Uwekezaji wa NHC - Mchechu awajibike

Uwekezaji wa NHC - Mchechu awajibike

Rudini nyuma mtusome wengine tulisema nini wakati ule wa uteuzi wake. Mimi ni miongoni mwa watu ambao ninaamini NHC ilipaswa ivunjwe na kurudishwa katika kazi yake ya kwanza kabisa siyo sasa hivi walivyoligeuza kuwa ni shirika la kibiashara.

Ngoja nianze na Game Theory kama ifuatavyo.........

Kwa kuanza tuu napenda niwafahamishe kuwa namfahamu BINAFSI huyu NEHEMIA hivyo sina kinyongo wala matatizo naye if anything nilimfahamisha what to expect alipopewa taarifa ya uteuzi huu miez kadhaa iliyopita.

By definition UFISADI pamoja na kuibia serikali ..tunaweza kusema ni kurudisha maendeleo nyuma na kuwa na upendeleo wa dhahiri kwenye ajira serikalini including NHC!

Nadhani mnakumbuka takriban miezi sita iliyopita nilileta thread ya uteuzi wa DG mpya wa NHC na nikaelezea jinsi uhuni ulivyokuwa umefanywa ili kukidhi profile ya baadhi ya watu. Uhuni huu haukufanywa na mwingine bali IKULU ambako walitoa maagizo kuwa tangazo la awali la nafasi hii iliyotolewa gazetini ibadilishwe...in short tangazo la nafasi ya hii la mwanzo lilitaka mtu mwenye qualifications kem kem baadae tangazo la pili lililotoka likawa limepunzuza sifa za anayetakiwa ...bila maelezo yoyote ile.


Ukweli wa uteuzi huu wa nehemia ni kama ufuatavyo:


1.Nehemia HAKUOMBA kazi hii kama ambayo sheria ilitaka afanye

2. Nehemia hakuitwa kwenye USAILI kama ambavyo sheria ilitaka ifuatwe

3. Nehemia kamapata kwa sababu ya presha na ufisadi wa hali ya juu uliyofanywa na Katibu Mkuu wa Ikulu bwana LUHANJO

4. Ambao walioomba na wakaitwa kwenye usaili hawajaandikiwa barua ni sababu zipi walikosa halafu kazi akaewa ambaye hakuomba hiyo kazi in the first place.



Sasa in the wake of haya ya kumsifia Nehemia na mengineyo tusisahau kuwa kuna uteuzi kama huu unaweza kuja kufanywa na rais na nadhani ni muhimu watu wasilalamike kuhusu FAIRNESS kama ambavyo hawalalamiki kuhusu procedures zilizotumika kumpata huyu Bwana NEHEMIA....isije ikawa Mkuki Kwa Nguruwe...


If anything hata kama Luhanjo alikuwa anamtaka kijana wake what was so difficult or worong UTARATIBU ukafuatwa?


 
Jamani It is common sense, NHC haiwezi kuepuka katika sakata hili, sema kwa kuwa serikali yetu ni ya kishikaji ni sawa tu, pamoja na kuwa na 30% bado interms of responsibility na authority katika ku protect national interest NHC inajukumu na majority shareholder na kama hili wakina Mchechu na mshikaji wake JK hawakulijua basi ni kichekesho. Mimi ni mmoja kati ya watu wachache sana waliokwisha sema hii habari ya roadshow media management ya wakina Mchechu ni time bomb na kashfa yake itazidi hata zile za EPA na Dowans, sasa ndugu yangu angalia hata hicho kiingereza chenyewe ni cha kikurungezi kweli (I am hear?) nakubaliana kabisa na Joshi Kanji tabia za wakina Pasco za upambe hazitusaidii, jengo la vioo la samora ndio litakalovunja rekodi zote ulimwenguni siku ya siku. Swali la msingi inamaana responsibility ya NHC kwenye joint venture hiyo ni kupata revenue tu mwisho wa siku? where were they wakati linaongezwa gorofa kwa 60% if the original BOQ? rubbish hatawapeani vyeo gani na kulindana vipi, siku ya siku kila aliyeua kwa 10% kama hoja zinajenwa kwa wakina Tony Blair na George Bush itakua hawa wa huku kwetu?

Mimi ni mpangaji wa NHC, nikitaka ongeza grill for my own security/protection kwenye nyumba yao naomba kibali, wanakuja kagua na kunijibu niweke au la?

Iweje kwenye kuongeza ghorofa? Na mbia mwenzao wasishirikishwe walikua wapi bana?

