Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Povu linakutoka WEWE. Nakuuliza na wewe wapi nimeunga MKONO? Hiyo sala sioni mahali ameitaja familia.

...yes povu la kicheko lanitoka...
Unaweza kuombea chakula pasina kukitaja pia. hiyo inawezekana mkuu.
 
Haya ndiyo maombi ya Kadinali Pengo wakati akizindua kitabu cha mama Lowasa nyumbani kwa Mh. Lowasa:

"Mungu Baba Mwenyezi wewe ni mpaji wa mema yote. Paji hilo ni zuri lakini kwa bahati mbaya sisi wanadamu badala ya kukushukuru paji hilo kulipokea kwa mikono miwili, tukamtendea mwanao kama tulivyomtendea, na bado wewe, kuonyesha kwamba bado unataka kutuokoa na kutufikisha mahali pa heri, ulimfufua mwanao kutoka wafu, yeye ambaye tulikuwa tumemuua. Naomba msamaha kwa utovu huo wa maadili.
Naomba mwanga wa ufufuko wa mwanao, uangaze zaidi ndani mioyo yetu, kusudi wale wote tunamheshimu Yesu tuweze kuuambia ulimwengu kwamba nyuma yetu ndiyo msingi wa hali bora katika maisha.
Tunakushukuru pia kwa kutukusanya jioni ya leo, kwa lengo maalumu mwanao anatenda kazi ndani ya wanadamu kwa njia mbalimbali., na mojawapo ni huu mwanga ambao anaweza kuwapa watu wakaweza kuwaelekeza wenzao mahali anapopatikana huyu mwanao.
Tunakuomba ubariki jumuiya hii, ubariki kila kilicho chema tutakachokifanya. Tunaomba hayo yote kwa njia ya Kristu Bwana wetu, Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina".

(Rai Nguvu ya Hoja)

Sala hii ni kweli. Magazeti ya jana yanaonyesha picha ambapo Mhadhama Kardinali PolicarP Pengo akiwa na Mhasham Askofu Malasusa (KKKT) na Askofu Mstaafu Elinaza Sendoro wakiwa nyumbani kwa Lowasa kuzindua kitabu cha Regina. Lowasa na Regina wanaonekana kwenye picha pia.
Ila kwa watanzania kuna jambo moja la kujiuliza: Ni kweli Mungu yupo ndani ya Makanisa? Ni kweli Maaskofu wetu (hata mashemasi na wachungaji) ni watiwa mafuta wa Mungu au ni watumishi wa Kanisa?
Ni wazi kuwa kuna tofauti kubwa kati ya Kanisa kama taasisi na Mungu kama imani. Kunaweza kuwa na taasisi ya ya dini lakini haina imani (Mungu) ndani yake. Muda mwingi unaweza kuwa unapotezwa kuangalia taratibu za Kanisa (katekisimu, mtaguso) badala ya kushughulikia masuala ya imani (Mungu).
Kama ilivyo kwa watumishi wa serikali (Alfa Lowasa & Co.) wasiokuwa waadilifu ndivyo inavyoweza kuwa kwa watumishi wa Kanisa wasiokuwa waadilifu. Hawa waweza kuwa marafiki kwa maana lao moja. Wanaweza kutembeleana na kupongezana, hata kuzindua vitabu! Pengo, Malasusa, na Sendoro kwenda kubariki/ kusali/ kuombea familia ya Lowasa (tamka Alfa & Co.) ni ishara ya marafiki kuinuana. Sidhani kuwa katika hili walikuwa na Mungu.
 
Sasa hapa mnamlaumu nini Pengo kwenye hiyo sala? Yeye ameombea "kila kilicho chema", kwani hakuna chema katika hiko kitabu kilichoandikwa na muumini wake wa kanisa katoliki mama Regina Lowassa?

Pengo hakuombea ufisadi wa Lowassa, kosa lake tu ni kwenda kwenye hilo tukio bila kujua kwamba wakina Rostam na Lowassa wao kila tukio ni fursa kwao ya kumsafisha Lowassa kupitia Habari Corporation.

Kanisa Katoliki linapaswa kutoa tamko la haraka kuwa tukio hilo sasa linatafsiriwa tofauti.

Ileweke kwamba hata Yesu alikwenda kula nyumbani kwa wadhambi, lakini hakutangaza kuyasafisha madhambi yao. Kwa hiyo Pengo kwenda nyumbani kwa Lowassa sio tatizo kama hakutangaza kumsafisha Lowassa na uchafu wake

SM
 
Kuna suala la kuua soo hapa.Baada ya kupata negative response katika yale matamshi ya 'kusulubiwa...' naona hii ndo imefuata ili kupoza!!Suala ni kuwa hayo ya kuwa tuache kusulubiana aliyasema au la??Alimaanisha nini?
 
