kuwakataa waumini wake wanaohusishwa na matukio ya ufisadi nchini kwa sababu kuwafukuza kundini si kuwasaidia, bali ni wajibu wa kanisa kuwaelimisha na kuwajenga watu katika maadili mema.

“Sisi si polisi au mahakama, kwa hiyo hatuna jukumu la kumtaja mtu binafsi hadharani au kanisani, kama muumini anashiriki katika mamabo ya kifisadi, tunalo jukumu la kumrekebisha au kumkemea, lakini si kumtaja hadharani.

“Lakini ifahamike kuwa yanapotokea matukio makubwa nchini kama haya ya ufisadi na serikali ikachukua hatua au kutochukua hatua, ni lazima kanisa lizungumze.

Hata hivyo hatua iliyokwishachukuliwa na serikali ya kuwafikisha watuhumiwa wa EPA na wengine waliotumia madaraka vibaya mahakamani wakati wakiwa madarakani ni nzuri, ila ieleweke kuwa kanisa halisemi kuwa watuhumiwa wamekwisha, haliwezi kusema hivyo.

“Kanisa linathamini na kutambua hatua za awali zilizokwisha kuchukuliwa na serikali za kuwafikisha watuhumiwa mahakamani, hatujui wapo wangapi, tunavuta subira kusikiliza kazi ya vyombo vya uchunguzi inayoendelea ili kuwafikisha wote mahakamani,” alisema Kilaini.

Akizungumzia mauaji ya albino, alisema kanisa linasikitishwa na hali inayoendelea nchini ya mauaji ya albino, vitendo ambavyo ni vya kikatili na ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyoweza kuvunja umoja wa kitaifa.

Alisema mauaji ya albino yanakera, yanaitia aibu nchi na kuikosesha heshima machoni pa jumuiya ya kimataifa. Kwamba dunia inawashangaa Watanzania wanaishi karne ipi.

Alisisitiza kuwa matukio ya mauaji ya albino yameichafua nchi kiasi cha wageni kuiona Tanzania kama mahali pasipofaa kuishi.

“Wageni nao wanaanza kuogopa kuja kwani albino wakiisha nchini watafuata kundi jingine la watu, na kwa mtiririko huo, baadaye Watanzania wote wataanza kuuana. Serikali inatakiwa ilitangaze suala hili kuwa janga la kitaifa.

“Kama taifa tunapaswa kuchukua hatua madhubuti kupambana na kukomesha mauaji haya kwa vile tunakoelekea ni kubaya, wakimaliza albino, watawataka wenye kipara, baadaye watu weusi au wa kabila fulani, tukifika hapo ni vita ya wenyewe kwa wenyewe.

“Kanisa linaitaka serikali kutumia mbinu zozote, kutoa elimu kwa raia wake ikiwezekana kuanzia kwenye shule za msingi na sekondari juu ya madhara ya muaji hayo. Kanisa linaiomba serikali iunde idara maalumu ya usalama wa taifa, makachero watumwe vijijini kuangalia kazi inayofanywa na waganga wa kienyeji, wachunguze kazi zao, wanavyopiga ramli na kupata ufumbuzi wa chimbuko na misingi ya mauaji hayo,” alisema Askofu Kilaini.

Akizungumza sababu ya kanisa kuchukua hatua ya kuanzisha mkakati wa kuomba ili kunusuru taifa na hali yoyote ya uvunjifu wa amani, alisema, imetokana na hofu ambayo kanisa limeipata baada ya kuwapo kwa ongezeka kubwa la matukio ya ajabu ambayo kwa kipindi cha miaka mingi hata kabla ya uhuru hayakuwahi kutokea.

=============

Hapa ndipo mtu unapochoka na wabongo mmeanzisha vita dhidi ya ufisadi washitakiwa walitajwa katika list of shame sasa wanaenda korti, Woga unaanza na sababu lukuki kwamba amani itavunjika. Kufikisha mtu mahakamani ni amani gani itakayo vunjika wakati huko ndio haki ilipo. Viongozi wa dini kuweni wajasiri kukemea maovu bila ya kujali nani anayafanya, mpango wenu wa kuchagua watu ndio utakao leta vita. Na pia chungeni na kauli zenu sio kila jambo basi nyie ndio wasemaji hata mkikaa kimya pia sawa mkawaacha wapiganaji wakasonga mstari wa mbele katika kupiga vita ufisadi. Kuliko kutoka na kauli tata za kukatisha tamaa.

Kuna mfanyakazi wa almashauri songea kapigwa miaka kibao kwa ufisadi, hakuna kiongozi wa dini aliyesema amani itavunjika. Sasa mawaziri na makatibu wakuu wanatinga kwa pilato mcheche unaanza.

Watue wamekichafua acheni kichafuke kwani nini!
 
Nadhani kauli ya Kilaini iko straight forward. Sio kanisa kuonyesha woga kwamba amani itavunjika, bali ni kutahadharisha kwamba amani inaweza kuvunjika. Na kuvunjika huku sio kwasababu ya kuwafikisha mafisadi mahakamani, bali amani itaweza kuvunjika kama hawa mafisadi wote hawatafikishwa mahakamani. Amani itavunjika kama serikali itashindwa kudhibiti mauaji ya maalbino nk. Tuunge mkono juhudi za kanisa katika kuliombea taifa hili mema. Tuombe amani izidi kudumu na kudumu.