Mchechu has to go yuko pale pale kwa maslahi ya kisiasa hence miradi mingi imekaa kisiasa siasa tu
 
Mkuu sana Masanja akaja na hi yake hapa chini......

WoS, heshima mbele,

I beg to respectifully disagree. Head hunting inafanyika katika juhudi za ku-widen pool ya applicants. Huwezi amua kumchukua Masanja from Nowhere, bila kumshindanisha na wengine ukasema kwamba hiyo ni head hunting. What happened to merit? Unless hiyo inafanyika hapa TZ tuu. Assume you go by what you say "head hunting". This will set a VERY dangerous precedent, maana you no longer subscribe to merit na utakuwa huna haja ya kuinvite applications. Yes applicants wanaweza wasiwe na vigezo, its precisely because of that....you will ask specific people to submit their applications for consideration. Otherwise, you kill the whole thing of merit na credibility ya eventual winner.

Kama NEHEMIA aliomba hi kazi, akashindanishwa na wengine, akaibuka mshindi. I will buy your argument ya head hunting. Maana siku hizi hata mashirika makubwa iwe UN, WB au kwingineko, head hunting inafanyika, lakini inaishia "kukuomba" uwasilishe maombi yako kama wengine. Hii inasaidia kuwa na strong pool ya applicants. Lakini hii kwamba mtu atoke from nowhere, umkabidhi kitengo...harafu useme ni head hunting, we miss a point.

In all, naamini kama mkuu Waberoya alivyoshusha maswali legit hapo juu, as we move forward ukweli utafahamika. Trust my word. Na kama kweli itakuwa hivyo, hata credibility ya Nehemia itashuka maana hata wenzake waliokuwa wanamuona kijana hardworking..well..watamuona sasa kama ni mtu wa kubebwa which is a bad fit kwa kijana mwenzetu.

In anything you do especially when it involves public resources/interest, you ignore procedures at your own peril. Because, at some point, it will come to HAUNT YOU.

Masanja
 
Last edited by a moderator:
nimeshaona hoja. nhc isiache huyo mwekezaj afanye atakavyo kwenye kiwanja. lazima nhc ishirikishwe. ikiwezekana pitieni hiyo mikataba ya nyuma muhakikishe quality products among others zinakuwa produced. ila kuna maghorofa mengi mengine yanajengwa bila ubia wa nhc. japo msechu hausiki kwenye haya magorofa lakin ni hatari kwa maisha yetu na mali zetu. jamani vyombo vinavyohusika wajibikeni ipasavyo.
 
siku moja nilisafiri kwenda mkoani. usiku nikaenda disko kwenye ghorofa fulan. kufika kule juu nikaona ghorofa lina nesa ka muanzi. nikashuka fasta. kuuliza nikaambiwa jamaa alipewa kibali cha kujenga ghorofa 4 yeye kapiga 8. hapa si nhc wala msechu wanaohusika maana ni kiwanja cha mtu binafsi na kinajengwa na mtu binafsi. hapo pia roho za watu na mali zao viko hatarini.
 
Mkuu mwingine akaja na hii kuhus money laundering.....aisee.....halafu leo eti tunaambiwa "uchumi rahisi"...

Kwa sababu kuna hela za deal wanataka kuchukua.

Kuna mpango wa kujenga nyumba, CCM/ Ikulu inataka ku divert hizi hela ziende kwenye mifuko yao wakti wa kampeni.

Huyu bwana wanamuamini anaweza kuwafanyia kazi vizuri kwa sababu wakati mabenki karibu yote yalipokataa kushika pesa za EPA kwa kufuta kanuni za banking zinazokataza "money laundering" huyu mshashi ndiye aliyewaokoa na kuzi launder, kwa hiyo ni mtu wao hawana shaka naye.

Hawataki kumuwka just any qualifid candidate kwa sababu wanahofia kukutana na maskini jeuri mmoja atakayewaumbua vibaya vibaya tu.

At least that is what the accussing party is inferring.
 
Na hivi ndivyo jinsi alivyopatikana.....ikijibu maswali ya GT

Mkuu Kasheshe,

Utaratibu wa kuwapata ma-CEO/DG wa mashirika yaliyo chini ya serikali siku hizi umebadilishwa na kwamba wana-appoint on merit, lakini haiko hivyo.

Huu utaratibu mpya ni wa kuwa-fool WB, IMF na nchi wafadhili kwamba serikali inateua viongozi wa mashirika ya umma wenye sifa zinazotakiwa na wamepatikana kwenye soko la kazi kwa kushindanishwa.

