Uwekezaji wa NHC - Mchechu awajibike

Uwekezaji wa NHC - Mchechu awajibike

Huyu jamaa hana pa kutokea na inaonyesha kabisa kuna something fishy juu ya huu ujenzi anajua! Sasa hiyo foundation ya jengo ilikuwa designed kwa ghorofa kumi au kumi na sita.
 
Huyu mkurugenzi wa NHC awe accountable kwa ile mikataba ambayo imesainiwa akiwa amekwisha teuliwa ; kama aliteuliwa mwaka 2007 na mkataba wa ubia wakujenga hilo ghorofa lililopomoka uliingiwa 2006 then hana hatia!! Maadam hili janga limetokea ni vyema huyu huyu Mchechu achukue jukumu la kupitia upya ile mikataba inayotekelezwa ambayo aliikuta na kuhakikisha kuwa mapungufu yanayoweza kutuletea majanga yanarekebishwa kwani kasi ya ujenzi wa haya maghorofa ya ubia kati ya NHC na wahindi hapo CBD inatisha!!

Oohh really? si ushasema hahusiki na mikataba ya zamani? sasa aipitie upya kivipi? huu ulioangusha ghorofa kwa nini 'hakuupitia upya".

Hoja yako ni kuwa mikataba kaikuta hahusiki, basi tuendelee hivi hivi maana jengo la jirani nalo pia tuna hesabu siku lakini kwa kuwa Mchechu hahusiki tuache tu au sio?
 
NKM....mkuu jitihada zako za kufufua maiti(NHC) zinaonekana na sasa inapiga chafya..haya ni maajabu makubwa tunakupongeza

Swali langu moja..ni vipi pale Shekilango muwaongezee adha wapangaji wenu kwa kuwajengea ghorofa kati ya ghorofa?

Wapaki wp magari?watoto wao wacheze wapi? Nguo waanike wapi? Na majanga kama moto yakitokea hali itakuwaje maana hata gari ya Fire & rescue haitaweza kuingia

Je hamna viwanja vipya au vya zamani venye nafasi hata nje ya jiji mkaviendeleza kuliko kuchafua jiji namna ile? Kumiliki vile viwanja sio maana yake lazima uvijenge!!!

kwa ahadi yako kuwa utajibu ukiwa na wasaa naomba hili pia lijibu katika press conference kwa ufasaha

kama ikitokea kama janga la Indira Gadhi itakuwaje??
 
Mchechu si mjui sana lakini kazi zake na ukombozi wake juu ya shirika lilokuwa linakwenda kufa nautambua kwa dhati, nashauri anaweza kuwa anahusika indirect lakini mimi nasema ni bahati mbaya amejifunza nasema hivyo kwa sababu kukuta mkataba ni moja lakini kuagiza mainjinia katika ofisi yake kumhakikishia ubora wa majengo ni jambo lingine. yeye ni binadamu amepitiwa tu lakini mainspector na waratibu wa majengo ya ubia wake wahojiwe na wawajibishwe kwa mujibu wa sheria, tumpe Mchechu onyo la mwisho, lakini wahusika wa karibu wa ufuatiliaji kutoka taasisi zote wajibu mpaka yanatikea walikuwa wapi, jengo kubwa kama hili walitakiwa kuwa makini sana sasa kama walikula ten pasent waonje hara yake
 
Mchechu si mjui sana lakini kazi zake na ukombozi wake juu ya shirika lilokuwa linakwenda kufa nautambua kwa dhati, nashauri anaweza kuwa anahusika indirect lakini mimi nasema ni bahati mbaya amejifunza nasema hivyo kwa sababu kukuta mkataba ni moja lakini kuagiza mainjinia katika ofisi yake kumhakikishia ubora wa majengo ni jambo lingine. yeye ni binadamu amepitiwa tu lakini mainspector na waratibu wa majengo ya ubia wake wahojiwe na wawajibishwe kwa mujibu wa sheria, tumpe Mchechu onyo la mwisho, lakini wahusika wa karibu wa ufuatiliaji kutoka taasisi zote wajibu mpaka yanatikea walikuwa wapi, jengo kubwa kama hili walitakiwa kuwa makini sana sasa kama walikula ten pasent waonje hara yake
NHC imewahi karibia kufa? Lini hiyo?
 
Are you serious? Walipoingia makubaliano yalikuwa ya kujenga jengo la aina gani, ukubwa gani na ghorofa ngapi? Unataka kuniambia hawakupewa hata michoro, bills of quantities, mkataba wa ujenzi n.k.? Sasa kama hawakupewa vyote hivyo wangejuwaje thamani ya hiyo asimilia 25? Au na yenyewe walingojea Ladha awaambie? Yote haya ni maswali ya kujiuliza.