Mambo ya "long sleeve or short sleeve" (quoted from Blood Diamonds movie) sio mazuri. Tusije kufikia ukatili kama huo wa kukatana mikono tena kwa mkatwaji kuulizwa kama anataka long sleeves or short sleeves. For those who have seen the movie wanaelewa nasema nini.
 
..tatizo ninaloliona ni fisadi mmoja kumburuza fisadi mwenzake mahakamani.

..tulipaswa kuchagua viongozi waadilifu, wasiokuwa na historia ya kampeni na siasa za kifisadi.
 
..tatizo ninaloliona ni fisadi mmoja kumburuza fisadi mwenzake mahakamani.

..tulipaswa kuchagua viongozi waadilifu, wasiokuwa na historia ya kampeni na siasa za kifisadi.

Mkuu yani umelenga mulemule!Wana wasiwasi wa kaubaguzi fulani katika hii kamatakamata.
 
..tatizo ninaloliona ni fisadi mmoja kumburuza fisadi mwenzake mahakamani.

..tulipaswa kuchagua viongozi waadilifu, wasiokuwa na historia ya kampeni na siasa za kifisadi.

JokaKuu:

Unaloliona ni tatizo lakini tatizo hilo sio kubwa kuliko lile la fisadi kuficha matatizo ya fisadi mwenzake.
 
- Hivi hawa wakuu wa dini sio ndio waliosema kua muungwana ni nabii? I mean wangenyamaza tu maana no body cares hata kama wapo, kwa nini wanapenda sana attention, yakishatokea makubwa tu ya taifa lazima wajitokeze na blah! blah! as if kuna anaye-care!

- Kilaini ndio nani hasa? Wakati Mtandao wanafanya uhuni kwenye uchaguzi wa rais alikuwa wapi huyu mbona hatukumsikia? Wakati Mtandao wanasema Salim alimuua Karume alikuwa wapi huyu mkuu?
 
Udini huko CUF. Ukabila huko CHADEMA. Hii ni kazi ya CCM, hako kaubaguzi kanatoka wapi?

Wewe Kingunge Ngombare Mwiru nini?Yaani umekunywa maji ya CCM?Wewe unaangalia kwa nje,wenzio wanaoangalia kwa ndani wanajua nini kinachoendelea.
 
- Hivi hawa wakuu wa dini sio ndio waliosema kua muungwana ni nabii? I mean wangenyamaza tu maana no body cares hata kama wapo, kwa nini wanapenda sana attention, yakishatokea makubwa tu ya taifa lazima wajitokeze na blah! blah! as if kuna anaye-care!

- Kilaini ndio nani hasa? Wakati Mtandao wanafanya uhuni kwenye uchaguzi wa rais alikuwa wapi huyu mbona hatukumsikia? Wakati Mtandao wanasema Salim alimuua Karume alikuwa wapi huyu mkuu?

Siyo wote walisema kuwa Muungwana ni chaguo la Mungu na ze dataz ni kuwa hawa wakulu walikuwa wanamtaka Salim kwavile ndiyo lilikuwa chaguo la Nyerere.
Kilaini ni askofu msaidizi jimbo kuu katoliki Dar.Viongozi wote wa dini wanaheshimika sana na waumini wao ambao ndiyo wapiga kura wa viongozi wa serikali.Kwahiyo wana haki kutoa maoni yao wanapoona tatizo ambalo linaweza kuvuruga mshikamano wa wananchi.
 
Viongozi wote wa dini wanaheshimika sana na waumini wao ambao ndiyo wapiga kura wa viongozi wa serikali.Kwahiyo wana haki kutoa maoni yao wanapoona tatizo ambalo linaweza kuvuruga mshikamano wa wananchi.

- Wakati Mkapa anaiba Kiwira walikuwa wapi? Mbona hatukuwasikia? Ni lini waliwahi kumchagua mgombea wa chaguo lao akawa rais wa bongo kama sio mkatoliki mwenzao fisadi Mkapa??
 
- Wakati Mkapa anaiba Kiwira walikuwa wapi? Mbona hatukuwasikia? Ni lini waliwahi kumchagua mgombea wa chaguo lao akawa rais wa bongo?

Mkuu katiba inasema kuwa kila mtu atahesabika hana hatia mpaka mahakama itakapothibitisha vinginevyo.Kwahiyo wao na heshima yao unataka waanze kuropokaropoka Mkapa mwizi kama sisi wengine hapa kabla ya huo wizi kuthibitishwa mahakamani?
Hawana uwezo wa kumchagua mtu kuwa Rais wa Tanzania.Lakini kumbuka kwamba linapokuja swala la uchaguzi basi kila mtu atakuwa na mtu wake ambaye angependa kuona anakuwa kiongozi wa ngazi fulani hata kama mwisho wa siku lile chaguo lake litashindwa.Kwahiyo wao nao wako katika mkondo huo na ndiyo mana hata wanasiasa nao wanajaribu sana kuwa karibu yao wakitafuta kuungwa mkono kwa nguvu yao waliyonayo kwa wale waumini wanaowasimamia.
 
Back
Top Bottom