Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Wenye macho hawahitaji kuambiwa tazama. Viongozi wa dini hawakutaka tu kuwaambia CCM kuwa mchawi wao ni Kikwete. CCM wakiachana na JK na siasa zake za kulindana na kupendeleana, nchi inaweza ikawa na serikali ya kuwajibika na kuiepusha na mabalaa.

Please, Please CCM or Bunge, get rid of JK sooner than 2010 to rescue the country from self destruction.


Viongozi wa dini waonya nchi inaelekaa pabaya
*Washauri Rais apunguze safari za nje

Na Waandishi Wetu, Mwananchi




Habari hii imeandaliwa na Salim Said, Peter Edson na Mussa Juma

VIONGOZI wa dini wamesema kukithiri kwa migomo, maandamano, vitendo vya kikatili, na migogoro kati ya serikali na watumishi wa umma ni ishara tosha kwamba, mambo hayako sawa nchini.

Wakizungumza na Mwananchi nyakati tofauti jana, viongozi hao walisema hali hiyo inaipeleka nchi pabaya na kuitaka serikali kutafuta suluhisho la matatizo hayo haraka iwezekanavyo.

Walisema kuwa kinachotokea sasa ni matokeo ya ahadi zisizotekelezeka na kwamba njia pekee ni kuyashughulikia madai hayo ya wananchi.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Kanisa la Katoliki jijini Dar es Salaam, Mhashamu Methodius Kilaini alisema, iwapo hali hiyo haitashughulikiwa mapema itasababisha hali kuwa mbaya zaidi nchini.

Kauli hiyo imeungwa mkono na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ramadhan Sanze aliyesema kuwa, ili kuondoa mitafaruku iliyopo nchini serikali lazima iwe tayari kuwajibika kwa jamii kisheria, kisiasa.

Aliishauri serikali kuyashirikisha makundi mbalimbali ya kijamii na kisiasa katika kupanga na kubuni sera mbalimbali kiutawala na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Sanze alimwomba Rais Jakaya Kikwete kupunguza safari za nje na hasa Marekani, akidai kuwa nchi hiyo si marafiki wazuri kwa ustawi wa taifa la Tanzania.

“Sidhani kama rais safari hizi za Marekani anapanga mwenyewe au anapangiwa, kama anapangiwa basi itifaki hii sio nzuri, hivyo tunamwomba apunguze safari za huko,” alisema Sheikh Sanze.

Alifafanua kuwa, ni vema kwa sasa rais akabakia nchini kuwatumikia Watanzania na kutuliza mitafaruku iliyopo badala ya kusafiri safiri tu huku nchi ikiwa inateketea kwa kuzongwa na migogoro ya kijamii.

Sheikh Sanze alionya kuwa, ikiwa hali itaendelea kama ilivyo sasa bila hatua madhubuti kuchukuliwa, basi kwa mara ya kwanza historia inaweza kubadilika kwa kuwa na rais wa kipindi kimoja.

Awali, Askofu Kilaini alisema ingawa tatizo la migomo linaonekana kuwa ni la miaka mingi, lakini ishara ya sasa inatia mashaka kwani serikali imekuwa ikitoa ahadi nyingi kwa wananchi na mambo machache tu ndiyo yanatekelezwa

“Hatuwezi tukasema kuwa mambo haya yanayoendelea kujiri ni ishara ya kukua kwa demokrasia, bali inatubidi tufahamu kuwa, serikali isipotekeleza ahadi zake kwa wananchi tutaendelea kushuhudia vitendo hivi kila mara.

Alisema uchumi wa dunia unapotikiswa, nchi zinazoendela ndizo zinazoathirika zaidi, hivyo ni vema serikali kupitia wizara zake ikatafuta mbinu zaidi za kuhakikisha kuwa suala la mfumuko wa bei unadhibitiwa ili mwananchi wa kawaida aweze kumudu maisha.

Alisema watu wanapochoka, na kukata tamaa na serikali yao, hutafuta njia nyingine kujinasua na matatizo yanayowakabili.