Kama NHC, ambaye alikuwa na asilimia 25 ya hisa katika jengo alimuachia mwenzake afanye atakavyo basi alikuwa mzembe wa kutupwa. Kuwa na asilimia ndogo hakukuzuii kuwa na mikutano na mbia mwenzako na kuhoji utendaji wake. Hili lilifanyika? NHC ina wataalamu wa ujenzi (tusisahau kuwa ni washauri na makandarasi pia), je walikuwa wanahudhuria mikutano ya sait? Je walikuwa wanapewa ripoti ya maendeleo ya mradi? Kama walikuwa hawapewi, waliwahi kudai? Waliwahi kutuma wataalamu wao sait wakafukuzwa kwa sababu wana hisa kiduchu?

Na hili ni fundisho kwa wale wote wanaoingia ubia wa kupatiwa viji-apartment Upanga. Janga likitokea utahusishwa moja kwa moja kwa hiyo ni bora udai kushirikishwa kikamilifu katika ujenzi wa jengo lenu ama sivyo ujitoe katika ubia, chukua kiwanja chako umuachie jengo.

Amandla........
mkuu nakupatia LIKE!
 
Wakati taifa lipo katika kuombeleza janga la kuanguka kwa jengo la ghorofa kati kati ya jiji, kuna mambo kadhaa yamejitokeza kuhusiana na mkasa huu.

Shirika la Umma kama NHC kuingia ubia wa kimagumashi magumashi na wafanyabishara wababaishaji kumepelekea kupotea kwa maisha ya ndugu zetu takriban 20+. Inakuwaje uwekezaji mkubwa kama huu NHC wanaacha kila kitu kiendeshwe kienyeji enyeji tu? kibaya zaidi sasa wanaibuka na kusema wanapitia upya sera yao ubia ili washirikishwe zaidi!.

Kwa mshangao mkubwa juhudi zote za uokoaji zinazo endelea si Mchechu au kiongozi yeyote mwandamizi wa NHC alie thubutu walau kufika site kujionea hali halisi. Rais pamoja na majukumu yake mengi ameshatembelea eneo husika mara mbili.

Imefika wakati mkurugenzi mkuu wa NHC akamatwe na awajibishwe na mamlaka za uteuzi. Taifa haliwezi kuingia katika janga kubwa kama hili wakati wahusika wala hawana habari.

Mchechu has to go....

==========
Majibu ya Nehemiah Kyando Mchechu:

Ndugu yangu kuondoka ni kazi,kwani ile asilimia kumi waligawana wangapi?Ndio hapo rushwa itakapotumaliza watanzania.
 
Kaka acha mawazo mgando, kufungwa mkataba hakujazuia shirika la nyumba wasifuatilie huo mradi. Kubadilisha shirika sio warrant ya kufanya madudu, ina maana baaada ya mkataba ofisi ya shirika la nyumba ilifungwa. Acha hizo hiyo hoja bado ina mashiko tu labda kama una maslahi binafsi na hilo
 
Mkuu,

Kama una chuki binafsi na mchechu sema but hoja yako haina mashiko. Mchechu ameingia after 2007 na ameinadilisha shirika lililokuwa mbioni kufa sasa wanatembelea hilux kwenye kazi zao. Pia hoja yako haina mashiko kwasababu mkataba wa kujenga lile jengo ulifungwa mwaka 2006, sasa Nehemiah Mchechu anahusikaje? Mie namtetea labda ulete sababu zenye mashiko but hii sio mkuu.


Kaka acha mawazo mgando, kufungwa mkataba hakujazuia shirika la nyumba wasifuatilie huo mradi. Kubadilisha shirika sio warrant ya kufanya madudu, ina maana baaada ya mkataba ofisi ya shirika la nyumba ilifungwa. Acha hizo hiyo hoja bado ina mashiko tu labda kama una maslahi binafsi na hilo.
 
Mchechu ni contractor au consultant au ni nani hadi awajibishwe? tuwe na bu7ara sometimes.

Hilo swali muulize mjomba, ukishangaa la musa utaona la filauni. Muhasibu mkuu wa serikali alikuwa KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA JE KUNA LOLOTE ANAFAHAMU KUHUSU AFYA, NENDA TENA KAMUULIZE MJOMBA INAKUWAJE UKIPATA MAJIBU TULETEE WANA JF TUYATAFAKARI.
 
kuna vyombo vipo kufuatilia kama idadi ya ghorofa kama ni 10 zinajengwa 10 kweli, kama vifaa vya kujengea vinakidhi ubora na nk. hvo vyombo vikifanya kazi zao ipasavyo ndugu zetu hawatokufa au kuumia na mali hazitoharibiwa. nhc kufanya hzo kazi ni kujiongezea mzigo na muingiliano wa kazi. ndo hyo inaletaga sijui beauracracy. kazi moja watu kibao - kurefusha kazi, low efficiency etc.
 
