Rais Samia, usipuuze maono na ushauri wa viongozi wa dini.

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Wakati wa utawala wa Magufuli madhehebu ya dini ya Kikristo yalipoona uminywaji wa demokrasia na uhuru wa kujieleza, kupotea kwa watu uliokuwa ukifanywa na serikali, hayakukaa kimya yalitoa Nyaraka mbali mbali kumuonya Rais Magufuli na serikali yake.

Lilianza Baraza la Maaskofu wa kanisa la Katoliki;

WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

Wakafuata Maaskofu wa KKKT nao wakaonya,

Maaskofu KKKT: Tunasikitishwa na matukio ya kupotezwa watu, kubanwa kwa Uhuru wa Mahakama, Bunge na Tume ya Uchaguzi...

Likafuata Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship la Askofu Zachary Kakobe Rais akaagiza TRA wamkague,

Askofu Zakaria Kakobe: Tanzania siyo nchi ya chama kimoja! Amtaka Rais Magufuli atubu

Na mimi pia Quinine nilionya;

Wakati huo jumuiya za dini ya Kiislam zilikaa kimya hatukusikia zikisema Maaskofu wanachanganya dini na siasa.

Pamoja na maoni, ushauri binafsi uliotolewa na Maaskofu, Wachungaji na watu binafsi, Rais na serikali yake waliendelea kupuuza.

Namkumbusha tena Rais aliyepo madarakani Samia asipuuze maoni ya watumishi wa Mungu kama mwenzake alivyopuuza.
 
nakumbuka waislamu hawakukaa kimya bali walimuunga mkono kwa uchafu uliokuwa unatendeka wazi wazi

Waislamu wa Tanganyika ni waoga tangu lile saga la Shehe Ponda
 
Back
Top Bottom