“ Ukizingatia kuwa suala la maandamano au migomo ni haki za msingi za wafanyakazi, hivyo kama serikali inataka kupunguza masuala haya ni vema ikabeba gharama na siyo kukwepa,” alisema Askofu Kilaini na kuongeza:

“Ninawaomba wananchi wenzangu watafute madai yao kwa kufanya mazungumzo na si kushiriki kwenye vurugu na migomo na pia serikali inapaswa kuwajibika kwa ahadi zake na si kuwayumbisha Watanzania.”

Hata hivyo, Askofu Kilaini alipoulizwa kwamba alishawahi kutamka kuwa Rais Jakaya Kikwete ni chaguo la Mungu na hivi sasa ana maoni gani, alisema kuwa kiongozi yeyote anayechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi ni chaguo la Mungu.

“Ni vema nikaeleweka kuwa maandiko ya Mungu yanasema uongozi na mamlaka yote hutoka kwa Mungu, hivyo basi rais aliyechaguliwa kwa ridhaa ya wananchi wenyewe ndilo chaguo la Mungu na sisi tutaendelea kuwa na msimamo huo,” alisema Askofu Kilaini.

Alisema pamoja na kwamba Rais Kikwete ni chaguo la Mungu, anahitaji kusaidiwa katika kutekeleza sera na kutimiza ahadi zote zilizoahidiwa katika serikali yake, kwa sababu viongozi wengine wakimwachia na kushughulikia zaidi maisha yao binafsi, hakuna jambo litakalotekelezeka.

Aliwataka mawaziri na watendaji wengine serikalini wakawa mstari wa mbele kumshauri Rais mambo mema na si kumpotosha ili aweze kutekeleza.

Naye Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Salum Fereji na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Padri Charles Kitima walisema jana kwenye semina ya waandishi wa habari toka mikoa mbalimbali nchini inaendelea katika Hoteli ya Isamo mkoani hapa kuwa sera na sheria na madini vimetungwa kwa masilahi ya watu wachache walafi ambao wanajali masilahi yao na hivyo lazima vibadilishwe sambamba na mikataba yote ambayo makampuni ya wawekezaji yameingia katika uchimbaji wa madini hapa nchini.

Sheikh Ferej alisema ni lazima serikali kuamka kwa kuwa sasa nchi inaelekea pabaya kutokana na rasilimali muhimu kama madini kuachiwa watu toka nje ya nchi kuwaacha Watanzania kuendelea kuisha katika umaskini uliotopea.

"Ndugu zangu, sisi kama viongozi wa dini tulitembelea maeneo ya migodi yote, kule hali ni mbaya Watanzania wanaishi maisha ya dhiki, wamefukuzwa katika maeneo yao na watu toka nje ya nchi ndio wananufaika na madini haya kwa kupeleka kwao," alisema Sheikh Fereji.

Alisema wao kama viongozi wa dini wamebaini serikali imefanya makosa katika kuingia mikataba na wawekezaji toka nje ya nchi kwa sababu Watanzania hawanufaiki na madini hayo ambayo miaka michache ijayo yatakuwa yamekwisha na kuacha mashimo.

Naye Padri Kitima alisema bila serikali kufanyika marekebisho sheria na sera za madini Tanzania itaendelea kuwa maskini na siku zijazo yanaweza kukatokea mapigano kama ilivyo katika nchi nyingine barani Afrika ambapo kulikuwa na madini.

Alisema mikataba mingi ya wawekezaji ni mibaya na inatakiwa irekebishwe, lakini inavyoonekana hakuna wa kubadilisha hadi vyombo vya habari na wananchi washikamane na kudai mikataba hiyo ivunjwe au kurekebishwa.

Padri Kitima alisema katika mazingira ya sasa angependa yafanyike mabadiliko makubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kabla ya mwaka 2010 na kuwa na kundi la wafuasi wa Nyerere ambao watatetea rasilimali za nchi hii.

"Mimi binafsi kwa hali ilivyo ningependa CCM igawanyike najua kuna watu wazuri ndani ya CCM, lakini wanashindwa kuifanya nchi hii kuwa mikononi mwa Watanzania badala yake kundi la watu wabinafsi ndilo lina nguvu nahata katika kambi ya upinzani kuna matatizo makubwa ya ubinafsi na kuwepo viongozi wasio na sifa," alisema Padri Kitima.