Utaratibu mpya ni kwamba: Serikali inatangaza tender ya recruitment, kwa hiyo akina KPMG, E&Y, na kampuni nyingine za wazawa wanaomba hiyo tender.

Baada ya hapo mshindi wa tender akipatikana, ndipo anapewa terms, conditions na mengineyo.

Hatua inayofuata ni kampuni husika kutangaza tangazo la kazi hiyo na waombaji hutuma maombi yao kwa kampuni hiyo. Then shortlisting inafanyika na watu wanaitwa kwenye interview.

Finally, kampuni hupendekeza majina matatu ya watu walio perform vizuri kwenye mchakato huo. Then majina hayo hupelekwa Ikulu kwa ajili ya appointment. Rais habanwi kwamba lazima achague top, anaweza ku-pick any kati ya hao watatu. Nadhani hapo ndipo kama Usalama wa Taifa huwa wanafanya kazi, wanaweza kufanya vetting kwa hao watu 3 na finally akachaguliwa mmoja kati ya hao.

Tatizo la hii kashfa ni kwamba E&Y ndiyo walipewa jukumu la kuendesha mchakato na walipeleka majina matatu. Then from no where likatoka tangazo jingine la nafasi hiyo hiyo na lilitolewa na kampuni nyingine ya wazawa.

Maswali ya kujiuliza, kwanini mchakato wa E&Y ulifutwa? Je, ni kweli kijana Nehemia hakuwa mmoja wa waombaji kati ya walio omba E&Y? Je, ni kweli aliambiwa apeleke CV wakati mchakato unaendeshwa na kampuni ya wazawa? Kwanini alipeleka hakupeleka mwanzo kama alikuwa na nia ya kuomba hiyo nafasi? Je, wale watu 3 waliopendekezwa na E&Y wana qualifications ambazo ni za chini ukilinganisha na qualifications za Nehemia?
 
kwenye suala la ghorofa hilo kuporomoka kuna watu/ mamlaka wako/ ziko karibu zaidi na tukio au sababu za tukio kuliko nhc na msechu. kuna watoa vibali na wale wakuhakikisha ghorofa ni la ubora. au maisha na mali za wapanda magorofa ya nhc ndo vya maana zaidi? angalia - tukiwaweka sawa wanaotakiwa ku-ensure tuna quality gorofas hapa tz hatutahangaika na nhc/msechu na maisha na mali za watz vitakuwa salama.
 
Mkuu Rev Kishoka naye akashuka na ya kwake kama hivi...........

Ama kweli Tanzania ni Jamhuri ya Vyura!

Here is my take on this whole saga!

1. Why do we still have public corporations that are being run by the Government at this time where we are preaching and practicing Free Market economy? Why not privatize all the so Called Mashirika ya Umma so that they can run independent of Politics and Politicians?

2. Why does the President continues to have say in every appointment or his office? If a Corporation has BoD, should the BoD decide on hiring and firing of the DG, MD, GM, CEO? or kwa kuwa in Tanzania DG, MD, GM or CEO is also CoB then it is impossible?

3. What and why there is such high interest put forth on Wizara Mama? If Wizara Mama does not have; credible policies, credicle leadership, credible strategies and modes of operations, how can a Shirika or Taasisi being expected to perfom?

4. If head of Taasisi or Shirika la Umma is Political appointment, why there is such deception of Mchakato wa Usahili and even waste of time and money to create a recruitment process hata kama kuna Sheria as WoS stated? Why waste time and Money and not just make the appointment and live with the consequences of the descicion made?

Now if I turn to Nehemia himself I have the following questions;

1. Why didi he disclose to friends or whomever that he never applied for the job or did not even receive an interview?

2. In a period less than 7 years he worked for 4 different firms, in which 3 of them Citi, Barclays and Standard Chartered are very strong Banks with high reputation. Could he give an explanation on why he was wandering around? If I am a head hunter, those 7 years of Nehemia hopping like grasshopper, should be sufficient red flag!

3. As the CEO of UAB, can he explain why he violated the Money Laundering policies set by BOT and made such reckless descision which facilitated the wizi wa fedha za EPA? if he is Finance wizard as the bio claims, how could he allow his Bank to be a conduit of illicit money? Did he approve the opening and handling of EPA money accounts to make profit so that his Stats could show a track record of growth and profitability while disregarding true principles and regulations of Banking?

4. Can he give a testimony of why he is still a board member of NICOL an institution that has been severely tarnished with high degree of irregularities, dishonesty and it is almost bankrupt?