Sabayi
Haya ya kutetea Mchechu eti amefanya makubwa NHC ndio yaliyoifikisha hapa tulipo tz. Watu kama mchechu wapo wengi nchi tena wazalendo zaidi yake!. Ni opportunity tu alipewa huyu bwana Mchechu, anaweza kuja mtz mwingine na kufanya makubwa zaidi yake. Tatizo letu wabongo ni uzembe wa kufikiri. Huyu mtu lazima awajibike.

Mkuu sipingani na dhana ya uwajibishaji kama umenielewa nimesema hii nchi imeoza kwa sasa hivi kumbuka kuwa presidential appointments hazitolewi kulingana na uwezo au utendaji wa mtu bali ni kutokana na ushakaji/mtandao/udini au ukabila so kwake ni coincidence ameteuliwa na anaweza kazi akiwajibishwa akaondolewa ataletwa mtu mwingine kwa vigezo nilivyotaja hapo juu na shirika likarudi kule kule
 
yaleyale ya mtu kuchora Zombi kwenye mtihani halafu kapata zero mnataka waziri ajiuzulu.
 
Mkuu sipingani na dhana ya uwajibishaji kama umenielewa nimesema hii nchi imeoza kwa sasa hivi kumbuka kuwa presidential appointments hazitolewi kulingana na uwezo au utendaji wa mtu bali ni kutokana na ushakaji/mtandao/udini au ukabila so kwake ni coincidence ameteuliwa na anaweza kazi akiwajibishwa akaondolewa ataletwa mtu mwingine kwa vigezo nilivyotaja hapo juu na shirika likarudi kule kule

Soma signature yako mwenyewe halafu urudi tujadiliane
 
Soma signature yako mwenyewe halafu urudi tujadiliane

Naijua hata kabla ya kuisoma,Nehemia alishawahi kukutangazia ni mwanachama wa Chama gani? Hivi kila mjadala lazima tuingize vyama?
 
Mkuu sipingani na dhana ya uwajibishaji kama umenielewa nimesema hii nchi imeoza kwa sasa hivi kumbuka kuwa presidential appointments hazitolewi kulingana na uwezo au utendaji wa mtu bali ni kutokana na ushakaji/mtandao/udini au ukabila so kwake ni coincidence ameteuliwa na anaweza kazi akiwajibishwa akaondolewa ataletwa mtu mwingine kwa vigezo nilivyotaja hapo juu na shirika likarudi kule kule
Sabayi
Mbona sikuelewi? Ndugu yangu funguka fikra zako. Acha kujifungia ndani ya box rafiki yangu, wee unajua huyu ameletwa na nani? Narudia tena nafasi aliyopata nehemia ya uDG hapo NHC ni opportunity, mimi sio mtu wa kijizuia kufikiri kama wewe kwamba eti akijihuzulu nehemia eti shirika linarudi kule kule! Haya ni mawazo ya watu wazembe wa kutumia bongo zao. Ukiondoa interference za wanasiasa nchi hii ina wataalamu lukuki wanaoweza kufanya makubwa hapo NHC hata zaidi ya nehemia. Ukiyasoma maelezo ya nehemia mwenyewe na maelezo ya NHC kama taasisi utagundua kwamba pamoja na uzuri unaonekana kwa nje wa utendaji kazi wa nehemia na NHC kuna tatizo kubwa ktk utendaji wao na ikichunguzwa kwa makini mengi yatajitokeza!
 
Last edited by a moderator:
katika historia ya nchi hii sidhani kama alishawai kutokea kiongozi mwenye akili kama nehemia
jamaa ana maono ya mbali,
huo ubia wala hakuingia yeye na kuvunja mkataba sio jambo rahisi kama unavodhani.
ungeanza kulaumu tbs wanaokubali vifaa feki vya ujenzi kuingia nchini

NKM anavuta sana uliza mmiliki wa zile appartemnt za pale OASIS mbezi beach ni nani kama hujaambiwa ni huyo huyo Mchechu?

Kaangalie zile nyumba za NHC kigamboni contractors ni kina nani? Na kama utaona sticker za CRB kwenye ule ubao wa mradi?
 
Mbona mada ni ya kiswahili lakini Mchechu amekuja kutujibu kwa kizungu, kizungu ambacho hakijakaa sawa pia. Next time namuomba bwana Mchechu atumie secretary wake ku post comment hapa maana kingereza chake kidogo kina walakin!
 
Back
Top Bottom