Sioni tatizo, nadhani Pengo hakudiriki kutaja jina la Lowassa kwani yeye mwenyewe anajua kabisa Lowassa ni mchafu ambae anaitaji kubatwiza upya.

Mkewe amezindua kijalida akionyesha anamjali Mungu, what a nonsense..... She was supposed to write a book title "Lowassa and the devils, how did they achieved the mission"
 
Sasa hapa mnamlaumu nini Pengo kwenye hiyo sala? Yeye ameombea "kila kilicho chema", kwani hakuna chema katika hiko kitabu kilichoandikwa na muumini wake wa kanisa katoliki mama Regina Lowassa?

Pengo hakuombea ufisadi wa Lowassa, kosa lake tu ni kwenda kwenye hilo tukio bila kujua kwamba wakina Rostam na Lowassa wao kila tukio ni fursa kwao ya kumsafisha Lowassa kupitia Habari Corporation.

Kanisa Katoliki linapaswa kutoa tamko la haraka kuwa tukio hilo sasa linatafsiriwa tofauti.

Ileweke kwamba hata Yesu alikwenda kula nyumbani kwa wadhambi, lakini hakutangaza kuyasafisha madhambi yao. Kwa hiyo Pengo kwenda nyumbani kwa Lowassa sio tatizo kama hakutangaza kumsafisha Lowassa na uchafu wake

SM

Nadhani hakuna haja ya kudhani kuwa LA na EL wanatumia fursa kujisafisha kupitia magazeti yao ya New Habari Corporation. Hapana. Kila kitu kinakuwa kumepangwa barabara. Hilo tukio lilipangwa pia. Ni mkakati wa kujisafisha. Kijarida cha Regina Lowasa ni sehemu ya mkakati huo.
 
Sasa hapa mnamlaumu nini Pengo kwenye hiyo sala? Yeye ameombea "kila kilicho chema", kwani hakuna chema katika hiko kitabu kilichoandikwa na muumini wake wa kanisa katoliki mama Regina Lowassa?

Pengo hakuombea ufisadi wa Lowassa, kosa lake tu ni kwenda kwenye hilo tukio bila kujua kwamba wakina Rostam na Lowassa wao kila tukio ni fursa kwao ya kumsafisha Lowassa kupitia Habari Corporation.

Kanisa Katoliki linapaswa kutoa tamko la haraka kuwa tukio hilo sasa linatafsiriwa tofauti.

Ileweke kwamba hata Yesu alikwenda kula nyumbani kwa wadhambi, lakini hakutangaza kuyasafisha madhambi yao. Kwa hiyo Pengo kwenda nyumbani kwa Lowassa sio tatizo kama hakutangaza kumsafisha Lowassa na uchafu wake

SM
Pengo ajue kuwa ni mwakilishi wa Papa hapa Tanzania hivyo asijiingize kwenye kashfa zinazoweza kuligharimu Kanisa.Mwaka 2005 alikubaliana na waliosema JK ni chaguo la Mungu,amesikika akimtetea Mkapa kwa ufisadi wake asvuliwe kinga ya kushitakiwa.Sasa hili la Lowassa angefanya kama YESU alipomwambia Tajiri mwenye dhambi kuwa akauze mali zake zote na kuwagawia masikini ndipo akatubu dhambi zake.
 
Si ajabu sasa hapa Tanzania kuwaona Viongozi wa Dini wakijihusisha kisiasa.Kiongozi wa dini Getrude Lwakatare ameteuliwa na Rais kuwa Mbunge na anaweza hata kumteua kuwa Waziri.Kadinadi Pengo amekuwa akijihusisha na maswala yanayoshabihiana na siasa.Mtikila hali kadhalika.Kama hali ndio hii imani itasimamiwa na nani kama viongozi wa dini watazama katika siasa kama wafanyavyo wataalamu wetu.Je sasa itangazwe wazi kuwa viongozi wa dini wajihusishe wazi na siasa?Naomba nielimishwe.
 
Watumishi wa mungu wote ni binadamu! Utashi na misimamo yao vinaongozwa na nafsi zao zinaongozwa na hekima za kibinadamu na ufunuo wa mungu!
 