5. On his association with the UD advisor, what can he tell the mass of their relatioship and the mentoring piece that he received? IS his personality as a Banker shaped through visions and advisory of this mentor who is assumably disgraced?

And lastly to us Jamhuri ya Vyura

1. What on hell do we expect to function to any standards in the current environment Tanzania is in? There was Jubilation of his appointment, eti ni Kijana mwenzetu, zimepanda and all sorts of accolades driven by Getorade adrenaline and sensation of LSD, now we see the other side of the coin and discrepancies, the LSD is wearing off and we are now reactionary!

2. If we are looking for fairness and better things, we need to have an overhaul of everything and nothing spared, no stone unturned! This means change of ideology, change of practice and change of so many things!

Yangu hayo machache kwenu Jamhuri ya Vyura!
 
Kuna jamaa mwingine akaja kuweka mambo sawa kama hivi.....
Mimi namfahamu huyu na kwa kweli CV yake ni nzito, ni mtu msafi na mchapa kazi na uteuzi haukuwa na mizengwe isipokuwa wale waliokosa kazi hii ndyiyo wanataka kila mtu aamini kuwa kulikuwa na mizengwe.

Nimefuatilia kwenye source muhimu ndani ya E&Y na hii ndo hadithi kamili. Jamaa aliomba hiyo kazi na ni kati ya watu 26 waliokuwa shortlisted na E&Y kuwa wanafaa kwa kazi hiyo. Lakini badala yake E&Y walisaili majina kumi na moja tu kati ya 26 na baada ya waiziri kutoridhika na mapendekezo alichagua kampuni nyingine iliyofanya usaili kwenye majina yaleyale ishirini na sita na mshikaji aliwapiga watu mbali vibaya sana. Na ukweli uko wazi hakuna aliyekuwa na CV inayokaribiana na yake na jamma ana track record nzuri kwa yale aliyofanya akiwa stanchart kwa miaka mitano kwenye nafasi za juu na pia CBA akiwa CEO kwa miaka mine. Hizi ni kelele za kukosa kazi na tunataka tuambiwe ni nani anajihisi alikuwa bora kuliko yeye katika wale 26 na tujadili. Mimi nilikuwa ni mmojawapo wa waliokuwa kwenye mchakato na nilipojua kuwa jamaa yupo kwenye mchuano nilijua basi nipo nje ya game. Na mwisho Bodi waliajiri E&Y iliwaweze kumshauri waziri na kisheria waziri na wajibu ndiye mwenye wa kuteua na si lazima afuate mapendekezo.

Pia nimefuatili pale CBA kujua jamaa alianza kazi na uhusiano wake na hizo EPA, jamaa alijiunga na CBA mwaka 2006 na EPA ilipita mwaka 2004 sasa uhusiano na ufisadi uko wapi. Jamani inabidi watu tufanye utafiti kabla ya kuandika andika na kuchangia habari zisizo na utafiti wala kichwa!

Huyu jamaa ni mtu wa Tanga na sasa hayo mambo ya kusini yanatoka wapi na tatizo liko wapi if he is a perfomer?

GT wewe unasema unamfahamu huyu jamaa na rafiki yako, hebu tuambie credentials zako na achievement zako ili tuweze kukuchambua na kukujua, vipi uwe na rafiki halafu unajificha na kutuletea habari hapa au na wewe ulikuwa kwenye mchakato huo na ukakosa hiyo kazi.

Jamaa anaheshimika na resource nzuri na kwenye CV nimeona yuko kwenye Bodi nafikiri kwasababu ya ubora wake, huyu jamaa ni Board member Ardhi University Real Estate School, pia ni Bodi Member na mwenyekiti wa Audit Committee wa Tumaini University (TURDACO), Ni mwenyekiti wa Bodi wa Rightway Schools, Ni Board Member na mwenyekiti wa Audit Committee wa PTF, Ni Board member wa CEOrt, CEO roundtable of Tanzania, kwa uchache tu! GT hivi kwakuleta hoja hii inasaidia vipi watanzania leo?

Wakichagua wazee malalamiko, vijana malalamiko, wakiletwa watu waliotoka nje ya system ilikuleta ufanisi wao malalamiko, wakichaguliwa wa ndani mnasema ni walewale, wakija wakenya mnalalamika, mghana mnalalamika, wahindi mnalalamika n.k. hivi watanzania tunataka lipi. Serikali taratibu imeanza kuvutia watu wa private sector basi tuwaunge mkono maana na wewe watakufikia as long as your competent.