Alisema nchi imepoteza agenda muhimu alizoziacha hayati Mwalimu Julius Nyerere alipounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sasa ubinafsi umetawala hadi kutishia kuvunja Muungano.



Kikwete ndiye mchawi wa CCM na ndiye aliyeiharibu CCM mpaka sasa hivi waTZ wengi wanaona nafuu kumpa kura Jambazi Lowassa kuliko CCM, hilo ni kosa. Mwana akikosa hatupwi, hukemewa na kupewa nafasi ya kujirekebisha.

Tuombe Mola wawepo waTZ wengi wa kumpigia kura Magufuli ili kuliokoa taifa. Baada ya hapo, Magufuli ni lazima afanye kazi ya kuisafisha CCM kama atataka kukaa ikulu miaka 10.
 
Kanisa Katoliki sasa latishituka

Waandishi Wetu Disemba 10, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo


  • Askofu Kilaini asema nchi inahitaji maombi isiangamie

KUYUMBA kwa mshikamano wa kitaifa kutokana na kuibuka kwa mgawanyiko katika jamii, ufisadi na mauaji ya watu wasio na hatia ni miongoni mwa mambo yaliyolishitua Kanisa Katoliki nchini na sasa limeamua kufanya ibada maalumu nchi nzima kumuomba Mungu ainusuru nchi isizidi kuangamia, imefahamika.

Tayari waraka maalumu umekwisha kusambazwa na kuanza kufanyiwa kazi nchi nzima na waumini wote wa kanisa hilo kubwa lenye waumini wengi kuliko madhehebu mengine ya Kikristo nchini.


Hali ilivyo sasa imeelezwa kulitikisa Taifa katika nyanja mbalimbali na kutishia mustakabali wa amani na utulivu uliodumu kwa miaka 47 tokea kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika. Jana Jumanne Tanganyika ilikuwa inaadhimisha miaka 47 tangu ipate Uhuru Desemba 9, 1961.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini ameliambia Raia Mwema wiki hii kwamba silaha kuu ya Kanisa ni ibada kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mwenye uwezo wa kuwaongoza binadamu kuhimili majaribu yanayowakabili.

“Kwa kweli tunaipongeza Serikali kwa hatua inazochukua lakini tuna kawaida ya kuombea taifa mara kadhaa na tumekuwa tukifanya hivyo katika serikali za awamu zote. Sasa siku hizi kuna mambo mengi yamelikumba taifa letu kama vile hii vita ya rushwa na ufisadi na hivyo kama viongozi wa kiroho kazi ya kwanza ni kuongoza waumini wetu kusali na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunasaidiana na Serikali,” alisema Askofu Kilaini katika mahojiano maalumu na Raia Mwema.

Alisema misa inafanyika kila mahali nchi nzima kuanzia ngazi ya kaya hadi kanisani kwa waumini wote wa Kanisa Katoliki ili kuhakikisha nchi inakuwa katika hali nzuri.

“Tumeanza misa maalumu kila mahali kuliombea taifa, viongozi na wananchi wetu. Tunamuomba Mungu tuwe na amani, atuepushe na mpasuko wa kidini na kikabila ambayo imeanza kuikumba nchi yetu,” alisema na kuongeza;

“Tumesikia sasa kuna mambo mazito kama haya ya ufisadi mkubwa wa kutisha wa mabilioni ya fedha na tunaambiwa ya kuwa kuna mabilioni mengine hayajatajwa. Pia hivi sasa kuna haya mauaji ya binadamu wenzetu maalbino kwa kuwa kuna watu wanatafuta viungo vyao kupata utajiri. Hatuna silaha ya kukabiliana na matatizo haya ndiyo maana sasa tunamuomba Mungu.”


Alisema wanaoua albino wanasukumwa na nguvu ya shetani na upumbavu na kuongeza kwamba watu hao wakiachwa wataanza kutaka kuwaua watu wenye maumbile tofauti ama hata wenye rangi tofauti na wao.

Tayari Baraza la Maskofu wa Katoliki Tanzania (TEC) limetangaza utaratibu mpya wa sala maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa na kuziamuaru Parokia na waumini wote wa kanisa hilo nchini, kufuata utaratibu huo ambao umekwishaanza kutekelezwa nchi nzima na katika ngazi zote.

Waraka maalumu wa Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadhama Polycarp Kardinali Pengo kwa maparoko, mapadre na waumini wa jimbo lake, umekariri agizo la Rais wa TEC kwa waumini wa kanisa hilo nchini.


Waraka huo umenukuu agizo la Rais wa TEC, Askofu Thaddeus Ruwaichi la kusali kwa ajili ya kuliombea Kanisa nchini na kuliombea Taifa kwa kuelemea zaidi hali na mwelekeo wa Taifa kwa sasa.

“Sisi kama wana kanisa na jumuiya nzima ya waamini hatuna budi kujiweka chini ya ulinzi wa Mungu zaidi katika kipindi hiki kigumu kwa kanisa na Taifa letu,” imeeleza sehemu ya waraka huo ukitoa utaratibu maalumu wa jinsi ya kuendesha ibada.

Sehemu ya sala hiyo ambayo imekuwa ikiendeshwa katika kila Kanisa Katoliki nchini inaanza kwa kusema, “-Baba yetu, Salamu Maria, Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, Tunaukimbilia ulinzi wako, Bikira Maria Malkia wa Amani, Utuombee”.


Mbali ya sala hiyo maalumu agizo hilo limewaelekeza waamini wote wa kanisa hilo iwe mtu binafsi au katika vyama vya kitume, jumuiya ndogondogo au parokia kuwa na sala ya Rozari Takatifu maalum kwa ajili ya nia hiyo.

Pamoja na Askofu Kilaini kubainisha kwamba ibada kama hiyo imekuwa ikiendeshwa mara kadhaa na hata katika kipindi cha serikali zilizopita, ibada ya sasa inedhihirisha nchi kukumbwa na mtikisiko mkubwa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo, hali ambayo si ya kawaida.

Miongoni mwa mambo yaliyoitikisa nchi ni pamoja na kuzidi kushamiri kwa tuhuma za ufisadi zinazowakabili viongozi na wafanyabiashara wakubwa nchini, baadhi wakiwa ni wale wenye uhusiano wa karibu mno na watawala wa sasa na wa zamani.

Miongoni mwa tuhuma zimesababisha hata kutikisika kwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kwa mara kadhaa ikiwa ni pamoja na sakata la umeme wa dharura uliokabidhiwa kampuni tata ya Richmond Development LLC ya Marekani, sakata lililowaangusha mawaziri watatu akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Mbali ya Lowassa mawaziri waliowahi kuongoza Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi, nao walianguka na wote walilazimika kujiuzulu mbele ya Bunge mjini Dodoma.

Sakata la ununuzi wa rada ya kijeshi nalo liliitikisa serikali baada ya Rais Kikwete kulazimika kufanya mabadiliko ya baraza lake, siku chache baada ya kumrudisha katika serikali yake, Andrew Chenge, mwanasiasa ambaye kwa miaka 10 alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Benjamin Mkapa.

Wakati sakata la Richmond likiwa halijapoa, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilitikisika kwa kuibuka kwa kashfa za mfululizo ambazo hadi sasa hazijapoa ikiwamo kashfa maarufu ya wizi katika Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) huku aliyekuwa Gavana wake, Marehemu Dk. Daudi Ballali, akiondoka nchini kwa utata mkubwa na baadaye kuondolewa katika nafasi yake huku akiwa ameandika barua ya kujiuzulu. Wakati hayo yakitokea Dk. Ballali alikuwa mgonjwa nchini Marekani na hatimaye alifariki dunia.


Mbali ya sakata la EPA, Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikitajwa kuguswa na upotevu mkubwa wa fedha za umma, ikiwa ni pamoja na zile zilizokwenda katika kampuni kadhaa tata ikiwamo Meremeta Gold, Tangold na Deeo Green, kashfa ambazo hadi sasa zinaendelea kufukuta.

Hali hiyo imesababisha hata wananchi kuanza kupoteza imani na serikali yao pamoja na kuwa sehemu kubwa ya kashfa zilizoibuka sasa ni zile zilizotokea wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya tatu ya Rais Benjamin Mkapa, ambaye yeye binafsi pamoja na familia yake wametajwa moja kwa moja kuhusika na baadhi ya kashfa hizo.

Tayari serikali imekwisha kuwafikisha mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka mawaziri wawili ambao Mkapa alikuwa akiwaamini, Basil Mramba aliyekuwa Waziri wa Fedha na Daniel Yona aliyewahi pia kuongoza Wizara ya Fedha na pia wizara nyingine nyeti ikiwamo ya Nishati na Madini, Makamu wa Rais na Mipango.

Baadhi ya wanasiasa na wanasheria wamekwisha kuweka bayana nia yao ya kutaka kuondolewa kinga kwa Mkapa ili naye ashitakiwe kwa tuhuma zinazomkabili ikiwa ni pamoja na kujihusisha na biashara kwa kutumia madaraka yake na hata rasilimali za umma ikiwamo majengo ya Ikulu.

Wakati watuhumiwa 20 wakiwa wameburuzwa mahakamani kujibu mashitaka kwa tuhuma za kuhusika na wiza wa fedha za EPA, bado hali ni tete baada ya wahusika wa kampuni nyingine kadhaa kutajwa kuwa katika za hatua ya mwisho za kushitakiwa.

Matukio mengine yaliyoitikisa nchi ni pamoja na migomo na maandamano kutoka kwa wanafunzi, waalimu, madaktari na hata maandamano ya wastaafu wa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977.

Hatua ya wastaafu hao kulala barabarani imeelezwa kuwa ilivitisha hata vyombo vya dola kutokana na jinsi walivyojikusanya bila kufahamika na kwamba serikali ilishitukizwa kukuta wazee hao wakiwa wamefunga barabara katika eneo la daraja la Selender, huku wengine wakivua nguo.

Hii si mara ya kwanza kwa Kanisa Katoliki kushitushwa na hali ya nchi, kwani gazeti hili liliwahi kuandika maoni ya Askofu Kilaini, aliyetahadharisha kwamba kwamba baadhi ya viongozi wa Serikali wanapokea pesa kutoka kwa wawekezaji wa nje, na hivyo kumfanya Rais Kikwete kuwa na wakati mgumu katika kuongoza vita dhidi ya ufisadi wa kimataifa.

Askofu Kilaini aliliambia Raia Mwema katika toleo hilo la miezi kadhaa iliyopita kwamba anamwonea huruma Rais Kikwete kwa kuwa lengo lake jema, la kupambana na rushwa kubwa au ufisadi wa kimataifa, linahujumiwa na baadhi ya viongozi walioko chini yake.

"Wanakuja na vitu vyao na mapesa mengi sana. Sasa wanapofika hapa wanayatumia mapesa haya kuwapa viongozi walioko madarakani. Viongozi wa aina hii, ambao ndio walipaswa kumsaidia Rais Kikwete, ndio hao hao wanakuwa wa kwanza kumkwamisha.

"Hao ndio wanaofanya dhamira nzuri ya Rais Kikwete, ya kupambana na rushwa hii kubwa, iwe ngumu kuitekeleza," alisema.


Askofu Kilaini anasema suala la ufisadi wa kimataifa lilianza kujitokeza wakati wa utawala wa Awamu ya Tatu pale milango ya uwekezaji ilipofunguliwa wazi ikigusa zaidi michakato ya mikataba.

Mara kadhaa wabunge wamekuwa wakilalamika ndani ya Bunge, kwamba mikataba hiyo ingekuwa inawekwa wazi mbele yao, lakini Serikali imekuwa ikipinga dhana hiyo kwa madai kuwa mambo mengi ni ya siri baina ya wale wanaoingia kwenye makubaliano ya mkataba.


Walitabiri kweli-kweli viongozi wa dini. Kama Lowassa anapigiwa deki barabara, ujue kuwa yetu nchi kweli iko hatarini.
 
Back
Top Bottom