Tutofautishe dini na siasa kwanza wandugu! Pengo hakwenda kwa EL kama mwanasiasa bali kama mchungaji, na kama mchungaji anapaswa kuwatafuta kondoo waliopotea, kuwahubiria habari za wokovu na hatimaye kuwarudisha kundini! So kama tunakubaliana kuwa EL ni mchafu (kibinadamu), basi Pengo na maaskofu wengine walioenda nyumbani kwao ilikuwa ndo mahala pao.....though ilipaswa mdhambi kukiri kwanza makosa yake kabla hajatakaswa na wachungaji wale!

So kwangu mimi wale maaskofu walifanya kitu sahihi kabisa kwenda kumwombea EL (Mwenye dhambi) ali amrudie muumba wake!
 
Nadhani sikosa kujihusisha na siasa. Tena itafurahisha zaidi kama watachangia kukemea uovu unaoendelea nchini. Lakini kama wataungana na mafisadi basi ni wazi watawakwaza waumini na hivyo kufifisha imani ya kanisa.
 
..wanaruhusiwa kushiriki siasa kupitia vyama vya siasa.

..zamani walikuwepo Padri Yohana Misigalo mbunge wa Tabora mjini, na Padri Supa wa Dodoma mjini. pia walikuwepo Sheikh Amri Abeid, Sheikh Jumanne Mikidadi...

..
 
Hivi ile kauri mbiu ya "... Msichanganye DINI na SIASA" inawahusu watu gani na katika mambo yepi!?
 
Kina mtu anaruhusiwa kujihusisha kwenye siasa, haina haja ya kutangazwa kitu.
 
Tutofautishe dini na siasa kwanza wandugu! Pengo hakwenda kwa EL kama mwanasiasa bali kama mchungaji, na kama mchungaji anapaswa kuwatafuta kondoo waliopotea, kuwahubiria habari za wokovu na hatimaye kuwarudisha kundini! So kama tunakubaliana kuwa EL ni mchafu (kibinadamu), basi Pengo na maaskofu wengine walioenda nyumbani kwao ilikuwa ndo mahala pao.....though ilipaswa mdhambi kukiri kwanza makosa yake kabla hajatakaswa na wachungaji wale!

So kwangu mimi wale maaskofu walifanya kitu sahihi kabisa kwenda kumwombea EL (Mwenye dhambi) ali amrudie muumba wake!

Contradiction: EL hakukiri na wala hana mpango wa kukiri dhambi zake. Amewaibia watanzania basi. Mipango yake ya mbele ni kuendelea kufanya hivyo: kuvuna mali kwa njia isiyofaa. To swindle public resources. Lengo lake kuu ni kupata mali na kutajirika kwa njia yoyote ile (hata ya wizi) kwa ajili ya kupata utukufu wa dunia. Tusisahau kuwa mpango wake wa 'kununua' mvua ilikuwa sehemu ya mipango yake ya kuliibia taifa. Kama ilivyokuwa kwa watanzania, EL anawahitaji maaskofu kwa ajili ya kusafisha uchafu wake wa duniania tu, siyo kumpendeza Mungu kwa ajili ya maisha baada ya kufa (ahera). Pengo na wenzake walipaswa kutambua hilo.
 
Ndugu yangu, mwanzoni mwa post yangunilisema ''tusichanganye dini na siasa'' hapa, we unasema EL hakukiri na hana mpango wa kukiri dhambi zake, nani ka kwambia hayo? wewe ni padre?

Kwa kukusaidia tu, RC kuna kitu kinaitwa Kitubio (Confession) ambapo mwenye dhambi huungama kwa padre madhambi yake wakiwa faragha, na padre hatakiwi kudisclose hiyo fact indefinately! Sasa how do you know EL hakufanya hivyo?

Usinielewe vibaya, sisemi EL hana makosa hapa TZ, ninachotaka kueleza hapa ni tofauti ya taratibu za kiroho (hasa RC) na za kisiasa!
 
Kama dini na siasa havipaswi kuchanganywa ni kwa nini basi Bunge huwa linaanza kwa sala au kwa kuomba dua? Je, hao wabunge na viongozi mbalimbali wa serikali hawana dini? Je, kuna mahali popote katiba ya nchi inasema mtu akiwa kiongozi wa dini hatakiwi kushiriki siasa?

Kwa mujibu wa katiba ya nchi kila raia wa Tanzania ana haki ya kushiriki siasa mradi tu ana sifa zinazotakiwa kwa nafasi anayogombea au kuteuliwa kwao.
 
Back
Top Bottom