Mchechu kachape kazi tunakuaminia kijana acha hawa watu wenye njaa zao wanaoshinda kujadili watu na matukio!!!!!
 
baadaye jamaa akajirudi mwenyewe kuwa GT alikuwa sahihi kama ifuatavyo...........

Well GT you had the right informantion, as I have confirmed from the most realiable source, na hii inaendana na informnation za GT espcially item 1&2.

  1. Ni kweli jamaa hakuomba kazi wala kufanya interview!
  2. Previous DG alimaliza kazi yake toka mwaka jana mwezi February 2009 and since then the Government was looking mtu atayeweza kubadili shirika hilo from a non perfoming to a perfoming Corporation with the view of providing more house kwa watanzania kama Tangazo la appointment lilivyotoka.
  3. Kwa hiyo katika search za muda mrefu sana Nehemia alionekana the right candidate to transform kampuni na ukizingatia kuwa JK ameamua kudeal na vijana watakaoweza kuleta mageuzi kwenye uongozi wa taasisi za serikali na historia ya jamaa ya utendaji kazi inajieleza wazi!!!
  4. Na kwa taarifa kuna orodha ndefu ya vijana watendaji wazuri watakao ingizwa serikali kuchukua nafasi kubwa kutoka private sector ndani ya mwaka huu na hii ya jamaa ni mwanzo tu. Nafikiri ni mwanzo mzuri wa serikali kubadili nchi na tuige Singapore, Malaysia na Dubai, hizi ni nchi zilizopiga hatua kubwa na mtu anakuwa handpicked for the good perfomance and the good vision kwenye taasisi fulani ya Umma.
  5. NAFIKIRI NI VIZURI TUKATUMIA THREADS HII KUELEZA MTIZAMO WETU WA NHC GANI TUNGEPENDA JAMAA HUYU AIJENGE, NA HII NDIYO MIJADALA YENYE TIJA!!!!
  6. NAOMBA SERIKALI IENDELEZE LIBENEKE LA KUTUPATIA WACHAPAKAZI, TUNAHITAJI MAENDELEO NA WATU WATAKAOSAIDIA MAENDELEO NA SIYO SIASA. JK ONGEZA KAZI KWENYE HAYA MABADILIKO UNAYOLETA AMBAYO TULIYAHITAJI SANA!
 
Ila mkurugenzi sio jambo jema kuwa eneo hilo ukiwa umelewa kwa sababu unaweza kutoa uamuzi wenye madhara kwa sababu ya pombe.
Nasema hivi kwa sababu kama wewe ni mswahili mwenzetu, confidence ya kuporomosha umombo, huku ukijua kabisa kiingereza chako ni kibovu kama cha kwangu lazima itakuwa imechangiwa na the power of kiroba...
Huwa tunavisikia sana hivi viingereza baa...

Joshi, NKM stands for Nehemiah Kyando Mchechu, and in future when you see such an ID just know that it's Mchechu responding on issues or commenting! I am not a person who will hide is ID since I believe in truth and transparent! Neither do you have so many people at my level in Public Sector and non political who stands by their ID's.

Just to prove you wrong I am now at the accident scene as I am writing to you and we are not more than 70 people, and I was hear yesterday up until 01:30am! I am following through all the comments in different threads, actually I have always been a good follower of JamiiForums but I was never a contributor! I think the series of threads which most are misleading without facts have pushed me to consider responding to all these issues. However, by obviously fact I do not expect to become an active member on contributions!

For now I have opted to focus on the task at hand here at the accident scene, and I will try to respond on these few in a very brief in the coming two days either by posting a thread or by calling a press conference where you can come and ask as many questions as you want and we will respond to all of them and I hope it Will be at your satisfactory level and to others as well! There is nothing to hide here, no politics, no partisans side and no blax2! I am sure the press conference has always enough participants who are members of JamiiForums and they gone through all the posted comments and certainly they will be looking for answers by asking the same sort of questions!

Thanks and stay relaxed till then!
 
siku moja nilisafiri kwenda mkoani. usiku nikaenda disko kwenye ghorofa fulan. kufika kule juu nikaona ghorofa lina nesa ka muanzi. nikashuka fasta. kuuliza nikaambiwa jamaa alipewa kibali cha kujenga ghorofa 4 yeye kapiga 8. hapa si nhc wala msechu wanaohusika maana ni kiwanja cha mtu binafsi na kinajengwa na mtu binafsi. hapo pia roho za watu na mali zao viko hatarini.

Taifa letu limekosa maadili na uzalendo! Haya ndio madhara ya kukosa mapenzi kwa nchi na raia wako na kutanguliza mapenzi ya pesa na mali. Watz kama taifa kwa kushirikiana na viongozi wetu wa kisiasa bila kujali itikadi za vyama hatuna budi kukaa pamoja na kutafakari hatima ya taifa letu, Tanzania lasivyo nchi hii inaweza kutumbukia ktk maangamizi makubwa.
 
NKM

Unachotueleza ni kwamba NHC inajali mapato yake kuliko usalama wa watu na mali zao

NHC inatakiwa kuelewa kuwa jukumu la usalama la jengo lolote linalonadiwa kwa jina la NHC, kwa hiyo hoja ya kuwa tunapaswa kuheshimu mkataba unaosema mbia ndie atashughulikia kila kitu ni hoja mfu na inaonyesha huko NHC kumekosa watu wenye maarifa hadi kuruhusu mikataba ya aina hiyo iruhusiwe kuendelea bila ya kubadili walau vipengele vichache kwenye mkataba
 
Last edited by a moderator:
Ila mkurugenzi sio jambo jema kuwa eneo hilo ukiwa umelewa kwa sababu unaweza kutoa uamuzi wenye madhara kwa sababu ya pombe.
Nasema hivi kwa sababu kama wewe ni mswahili mwenzetu, confidence ya kuporomosha umombo, huku ukijua kabisa kiingereza chako ni kibovu kama cha kwangu lazima itakuwa imechangiwa na the power of kiroba...
Huwa tunavisikia sana hivi viingereza baa...

na ma-pressure. mshikaji akaona ajimwage hivo hivo. ange jaribu kutumia Microsoft Word kunyoosha maneno
 
Naikubali hoja yako..

Mchechu anahusika kwa sana, awajibishwe pia
,ndugu yangu mbona huna hoja inayokusukuma kutaka huyo mchechu awajibishwe, hebu tupe hoja kisha uyaseme hayo unayoyataka vinginevyo ni chuki binaffsi.
 
Ila mkurugenzi sio jambo jema kuwa eneo hilo ukiwa umelewa kwa sababu unaweza kutoa uamuzi wenye madhara kwa sababu ya pombe.
Nasema hivi kwa sababu kama wewe ni mswahili mwenzetu, confidence ya kuporomosha umombo, huku ukijua kabisa kiingereza chako ni kibovu kama cha kwangu lazima itakuwa imechangiwa na the power of kiroba...
Huwa tunavisikia sana hivi viingereza baa...
Badala ya kuweka nyekundu tu ungemsahihisha pia ili siku nyingine asirudie makosa.
 
NKM....mkuu jitihada zako za kufufua maiti(NHC) zinaonekana na sasa inapiga chafya..haya ni maajabu makubwa tunakupongeza

Swali langu moja..ni vipi pale Shekilango muwaongezee adha wapangaji wenu kwa kuwajengea ghorofa kati ya ghorofa?

Wapaki wp magari?watoto wao wacheze wapi? Nguo waanike wapi? Na majanga kama moto yakitokea hali itakuwaje maana hata gari ya Fire & rescue haitaweza kuingia

Je hamna viwanja vipya au vya zamani venye nafasi hata nje ya jiji mkaviendeleza kuliko kuchafua jiji namna ile? Kumiliki vile viwanja sio maana yake lazima uvijenge!!!

kwa ahadi yako kuwa utajibu ukiwa na wasaa naomba hili pia lijibu katika press conference kwa ufasaha

Mkuu NKM bado nasubiri jibu
 
Last edited by a moderator:
Kuna jamaa mwingine akaja kuweka mambo sawa kama hivi.....


Achape kazi na uzembe huu wa kuangusha majengo na kuua watu. Nchi hii kwa mfumo wa utawala uliopo hata kama utumie E&Y bila mkono wa vigogo wa ccm ni vigumu kupata nafasi kama hizi ndugu yangu. Anachokifanya huyu jamaa ktk NHC ya leo si kwa faida ya masikini wa mijini na vijijini ila kwa matajiri na watu wa kati tu. Ni nani anakaa kwenye nyumba anazojenga nehemia kwa sasa? Tafakari.
 
Ogah umeua aisee!! Lakini pamoja na hayo magumashi dogo mpaka sasa amefanya vizuri tukubali hilo ili mjadala wa uwajibikaji wake usikwepe huu ukweli!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom